Madiwani waliotimuliwa CHADEMA wabanwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani waliotimuliwa CHADEMA wabanwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Aug 30, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Na Graca Masha, Arusha

  [FONT=&amp]WAKILI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Method Kimomogoro, ameiomba mahakama kuwapeleka magereza waliokuwa madiwani watano wa chama hicho jijini Arusha endapo mpaka Septemba 3, mwaka huu, watashindwa kuwasilisha mahakamani hapo utaratibu wa namna ya kulipa gharama zilizotumika kuendesha shauri lao lililotupwa na mahakama ya mkoa.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kimomogoro ambaye pia anamtetea Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika kesi hiyo ya madiwani hao kupinga kuvuliwa uanachama, alitoa ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Charles Magesa, anayesikiliza shauri hilo la kudai gharama linalowakabili John Bayo, Reuben Ngowi, Charles Mpanda, Rehema Mohamed na Estomii Mallah ambao wanatetewa na wakili, Severine Lawena.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kuwa amefikia kutoa ombi hilo baada ya kuona shauri hilo limeahirishwa zaidi ya mara nne mfululizo, huku madiwani hao wakishindwa kuieleza mahakama namna watakavyowalipa gharama zao walizotumia kwenye shauri la madai kiasi cha sh milioni 15.1 kama ilivyoamriwa na mahakama.[/FONT]

  [FONT=&amp]Aliongeza kuwa, wateja wake wamemweleza kuwa wako tayari kulipia gharama za madiwani hao waliotimuliwa CHADEMA kukaa jela mpaka hapo watakapoamua kulipa deni hilo ambapo kwa mujibu wa sheria wanaweza kukaa huko kwa kipindi kisichozidi miezi sita.[/FONT]
  [FONT=&amp]Agosti 10 mwaka jana mahakama ya hakimu mkazi mkoa iliyokaa chini ya hakimu Hawa Mguruta, ilitupilia mbali shauri la madai lililofunguliwa na madiwani hao dhidi ya Mbowe na CHADEMA baada ya kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu ya kisheria.[/FONT]
  [FONT=&amp]Madiwani watano walikuwa wakipinga kuvuliwa uanachama wa CHADEMA, baada ya kufikia muafaka wa uchaguzi wa umeya wa Jiji la Arusha bila kupata baraka za chama.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hakimu Mguruta wakati akisoma hukumu yake hiyo, alisema kuwa mahakama haiwezi kuingilia maamuzi ya CHADEMA kwa kuwa ni chama kilichosajiliwa kisheria kama chama cha siasa, hivyo maamuzi yaliyotolewa na Kamati Kuu (CC) kwa kufuata katiba yake ni sahihi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pia, Mguruta aliwataka madiwani hao kulipa fidia ya gharama ya kesi hiyo kwa CHADEMA na Mbowe.[/FONT]
  [FONT=&amp]Hakimu huyo alisema kuwa mahakama yake inakubaliana na pingamizi zote tano zilizotolewa na wakili wa utetezi, ambazo ni kukataa CHADEMA kushtakiwa kwa jina lake, Mbowe kushtakiwa binafsi, mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kutengua maamuzi ya chama isipokuwa Mahakama Kuu.[/FONT]
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Kumbe ARS mambo moto bado,ila hao madiwani walidanganywa na mzee wa liwalo,sasa imekula kwao mbaya!
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Nape wasaidieni jamaa zenu kwani kazi mliowatuma walimaliza na matokeo ndio hayo. Au ndio mkishwatumia mnawatupa kama nanihiiii....?
   
 4. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Masikini madiwani hawa..they signed a deal with the devil (CCM) and this is the price they are paying. CCM wao kimyaa..
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Wacha iwapate . Hata leo nimemwona Malla pale eneo la parking ya Arusha Palace Hotel akiwa amejikatia tamaa mbaya. Malipo ya usaliti ndiyo hayo.
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  M4C itafagia takataka zote ndani ya CDM wabaki walio wasafi tuu shibuda tayari alishafyata mkia alikiogopa kimbunga cha M4C
   
 7. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Wameshaanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe.Hao madiwani wakamwangukie tu mzee Mtei bhaaaaaaaaaaass!!
   
 8. c

  christmas JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  maskini wamepoteza bara na pwani nyambaffff
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  akili nyingi mbele giza ndio haya yaliyowapata hawa madiwani walitumiwa lakini sasa wako peupe kama jangwani hawana kitu chochote
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Ila wakienda ccm wanaweza kupata ukuu wa wilaya embu washaurini tu jamani
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,821
  Trophy Points: 280
  Waende zao wasijidai wanang'ang'ania nini wanafiki?
   
Loading...