Madiwani waliofukuzwa wamvaa Mkurugenzi Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani waliofukuzwa wamvaa Mkurugenzi Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Madiwani waliofukuzwa wamvaa Mkurugenzi Arusha [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 06 October 2011 21:12 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Peter Saramba, Arusha
  MADIWANI watano waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamedai kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha,Estomih Chang’a, alikurupuka kutangaza kutowatambua kwa maelezo kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo bila kibali au maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa).

  Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, John Bayo aliyekuwa diwani wa Kata ya Elerai na Reuben Ngowi, aliyekuwa diwani wa Themi, walisema kitendo cha mtendaji huyo kutowaalika katika kikao cha kujitambulisha kwa viongozi na watendaji wa Wilaya na Manispaa ya Arusha, kilichoitishwa na mkuu mpya wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, kilikuwa ni cha kuwadhalilisha kwa sababu wao bado ni wawakilishi ‘halali’ wa wananchi katika kata zao.

  “Baada ya Chadema kutangaza kutufukuza uanachama na sisi kupinga mahakamani, waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa aliwaagiza meya na mkurugenzi, kuendelea kututambua na kuturuhusu kuhudhuria vikao
  vyote vya manispaa. Hakuna maagizo mengine hadi sasa na kama yapo tuna haki ya kuelezwa badala ya kuanza kubaguliwa kwenye shughuli za umma tunazoamini kuwa tuna haki nazo kuhudhuria,” alisema Bayo.

  Alisema baada ya agizo la Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika la kutaka wao kuruhusiwa kuhudhuria katika vikao na kulipwa posho, Kaimu mkurugenzi hajapokea maelekezo mengi na kwamba kwa kutenda cha kutowaruhusu kuingia katika kikao cha kujitambulisha, ameonyesha utovu wa nidhamu kwa mamlaka yake ya ajira ambayo ni wizara.

  Alisema wakati mtendaji huyo akiwabagua kwa kutowaalika na hata kufuta majina yao kwenye orodha ya madiwani waliostahili kulipwa posho, siyo wao wala manispaa iliyokuwa imepokea nakala ya hukumu ya mahakama iliyotupilia mbali madai ya kuomba kurejeshewa uanachama wao.

  Kwa upande wake, Ngowi alisema baada ya kesi yao kutupwa, Hakimu Mkazi, Hawa Mguruta, aliwapa siku 30 za kukata rufaa na kwa msingi huo, haikuwa sahihi kwa Chang’a kuanza kutowatambua kabla siku hizo hazijamalizika na waziri kutoa maelekezo.

  Hali kadhalika kuitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi,kuhusu nafasi zao kuwa wazi ili kuruhusu uchaguzi mdogo kwenye katazao.

  “Nakala ya hukumu ya kesi yetu tumeipokea mchana Septemba 28 na kwa taarifa tulizopata kutoka manispaa, hata wao waliipokea siku hiyo hiyo. Sasa mamlaka ya kutotutambua Kaimu mkurugenzi anayatoa wapi kama hakuwa
  na nakala ya hukumu wala maelekezo mapya kutoka kwa waziri,” alisema na kuhoji Ngowi.

  Ngowi na Bayo ambao walisema wanazungumza kwa niaba ya wenzao
  Estomih Mallah, Charles Mpanda na Rehema Mohamed, walimtaka mkurugenzi huyo kuwajulisha kutowatambua kwa maandishi kama alivyofanya alipopokea barua ya waziri Mkuchika badala ya kufuta majina yao kwenye orodha ya wajumbe wa vikao.

  Hat hivyo Chang’a hakuwa tayari kuzungumzia madaia ya waliokuwa madiwani hao kwamba hana mamlaka ya kutangaza kutowatambua wala kuwazuia kuhudhuria vikao vya Baraza la madiwani.

  Kaimu Mkurugenzi huyo amekuwa kwenye mazingira magumu tangu kuanza kwa mgogoro wa umeya katika Manispaa ya Arusha ambapo awali alidaiwa kuvuruga uchaguzi na baadaye alituhumiwa kuwabeba madiwani waliofukuzwa na sasa amegeukwa na aliodaiwa kuwapendelea.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa sasa wanatapa tapa kweli sasa hivi.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wabaka demokrasia na matapeli wa kisiasa.Sasa wameanza kugeukwa na waliowatuma.
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,456
  Trophy Points: 280
  Ina maana hao wasaliti wanasubiri hotuba/mwongozo wa waziri wa TAMISEMI? Hawajui wajibu na mipaka ya mihimili ya dola? Wao walipokuwa wanatumika (kutumikia matumbo yao na tamaa zao) hawakujua suala la uwakilishi wa wananchi wa kata zao? Ni mpaka maslahi yao yaguswe ndio waseme, nashangaa hata publicity wanayopewa kama kweli inafungamana na maadili na sheria za utawala bora.

  Kweli Tz ina safari ndefu na ngumu ya ukombozi!
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kushnei wamekwisha hao tujadili jinsi ya kushinda uchaguzi mdogo!
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,456
  Trophy Points: 280
  Ishu yao ndio hivyo tena, walipewa nafasi na heshima kwa ujinga na tamaa zao wakachezea. uchu wa madaraka, rushwa na ahadi nyingine tam za ccm ziliwapofusha akili zao.

  By the way nimesoma uzi mwingine juu ya mabalozi waliotumika kununua vote cards, na ushenzi mwingine wa ccm Igunga really you are left gobsmacked! Kama ccm hawataki na hawako tayari kwa mfumo wa siasa shindanishi za vyama watangaze hivyo. Mihela yote, mawaziri, serikali majeshi na taasisi za dini vyote kutumika namna ya Igunga ni hatari sana kwa usalama wa Tz.

  Nadhani pamoja na suala la hawa madiwani wasaliti wachunguzwe juu ya tuhuma za rushwa na kisha wapelekwe ktk mahakama na katu wasirihusiwe kujihusisha na siasa ktk kipindi fulani. Uongozi Tz sasa ni ovyo....no maadili, no ethics, no vision, no patriotism. ABSOLUTELY NOTHING is desirable up there!
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  ccm mbona imetelekeza mamluki wao waliowapandikiza ndani ya chadema?
  Is this not a use and dump policy well executed by ccm for a long time now?
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  wanalilia posho
   
 9. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukiona Manyoya ujue kuwa kaliwa , hawa jamaa tayari wameliwa sasa wanalilia nini na nani wanamlilia?
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Inatia huruma kwani inaonyesha hawa jamaa hawana foresight hata kidogo la sivyo wange baini mapeeema kabisa kuwa mbele kuna hatari na hivyo wangesita kufanya ubishi walioifanyia CDM. Inaonyesha hawakujua impact ya usaliti.
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Wanatapatapa, hawana pa kujishika. Wahamie kwenye kilimo.
   
 12. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  CCM imeshawatumia kama toilet pepa na kuwatupa. Sasa hawana pa kwenda. Wenzenu wa Igunga walitumika kama nyie na sasa mabalozi kibao wanalalamika kuwa CCM ilihonga. Mtazidi kujutia maishani
   
 13. P

  Positive Thinker Senior Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanahitaji kupelekwa mirembe ukishavuliwa uanachana unawakilisha akina nani tena
   
 14. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Red and bolded, bado wasomi tuna safari ndefu sana na hizi lugha mbili
   
 15. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Ukisikia yalaaaaa! Ujue limewapata
   
Loading...