Simon Templar
Member
- Mar 3, 2016
- 18
- 21
Wandugu,
Lile sekeseke la kufutwa kazi kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, kwa tuhuma za kulewa akiwa kazini limechukua sura mpya ambapo sasa madiwani wa Wilaya ya Misungwi katika jimbo ambalo analiwakilisha Kitwanga, wamekuja na kali baada ya kuamua kufungua kesi mahakamani dhidi ya Bunge kwa uonevu dhidi ya mbunge huyo.
Taarifa ambayo wameitoa leo hii jijini Mwanza inajieleza yenyewe hapa chini:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MWANZA
08/06/2016.
Baada ya Bunge kushindwa kuthibitisha tuhuma walizomhusisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mbunge wa jimbo la Misungwi ndugu Charles Kitwanga kuwa aliingia Bungeni akiwa amelewa, Madiwani wa Misungwi tunatarajia kuchukua hatua za kisheria Juni 10 mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuhusu tukio hilo la Mei 20, mwaka huu, lililopelekea kuvuliwa uongozi.
Wakizungumza na waandishi wa habari Mwanza leo Ndugu Baraka Kingamkono,na IDDY Majumuisho pamoja na madiwani ambao walikuja Dodoma kwa mwaliko wa mbunge wa jimbo hilo Charles Kitwanga,wamesema kuwa wanachukua hatua za kisheria dhidi ya bunge hilo,baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo kisheria,kikemia,na kisayansi.
Ndugu wananchi na waandishi wa habari mtakumbuka kuwa Mei 22 tulizozungumza na nyie na kutoa maazimio nane (8) na katika maazimio hayo tuliwaagiza waliotoa tuhuma hizo kuthibitisha kwa maandishi, kisheria, kisayansi na kikemia jambo ambalo hawakulifanya hadi sasa.
Ndugu wanahabari azimio pekee ambalo lilijibiwa na sisi madiwani kulipata ni lile lililohusu ofisi ya habari na mahusiano ya Bunge ambalo lilikuwa namba nne (4) kati ya yale maazimio nane (8), ambapo maazimio mengine saba (7) wameshindwa kujibu jambo ambalo linapelekea sisi kama madiwani kuchukua hatua za kisheria ili haki itendeke kwa mbunge wetu ambaye tunaamini hakutendewa haki ikiwa ni pamoja na kujitetea.
Ndugu waandishi wa habari baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia wananchi wema, baadhi ya wabunge wa chama tawala na UKAWA tumegundua na kupata uthibitisho kwamba mbunge wetu kuanzia mei 18 hadi mei 22 alikuwa anaumwa na aliandikiwa dawa za kutumia kwa siku nne na kwa mujibu wa daktari kama mbunge wetu angekaidi masharti na kunywa kilevi chochote angehatarisha maisha yake kutokana na dawa alizokuwa amepewa na daktari.
Aidha sisi Madiwani wa misungwi tunamshukuru kwa dhati mbunge wa Arusha Mjini Chadema kwa ufafanuzi wake wa mei 6 mwaka huu katika moja ya chombo kimoja cha habari ambapo alisema Mhe Kitwanga hakutendewa haki na adhabu aliyopewa ilikuwa kubwa sana kulingana na kosa lenyewe.
Lema alisema kuna mawaziri na wabunge ambao wamekuwa na kashfa nzito za ufisadi lakini wapo ndani ya bunge na ni mawaziri kulinganisha na kosa la mbunge huyo wa misungwi ambalo halikuwa na uzito wowote hadi kupewa adhabu hiyo.
Ndugu wanahabari pia tunachukua nafasi hii kumshukuru mkuu wa kambi ya upinzani bungeni kwa busara na hekima zake namna alivyotumia busara kubwa katika suala hilo la Mhe Kitwanga ambapo naye hakuona mantiki ya adhabu aliyopewa.
Wakati huohuo sisi madiwani wa jimbo la Misungwi tunapenda kumshukuru rais wetu mpendwa John Magufuli kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa taifa letu na tunawaomba wananchi wazidi kumuombea na kumpa ushirikiano wa dhati ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri.
Sisi madiwani wa misungwi tutaendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na mbunge wetu Charles Kitwanga ili naye aweze kutimiza majukumu yake kwa upande wa jimbo letu na Tanzania kwa ujumla na tunaamini haki itatendeka kwake na kurejea kulitumikia taifa letu tukufu la Tanzania.
KATIKA MAAZIMIO YETU MEI 22 TULIOMBA HIVI:
1. Tunaliomba Bunge kumuomba radhi mhe Charles Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake.
2. Tunaliomba bunge litoe taarifa ya kidaktari kuthibitisha kama kweli mhe Charles Kitwanga alionekana kulewa.
3. Tunaliomba bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote walisambaza ile video inayoonyesha ndugu Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri
4. Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
5. Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo kugundua kilevi cha mtu.
6. Tunaomba watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu kwamba ile video ambayo imemtia hatiani ndgugu Charles Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia wafanyakazi wa bunge ambao wanapitia zile asad za bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu huo.
7. Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .
8. Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.
Asanteni na Mungu awabariki.
Imeandaliwa na Madiwani wa Misungwi na kusomwa kwenu na Iddy Majumuisho.