Madiwani wamuumbua Ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani wamuumbua Ngeleja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 26, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Baadhi ya madiwani wa Sengerema mkoani Mwanza, wamemuumbua aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, baada ya kubainika kutojua taratibu na kanuni za uendeshwaji wa mabaraza ya halmashauri hiyo kutokana na kutohudhuria vikao tangu alipochanguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Sengerema.

  Hatua hiyo ilikuja baada ya Ngeleja kuchangia hoja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani akiwa amekaa chini, kitendo kilichosababisha diwani wa kata ya Nyehunge Msheleja (Chadema) kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Methew Lubongeja, kusimamia sheria, taratibu na kanuni zinazoelekeza kila mjumbe anapochangia hoja lazima asimame isipokuwa mwenyekiti pekee.
  Diwani huyo alitoa hoja hiyo, muda mfupi baada ya mbunge huyo kumaliza kuchangia taarifa ya diwani wa kata ya Busisi (CCM), Joseph Njiwapori, kuhusu uhaba wa chakula unaoikabili kata hiyo ambapo alisema kutokana na mazao yaliyolimwa katika msimu uliopita kukauka wakazi wa kata hiyo wanahitaji tani 1877 za mahindi ili kujikwamua balaa la njaa.

  Ngeleja wakati akichangia taarifa hiyo huku akiwa amekaa, alionyesha kusikitishwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Juma Mwanjombe, kutokuwa na takwimu sahihi za kaya zinazokabiliwa na uhaba wa chakula kwa wilaya nzima, ambapo mwenyekiti alizitaja baadhi ya kata zinazokabiliwa na tatizo kuwa ni Kalebezo, Busisi, Nyakasungwa, Buyagu na Igalula.
  Wakizungumza na gazeti hili nje ya ukumbi wa baraza hilo, baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo walidai hatua ya Ngeleja kutojua taratibu na kanuni za uendeshwaji wa vikao, zinatokana na kutohudhuria vikao hivyo tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Sengerema mwaka 2005 na amekuwa akielewa zaidi kanuni za Bunge la Jamhuri ya Muungano badala ya zile za vikao vya halmashauri.
  Mbali na kupongeza matumizi mazuri ya fedha za mfuko wa jimbo katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wa Sengerema, madiwani hao wamesema wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao wameanza kususia kuhamasisha shughuli za maendeleo kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa kipindi kirefu.  CHANZO: NIPASHE

   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hazielewi sheria, au dharau tu?
   
 3. R

  Ramso5 Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli sheria anazifahamu ila ni dharau tu kama ilivyo kwa huyo mshirika wake joseph njiwapori (Diwani-Busisi).Ameagizwa na mahakama kuu kurudisha nyumba aliyopora lakini kwa dharau hongo na rushwa na kiburi cha pesa kwa kiongozi huyu wa ccm anajiona yuko juu ya sheria.chama kimekua ni pango la waharifu.watu wanagombea vyeo ili kuficha maovu yao
   
 4. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mtoa hoja alikuwa nani? tangu lini amekuwa diwani? atoe vielelezo tangu 2005 vikao vya halmashauri vimefanyika vingapina wajumbe waliohudhuria maana si kweli kwamba Williasm ndiyo mara ya kwanza kuhudhuria vikao vya halmashauri
   
Loading...