Madiwani CCM Wachapana Ngumi Kikaoni

Madiwani CCM Wachapana Ngumi Kikaoni

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,308
JESHI la Polisi wilayani Kwimba mkoani Mwanza, linawashikilia madiwani wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kosa kuchapana ngumi wakati wa kikao cha baraza la madiwani jana. Madiwani hao na kata zao kwenye mabano ni Shija Malando (Hungumalwa)na Tabu Maganga (Mhande).

Tukio hilo, ambalo lilionekana kuwashangaza madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Kwimba, lilitokea jana saa 5 asubuhi na kusababisha shughuli zote kusimama kwa muda.

Kutokana na kuchapana ngumi ovyo ovyo, madiwani waliumizana vibaya sehemu za usoni.

Akidhibitisha kukamatwa kwa madiwani hao, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba (OCD),Dk. Enock Rukiyaa alisema mpaka jana mchana viongozi walikuwa wanaendelea kushikiliwa kwa vile kupigana ni kosa.

Alisema kwa mujibu wa maelezo ya awali, madiwani hao wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu kutokana na mambo yao binafsi.

"Tumepata maelezo yao ya awali, inaonekana wamekuwa na ugomvi wao binafsi kwa muda mrefu… lakini inaonekana wamekuwa wakiwindana mno,"alisema OCD Dk.Rukiyaa.

Alisema anasikitishwa kuona viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi, wanaamu kupigana baadala ya kutetea matatizo ya wapiga kura wao.

Akizungumzia suala la dhamana, OCD Rukiyaa alisema bado wanaendelea kuwahoji kwa kina zaidi ili wafikishwe mahakamani kujibu kosa linalowakabili.

"Hapa suala la dhama kwa sasa halipo,haiwezekani waheshimiwa hawa wapigane mbele ya hadhara mchama kweupe, kisha tukaharakisha kutoa dhamana…bado tutaendelea kuwashikilia na kuwachukua maelezo zaidi,kitendo walichokifanya ni cha ajabu kabisa",alisema OCD Dk Enock.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba, Abbas Mwijuki alisema amesikitishwa na kitendo hicho na amepanga kukutana na OCD ili kujua ni hatua gani zaidi zitachukuliwa dhidi ya madiwani hao.

Alisema wakati madiwani hao wanapigana, alikuwa hajaingia ukumbini na alipata taarifa za tukio hilo wakiwa tayari wamefikishwa kituoni.

Kuhusu hatua ambazo CCM,itachukua baada ya madiwani hao kuonyesha utovu wa nidhamu,Mwijuki alisema kuna mambo mawili ambayo yanatarajiwa kufanyika.

Alisema kama madiwani hao, litafikishwa mahakamani chama hakiwezi kuchukua hatua zozote za kisheria na kinidhamu.

Pili endapo suala hilo, litashindikana kupelekwa mahakamani basi chama kinatarajia kuwaita na kuwahoji madiwani haraka iwezekakanvyo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kupitia kamati husika, zikiwamo za Kamati ya Maadili na Kamati ya Siasa ili iwe fundisho kwa wengine.

Juhudi za MTANZANIA kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Zephania Masangu hakufanikiwa kutokana na simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.

CHANZO: Mtanzania
 
Wapigane wauwane wenyewe wasituuimize na sie tusio na hatia
 
babalao 2 kuna majina ambayo ukimpa mtoto yataakisi tabia yake mfano Mahangaiko, Tabu, Sikujali, Masumbuko n.k.
 
Last edited by a moderator:

Hizi habari haziwafurahishi Magamba maana wanajua vinara wa Vurugu ni Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Hiki chama sasa kimekuwa chama cha wahuni kwelikweli!
 
Dalili ya anguko ni kukosa kuvumiliana, uchu wa madaraka, rushwa, ufisadi ....... unaweza kuongezea na wewe, ccm bye bye, Kagera hivyo hivyo, Tarime hivyo hivyo, acha wachapane tu kudadadeck.
 
Hiyo ndiyo CCM na Hao ndiyo wawakilishi wao:rockon:
 
hao lazma wawajibike haiwezekani ugomvi wao waje ku2haribia chama chetu !fukuza waende kujiunga na chama cha mabondia maana kule ndo kuna maandamano na vurugu kila cku..(CDM)
 
Wengine wanachukua chao mapema na mali za chama,wengine wanalambana bakora,wengine wako na CDM wanampinga meya wao n.k
 
Ni kawaida kwa sisiemu kuzichapa kavukavu, sio mara ya kwanza. In case mmesahau, nawakumbusha hizi:-
  • Shyrose Bhanji hivi majuzi alikwidana shati na kutaka kuzichapa na mashabiki wa Sofia Simba pale Shyrose alipokuwa anabishana nao kuhusu kukithiri kwa rushwa kwenye chaguzi zao UWT
  • Sophia Simba alizichapa kavukavu na Halima Mamuya pale walipokuw wameshindwa kuelewana kwenye mikutano yao ya ndani.
  • Florence Kyendesya, mjumbe wa zamani wa UWT Mbeya alikwidana mashati na wenzake mkutanoni baada ya kushindwa kuelewana, mwishowe akavua nguo ya ndani na kumrushia mgomvi mwenzake, ili kumaliza hasira
  • Hizo picha hapo juu ni ushahidi tosha kwamba mambo si mambo huko ndani kwao!
 
IJUMAA, MACHI 01, 2013 04:25 NA JOHN MADUHU, MWANZA

JESHI la Polisi wilayani Kwimba mkoani Mwanza, linawashikilia madiwani wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kosa kuchapana ngumi wakati wa kikao cha baraza la madiwani jana. Madiwani hao na kata zao kwenye mabano ni Shija Malando (Hungumalwa)na Tabu Maganga (Mhande).

Tukio hilo, ambalo lilionekana kuwashangaza madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Kwimba, lilitokea jana saa 5 asubuhi na kusababisha shughuli zote kusimama kwa muda.

Kutokana na kuchapana ngumi ovyo ovyo, madiwani waliumizana vibaya sehemu za usoni.

Akidhibitisha kukamatwa kwa madiwani hao, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba (OCD),Dk. Enock Rukiyaa alisema mpaka jana mchana viongozi walikuwa wanaendelea kushikiliwa kwa vile kupigana ni kosa.

Alisema kwa mujibu wa maelezo ya awali, madiwani hao wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu kutokana na mambo yao binafsi.

“Tumepata maelezo yao ya awali, inaonekana wamekuwa na ugomvi wao binafsi kwa muda mrefu… lakini inaonekana wamekuwa wakiwindana mno,”alisema OCD Dk.Rukiyaa.

Alisema anasikitishwa kuona viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi, wanaamu kupigana baadala ya kutetea matatizo ya wapiga kura wao.

Akizungumzia suala la dhamana, OCD Rukiyaa alisema bado wanaendelea kuwahoji kwa kina zaidi ili wafikishwe mahakamani kujibu kosa linalowakabili.

“Hapa suala la dhama kwa sasa halipo,haiwezekani waheshimiwa hawa wapigane mbele ya hadhara mchama kweupe, kisha tukaharakisha kutoa dhamana…bado tutaendelea kuwashikilia na kuwachukua maelezo zaidi,kitendo walichokifanya ni cha ajabu kabisa”,alisema OCD Dk Enock.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba, Abbas Mwijuki alisema amesikitishwa na kitendo hicho na amepanga kukutana na OCD ili kujua ni hatua gani zaidi zitachukuliwa dhidi ya madiwani hao.

Alisema wakati madiwani hao wanapigana, alikuwa hajaingia ukumbini na alipata taarifa za tukio hilo wakiwa tayari wamefikishwa kituoni.

Kuhusu hatua ambazo CCM,itachukua baada ya madiwani hao kuonyesha utovu wa nidhamu,Mwijuki alisema kuna mambo mawili ambayo yanatarajiwa kufanyika.

Alisema kama madiwani hao, litafikishwa mahakamani chama hakiwezi kuchukua hatua zozote za kisheria na kinidhamu.

Pili endapo suala hilo, litashindikana kupelekwa mahakamani basi chama kinatarajia kuwaita na kuwahoji madiwani haraka iwezekakanvyo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kupitia kamati husika, zikiwamo za Kamati ya Maadili na Kamati ya Siasa ili iwe fundisho kwa wengine.

Juhudi za MTANZANIA kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Zephania Masangu hakufanikiwa kutokana na simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Back
Top Bottom