Madiwani wa CHADEMA Mwanza washitakiwa TAKUKURU na Meya

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Ilemela: Madiwani wanne wa CHADEMA (Josephat Manyerere, Rose Brown,Gladys Kiwia na Lucy Kazungu) washtakiwa TAKUKURU kwa kupokea posho ya zaidi ya Sh milioni 3 bila kusafiri.

Meya anayejiita 'wa Mahakama' wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata amewaburuza TAKUKURU madiwani wanne wa CHADEMA, FikraPevu imebaini.

Fikra Pevu imebaini madiwani hao, JOSEPHAT MANYERERE, ROSE BROWN, GLADYS KIWIA na LUCY KAZUNGU, wanatuhumiwa kupokea posho ya zaidi ya Sh milioni 3 bila kusafiri.


Madiwani hao wanatuhumiwa na Meya kwamba kila mmoja alipokea posho ya ya shilingi 80,000/- kwa siku kumi kila mmoja kwa safari ya kwenda Mbeya kikazi lakini hawakwenda.

Habari za uhakika zilizothibitishwa na maofisa wa Takukuru, Mwanza, taarifa imewasilishwa kwao jana.

Kwa mujibu wa Meya huyo, madiwani hao wanastahili adhabu kwa mujibu wa Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 329 ya mwaka 2002.

Meya huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri alipata udiwani kwa tiketi ya Chadema kabla ya kuvurugana na Chama chake na kamati kuu kuamua kumtimua uanachama na yeye kukimbilia mahakamani kuzuia kutimuliwa, kesi hiyo iko Mahakama kuu inaendelea kuunguruma.

Amekuwa akijiita Meya wa Mahakama kwa kuwa Mahakama ndiyo ilizuia kufukuzwa kwake na hivyo kumfanya aweze kugombea umeya ambao alishinda kwa kuungwa mkono na CCM.

Matata tayari ameshawafukuza udiwani madiwani wawili wa Chadema, Kahungu wa kata ya Kirumba na Abubakari Kapera wa kata ya Nyamanoro kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo wakati wakigomea vikao wakigoma kumtambua yeye kama Meya.

Manyerere ambaye ndiyo alikuwa Meya wa Jiji la Mwanza baada ya uchaguzi Mkuu wa 2010 kabla halijagawanywa kuzaa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza lenyewe, aliondolewa katika kiti hicho kwa zengwe lililoanzishwa na diwani wa Igoma kupitia Chadema Adam Chagulani, na kuungwa mkono na Matata na madiwani we CCM na CUF. Chagulani alifukuzwa Chadema kufuatia kuanzisha hoja ya kutokuwa na Imani na Meya wa Chama chake, yeye pia alifungua kesi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama.

- See more at: Madiwani wa CHADEMA Mwanza washitakiwa TAKUKURU na Meya | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 

Attachments

  • mwanza-.pdf
    321.3 KB · Views: 786
Tembo wanakwisha majangili yameshindwa kupatikana wanakuja na hekaya za abunuwasi huku.

Ni aibu sana kwa taifa kwa mambo ya kipuuzi kama haya.
 
Toa taarifa iliyokamilika mkuu, hao madiwani walihongwa ili wafanyeje? Pia walipopewa hizo pesa walipozipokea na kuamua kuacha walichopaswa kufanya wakaghairi, ndipo waliowahonga walipokwenda kulalamika TAKUKURU? Ufafanuzi zaidi tafadhali.
 
Mtoa mada kama unausingizi lala kwanza ili baadaye uje na hbr inayojitosheleza.
 
Atakuwa alikesha VILLA PARK na dada poa..Lala,ukiamka tuletee habari kamili,ikiwezekana uje na uthibitisho wa kutosha!
 
Sasa hivi gumzo la mjini wakinanani wamemuua Dr.Mvungi kwa kusaka nyaraka na Laptop? Msituhamishe kwenye mada
 
Chadema ni majambazi wanafahamika juzi diwani wa chadema huko tabora aliiba simu na kuficha kwenye nguo za ndani.
 
Hawa wangepewa nchi ingekuwa balaa. Mungu amewaongoza vizuri watanzania wasichague Chadema...
 
Mbona maccm ni wezi wakubwa wa mabilioni,rasilimali za nchi hii hamsemi?shame on you na tukichukua hii nchi mtatukoma mbwa koko nyie.
Tutawafilisi mxxxxiiiiiuuuuuuuu
 
walijiona wajanja kudanganya wamesafiri wkt hawajasfr ndo kawaida yao hata viongozi wao wanalipana posho na hawasafiri ni sera yao awa
 
Hawa wangepewa nchi ingekuwa balaa. Mungu amewaongoza vizuri watanzania wasichague Chadema...

[h=3]DIWANI WA CCM ANAYETUHUMIWA KWA MAUAJI APANDISHWA KIZIMBANI ATUPWA MAHABUSU[/h]
Watuhumiwa watatu wa mauaji ya kijana Denisi Kiluka mkazi wa Isoka kata ya Mwangata mjini Iringa akiwemo diwani wa CCM kata ya Maboga Flugence Lutego wamepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauwaji hayo.


Waliopandishwa Kizimbani ni mtuhumiwa namba moja Bensony Mdongwe (30) diwani Flugence Lutego (41) na Joel Kihwelo (39) wote watatu wanatuhumiwa kumuua kijana mwendesha Piki piki Denis Kiluka na hawakutakiwa mujibu chochote kutokana na mahatma hiyo ya wilaya kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa wote wanadaiwa kufanya mauaji hayo ya kinyama katika kijiji cha Makombwe kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.

Hivyo imesogwezwa hadi machi 13 mwaka huu itakapotajwa kwa Mara ya pili mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mary Senapee
 
Toa taarifa iliyokamilika mkuu, hao madiwani walihongwa ili wafanyeje? Pia walipopewa hizo pesa walipozipokea na kuamua kuacha walichopaswa kufanya wakaghairi, ndipo waliowahonga walipokwenda kulalamika TAKUKURU? Ufafanuzi zaidi tafadhali.
Taarifa ndio hiyo, unalialia nini? Acha uzuzu
 
walijiona wajanja kudanganya wamesafiri wkt hawajasfr ndo kawaida yao hata viongozi wao wanalipana posho na hawasafiri ni sera yao awa

[h=2]
icon1.png
Diwani wa CCM aiba saruji mifuko 100![/h]
Jeshi la polisi mkoani Simiu inamshikilia Diwani wa viti maalum CCM Mery Misangu kwa kosa la kuiba sementi mali ya serikali mifuko 100 na bati moja.

Diwani huyo alifikishwa mahakamani siku ya tar 26 June yeye na mwenzake Gabriel ambapo Diwani huyo alifanikiwa kupata dhamana huku Gabriel akipelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Source; Radio free Afrika.​
 
Taarifa ndio hiyo, unalialia nini? Acha uzuzu

Senior Member Array


Join Date : 20th February 2009
Location : Chitipa
Posts : 211
Rep Power : 590
Likes Received49
Likes Given11


[h=2]
icon1.png
M/kiti wa CCM mkoa wa Ruvuma aifilisi halmashauri ya Mbinga[/h]
Wadau,
M/kiti wa CCM mkoa ndg. Oddo Mwisho amefanya ufisadi wa kutisha ktk halmashauri ya wilaya ya Mbinga ambako alikuwa mwenyekiti wa halmashauri.

Akishirikiana na mkurugenzi aliyekuwepo ndg Shaibu Nnunduma walihujumu miradi ya maendeleo wakiitumia kampuni ya GS CONTRACTORS ambapo miradi yote mikubwa ilikuwa inafanywa na kampuni hii kwa shinikizo la mtu huyu na mkurugenzi kwa sasa mwenyekiti huyu ni mwenyekiti wa halmashauri wilaya mpya ya Nyasa na amehama na aliyekuwa mkurugenzi wa Mbinga ili wakaendeleze mambo yao wilaya mpya kifupi jamaa ni mwizi mkubwa.

Kazi mnayo wanyasa​
 
Sasa hivi gumzo la mjini wakinanani wamemuua Dr.Mvungi kwa kusaka nyaraka na Laptop? Msituhamishe kwenye mada

Nyingine ni Profesa Kapuya kubaka mtoto wa miaka 14 na kumuambukiza Ukimwi ndio habari ya mujini kwa sasa...
 
Kama wanadamu tumepewa utashi wa kufikiria na kuwa na kumbukumbu. naomba mjaribu kutumia sifa hizo kujaji mambo. sababu za madiwani wa chadema kutokusafiri zinajulikana. Maana siku hiyo ya safari walishushwa kwenye gari na Meya wa kichina na naibu meya ambaye ni gamba(Habari hii ilitangazwa itv na startv wiki mbili zilizo pita. Sasa hao wapumbavu wanaoenda kushitaki takukuru na huo takukuru kulifanyia kazi swala hili watakuwa wapumbavu kabisaa
 
Toa taarifa iliyokamilika mkuu, hao madiwani walihongwa ili wafanyeje? Pia walipopewa hizo pesa walipozipokea na kuamua kuacha walichopaswa kufanya wakaghairi, ndipo waliowahonga walipokwenda kulalamika TAKUKURU? Ufafanuzi zaidi tafadhali.

Walijiundia safari bandia ya kwenda mbeya kwa posho ya 80,000 kila mmoja kwa siku kumi, wakachukua pesa lakini hawakusafiri
 
Sasa hivi gumzo la mjini wakinanani wamemuua Dr.Mvungi kwa kusaka nyaraka na Laptop? Msituhamishe kwenye mada

TUSIPEPESE MACHO, WALOHUSIKU KUMUUA Dr. NI LILE GENGE LINALOOGOPA SERIKALI TATU, NA DR ALIKUWA AKIJITAHIDI KUELIMISHA JUU YA SERIKALI TATU
 
Back
Top Bottom