Madiwani kumburuza Mbunge Kigwangala Mahakamani!!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamesema wanakusudia kumpeleka mahakamani Mbunge wa Nzega kupitia CCM mh Kigwangala kwa kuwaita wala Rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Nzega mh BEN IZENGO amesema kuwa ktk kikao cha halmashauri kilichokuwa kikifanyika juzi Mh Kigwangala aliwatuhumu Madiwani hao kwa kuwaambia wamekula Rushwa.kitendo ambacho sio cha kweli na kimewachukiza sana. Amesema kuwa pamoja na kuwa mh Kigwangala aliomba Msamaha lakini Nia yao ya kumpeleka mahakamani ipo pale pale!

Source; Radio Free Afrika.
 
Huyu jamaa anatakiwa hata ikiwezekana afungwe hata miaka Sita ni mropokaji mkubwa sana! Yeye alivyokuwa akihonga vitumbua ameshasahau?
 
Kwanza huyu Kigwangala huo ubunge wenyewe umemuangukia kama Zali tu!? Kama sio ubaguzi wa kikabila wa MAGAMBA kumuita Hussein Bashe ni Msomali na sio raia wa Tanzania leo si angekuwa bado anafanya kazi ya usafi aliokuwa anaifanya huko WAMA?!

Mwanzoni alitaka kuonyesha kuwa yeye yupo kwa maslahi ya Wana Nzega kwa kuwa Mbunge wa kwanza CCM kuitisha maandamano ya kupinga wawekezaji wa Mgodi wa Dhahabu Nzega!
Lakini baada ya kupewa kitu kidogo hatukumsikia tena. Zaidi ya kumuona bungeni akitafuta Umaarufu kwa mgongo wa LISSU!
Huyu nae hamna jipya! Amesahau kuwa kusema ukweli ndani ya CCM unakuwa Adui?
 
Inawezekana tatizo la paka kwa panya
lingekwisha kama paka angefungiwa
kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa
kuifanya kazi hiyo. Na
panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa
paka watajifunga au watafungana kengele shingoni" - Mwl. J. K.
Nyerere
 
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamesema wanakusudia kumpeleka mahakamani Mbunge wa Nzega kupitia CCM mh Kigwangala kwa kuwaita wala Rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Nzega mh BEN IZENGO amesema kuwa ktk kikao cha halmashauri kilichokuwa kikifanyika juzi Mh Kigwangala aliwatuhumu Madiwani hao kwa kuwaambia wamekula Rushwa.kitendo ambacho sio cha kweli na kimewachukiza sana. Amesema kuwa pamoja na kuwa mh Kigwangala aliomba Msamaha lakini Nia yao ya kumpeleka mahakamani ipo pale pale!

Source; Radio Free Afrika.

Wamefanikiwa kumpindua Mwenyekiti wa Halmashauri Bw. Patrick Mbozu?, laana ya kumkataa DED Kitundu
 
huyu bwamdogo huwa ananikera sana,2015 inabdi apigwe chini arudi WAMA
 
Amekalia kuzunguka kwenye mabaa hasa maeneo ya MOTEL oposite na NMB huku akionyesha ufahar wa kutapanya posho za bungen.
 
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamesema wanakusudia kumpeleka mahakamani Mbunge wa Nzega kupitia CCM mh Kigwangala kwa kuwaita wala Rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Nzega mh BEN IZENGO amesema kuwa ktk kikao cha halmashauri kilichokuwa kikifanyika juzi Mh Kigwangala aliwatuhumu Madiwani hao kwa kuwaambia wamekula Rushwa.kitendo ambacho sio cha kweli na kimewachukiza sana. Amesema kuwa pamoja na kuwa mh Kigwangala aliomba Msamaha lakini Nia yao ya kumpeleka mahakamani ipo pale pale!

Source; Radio Free Afrika.

Rushwa CCM ni kama vazi. Kuna mwana CCM asiyevaa vazi la Chama? Tunajua yanatofautiana intensity tu ya rangi ila yote ni sare ya chama.
 
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamesema wanakusudia kumpeleka mahakamani Mbunge wa Nzega kupitia CCM mh Kigwangala kwa kuwaita wala Rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Nzega mh BEN IZENGO amesema kuwa ktk kikao cha halmashauri kilichokuwa kikifanyika juzi Mh Kigwangala aliwatuhumu Madiwani hao kwa kuwaambia wamekula Rushwa.kitendo ambacho sio cha kweli na kimewachukiza sana. Amesema kuwa pamoja na kuwa mh Kigwangala aliomba Msamaha lakini Nia yao ya kumpeleka mahakamani ipo pale pale!

Source; Radio Free Afrika.

Mpelekeni mapema nitamwambia Lissu awe wakili wenu.
 
Ningekuwa sina ushahidi wangekuwa na kesi, lakini kwa kuwa ninao sina shaka...

aliyewapa na waliochukua wote watajishtaki.

Hata hivyo hawajui kuwa ukisema mambo kwenye Baraza la madiwani unakuwa na kinga? maskini madiwani wangu...hawatoweza kupambana na Mbunge wao.

Wakiendelea kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kwa kudanganywa na vibaraka wao nitawashtaki kwa wananchi ili wahukumiwe kisiasa 2015...

Wakiwa wajanja na wakitumikisha bongo zao watanyamaza na kuja kuomba radhi kwangu kama ambavyo huwa wanafanya mara nyingi tu...kinyume cha hapo sintowasamehe...nitawashataki kwa wananchi madiwani wote wenye tuhuma za rushwa na za ubadhirifu wa pesa za mfuko wa jimbo na za miradi ya maendeleo
 
Mbona inasemekana wewe ndiye ulie omba msamaha ili yaishe?
 
mkuu umemaanisha kabisa kuuliza hilo swali? hii ndiyo mambo nzuri co kusifiana tu hata akiharubu aje ajibu hili swali lako kwanza.
 
Ningekuwa sina ushahidi wangekuwa na kesi, lakini kwa kuwa ninao sina shaka...

aliyewapa na waliochukua wote watajishtaki.

Hata hivyo hawajui kuwa ukisema mambo kwenye Baraza la madiwani unakuwa na kinga? maskini madiwani wangu...hawatoweza kupambana na Mbunge wao.

Wakiendelea kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kwa kudanganywa na vibaraka wao nitawashtaki kwa wananchi ili wahukumiwe kisiasa 2015...

Wakiwa wajanja na wakitumikisha bongo zao watanyamaza na kuja kuomba radhi kwangu kama ambavyo huwa wanafanya mara nyingi tu...kinyume cha hapo sintowasamehe...nitawashataki kwa wananchi madiwani wote wenye tuhuma za rushwa na za ubadhirifu wa pesa za mfuko wa jimbo na za miradi ya maendeleo

Kigwangala msomi mkubwa mbona unashindwa kuelewana na madiwani wako tatizo nini? Mbona majibu yako siyo kama ya kiongozi tena mbunge unakua kama muimba taarabu nani kakuloga wewe mbunge wa nzega? Utawashtaki au unajishataki kwa wananchi kwani hata wao wamekuchoka. Ushajaribu kujiuliza niwapi ulipojikwaa au bado una kiburi kwamba wewe ni msomi (medical) hukoseagi. Jifunze kuacha dharau kidogo uweze kuwatumikia wana nzega kwa miaka iliyobaki.
 
Kuburuzwa mahakamani sawa na kwenda hospitali, guilty ndio balaa. Dr. K kama unao ushahidi wa kutosha kisheria, get attorney ASAP.
 
HKigwangalla Kwa nini kama kweli we ni mzalendo, ushahidi wa rushwa unao usubiri mpaka 2015 ndio uwashtaki? Umeapa kuilinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya muungano. ..Peleka ushahidi PCCB ili wachukuliwe hatua za kisheria...Though na wao wanaweza kuamsha VITUMBUA saga
 
Last edited by a moderator:
Ningekuwa sina ushahidi wangekuwa na kesi, lakini kwa kuwa ninao sina shaka...

aliyewapa na waliochukua wote watajishtaki.

Hata hivyo hawajui kuwa ukisema mambo kwenye Baraza la madiwani unakuwa na kinga? maskini madiwani wangu...hawatoweza kupambana na Mbunge wao.

Wakiendelea kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kwa kudanganywa na vibaraka wao nitawashtaki kwa wananchi ili wahukumiwe kisiasa 2015...

Wakiwa wajanja na wakitumikisha bongo zao watanyamaza na kuja kuomba radhi kwangu kama ambavyo huwa wanafanya mara nyingi tu...kinyume cha hapo sintowasamehe...nitawashataki kwa wananchi madiwani wote wenye tuhuma za rushwa na za ubadhirifu wa pesa za mfuko wa jimbo na za miradi ya maendeleo
hivi lile suala la msamaha wa kodi wa kampuni yako na vifaa kuviuza nje ya makubaliano ya msamaha huo limeishia wapi? Hebu tujuze
 
Back
Top Bottom