OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
'Ungeni mkono uchimbaji Urani' Serikali | Send to a friend |
Monday, 24 October 2011 09:27 |
0diggsdigg Mwandishi Wetu SERIKALI imewataka Watanzania na wadau mbalimbali wa madini kuunga mkono uchimbaji wa madini ya Urani unaotarajiwa kuanza hivi karibuni chini ya Kampuni ya Madini ya Mantra Resources Limited. Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarishi Kibenga akizungumza katika semina kwa wadau wa madini ikiwahusisha wajumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili na Utalii alisema Serikali itahakikisha uchimbaji wa madini hayo unakuwa na manufaa kwa Watanzania. Katika semina hiyo mada mbalimbali ziliwasilishwa ambapo pamoja na mambo mengine ni mada za sheria ya madini, uhifadhi wa mazingira na athari zake, taarifa ya mradi wa madini ya Urani wa Mto Mkuju wa Namtumbo na athari za mionzi ya madini ya Urani. Alisema tayari kampuni ya Mantra ipo katika mchakato wa upembuzi yakinifu kuhusiana na uchimbaji huo katika Mkoa wa Ruvuma Wilaya ya Namtumbo na kwamba hatua hizo zipo mwishoni kumalizika. Aliwataka Watanzania na wadau wengine ndani ya sekta hiyo kuunga mkono hatua za utekelezaji wa kufanikisha mradi huo ambao anaamini utakuwa na manufaa makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla. "Serikali tayari tumetoa idhini kwa Kampuni ya Mantra kufanya tathimini na upembuzi katika kuelekea uchimbaji hivyo tunatakiwa kuunga mkono hatua hii ambayo Serikali inaamini itakuwa na manufaa makubwa kwetu sote," alisema Kibenga. Kwa upande wao wajumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili na Utalii pia walionyesha kuunga mkono uchimbaji huo lakini wakitahadharisha juu ya umakini katika kuchukuliwa tahadhari za athari za madini hayo. James Lembeli, Mbunge wa Kahama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo alisema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya mradi huo na kwamba jambo la muhimu ni kuhakikisha madini hayo yanawanufaisha Watanzania. Alisema kamati hiyo imepata nafasi ya kutembelea eneo la mradi wa Mto Mkuju wa Namtumbo na kujionea hali halisi ambapo madini husika yakionyesha kuwepo kwa kiasi kikubwa katika ardhi ya Namtumbo. Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka alisema Serikali inapaswa kuwa makini kuhakikisha mikataba ya madini husika inatekelezwa hususani upande wa tahadhari kuhusiana na madhara ya madini hayo kwa wakazi wa maeneo husika. Alisema walitembelea eneo la mradi na kupata maelezo kutoka kampuni husika yakionyesha tahadhari kubwa zinachukuliwa katika kuhakikisha uchimbaji wa madini hayo hauleti madhara kwa wahusika na unakuwa na tija kwa taifa. source: Mwananchi |