Madiwani waliohama Chadema na kutemwa CCM warudishwa

Madiwani waliohama Chadema na kutemwa CCM warudishwa

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,983
Reaction score
30,174
Arusha.
Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Arusha, kimewateua wagombea wanane wa udiwani, watakaoshiriki uchaguzi mdogo, watatu wakiwa ni madiwani ambao walijiuzulu Chadema ili kumuunga mkono Rais John Magufuli, lakini wakadondoshwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe amesema leo Ijumaa kuwa madiwani hao watapeperusha bendera ya CCM, katika uchaguzi huo mdogo. Uchaguzi unafanyika baada ya waliokuwa madiwani wa kata nane kupitia Chadema kuachia ngazi kwa hiyari yao wakiunga mkono jitihada za Rais Magufuli.

Mdoe amesema miongoni mwa waliopitishwa ni madiwani watatu waliojiuzulu udiwani Chadema na kujiunga na CCM kisha kupokelewa na mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli ambapo alishauri vikao vya kikatiba kuwarejesha katika nafasi zao kama bado wanazo sifa.

Madiwani waliokuwa Chadema na kujiuzulu ambao walishindwa kura za maoni ndani ya CCM na jana kupitishwa ni Japhet Joseph Jackson (Ambureni), Anderson Sikawa (Leguruki) na Solomon Laizer (Ngabobo).

Mdoe amesema katika kikao hicho cha leo makada wengine walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM na majina ya kata zao katika mabano ni pamoja na Francis Mbise (Muriet) iliyopo katika jiji la Arusha, Flora Zelothe (Mussa) iliyoko wilayani Arumeru. Wengine ni pamoja na Prosper Damuni MeyanI (Moita), iliyoko wilayani Monduli, Samson Laizer (Makiba) na Yona Kaaya (Maroroni) halmashauri ya Meru.

Amesema katika kikao hicho wajumbe wote na kwa kauli moja walikubaliana kuhakikisha ushindi unapatikana kwa chama cha mapinduzi na kuzitwaa kata hizo ambazo zilikua zikishikiliwa na madiwani wanaotokana na Chadema.

source; Gazeti la Mwananchi

My verdict,
madiwani waliojiuzulu na kuhamia CCM walikua 8 lakini waliopitishwa ni 3 tu. Means mission imekua failed kwa 5/8 = 62.5%. Hii iwe fundisho kwa madiwani wengine wenye mtazamo wa kua wakiondoka Chadema basi CCM itaendelea kuwajali
 
Mbona umeandika kishabiki ndugu yangu, hebu tuache siasa hizo wao ni wana ccm so wanahaki kupeperusha bendera...Ukiliona hilo sio jema tukumbuke tuliwapa Masha,Bulaya,Lembeli n.k kwani wana Chadema wenzetu hawakuwepo?? Wewe ndo kijana tukutegemee kujenga nchi??
 
Haiwezekani madiwani watoke chadema na kujiunga CCM yenye wanachama lukuki then uchaguzi unaitishwa upya halafu yake Chadema washinde tena. Kiukweli safari hii wanaccm hatutakubali ni lazima uongozi mzima wa mkoa utumbuliwe hata kama Chadema watashinda kiti kimoja, sisi tunataka kata zote. Dah hadi naikumbuka Yanga ya zamani ukileta ujinga ni bakora tu!
 
8ad31e934a0b3cb63712b7a4084cd417.jpg
watauana mwaka huu
 
  • Thanks
Reactions: K11
Na fikiri wameamua kuangalia uwezo wa binafsi wa madiwani (as how they are influential) kwenye kata zao.
1. Kama je yeye binafsi huyo diwani anauwezo na kundi lililopo nyuma yake.
Huo mchujo poa sana
 
Makijani yatashinda kwa kuiba kura, hivyo kuwa sana makini huko makamanda!
 
Back
Top Bottom