mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni tunawaomba muhiangalie Kwa jicho la karibu Idara ya Utumishi kwani imekuwa kikwazo kikubwa Kwa watumishi kupanda madaraja (Vyeo) licha ya kuwa Na waraka wa kila Idara unaoelekeza sifa Na utaratibu wa mtumishi kupanda cheo.Maafisa hao wamekuwa hawajibu Barua Na endapo wakijibu utaambiwa suala lako linashughulikiwa utajibiwa hapo hutapata jibu tena.Tunaamini kila Idara INA waraka wake ambao unawaongoza Maafisa hao kupandisha vyeo.Pia katika upandishwaji vyeo kuna utaratibu wa kupanda Kwa kufanya mitihani Na Kwa kada ambayo haifanyi mitihani kuna vigezo vimewekwa ikiwa no pamoja Na utendaji mzuri wa Kazi n.k. lakini Maafisa hao wanang'ang'a wote mkafanye mitihani kitu ambacho waraka hauelekezi hivyo.Tunawaomba madiwani wetu hebu fuatilieni suala hili kwani linatuondolea morali wa kufanya Kazi.