Hapa ndipo patamu ni mtego yaani walete hadidu za rejea za kikao walichokaa kupinga maamuzi ya kamati kuu, kama hatabaki Malah pekee mtaniambia.Alisema kufuatia upungufu huo, alimtaka mwenyekiti huyo kuwasilisha ushahidi utakaobanisha madiwani walivyohusika katika kikao cha kupinga uamuzi wa kamati kuu na msimamo wa chama.
Source!KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema madiwani watano wa chama hicho kati ya 11 waliodai kuhusika na uingiaji mwafaka na CCM, wamewasilisha barua za kuomba radhi ofisini kwake.Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na barua ya kukata rufaa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa madaiwani hao, Estomi Mallah, kupinga uamuzi wa kamati kuu wa kutengua maridhiano yaliyofikiwa na madiwani hao.Dk Slaa alisema tayari amepokea barua kutoka kwa madiwani watano kati ya 11 waliokuwa wameorodheshwa kwenye barua ya kukata rufaa."Baada ya uamuzi kutolewa na kamati kuu, niliwaandikia barua za kuwataka wajiuzulu nyadhifa zao ndani ya siku tatu, lakini wao wakapinga hatua hiyo na mwenyekiti wao akawasilisha barua ya kukata rufaa," alisema Dk Slaa.Alisema barua hiyo iliyowalishwa kwake, ilikuwa na upungufu kutokana na kuorodhesha majina ya madiwani wote 11 wa chama hicho, huku sahihi zikikosekana kwa baadhi ya majina.Alisema kufuatia upungufu huo, alimtaka mwenyekiti huyo kuwasilisha ushahidi utakaobanisha madiwani walivyohusika katika kikao cha kupinga uamuzi wa kamati kuu na msimamo wa chama."Mimi bado sijapata ushahidi kutoka kwa mwenyekiti huyo hadi sasa, nilichopokea ni barua tano kutoka kwa baadhi ya madiwani walioshiriki mwafaka huo za kuomba radhi," alisema Dk Slaa bila kutaja majina ya madiwani hao.Kuhusu hatua za kinidhamu, Dk Slaa alisema: "hapa hakuna siri hilo linasubiri vikao vya chama." Alisema Chadema kina taratibu za kufanya uamuzi kupitia vikao na vitakapopangwa, wananchi watajulishwa.Mgogoro wa Chadema ulianza kujitokeza pale kamati kuu ya chama hicho ilipotangaza kutotambua mwafaka baina ya CCM, Chadema na TLP kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, baada ya madiwani kugoma kujiuzulu wakitaka chama kiwasafishe na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yao.Januari 5, mwaka huu watu watatu akiwamo raia wa Kenya waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa umeya, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakifikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali kuhusu maandamano hayo.
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema madiwani watano wa chama hicho kati ya 11 waliodai kuhusika na uingiaji mwafaka na CCM, wamewasilisha barua za kuomba radhi ofisini kwake.
Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na barua ya kukata rufaa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa madaiwani hao, Estomi Mallah, kupinga uamuzi wa kamati kuu wa kutengua maridhiano yaliyofikiwa na madiwani hao.
Dk Slaa alisema tayari amepokea barua kutoka kwa madiwani watano kati ya 11 waliokuwa wameorodheshwa kwenye barua ya kukata rufaa."Baada ya uamuzi kutolewa na kamati kuu, niliwaandikia barua za kuwataka wajiuzulu nyadhifa zao ndani ya siku tatu, lakini wao wakapinga hatua hiyo na mwenyekiti wao akawasilisha barua ya kukata rufaa," alisema Dk Slaa.
Alisema barua hiyo iliyowalishwa kwake, ilikuwa na upungufu kutokana na kuorodhesha majina ya madiwani wote 11 wa chama hicho, huku sahihi zikikosekana kwa baadhi ya majina.
Alisema kufuatia upungufu huo, alimtaka mwenyekiti huyo kuwasilisha ushahidi utakaobanisha madiwani walivyohusika katika kikao cha kupinga uamuzi wa kamati kuu na msimamo wa chama.
"Mimi bado sijapata ushahidi kutoka kwa mwenyekiti huyo hadi sasa, nilichopokea ni barua tano kutoka kwa baadhi ya madiwani walioshiriki mwafaka huo za kuomba radhi," alisema Dk Slaa bila kutaja majina ya madiwani hao.
Kuhusu hatua za kinidhamu, Dk Slaa alisema: "hapa hakuna siri hilo linasubiri vikao vya chama." Alisema Chadema kina taratibu za kufanya uamuzi kupitia vikao na vitakapopangwa, wananchi watajulishwa.
Mgogoro wa Chadema ulianza kujitokeza pale kamati kuu ya chama hicho ilipotangaza kutotambua mwafaka baina ya CCM, Chadema na TLP kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, baada ya madiwani kugoma kujiuzulu wakitaka chama kiwasafishe na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yao.
Januari 5, mwaka huu watu watatu akiwamo raia wa Kenya waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa umeya, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakifikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali kuhusu maandamano hayo.
Malah leo ndio anaona umuhimu wa kutumia vikao mbona awali aliita waandishi wa habari alidhani watamsaidia,
halafu anataka kuwalazimisha na wengine waliokwisha omba radhi yeye aendelee na sarakasi zake za kujipima ubavu na kamati kuu.
katika hao madiwani watano yupo Nanyaro Ephata?
1. Sabina Francis
2. Viola Lazaro
3. Isaya Doita
4. Chrispin Tarimo
we hata Arusha huijui kaa kimyamallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.
mkuu source tunayo, ila nilikuwa nafanya utafiti kujua huyo diwani wa tano, kama siyo Elibariki Malle basi atakuwa ni Nanyaro. Kuna lobbying ilikuwa inafanyika kuwagawa madiwani, kama unakumbuka kuna thread ilikuwa inaelezea kugawanyika kwa madiwani.lete ushahidi kwamba hawa ndio wameandika barua za kuomba radhi.
Kumuekea! Du!! Zao la shule za kataQuinine, kuna mtu anataka chill source na tomato source, usisahau kumuekea na chips na mayai ya mbuni.
mkuu source tunayo, ila nilikuwa nafanya utafiti kujua huyo diwani wa tano, kama siyo Elibariki Malle basi atakuwa ni Nanyaro. Kuna lobbying ilikuwa inafanyika kuwagawa madiwani, kama unakumbuka kuna thread ilikuwa inaelezea kugawanyika kwa madiwani.
Huyu Mallah anaonekana ana uchu wa madaraka. Aligombea ubunge mara mbili akakosa, nadhani akaona udiwani utampatia umeya. Ccm walipochakachua, akaona angalau unaibu meya, sasa anaona chama kinambania tena. Huu ni uchu wa madaraka na kwa cdm ataangukia pua!
Kumuekea! Du!! Zao la shule za kata