Madiwani CCM, CHADEMA nusura wazipige kikaoni

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Vurugu kubwa ziliibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni, jana baada ya madiwani wa Chadema kuhoji matumizi ya sh. 44 milioni zilizodaiwa kutengwa kwa ajili ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM.

Vurugu hizo ziliibuka mwishoni mwa kikao baada ya madiwani wa Chadema kuhoji na kutaka kubadilishwa matumizi ya fedha katika Bajeti ya Halmashauri ya mwaka 2011/12 walizodai kuwa zimepangwa kwa ajili ya kuandaa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Kauli ya madiwani hao iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee na madiwani wa CCM wakiwa na jazba walikuja juu na kutaka mjadala ufungwe.

Wakati mzozo ukiendelea Diwani mmoja wa CCM alisimama na kusema "CCM oyeee!" na kuitikiwa "Oyeeeeee!"

Diwani wa Chadema naye akasimama na kusema "peoples!" na kuitikiwa "power!!!"


NAWAKILISHA!!!!!!!
 
Nimefurahishwa na yanayofanywa na wawakilishi toka CHADEMA, ni kweli katika kipindi hicho pamoja na mfumo wa vyama vingi vya siasa bado CCM inaigiza mchezo kwa kuitaka serikali badala ya kutekeleza Ilani ichangie fedha katika kampeni zake. Kumbukeni barua ya Mkuu mmoja wa Mkoa kwenda kwa watumishi katika mkoa wake kuwataka wachangie kampeni za CCM. Naomba CHADEMA wakaze uzi kuhoji kwa nini fedha za kuzoa taka zisiwepo, fedha za kupima viwanja zisiwepo, fedha kwa ajili ya kununua madawati ya shule za msingi na sekondari zisipatikane lakini milioni 40 za kuandaa Ilani ya CCM zipatikane? Kweli Tanzania sio masikini wa mali bali ni masikini wa akili. Kama vipaumbele vya manispaa ya Kinondoni ni Ilani badala ya maisha ya wananchi!!!!!!
 
SHIDA kubwa ni kuwa watabaki wanalalamikiana na kushabikiana tu! Wananchi waliwachagua wawatumikie. Ni wakati wa kusahau mambo ya vyama!
 
SHIDA kubwa ni kuwa watabaki wanalalamikiana na kushabikiana tu! Wananchi waliwachagua wawatumikie. Ni wakati wa kusahau mambo ya vyama!

vyama vinahusika directly, angalia halmashauri ya moshi!! bajeti ya chai watu wameikata had mama kinabi imebidi wampoze na tuzo kwa sababu hana sehemu ya kula tena
 
Kwanini bado sijasikia ile hoja yao ya ki-siku hizi dhidi ya Chadema -- 'WAMEKURUPUKA?'
 
Watanzania wenzangu katika hiyo Bajeti ya Manispaa ya Kinondoni kuna kitu kingine kilibishaniwa nacho ni bajeti ya mavazi ya madiwani 1 bilion! Gazeti la Tanzania Daima la leo.

Wadau sijaelewa kama kweli hiyo figure ya 1 billion ni sahihi au mwandishi kakosea lakini kama ni sahihi basi hii nchi haitakaa iendelee! Pesa ya walipakodi lazima itumiwe kwa uhangarifu jamani!

TAFAKARI!
 
Back
Top Bottom