Madiliko ya msingi ya katiba yazingatie mambo yafuatayo

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
411
WanaJF nadhani sasa ni muda muafaka wa kujadili nini kiwemo, nini kisiwemo katika katiba mpya inayo kuja. Bila shaka kubwa orodha ndefu ya mabadiliko tunayoyahitaji yaiongoze nchi yetu miaka mingine 50. MFANO:

1. UWEPO WA JMT,
- KATIBA ITAMKE KUWA TANZANIA NI JAMHURI YA MUUNGANO WA NCHI MBILI, TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

-MKUU WA SERIKALI YA TANGANYIKA ATAKUWA WAZIRI MKUU, NA MKUU WA ZANZIBAR ATAKUWA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZNZ

-RAIS WA JMT ATACHAGULIWA NA WANANCHI WOTE WA TANZANIA KATIKA UCHAGUZI MKUU UTAKAOCHAGUA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA,MADIWANI, NA WABUNGE.

-WAZIRI MKUU ATACHAGULIWA KWA KUPIGIWA KURA NA WABUNGE, WAZIRI KIONGOZI ACHAGULIWE NA BARAZA LA WAWAKILISHI

-ASILIMIA 50 YA WAWAKILISHI ZANZIBAR, NA ASILIMIA 50 YA WABUNGE TANGANYIKA WATAINGIA KATIKA BUNGE LA JAMHURI, AMBALO LITAKETI KUJADILI MAMBO YA MUUNGANO TU, NA SI WAJUMBE WA KUDUMU. NA JINA LA BUNGE LA JMT LITAITWA BARAZA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.AMBALO HALITAKUWA NA OFISI RASMI. HIVYO VIKAO VYAKE VITAFANYIKA ZNZ AU TANGANYIKA.

-RAIS HATAKUWA NA OFISI MAALUMU. AWEZA KUWEKA OFISI ZAKE IKULU YA TANZANIA, AU IKULU YA ZANZIBAR.

-RAIS HATAKUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA, ATAKUWA TAASISI HURU, ATAKAYEWEZA KUZITEUA NA KUAPISHA TAASISI HURU.

JE UNA ZAIDI........??


-
 
Tunapo zungumzia katiba mpya sio muundo wa utawala peke yake ni pamoja na kuitaka katiba mutu mwizi anaye hujumu uchumi ama aliwahi kuhujumu uchumi ataifishwe mali zake zote na kufungwa maisha huyo ni muuaji na mali zote akauti zifungwe na kurejeshwa nchini kwa ajili ya kuendeleza nchi yetu.pia tunataka katiba itamke wazi kuwa lugha ya kiswahili itumike kufundishia masomo yote kwanzia chekechea hadi chuo kikuu,kama tunataka wataalamu wakutuwaki.lisha kwenye maswala mengine basi pawepo kundi maalumu la kujifunza kwa lugha ya kigeni .tunataka katiba itamke wazi juu mikataba ya kimataifa kuwa haitapitishwa bungeni bilia kuwashirikisha wananchi ,tunataka katiba itamke wazi kuwa elimu ni bure hadi chuo kikuu. yapo mengi bwana
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
1​
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA_____________KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA YA MWAKA 1977(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katibaya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.​
Dar es Salaam, A.J.CHENGE1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu​
2000KIMEPIGWA CHAPA NA MPIGACHAPA WA SERIKALIDAR ES SALAAM - TANZANIA​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
2​
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAYA MWAKA 1977____________YALIYOMO_____________​
Ibara Kichwa cha Habari​
UTANGULIZISURA YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NASIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEASEHEMU YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO NA WATU​
1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano.2. Eneo la Jamhuri ya Muungano.3. Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi.4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.5. Haki ya kupiga kura.​
SEHEMU YA PILIMALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEOWA SHUGHULI ZA SERIKALI​
6. Ufafanuzi.7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili.8. Serikali na Watu.9. Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.10.[Imefutwa na Sheri Na. ……… ibara ya ……..].11.Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo.​
SEHEMU YA TATUHAKI NA WAJIBU MUHIMU​
Haki ya Usawa​
12.Usawa wa Binadamu.13.Usawa mbele ya sheria.​
Haki ya Kuishi​
14.Haki ya kuwa hai.15.Haki ya uhuru wa mtu binafsi.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
3​
16.Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.17.Uhuru wa mtu kwenda atakako.​
Haki ya Uhuru wa Mawazo​
18.Uhuru wa maoni.19.Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.20.Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.21.Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.​
Haki ya Kufanya Kazi​
22.Haki ya kufanya kazi.23.Haki ya kumiliki mali.24.Haki ya kupata ujira wa haki.​
Wajibu wa Jamii​
25.Wajibu wa kushiriki kazini.26.Wajibu wa kutii sheria za nchi.27.Kulinda mali ya Umma.28.Ulinzi wa taifa.​
Masharti ya Jumla​
29.Haki na wajibu muhimu.30.Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.​
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi​
31.Ukiukaji wa Haki na uhuru.32.Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.​
SURA YA PILISERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZARAIS​
33.Rais wa Jamhuri ya Muungano.34.Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.35.Utekelezaji wa shughuli za Serikali.36.Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka.37.Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais n.k.38.Uchaguzi wa Rais.39.Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.40.Haki ya kuchaguliwa tena.41.Utaratibu wa uchaguzi wa Rais.42.Wakati na muda wa kushika madaraka ya Rais.43.Masharti ya kazi ya Rais.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
4​
44.Madaraka ya kutangaza vita.45.Uwezo wa kutoa msamaha.46.Kinga dhidi ya mashtaka na madai.46A. Bunge laweza kumshtaki Rais.46B. Wajibu wa viongozi Wakuu wa vyombo vya Mamlaka ya Utendajikudumisha Muungano.​
SEHEMU YA PILIMAKAMU WA RAIS​
47.Makamu mmoja wa Rais, kazi na Mamlaka yake.48.Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka.49.Kiapo cha Makamu wa Rais.50.Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka.​
SEHEMU YA TATUWAZIRI MKUU, BARAZA LAMAWAZIRI NA SERIKALI​
51.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.52.Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu.53.Uwajibikaji wa serikali.​
Baraza la Mawaziri na Serikali​
53A. Kura ya kutokuwa na imani.54.Baraza la Mawaziri.55.Uteuzi wa Mawaziri.56.Kiapo cha Mawaziri na Naibu Mawaziri.57. Wakati na muda wa Mawaziri kushika madaraka.58.Masharti ya kazi ya Mawaziri.59.Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.60.Katibu wa Baraza la Mawa ziri.61.Wakuu wa Mikoa.​
SURA YA TATUBUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZABUNGE​
62.Bunge.63.Madaraka ya Bunge.64.Madaraka ya kutunga Sheria.65.Muda wa Bunge.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
5​
SEHEMU YA PILIWABUNGE, WILAYA ZA UCHAGUZI NA UCHAGUZIWA WABUNGE​
66.Wabunge.67.Sifa za mtu kuwa Mbunge.68.Kiapo cha Wabunge.69.Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya Viongozi.70.Wabunge kutoa taarifa ya mali.71.Muda wa Wabunge kushika madaraka kama Wabunge.72.Watu wenye madaraka Serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa.73.Masharti ya kazi ya Wabunge74.Tume ya Uchaguzi75.Majimbo ya Uchaguzi.​
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge​
76.Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi.77.Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa Majimbo ya Uchaguzi.78.Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge Wanawake wa kuchaguliwa na Bunge.79.Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge wa kuchaguliwa na Baraza laWawakilishi.80.[Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.27].81.Utaratibu wa kupendekeza majina ya wagombea uchaguzi wa WabungeWanawake.82.[Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.29].83.Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge au sivyo.​
SEHEMU YA TATUUTARATIBU, MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE​
Spika na Naibu wa spika​
84.Spika na Mamlaka yake.85.Naibu wa Spika.86.Utaratibu wa kumchagu Spika na Naibu wa Spika.​
Ofisi ya Bunge​
87.Katibu wa Bunge.88.Sekretariati ya Bunge.​
Utaratibu wa shughuli Bungeni​
89.Kanuni za Kudumu za Bunge.90.Kuitishwa kwa mikutano ya Bunge na kuvunjwa kwa Bunge.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
6​
91.Rais aweza kulihutubia Bunge.92.Mikutano ya Bunge.93.Uongozi wa vikao vya Bunge.94.Kiwango cha vikao vya Bunge95.Viti vilivyo wazi katika Bunge.96.Kamati za Kudumu za Bunge.​
Utaratibu wa Kutunga Sheria​
97.Namna ya kutumia madaraka ya kutunga sheria.98.Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya sheria.99.Utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mambo ya fedha.​
Madaraka na Haki za Bunge​
100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli.101. Kuhifadhi na kutilia ng uvu uhuru wa majadiliano na wa shughuli.​
SURA YA NNESERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NABARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBARSEHEMU YA KWANZASERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARNA RAIS WA ZANZIBAR​
102. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka yake.103. Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na madaraka yake.104. Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar​
SEHEMU YA PILIBARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR​
105. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake.​
SEHEMU YA TATUBARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR​
106. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na madaraka ya kutunga Sheria zaZanzibar.107. Madaraka ya Baraza la Wawakilishi.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
7​
SURA YA TANOUTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO, TUMEYA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA BARA,MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR, MAHAKAMAYA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO NAMAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YAJAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZAUTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO​
107A. Mamlaka ya Utoaji Haki.107B. Uhuru wa Mahakama.​
SEHEMU YA PILIMAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO​
108. Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.109. Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.110. Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika madaraka.111. Kiapo cha Majaji.​
SEHEMU YA TATUMADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMU NA WATUMISHIWENGINE WA MAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NA TUME YAKUAJIRI YA MAHAKAMA​
112. Tume ya Kuajiri ya Mahakama.113. Madaraka ya kuajiri Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama.113A. Uanachama katika Vyama vya Siasa.​
SEHEMU YA NNEMAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR​
114. Mahakama Kuu ya Zanzibar.115. Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.​
SEHEMU YA TANOMAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO​
116. Tafsiri.117. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Madaraka yake.118. Majaji wa Mahakama ya Rufani na uteuzi wao.119. Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
8​
120. Muda wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kushika madaraka.121. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.122. Kiwango cha vikao vya Mahakama ya Rufani.123. Mashauri yanayoweza kuamuliwa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani.​
SEHEMU YA SITAUTARATIBU WA KUPELEKA HATI ZA KUTEKELEZAMAAGIZO YALIYOMO KATIKA HATI ZILIZOTOLEWANA MAHAKAMA​
124. Utekelezaji wa maagizo ya Mahakama utafanywa nchini Tanzania kote.​
SEHEMU YA SABAMAHAKAMA MAALUM YA KATIBAYA JAMHURI YA MUUNGANO​
125. Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.126. Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba127. Muundo wa Mahakama Maalum ya Katiba128. Utaratibu katika vikao vya Mahakama Maalum ya Katiba.​
SURA YA SITATUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORANA SEKRETARIET YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMASEHEMU YA KWANZATUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA​
129. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.130. Majukumu ya Tume na Taratibu za Utekelezaji.131. Mamlaka ya Tume na utaratibu wa shughuli zake.​
SEHEMU YA PILISEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA​
132. Sekretarieti ya Maadili.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
9​
SURA YA SABAMASHARTI KUHUSU MCHANGO WA SERIKALI NA MAMBOMENGINEYO YA FEDHA ZINAZOINGIA KATIKA HAZINA YASERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZAMCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO YAJAMHURI YA MUUNGANO​
133. Akaunti ya Fedha ya Pamoja.134. Tume ya Pamoja ya Fedha.​
SEHEMU YA PILIMFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHAZA JAMHURI YA MUUNGANO​
135. Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.136. Masharti ya kutoa fedha za matumizi kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali.137. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuuwa Hazina ya Serikali.138. Masharti ya kutoza kodi.139. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria ya matumizikuanza kutumika.141. Mfuko wa Matumizi ya dharura.142. Deni la Taifa.142. Mishahara ya watumishi fulani wa Serikali kudhaminiwa na Mfuko MkuuWa Hazina ya Serikali.143. Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri yaMuungano.144. Kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.​
SURA YA NANEMADARAKA YA UMMA​
145. Serikali za Mitaa.146. Kazi za Serikali za Mitaa.​
SURA YA TISAMAJESHI YA ULINZI​
146. Marufuku kuunda majeshi ya ulinzi yasiyo majeshi ya ulinzi ya Umma.148. Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.​
SURA YA KUMIMENGINEYO​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
10​
149. Maelezo ya mambo yanayohusika na madaraka ya kazi mbalimbalizilizoanzishwa na Katiba hii.150. Maelezo kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi katika Utumishiwa Serikali.152. Ufafanuzi.152. Jina kamili la Katiba, tarehe ya kuanza kutumika na​
NYONGEZA YA KWANZANYONGEZA YA PILI​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
11​
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANOWA TANZANIA YA MWAKA 1977UTANGULIZIMISINGI YA KATIBA​
Sheria ya 1984Na.15 ib.3​
KWA KUWA​
SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchiyetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu naamani:
NA KWA KUWA​
misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katikajamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa naBunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilishawananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibuwa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyokuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa nakulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGEMAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,​
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamiikama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzaniainaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasiana ujamaa.​
SURA YA KWANZA​
Sheria ya 1984Na.15ib.5​
JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA,WATU NA SIASA YA UJAMAA NAKUJITEGEMEASEHEMU YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO NA WATU​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
12​
KutangazaJamhuri yaMuunganoSheria ya 1984Na.15 ib​
1.​
Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Sheria ya 1992Na.4 ib.3​
2.​
-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote laTanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na nipamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzaniainapakana nayo.(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikaliya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katikamikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibuuliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa naBunge:Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Raiswa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katikaMikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Tangazo la nchiyenye Mfumo wavyama vingiSheria ya 1992Na.4 ib.5​
3​
.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia naya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshajiwa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwaajili hiyo.
Utekelezaji washughuli zaMamlaka ya NchiSheria ya 1984Na.15 ib.6​
4​
.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuriya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwilivyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlakaya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenyemamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji washughuli za umma.(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa niSerikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji hakivitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria nakusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa niBunge na Baraza la Wawakilishi.(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za ummakatika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wamadaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwakatika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kamayalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
13​
mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyoya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mamboya Muungano.(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwana kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengineyaliyomo katika Katiba hii.​
Haki ya kupigakuraSheria ya 1984Na.15 ib.6Sheria ya 2000Na.3 ib.4​
5​
.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miakakumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguziunaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwakufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na mashartimengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchiniTanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka mashartiyanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokanana yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;(b) kuwa na ugonjwa wa akili;(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoakitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kamampiga kura,mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyoteinayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.(3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuwekamasharti kuhusu mambo yafuatayo-(a) kuanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga kura nakuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katikaDaftari hilo;(b) kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapigakura na kupiga kura;(c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kuraaliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemunyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wautaratibu huo;(d) kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi nautaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwachini ya uongozi na usimamizi wa Tume yaUchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
14​
SEHEMU YA PILIMALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEOWA SHUGHULI ZA SERIKALI​
UfafanuziSheria ya 1984Na.15 ib.6​
6​
. Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwa kama maelezoyahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja naSerikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madarakaau mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.
Matumizi yamasharti yaSehemu ya PiliSheria ya 1984Na.15 ib.6​
7​
.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali,vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenyekutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheriaau madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wakuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote yaSehemu hii ya Sura hii.(2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu yakisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchinihaitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda aukukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kamasheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti yaSehemu hii ya Sura hii.
Serikali na watuSheria ya 1984Na.15 ib.6​
8​
.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuatamisingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikaliitapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwawananchi kwa mujibu wa Katiba hii;(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yaokwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombovyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwakuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuzaumoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
15​
Ujenzi waUjamaa naKujitegemeaSheria ya 1984Na.15 ib.6Sheria Na.4ya 1992 ib.6​
9.​
Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri yaMuungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wachochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana nakufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitizautekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingirayaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka yaNchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera nashughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamuzinaheshimiwa na kuthaminiwa;(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njiaambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifaunaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwamanufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuiamtu kumyonya mtu mwingine;(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwana kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazianafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuliyoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa nakudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo laDunia kuhusu Haki za Binadamu;(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya ummavinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwawaume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali yamtu;(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazomaendeleo ya wananchi na hasa zaidiyanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondoshaumaskini, ujinga na maradhi;(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njiazinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njiakuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachachebinafsi;(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi yademokrasia na ujamaa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
16​
Nafasi namamlaka yaChamaSheria ya 1984Na.15 ib.6​
10​
. [Ibara ya 10 ya Katiba imefutwa na Sheria Na.4 ya1992].
Haki ya kufanyakazi, kupataelimu nanyinginezoSheria ya 1984Na.15 ib.6​
11​
.-(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajiliya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki yakujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamiiwakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika halinyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila kuathiri haki hizo,Mamlaka ya Nchii itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwambakila mtu anaishi kwa jasho lake.(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raiaatakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikiaupeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.(3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watuwote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupataelimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuovinginevyo vya mafunzo.
SEHEMU YA TATUHAKI NA WAJIBU MUHIMU​
Haki ya Usawa​
Usawa wabinadamuSheria ya 1984Na.15 ib.6​
12​
.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa nakuthaminiwa utu wake.
Usawa mbeleya Sheria ya1984 Na.15 ib.6​
13​
.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele yasheria.
Sheria ya Na.4ya 1992 ib.8Sheria ya 2000Na.3 ib.5​
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlakayoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambaloni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombovinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwamujibu wa sheria.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
17​
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu aumamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheriayoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote yaMamlaka ya Nchi.(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hiineno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitajimengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa ainafulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni nakuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu waaina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faidailiyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno"kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikalikuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebishamatatizo katika jamii.(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatiamisingi kwamba -(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitajikufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombokinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa nahaki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, napia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine yakisheria kutokana na maamuzi ya mahakama auchombo hicho kingenecho kinachohusika;(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinaikutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpakaitakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosahilo;(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu yakitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa nikosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwaadhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabuiliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zotezinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo yajinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtuanakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katikakuhakikisha utekelezaji wa adhabu;(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyamaau kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
18​
Haki ya Kuishi​
Haki ya kuwa haiSheria ya 1984Na.15 ib.6​
14.​
Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamiihifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.
Haki ya Uhuruwa mtu binafsiSheria ya 1984Na.15 ib.6​
15​
.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kamamtu huru.(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru nakuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyotekukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini,kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wakevinginevyo, isipokuwa tu-(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa nasheria, au(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabuiliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au namtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Haki ya faraghana usalama wamtuSheria ya 1984Na.15 ib.6​
16​
.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhikwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake naunyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake namawasiliano yake ya binafsi.(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu waibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusuhali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na yausalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yawezakuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
Uhuru wa mtukwenda atakakoSheria ya 1984Na.15 ib.6​
17​
.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki yakwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katikasehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki yakutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuriya Muungano.(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenyemadhumuni ya -
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
19​
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako nakumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtukwenda anakotaka ili-(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;au(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibuwowote anaotakiwa na sheria nyinginekuutimiza; au(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla aukuhifadhi maslahi fulani mahususi aumaslahi ya sehemu fulani ya umma,kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyohaitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibarahii.​
Haki ya Uhuru wa Mawazo​
Uhuru waMaoni Sheria ya1984 Na.15 ib.6​
18​
.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko hurukuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombochochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wamawasiliano yake kutoingiliwa kati.(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimukwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masualamuhimu kwa jamii.
Uhuru wa mtukuamini diniatakayo Sheriaya 1984Na.15 ib.6Sheria ya 1992Na.4 ib…​
19​
.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imanina uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtukubadilisha dini au imani yake.(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri yaMuungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kuenezadini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, nashughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje yashughuli za mamlaka ya nchi.(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamikekwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, namaneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilonayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
20​
Uhuru wa mtukushirikiana nawengine Sheriaya 1984 Na.14ib.6​
20​
.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheriaza nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazohadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama aumashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi aukuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwahalali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambachokutokana na Katiba au sera yake-(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-(i) imani au kundi lolote la dini;(ii) kundi lolote la kikabila pahala watuwatokeapo, rangi au jinsia;(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote yaJamhuri ya Muungano;(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu aumapambano kama njia za kufikia malengo yake yakisiasa;(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zakeza kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri yaMuungano;(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi nakwa njia za kidemokrasia.(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka mashartiyatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka navigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusuuhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufukukwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote aushirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwakusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
Uhuru wakushirikishughuliza ummaSheria ya 1984Na.15ib.6Sheria ya 1994Na.34 ya ib.4​
21​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti yakuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushirikikatika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri yaMuungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wanchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishiwaliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatiautaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
21​
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifukatika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maishayake au yanayolihusu Taifa.​
Haki ya Kufanya Kazi​
Haki ya kufanyakaziSheria ya 1984Na.15 ib.6​
22​
.-(1) Kila mtu anayo haki ya kufanya kazi.(2) Kila raia anasta hili fursa na haki sawa, kwa masharti yausawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyochini ya Mamlaka ya Nchi.
Haki ya kupataujira wa hakiSheria ya 1984Na.15 ib.6​
23​
.-(1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote,anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watuwote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipokulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.(2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo yahaki.
Haki ya kumilikimaliSheria ya 1984Na.15 ib.6​
24​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchizinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki yahifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufukukwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni yakuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheriaambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili
Wajibu wakushiriki kaziniSheria ya 1984Na.15 ib.6​
25​
.-(1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii,ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu. Na kilamtu anao wajibu wa-(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazihalali na ya uzalishaji mali; na(b) kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikiamalengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamojayanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1),hakutakuwapo na kazi ya shuruti katika Jamhuri ya Muungano.(3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katika Katiba hii kwajumla, ifahamike kwamba kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni kaziya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi hiyo, kwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
22​
mujibu wa sheria ni-(a) kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amriya mahakama;(b) kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katikakutekeleza majukumu yao;(c) kazi ambayo mtu yeyote inabidi aifanye kutokana nakuwapo hali ya hatari au baa lolote linalotishia uhaiwa ustawi wa jamii;(d) kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya-(i) majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawiwa jamii;(ii) ujenzi wa taifa wa lazima kwa mujibu washeria;(iii) jitihada za taifa za kutumia uwezo wa kilamtu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarishajamii na uchumi wa taifa na kuhakikishamaendeleo na tija ya kitaifa.​
Wajibu wa kutiisheria za nchiSheria ya 1984Na.15 ib.6​
26​
.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii nasheria za Jamhuri ya Muungano.(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa nasheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katibana sheria za nchi.
Kulinda mali yaummaSheria ya 1984Na.15 ib.6​
27​
.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuriya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yoteinayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu maliya mtu mwingine.(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali yamamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifuna ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kamawatu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.
Ulinzi wa TaifaSheria ya 1984Na.15 ib.6​
28​
.-(1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi nakudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.(2) Bunge laweza kutunga sheria zinazofaa kwa ajili yakuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinziwa taifa.(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenyemkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi,wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyikowa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
23​
eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa,hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuriya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulianchi.(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosala juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.​
Masharti ya Jumla​
Haki ya wajibumuhimuSheriaya 1984 Na.15ib.6​
29​
.-(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki yakufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtukutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilzivyofafanuliwa katikaibara ya 12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hii ya Katiba.(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki yakupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithiwake.(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheomaalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingiya nasaba, jadi au urithi.(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa naKatiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughulizake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watuwengine au maslahi ya umma.
Mipaka kwahakina uhuru nahifadhi kwa hakina wajibuSheria ya 1984Na.15ib.6Sheria ya 1994Na.34 ib.6​
30​
.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yakeimeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmojakwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwakwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hiiya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wabinadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuiasheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwamujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengineau maslahi ya umma haviathiriwi na matumizimabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katikajamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango yamaendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi yamadini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
24​
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa yaumma;(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri yamahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madaiau la jinai;(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine aumaisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashaurimahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunzaheshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika yawatu binafsi nchini; au(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalolinastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hiiya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake auwajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa namtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anawezakufungua shauri katika Mahakama Kuu.(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katikaKatiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwamara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yakekwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuwekasheria kwa ajili ya-(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwamujibu wa ibara hii;(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikilizamashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka yaMahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuruna wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
25​
(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheriayoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali aumamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibumuhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, naMahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume chaKatiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahiya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatuahiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajiliya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebishahitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusikakatika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, nasheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa nihalali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au mudauliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupizaidi ndio uzingatiwe.​
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi​
Ukiukaji wa hakina uhuruSheria ya 1984Na.15 ib.6​
31​
.-(1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyoteiliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwambainawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, auwakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwawanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wataifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 zaKatiba hii.(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya(1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakatiwa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote,isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili yakushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wahali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendowa mtu anayehusika.(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hiihayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa haiisipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.(4) Kwa madhumuni ya ibara hii na ibara zifuatazo zaSehemu hii "wakati wa hali ya hatari" maana yake ni kipindichochote ambapo Tangazo la Hali ya Hatari, lililotolewa na Raiskwa kutumia uwezo aliopewa katika ibara ya 32, linatumika.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
26​
Madaraka yakutangaza haliya hatariSheria ya 1984Na.15 ib.6​
32​
.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa naBunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katikaJamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo-(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muunganoinakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita; au(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii aukutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri yaMuungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba nilazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amanina usalama; au(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani yajamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katikaJamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyoteambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumiamamlaka ya pekee; au(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au labaa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemuya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri nitishio kwa nchi.(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katikaJamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania bara nzima auTanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazohilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana naKiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano waBunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali yamambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwamkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili yawajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatarilililotolewa na Rais.(4) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusunyakati na utaratibu ambao utawawezesha watu fulani wenyekusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemumahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumiamadaraka aliyopewa na ibara hii kuhusiana na yoyote kati yasehemu hizo endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote katiya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya(2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia kwa ajiliya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa haliya hatari.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
27​
(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibuwa ibara hii litakoma kutumika-(a) iwapo litafutwa na Rais;(b) endapo zitapita siku kumi na nne tangu tangazolilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwakatika ibara ndogo ya (3);(c) baada ya kupita muda wa miezi sita tangu tangazohilo lilipotolewa; isipokuwa kwamba kikao cha Bungecha weza, kabla ya muda wa miezi sita kupita,kuongeza mara kwa mara muda wa tangazo hilokutumika kwa vipindi vya miezi mingine sita kwaazimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wakikao hicho wasiopungua theluthi mbili ya wajumbewote;(d) wakati wowote ambapo mkutano wa Bungeutalitengua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwamkono na kura za wajumbe waiopungua theluthi mbiliya wajumbe wote.(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuziau utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheriailiyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote, inayohusuutangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii,yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapohali hiyo ya hatari imetangazwa.​
SURA YA PILI​
Sheria ya 1984Na.15 ib 8​
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZARAIS​
Rais waJamhuriya MuunganoSheria ya 1984Na.15 ib.9​
33​
.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali naAmiri Jeshi Mkuu.
Serikali yaJamhuri yaMuungano namamlaka yakeSheria ya 1984Na.15 ib.9​
34​
.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muunganoambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muunganokatika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yoteyahusuyo Tanzania Bara.(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusuutekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yoteambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
28​
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu yamambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na piajuu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwaama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimumadaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hiihayatahesabiwa kwamba-(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheriayaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu aumamlaka yoyote ambayo si Rais; au(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote yakisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlakayoyote ambayo si Rais.​
Utekelezaji washughuli zaSerikaliSheria ya 1984Na.15 ib.9​
35​
.-(1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri yaMuungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba yaRais.(2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuniya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katikakanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katibahii.
Mamlaka yakuanzisha nakuwateua watuwa kushikanafasi zamadarakaSheria ya 1984Na.15 ib.9Sheria ya 2000Na.3 ib.6​
36​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katikaKatiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa namamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namnambalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushikanafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera zaidara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibikakusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazozimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbalizilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuziunaofanywa na Rais.(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), mashartimengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria yoyoteinayohusika, mamlaka ya kuwateua watu wengine wotewasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
29​
madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,na pia mamalaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoakatika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibitinidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononimwa Tume za Utumishi na mamlaka mengineyo yaliyotajwa nakupewa madaraka kuhusu nafasi za madaraka kwa mujibu waKatiba hii au kwa mujibu wa sheria yoyote inayohusika.(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayatahesabiwakuwa yanamzuia Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu yawatumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.​
Utekelezaji wakazi na shughulizaRais, n.k Sheriaya 1984 Na.15ib.9Sheria ya 1992Na.4 ib …Na.20ib.12,Sheria yua1994 Na.34 ib.6​
37​
.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katibahii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi nashughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuataushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu paleanapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanyajambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlakayoyote.(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezikumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba JajiMkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwiliau ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimiokama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watuwasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwamabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuuipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibukuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Raiskutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; naiwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku sabakutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basiitahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomokatika ibara ndogo ya (3) yatatumika.(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana namasharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti chaRais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapoRais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi nashuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwakufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kamanaye hayupo au ni mgonjwa; basi.(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kamanaye hayupo au ni mgonjwa; basi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
30​
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri yaMuungano.(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b)na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Raiskutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtanguliakatika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekelezakazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingineanayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kutelezakazi na shughuli za Rais.(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Raiskufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudukazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwakutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Raisataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindicha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotokaRais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais nauteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopunguaasilimia hamsini ya Wabunge wote.(6) Ifahamike kwamba kiti cha Rais hakitakuwa kiwazi naRais hatahesabiwa kwamba hayuko katika Jamhuri ya Muunganoendapo-(a) atakuwa hayupo katika mji ambao ndio makao makuuya Serikali ya Jamhuri ya Muungano;(b) atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano kwakipindi cha muda wa saa ishirini na nne; au(c) atakuwa ni mgonjwa lakini anatumaini kuwa atapatanafuu baada ya muda si mrefu.(7) Iwapo kutatokea lolote kati ya mambo yaliyotajwa katikaibara ndogo ya (6) na Rais akiona kuwa inafaa kuwakilishamadaraka yake kwa muda wa jambo hilo, basi aweza kutoamaagizo kwa maandishi ya kumteua yeyote kati ya watuwaliotajwa katika aya ya (a) au ya (b) za ibara ndogo ya (3) yaibara hii kwa ajili ya kutekeleza madaraka ya Rais wakati yeyehayupo au ni mgonjwa, na mtu huyo atakayeteuliwa atatekelezamadaraka hayo ya Rais kwa kufuata masharti yoyoteyatakayowekwa na Rais; isipokuwa kwamba masharti yaliyomokatika ibara hii ndogo yafahamike kuwa hayapunguzi walakuathiri uwezo wa Rais alionao kwa mujibu wa sheria nyingineyoyote wa kuwakilisha madaraka yake kwa mtu mwingine yeyote.(8) Rais aweza, akiona inafaa kufanya hivyo, kumwagiza kwamaandishi Waziri yeyote kutekeleza kazi na shughuli zozote zaRais ambazo Rais atazitaja katika maagizo yake na Wazirialiyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
31​
aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,atakuwa na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli hizo kwakufuata masharti yoyote yaliyowekwa na Rais, lakini bila ya kujalimasharti ya sheria nyingine yoyote; isipokuwa kwamba-(a) Rais hatakuwa na mamlaka ya kuwakilisha kwaWaziri kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogokazi yoyote ya Rais aliyokabidhiwa na sheria yoyoteinayotokana na masharti ya mkataba wowote uliotiwasahihi na Jamhuri ya Muungano iwapo kisheria Raisharuhusiwi kuwakilisha kazi hiyo kwa mtu mwingineyoyote;(b) ifahamike kwamba maagizo yanayotolewa na Raiskwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo, yakumwagiza Waziri yeyote kutekeleza kazi yoyote yaRais, hayatahesabiwa kwamba yanamzuia Raiskutekeleza kazi hiyo yeye mwenyewe.(9) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii-(a) Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanywa kwa ajiliya kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio kuhusu hali yaafya ya Rais utahesabiwa kuwa ni mkutano halalihata kama mjumbe yeyote wa Baraza hilo hayupo aukiti chake ki wazi, na itahesabiwa kuwa Barazalimepitisha azimio hilo ikiwa litaungwa mkono kwakauli ya wajumbe walio wengi waliohudhuria mkutanona kupiga kura.(b) Rais hatahesabiwa kuwa hayupo katika Jamhuri yaMuungano kwa sababu tu ya kupitia nje ya Tanzaniawakati yuko safarini kutoka sehemu moja yaTanzania kwenda sehemu nyingine, au kwa sababukwamba ametoa maagizo kwa mujibu wa masharti yaibara ndogo ya (7) na maagizo hayo badohayajabatilishwa.(10) Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katikaibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwamujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge,kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake aukufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.(11) Mtu yeyote atakayetekeleza kazi na shughuli za Raiskwa mujibu wa masharti ya ibara hii kama ni Mbunge hatapotezakiti chake katika Bunge wala hatapoteza sifa zake zakuchaguliwa kuwa Mbunge kwa sababu tu ya kutekeleza kazi nashughuli za Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.​
Uchaguzi waRais Sheria ya1984 Na.15 ib.9​
38​
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayowekamasharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
32​
kwa kufuata masharti ya Katiba hii.​
Sheria ya 1992Na.20 ib.5Sheria ya 1994Na.34 ib.​
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti chaRais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasihiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadriitakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mamboyafuatayo:-(a) baada ya Bunge kuvunjwa;(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bungekwanza:(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasimadaraka ya kuchaguliwa;(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu waKatiba hii, na kuondolewa katika madaraka;(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti yaibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezikumudu kazi na shughuli zake;(f) baada ya Rais kufariki.(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tuya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.​
Sifa za mtukuchaguliwa wakuwa RaisSheria ya 1992Na.4Sheria ya 1994Na.13 ib…Sheria ya 1994Na.34 ib….Sheria ya 2000Na.3 ib.7​
39​
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais waJamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwamujibu wa Sheria ya Uraia.(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa nachama cha siasa;(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbewa Baraza la Wawakilishi,(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yaUchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katikaMahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipakodi yoyote ya Serikali.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
33​
(2) Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoniyake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushirikishughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyotehatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais waJamhuri ya Muungano kama si mwananchama na mgombeaaliyependekezwa na chama cha siasa.​
Haki yakuchaguliwatenaSheria ya 1984Na.15 ib.9Sheria Na.34 ya1994 ib.9​
40​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katikaibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tenakushika kiti hicho.(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushikakiti cha Rais.(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa zakuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwasababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Za nzibar.(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwamujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopunguamiaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu auzaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Utaratibu wauchaguzi waRais SheriaNa.20 ya 1992Na.20 ib.5Sheria Na.34ya 1994Na.34 ib.10​
41​
.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jinginelolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 nainalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasakinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilishakwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina lamwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombeakatika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina lamwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasiya Makamu wa Rais.(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguziwa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku nasaa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, namtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kamakupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapigakura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwana Bunge.(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili yakuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombeammoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilishajina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali aukumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
34​
iliyotungwa na Bunge.(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywasiku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheriailiyotungwa na Bunge.(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi waRais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwana Bunge kwa ajili hiyo.(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.​
Wakati na mudawa kushikamadaraka yaRaisSheria ya 1984Na.15 ib.9​
42​
.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapemaiwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwakuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kablaya kupita siku saba.(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtualiyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katikaibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miakamitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kitihicho atakula kiapo cha Rais; au(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;au(c) siku atakapojiuzulu; au(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii.(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya aduina Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bungelaweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wamiaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hiiisipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila marahautazidi miezi sita.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
35​
(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuuwa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kinginechochote kinachohusika na utendaji wa kazi yakekitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.​
Masharti ya kaziya RaisSheria ya 1984Na.15 ib.9​
43​
.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, naatakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo auposho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipohayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho,vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali yaJamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti yaibara hii.(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Raishavitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshikamadaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Madaraka yakutangaza vitaSheria ya 1984Na.15 ib.9Sheria ya 1992Na.4 ib.14​
44​
.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwana Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa haliya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala yatangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada yakushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndaniya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitishamkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiriakupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vitalililotolewa na Rais.
Uwezo wakutoa msamahaSheria ya 1984Na.15 ib.9​
45​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katikaibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana nahatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na awezakutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwamasharti, kwa mujibu wa sheria;(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtuyeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosalolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo auasitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyotekwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
36​
aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote aukufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza,au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatiaambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano.(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwekautaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madarakayake kwa mujibu wa ibara hii.(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwana kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewaTanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bungeinayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayoyatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa TanzaniaBara kwa mujibu wa sheria.​
Kinga dhidi yamashataka yana madaiSheria ya 1984Na.15 ib.9Sheria ya 1992Na.20 ib…​
46​
.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshikamadaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufukukumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yakemahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madarakayake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufunguamahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosakulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla aubaada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau sikuthelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Raisatapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishikwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezokuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jinalake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasaanalodai.(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Raiskutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufukukumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au lakumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada yakuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeyekama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Raiskwa mujibu wa Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
37​
Bunge lawezakumshtaki RaisSheria ya 1992Na.20 ib.8Sheria ya 1995Na.12 ib.4​
46A​
.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakaniendapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwamujibu wa masharti ya ibara hii.(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hojayoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kamainadaiwa kwamba Rais-
Sheria ya ….​
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunjaKatiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadiliyanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasayaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Raiswa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja yanamna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hojakama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tukama-(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwamkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini yaWabunge wote itawasilishwa kwa Spika sikuthelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyoinakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosaaliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa KamatiMaalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguzemashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifailiyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwamasharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hojayametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hojakuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitakaBunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu yahoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi nakama ikiungwa mkono na Wabunge waiopunguatheluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina yawajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibarahii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambayeatakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
38​
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu waKanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wauwakilishi baina ya vyama vya siasavinavyowakilishwa Bungeni.(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalumya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazina madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti yaibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Raisjuu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewadhidi yake.(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzikuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi yaRais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuatautaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika mudausiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifayake kwa Spika.(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum yaUchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuatautaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzikuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadilitaarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kuraza Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Raisyamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti chaRais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi yaRais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiticha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tumeya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibikakujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bungelilipopitisha azimio hilo.(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana namashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupatamalipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezoalizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa naBunge.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
39​
Wajibu waviongozi wakuuwa vyombo vyamamlaka yautendajikudumishaMuunganoSheria ya 1995Na.12 ib.5​
46B​
.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katikaibara ya 28 ya Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vyenyemamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano vilivyotajwakatika, ibara ya 4 ya Katiba hii, watawajibika, kila mmoja waokatika kutekeleza madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hiiau Katiba ya Zanzibar, 1984, kuhakikisha kuwa analindakuimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano.(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kilammojwawapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlakaya utendaji katika Jamhuri ya Muungano kabla ya kushikamadaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea nakudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu waKatiba hii.(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hii:-(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;(c) Rais wa Zanzibar, na(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA PILIMAKAMU WA RAIS​
Mkamu mmojawa Rais, kazina mamlakayakeSheria ya 1994Na.34 ib.11Sheria ya 2000Na.3 ib.9​
47​
.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwandiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri yaMuungano kwa jumla, na hususan-(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa sikuhata siku za Mambo ya Muungano;(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kaziniau yuko nje ya nchi.(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu waRais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwapamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chakewakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais nawatapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Raisakichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwakufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muunganoatatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Raisatakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
40​
(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwamujibu wa sheria ya Uraia;(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa nachama cha siasa;(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbewa Baraza la Wawakilishi;(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yauchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakamayoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyoteya Serikali.(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyotekuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tukwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais waZanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibaranateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiticha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini yauongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwaRais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa naRais.​
Wakati waMakamu waRais kushikamadarakaSheria ya 1994Na.34 ibara 11​
48​
.-(1) Makamu wa Rais atashika madaraka ya Makamu waRais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.(2) Makamu wa Rais aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara ya50(3) ataapa na kushika madaraka yake baada ya uteuzi wakekuthibitishwa na Bunge.
Kiapo chaMakamu waRais.SheriaNa.34 ya 1994ib.11​
49​
. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yakeataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapocha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika nautendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
41​
Muda waMakamu waRais kushikamadaraka.Sheria ya 1994Ibara 11. Sheriaya 1995 Na.12ibara 6Sheria ya 2000Na.3 ib.10​
50​
.-(1) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi,mtu aliyechaguliwa, au kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 37(5),kuwa Makamu wa Rais, bila ya kuathiri masharti mengine yaibara hii, atashika kiti cha Makamu wa Rais kwa muda wa miakamitano tangu alipochaguliwa kuwa Makamu wa Rais.(2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-(a) muda wake utakapokwisha;(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;(c) atakapojiuzulu;(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Raiskuwa wazi;(e) atakapotiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinaloonyesha utovu wake wa uaminifu;(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi yaRais pamoja na Makamu wake;(g) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwaBungeni kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya(3) ya ibara hii;(h) atakapoacha kushika kiti cha Makamu wa Raisvinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(3) Bunge litakuwa na madaraka ya kumuondoa Makamu waRais madarakani kama yale liliyonayo kuhusiana na Rais,isipokuwa kwamba hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Raisitatolewa tu kama inadaiwa kwamba:-(a) Rais amewasilisha hati ya Spika inayoeleza kwambaMakamu wa Rais ameacha au ameshindwakutekeleza kazi za Makamu wa Rais;(b) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunjaKatiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;(c) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadiliyanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasayaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au(d) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Raiswa Jamhuri ya Muungano au kiti cha Makamu waRais,na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwilitangu hoja hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.(4) Ikitokea kwamba kiti cha Makamu wa Rais ki wazikutokana na masharti yaliyomo katika ibara ya 50(3), kifo aukujiuzulu basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote ndani yasiku zisizozidi kumi na nne baada ya kushika madaraka yake,Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huoutathibitishwa na Bunge kwa kura za Wabunge walio wengi.(5) Masharti mengine yote ya ibara ya 46A ya Katiba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
42​
yatatumika pia kuhusiana na Makamu wa Rais isipokuwa tukwamba Makamu wa Rais aliyeondolewa tena madarakani chiniya ibara ndogo ya (3) hatakuwa na sifa tena za kushika nafasi yaRais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wala Rais wa Zanzibar.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
43​
SEHEMU YA TATUWAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRINA SERIKALIWaziri Mkuu​
Waziri Mkuuwa Jamhuri yaMuunganoSheria ya1992 Na.20ibara 9​
51​
.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganoatakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii naambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Raiskwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwana Bunge.(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya sikukumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteuaMbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzianayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidiBungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabungewengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge waliowengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashikamadaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwana Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabungewalio wengi.(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, WaziriMkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;au(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au(c) siku atakapojiuzulu; au(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwaWaziri Mkuu; au(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibuwa masharti mengineyo ya Katiba hii.
Kazi namamlakaya WaziriMkuu Sheriaya 1984 Na.15ib.9​
52​
.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli zaSerikali ya Jamhuri ya Muungano.(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za SerikaliBungeni.(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuuatatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote aumambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
44​
Uwajibikaji waSerikaliSheria ya1984 Na.15ibara 9​
53​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuuatawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka yaRais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera yaSerikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuliza Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Kura yakutokuwa naimani.Sheria ya1992 Na.20ibara 10Sheria ya1995 Na.12ibara 7​
53A​
.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani naWaziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo naikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hojayoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na WaziriMkuu haitatolewa Bungeni endapo-(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya WaziriMkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, walahakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheriaya Maadili ya Viongozi wa Umma;(b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;(c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyoilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuuhaitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwamkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini yaWabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumina nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwaBungeni;(b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajiliya kuleta hoja yametimizwa.(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungenimapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tuiwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.(6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa WaziriMkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilishaazimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyotevile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja yakura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuuatatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwaWaziri Mkuu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
45​
Baraza la Mawaziri na Serikali​
Baraza laMawaziriSheria ya1984 Na.15ibara 9Sheria Na.4ya 1992 ib…Sheria Na.34ya 1994 ibara12​
54​
.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbewake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais waZanzibar na Mawaziri wote.(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiyeatkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basimikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawiliRais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongozaMikutano hiyo.(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) yaKatiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu chakumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezajiwa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, nalitamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolotelitakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizomaalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yoteya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wamikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katikamikutano hiyo.(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewana Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katikamahakama yoyote.
Uteuzi waMawaziriSheria ya1984 Na.15ibara 9​
55​
.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza laMawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baadaya kushauriana na Waziri Mkuu.(2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1),Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateuaNaibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe waBaraza la Mawaziri.(3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambaowatawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutokamiongoni mwa Wabunge.(5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokeakwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baadaya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambayealikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
46​
Kiapo chaMawaziri naNaibuMawaziriSheria ya1984 Na.15ibara 9​
56.​
Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpakaawe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na piakiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yakekitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
MawazirikushikamadarakaSheria ya1984 Na.15ibara 9​
57​
.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziriutaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
Sheria ya1992 Na.20ibara 9​
(a) endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufarikidunia;​
Sheria ya1992 Na.20ibara 11​
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbungekwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwaBunge;​
Sheria ya1995 Na.12ibara 8​
(c) ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazinimwenye madaraka hayo;(d) iwapo atachaguliwa kuwa Spika;(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazikwa sababu nyingine yoyote;(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka yaRais basi mara tu kabla Rais mteule hajashikamadaraka hayo;(g) iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitishakwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi waUmma.​
Masharti yakaziya MawaziriSheria ya1984 Na.15ibara 9​
58​
. Mawaziri na Naibu Mawaziri watashika madaraka yao kwaridhaa ya Rais, na watalipwa mshahara, posho na malipomengineyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
47​
MwanasheriaMkuu waSerikali yaJamhuri yaMuunganoSheria ya1984 Na.15ibara 9Sheria ya1992Na.4 ibara 16​
59​
.-(1) Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaJamhuri ya Muungano ambaye katika ibara zifuatazo za Katiba hiiatatajwa tu kwa kifupi kama "Mwanasheria Mkuu" ambayeatateuliwa na Rais.(2) Mtu yeyote hatastahili kuteuliwa kushika madaraka yaMwanasheria Mkuu isipokuwa tu kama kwa mujibu wa Katiba hiiana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 109(8)zinazomwezesha kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu yaJamhuri ya Muungano au Jaji wa Mahakam Kuu ya Zanzibar, naamekuwa na mojawapo ya hizo sifa maalum kwa mudausiopungua miaka mitano.(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali yaJamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo,atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muunganokuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughulinyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheriazitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza,na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwakwake na Katiba hii au na sheria yoyote.(4) Katika kutekeleza kazi na shughuli zake kwa mujibu waibara hii, Mwanasheria Mkuu atakuwa na haki ya kuhudhuria nakusikilizwa katika Mahakama zote katika Jamhuri ya Muungano.(5) Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifawake, na atashika madaraka yake mpaka-(a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au(b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka yaRais, na atalipwa mshahara, posho na malipomengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katibu waBarazala Mawazirisheria ya 1984Na.15ib. 9​
60​
. Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri ambayeatakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri,na atatekeleza shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumlaau maalum atakayopewa na Rais, yaani:(a) kuanda ratiba ya mikutano ya Baraza na kutayarishaorodha ya shughuli za kila mkutano;(b) kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano yaBaraza;(c) kutoa taarifa na maelezo ya maamuzi ya Baraza kwakila mtu au chombo cha umma kinachohusika nauamuzi wowote; na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
48​
(d) kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozoteatakazoagizwa mara kwa mara na Rais.​
Wakuu waMikoa Sheriaya 1984 Na.15ib.9​
61​
.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katikaJamhuri ya Muungano ambaye, bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3),atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa naRais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.(3) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar watateuliwa naRais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais.(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuuwa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi nashughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoaaliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zotezilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi aushughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yoteyatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.(5) Pamoja na wajibu na madaraka yake yaliyotajwa kwenyemasharti yaliyotangulia ya ibara hii, Mkuu wa Mkoa kwa mkoawowote katika Tanzania Zanzibar atatekeleza kazi za shughuli zaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atakazokabidhiwa na Rais waZanzibar, na kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar 1984 au sheria yoyote iliyotungwa na Baraza laWawakilishi.
SURA YA TATUBUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZABUNGE​
BungeSheria ya1984 Na.15ib.12​
62​
.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalolitakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.(2) Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katikaibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge.(3) Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa nasehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hiiau masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilohalitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ilampaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vilevile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
49​
Madaraka yaBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.12Sheria ya1992Na.4 ib.17Sheria ya1992Na.20 ib.11​
63​
.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekelezamadaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu chaJamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuriya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bungelaweza-(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusumambo ya umma katika Jamhuri ya Muunganoambayo yako katika wajibu wake;(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutanowa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa mudamrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwakatika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria yakusimamia utekelezaji wa mpango huo;(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitajikuwapo sheria;(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuriya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitajikuridhiwa.
Madaraka yakutungaSheria Sheriaya 1984 Na.12ib.12​
64​
.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambomengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuw mikononi mwaBunge.(2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika TanzaniaZanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muunganoyatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.(3) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishiinahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chiniya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka napia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambololote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi,sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka.(4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lo lotehaitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa mashartiyafuatayo-(a) sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumikaTanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar au iweinabadilisha, kurekebisha au kufuta sheria inayotukaTanzania Zanzibar; au(b) sheria hiyo iwe inabadilisha au kurekebisha au kufuta
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
50​
sheria iliyokuwa inatumika tangu zamani TanzaniaBara ambayo ilikuwa inatumika pia Tanzania Zanzibarkwa mujibu wa Mapatano ya Muungano waTanganyika na Zanzibar, ya mwaka 1964 au kwamujibu wa Sheria yoyote ambayo ilitamka wazikwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile TanzaniaZanzibar; au(c) Sheria hiyo iwe inahusu mambo ya Muungano, na kilainapotajwa Tanzania katika Sheria yoyote ifahamikekuwa sheria hiyo itatumika katika Jamhuri yaMuungano kwa mujibu wa Ufafanuzi uliotolewa namasharti ya ibara hii.(5) Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwamujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibaryasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu yasheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sherianyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii,Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasiinachokiuka Katiba itakuwa batili.​
Muda waBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.12​
65​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii maneno "maisha ya Bunge"maana yake ni ule muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bungejipya limeitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada yaUchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwaajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaidakufanyika.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
51​
SEHEMU YA PILIWABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NAUCHAGUZI WA WABUNGEWajumbe wa Bunge​
WabungeSheria ya1984 Na.15Ibara 13sheria ya 1992Na.4 Sheria1992 Na.4Ibara 18Sheria ya1995 Na.12Ibara 9Sheria ya2000Na.3 ib.11​
66​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwana aina zifuatazo za Wabunge, yaani-(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo yauchaguzi;(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanziaasilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya(a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tumeya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazetila Serikali baada ya kupata kibali cha Rais,watakaochaguliwa na vyama vya siasavinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wauwakilishi baina ya vyama hivyo;(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza laWawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;(d) Mwanasheria Mkuu;(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutokamiongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibaraya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya67(1)(b).(2) Rais na Makamu wa Rais kila mmojawao hatakuwaMbunge.(3) Endapo Mkuu wa Mkoa atachaguliwa kuwa Mbungeanayewakilisha wilaya ya uchaguzi au endapo Mbungeanayewakilisha wilaya ya uchaguzi atateuliwa kuwa Mkuu waMkoa, Bunge litahesabiwa kuwa lina idadi ya Wabungeinayohitajika na shughuli zake zitakuwa halali ingawaje idadi yajumla ya kawaida ya Wabunge kwa mujibu wa masharti ya ibarahii, itakuwa imepungua kutokana na uchaguzi huo wa Mkuu waMkoa au uteuzi huo wa Mbunge anayewakilisha wilaya yauchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
52​
Sifa za mtukuwa MbungeSheria ya1984 Na.15ib.13Sheria ya1992 Na.4ib.19 Sheriaya 1994 Na.34ib.13 Sheriaya 1995 Na.12ib.10Sheria ya2000Na.3 ib.12​
67​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtuyeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwakuwa Mbunge endapo-(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wamiaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma nakuandika katika Kiswahili au Kiingereza;(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa nachama cha siasa;(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yaUchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakamayoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyoteya Serikali.(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwakuwa Mbunge-(a) ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatiauraia wa nchi nyingine yote; au(b) ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katikaJamhuri ya Muungano imethibitishwa rasmi kwambamtu huyo ana ugonjwa wa akili; au(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyotekatika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu yakifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidimiezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote,vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wauaminifu; au(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tareheya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewaadhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovuwa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili yaViongozi wa Umma;(e) bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoniyake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wenginena kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheriaza nchi, ikiwa mtu huyo si mwanachama na mgombeaaliyependekezwa na chama cha siasa;(f) ikiwa mtu huyo ana masilahi yoyote katika mkataba waSerikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalumkwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapoamekiuka miiko hiyo;(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisamwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais awezaau anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu waKatiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;(h) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
53​
inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguziwa aina yoyote mtu huyo amezuiliwa kujiandikishakama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi waWabunge.(3) Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge wakuwakilisha jimbo la uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wowote ikiwawakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti chaRais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge katikauchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais.(4) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka mashartiyatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbuge wa kuwakilishajimbo la uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madarakayanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguziwa Wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajiliya uchaguzi wa Wabungel isipokuwa kwamba Sheria kama hiyohaiwezi kuweka masharti yatakayomzuia Spika wa Bungeasichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha wilaya ya uchaguzi,wala masharti yatakayosababisha mtu aliyechaguliwa kuwa Spikakupoteza kiti hicho cha Spika au kiti chake cha kawaida katikaBunge.(5) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka mashartiyatakayomuzia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilishawilaya ya uchaguzi kwa muda wowote utakaotajwa na Bunge (ilimradi muda huo usizidi miaka mitano) ikiwa mtu huyo atapatikanana hatia mbele ya mahakama kwa ajili ya aina yoyote ya makosayatakayotajwa katika Sheria hiyo yanayohusika na uchaguzi waWabunge.(6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufaa kwamujibu wa Sheria kwa mtu yeyote aliyethibitishwa rasmi kisheriakuwa ana ugonjwa wa akili au aliyehukumiwa na kupewa adhabuya kifo au ya kufungwa gerezani au aliyepatikana na hatia ya kosalolote lililotajwa katika Sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (5) yaibara hii, Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuwekamasharti yatakayoeleza kwamba hiyo hukumu inayopingwa namtu huyo haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa mashartiya ibara ndogo ya (2) au ya (5) ya ibara hii mpaka upite kwanzamuda utakaotajwa katika sheria hiyo.(7) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa ajili ya ufafanuzi wa ayaya ( c), ya (d) na ya (e) za ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, yaani-(a) ikiwa mtu amepewa adhabu mbili au zaidi zakufungwa gerezani na imeamuliwa afungwe kwa mudawa mfululizo, basi adhabu hizo zitahesabiwa kama niadhabu mbalimbali iwapo muda uliotajwa katika kilamoja ya adhabu hizo hauzidi miezi sita; lakini iwapomuda uliotajwa katika adhabu yoyote kati ya adhabuhizo unazidi miezi sita basi adhabu hizo zotezitahesabiwa kama ni adhabu moja;​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
54​
zitahesabiwa kama ni adhabu moja;(b) ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezaniikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewabadala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwasababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwakulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyohautahesabiwa.(8) Katika aya ya (f) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii"​
mkataba wa Serikali" maana yake ni mapatano yoyote yamkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali yaJamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idarayoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshirikikwa niaba ya Serikali.
[ibara ndogo ya (9), (10), (11) na ya 12 zimefutwa na SheriaNa.4 ya 1992 Ib.19 (d)]​
(13) Kwa ajili ya ufafanuzi wa maelezo kuhusu sifa zauchaguzi yaliyomo katika ibara zifuatazo, kila itakapotajwa katikaKatiba hii kwamba utekelezaji wa jambo lolote wahitaji mtumwenye sifa za uchaguzi au mtu ambaye hakupoteza sifa zauchaguzi, basi, isipokuwa kama maelezo yahitajia vinginevyo,ifahamike kuwa sifa zinazohusika ni zile zinazomwezesha mtukuchaguliwa kuwa Mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzikama ilivyoelezwa katika ibara ndogo ya (a) ya ibara hii.​
Kiapo chaWabungeSheria ya1984 Na.15ib.13​
68​
. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo chauaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakiniMbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kablahajaapishwa.
Tamko rasmila Wabungekuhusumaadili yaviongoziSheria ya1995 Na.12ib.11​
69​
.-(1) Kila Mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika sikuthelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama Mbungekuwasilisha kwa Spika nakala mbili za tamko rasmi kwambahajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d)ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67.(2) Tamko rasmi linalotakiwa kuwasilishwa kwa Spika kwamujibu wa masharti ya ibara hii litatolewa kwa kutumia fomumaalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa naBunge.(3) Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala mojaya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa mashartiya ibara hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
55​
(4) Katika ibara hii na katika ibara ya 70 na ya 84 "​
Kamishnawa Maadili" maana yake ni Kamishna aliyeteuliwa kuwa kiongoziwa Sekretariati ya Maadili iliyotajwa katika ibara ya 132 ya Katibahii.
Wabungekutoa taarifaya mali Sheriaya 1995 Na.12ib.12​
70​
.-(1) Kila Mbunge atatakiwa kuwasilisha kwa Spika nakalambili za taarifa rasmi ya maelezo ya mali yake na kadriitakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Taarifa itatolewa kwakutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheriailiyotungwa na Bunge na itatolewa mara kwa mara kamaitakavyoagizwa na Sheria hiyo.(2) Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala mojaya kila taarifa rasmi iliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa mashartiya ibra hii.(3) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka mashartikwa makusudi ya kusimamia hifadhi ya taarifa ya maliiliyowasilishwa na Mbunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, nakuhakikisha kwamba watu wasioruhusiwa au wasiohusikahawapati nafasi ya kuona taarifa ya mali wala kujua yaliyomokatika taarifa ya mali.
Muda waWabungekushikaMadarakaSheria ya1984 Na.15ib.13Sheria ya1992Na.4 ib.22Sheria ya1994 Na.34ib.14​
71​
.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chakekatika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwaMbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi auapoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa aukuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutanoya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti yaSheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chamaalichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwakuwa Mbunge;(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwaMakamu wa Rais;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
56​
(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi yamali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwaatashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wamasharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwamahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge,lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wajambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzuluau kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushikamadaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bungelitakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki nastahili zinazotokana na ubunge wake.(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka mashartiyatakayomwezesha Mbunge kukata rufaa, kwa mujibu wa sheriakupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ni mtu mwenyeugonjwa wa akili au kupinga adhabu ya kifo au kufungwagerezani, au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la ainailiyotajwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibaraya 67 ya Katiba hii na sheria hiyo yaweza kueleza kwamba hiyohukumu iliyopingwa na huyo Mbunge haitatiliwa nguvu kisheriampaka umalizike kwanza muda utakaotajwa katika sheria hiyo.​
Watu wenyemadarakaSerikalinikukomautumishiwanapochaguliwa Sheria ya1992Na.4 ib.23Sheria ya1995 Na.12ib.14​
72.​
Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi waSerikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g)ataamua:-(a) kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au wa nafasinyingine yoyote chini ya Katiba hii;(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama chasiasa kinyume na masharti ya ajira,mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangutarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombeauongozi katika chama cha siasa.
Masharti yakaziya WabungeSheria ya1984 Na.15ib.13​
73​
. Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwamujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipomengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
57​
Tume ya Uchaguzi​
Masharti yakaziya WabungeSheria ya1984 Na.15ib.13Sheria ya2000Na.3 ib.14​
74​
.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri yaMuungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwana Rais:-(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama yaRufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtuanayeshika, aliyewahi kushika au anayestahilikuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa MahakamaKuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwana Bunge.(2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume yaUchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtuanayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa nimtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe waTume ya Uchaguzi yaani-(a) Waziri au Naibu Waziri;(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwamahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba nimwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwamjumbe wa Tume ya Uchaguzi;(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madarakaya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bungekwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogoya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii.(d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbewa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolotekatika ya mambo yafuatayo-(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangualipoteuliwa; au(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kamaasingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiwezekuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe waTume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazizake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, aukwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa niKatibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________
58​
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kurakatika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuriya Muungano;(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi waRais na Wabunge;(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri yaMuungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili yauchaguzi wa Wabunge;(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura nauendeshaji wa uchaguzi wa madiwani;(e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu waSheria iliyotungwa na Bunge.(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yakeyaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idarahuru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusuutekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuuatakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa nakufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa naBunge.(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka mashartiya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabungewanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.(9) Tume ya Uchaguzi yaweza kutekeleza shughuli zake bilaya kujali kwamba kuna nafasi miongoni mwa viti vya wajumbe aukwamba Mjumbe mmojawapo hayupo, lakini kila uamuzi wa Tumeya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengikati ya Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi.(10) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwekamasharti ya kuweka utaratibu wa kuwateua Wajumbe wakusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo yauchaguzi na, bila ya kuathiri masharti ya Sheria kama hiyo aumaagizo ya Tume ya Uchaguzi, madaraka ya Tume ya Uchaguziya kusimamia uchaguzi yaweza kutekelezwa na wajumbe hao.(11) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuataamri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, aumaoni ya chama chochote cha siasa.(12) Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katikakutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(13) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu waKatiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muunganoitashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya TanzaniaZanzibar.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
59​
(14) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzikujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kilammoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibaraya 5 ya Katiba hii.(15) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watuwanaohusika na uchaguzi ni-(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wotewa Tume ya Uchaguzi,(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilayazote.​
Majimbo ya Uchaguzi​
Majimbo yauchaguziSheriaya 1992 Na.4ib.24​
75​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyo katika ibarahii, Jamhuri ya Muungano itagawanywa katika majimbo yauchaguzi kwa idadi na kwa namna itakavyoamuliwa na Tume yaUchaguzi baada ya kupata kibali cha Rais.(2) Bila ya kuathiri sheria yoyote inayotumika kuhusu mambohayo, Tume ya Uchaguzi, baada ya kupata kibali cha Rais itakuwana mamlaka ya kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi.(3) Katika kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi, Tume yaUchaguzi itazingatia ipasavyo upatikanaji wa njia za mawasiliano,na pia hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywakatika majimbo ya uchaguzi.(4) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii na ya sheria yoyoteinayohusika na mgawanyo wa nchi katika majimbo ya uchaguzi,Tume ya Uchaguzi yaweza mara kwa mara, na angalao kila baadaya miaka kumi, kuchunguza mgawanyo wa Jamhuri ya Muunganokatika majimbo ya uchaguzi, na yaweza kubadilisha majimbo yauchaguzi kama matokeo ya uchunguzi huo au kutokana namatokeo ya hesabu ya watu wote katika Jamhuri ya Muungano.(5) Endapo baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu mgawanyowa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzikunafanyika mabadiliko katika majimbo ya uchaguzi, au katikaidadi ya Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi aumabadiliko kwa idadi ya majimbo ya uchaguzi au idadi yaWabunge, basi mabadiliko yatakayotokea katika idadi yaWabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi yataanzakutumika wakati Bunge litakapovunjwa tena baada ya kutokeamabadiliko hayo ya idadi ya majimbo au idadi ya Wabunge katikamajimbo ya uchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
60​
(6) Bila kujali masharti mengineyo ya ibara hii, hakunaMahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguzajambo lolote lililotendwa na Tume katika utekelezaji wake wakugawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi.​
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge​
Uchaguzikatikamajimbo zauchaguziSheriaya 1984 Na.15ib. 13Sheria ya2000Na.3 ib.15​
76​
.-(1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa nauchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katikajimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwakuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyoteisiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.(3) Bila ya kujali masharti ya ibara hii yaliyotangulia, ifahamikekwamba ikiwa tarehe ya kuvunjwa Bunge imetangazwa auinafahamika kutokana na matukio yaliyoelezwa katika ibara ndogoya (3) ya ibara ya 90, basi uchaguzi wa namna hiyo hautafanywakatika kipindi chote cha miezi kumi na mbili ya nyuma ikihesabiwatangu tarehe hiyo.
Utaratibu wauchaguzi wawabunge wamajimbo yauchaguziSheria ya1992Na.4 ib. 25​
77​
.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguziwatachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii navile vile masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu waKatiba hii inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabungewanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.(2) Isipokuwa pale ambapo Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajilihiyo, itaagiza vinginevyo, kutachaguliwa Mbunge mmoja tu katikajimbo la uchaguzi.(3) Wagombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi watatakiwawatimize masharti yafuatayo-(a) wawe wamependekezwa mmoja mmoja, na chamacha siasa kinachoshiriki uchaguzi katika jimbo hilo;(b) wamewasilisha majina yao kwa Tume ya Uchaguzikwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheriailiyotungwa na Bunge au uliofafanuliwa na Tume yaUchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
61​
Utaratibu wauchaguzi waWabungewanawakeSheria ya1992 Na.4ib.26Sheria ya2000Na.3 ib.16​
78​
.-(1) Kwa madhumuni ya uchaguzi wa Wabunge, Wanawakewaliotajwa katika ibara ya 66(1) (b), vyama vya siasa vilivyoshirikiuchaguzi, kwa kufuata utaratibu uliowekwa, vitapendekeza kwaTume ya Uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia mashartiya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vilivyoshinda uchaguzikatika majimbo na kupata viti Bungeni. Tume ya Uchaguziikiridhika kuwa mtu yeyote aliyependekezwa anazo sifa za kuwaMbunge itamtangaza kuwa amechaguliwa kuwa Mbunge, namasharti ya ibara ya 83 ya Katiba hii yatatumika kuhusukuchaguliwa kwa mtu huyo kuwa Mbunge.(2) Mtu yeyote hataweza kupendekezwa na chama chochotecha siasa kwa ajili ya uchaguzi kwa mujibu wa ibara hii ila tu iwapoanazo sifa za kustahili kuchaguliwa zilizotajwa na masharti yaibara ya 67 ya Katiba hii.(3) Majina ya watu waliopendekezwa kwa mujibu wa ibarandogo ya (1) na Tume ya Uchaguzi yatatangazwa kama matokeoya uchaguzi baada ya Tume ya Uchaguzi kuridhika kwambamasharti ya Katiba na Sheria yanayohusika yamezingatiwa.(4) Orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyowasilishwakwa Tume ya Uchaguzi na kila chama kwa ajili ya uchaguzi mkuundiyo itakayotumiwa na Tume ya Uchaguzi baada ya kushaurianana chama kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi yoyoteya Mbunge wa aina hii inapotokea wakati wowote katika maishaya Bunge.
Utaratibu wauchaguzi waWabunge wakuchaguliwana​
79​
. Baraza la Wawakilishi litaweka utaratibu litakaoufuata kwaajili ya kufanya uchaguzi wa Wabunge waliotajwa katika ibara66(1) ( c) ya Katiba hii.
Baraza laWawakilishiSheria ya1984 Na.15ib.13​
80. [Ibara 80 ya Katiba imefutwa​
na sheria Na.4 ya 1992Ibara 27].
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
62​
Utaratibu wakupendekezamajina yawagombeaUchaguzi waWabungewanawakeSheriaya 1992 Na.4ib.29​
81​
. Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Tume yaUchaguzi yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibuutakaotumiwa na vyama vya siasa kwa ajili ya kuchagua nakupendekeza majina ya Wabunge wa aina iliyotajwa katika ibaraya 66(1) (b).
82.​
[Ibara ya 82 ya Katiba imefutwa na Sheria Na.4 ya1992 ibara 29.Uamuzi wasuala kamamtu ni MbungeSheria za1979, Na.14Ibara 8 1984Na.15 Ibara 131990 Na.141992 Na.4Ibara 30
83.​
-(1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala -(a) kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa mbungeulikuwa halali au sivyo; au(b) kama Mbunge amekoma kuwa Mbunge na kiti chakekatika Bunge ki wazi au hapana,litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuathiri masharti yaibara ndogo ya (2) ya ibara hii.(2) Iwapo Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yakekwa mujibu wa masharti ya ibra ya 41(3) ya Katiba hiiimemtangaza Mbunge yeyote kwamba amechaguliwa kuwa Raisbasi hakuna mahakama wala chombo chochote kinginekitakachochunguza zaidi suala lolote linalohusu kiti cha Mbungehuyo kuwa wazi.(3) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka mashartikuhusu mambo yafuatayo-(a) watu wanaoweza kufungua shauri katika MahakamaKuu kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwamujibu wa masharti ya ibara hii;(b) sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo,utaratibu wa kufungua shauri na mashartiyanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo; na(c) kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kamahilo na kueleza utaratibu wa kuskiliza shauri lenyewe.(4) Kutakuwa na haki ya kukata rufaa mbele ya Mahakama yaRufani ya Tanzania kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu juu yashauri lolote lililosikilizwa kwa mujibu wa mahsarti ya ibara hii.
SEHEMU YA TATU​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
63​
UTARATIBU, MADARAKA NAHAKI ZA BUNGESpika na Naibu wa Spika​
Spika namamlaka yakeSheria ya1984 Na.15ib.14 Sheriaya 1992Na.4 ib.31Sheria ya1995 Na.12ib.15​
84​
.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa naWabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge auwenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bungena atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote njeya Bunge.(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya ainanyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwamadhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kablaya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake,kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa zauchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya(2) ya ibara ya 67. Tamko hilo litatolewa kwa kutumia fomumaalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa naBunge.(4) Rais atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala mojaya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa mashartiya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii.(5) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili zataarifa rasmi ya maelezo ya mali ya huyo Spika na, kadriitakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Spika atatoa taarifahiyo kwa kutumia fomu maalum iliyowekwa kwa ajili hiyo kwamujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na atatoa taarifa yanamna hiyo mara kwa mara kadri itakavyoagiza sheria hiyo.(6) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) ya ibara ya 70yatatumika pia, kwa kadri itakavyowezekana, kwa taarifa ya maliyoyote itakayotolewa na Spika, kwa mujibu wa masharti ya ibarahii.(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spikalitokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwaWabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwasababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;au(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kamaasingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe nasifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi waSpika; au(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada yaUchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
64​
masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 yaKatiba hii; au(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka yaSpika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono naWabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili yaWabunge wote; au(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Raistamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo(5) ya ibara hii; au(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoahabari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria yaKanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewakwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibarahii; au(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Raistaarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogoya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwakwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa naBunge;(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti yaSheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;(8) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge(isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti chaSpika kitakuwa ki wazi.(9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwaSpika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake,kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.​
Naibu waSpika Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
85​
.-(1) Kutakuwa na Naibu wa Spika wa Bunge ambayeatachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge.(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya ainanyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwamadhumuni ya ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu waSpika.(3) Wabunge watamchagua Naibu wa Spika nyakati zifuatazo-(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada yaUchaguzi Mkuu au mapema iwezekanavyo baada yawakati huo; na(b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya kiti chaNaibu wa Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyoteisiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapemaiwezekanavyo baada ya kikao hicho.(4) Naibu wa Spika, atakoma kuwa Naibu wa Spika na ataachakiti cha Naibu wa Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayoKatibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________
65​
(a) ikiwa mtu huyo atakoma kuwa Mbunge; au(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo kamaasingekuwa Naibu wa Spika, lingemfanya mtu huyoasiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguziwa Naibu wa Spika; au(c) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka yaNaibu wa spika kwa azimio la Bunge.​
Utaratibu wakumchaguaSpika naNaibu waSpikaSheria 1984Na.15Ib.14​
86​
.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao chakwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikaocha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi katika kiticha Spika.(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu wa Spika wakati wo wotekatika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya utakaoteuliwa naBunge na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge marabaada ya kutokea nafasi katika kiti cha Naibu wa Spika.(3) Uchaguzi wa Spika, na vile vile uchaguzi wa Naibu waSpika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuatautaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
Ofisi ya Bunge​
Katibu waBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
87​
.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa naRais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisiya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bungekwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na ya sheria inayohusika.
Sekretariati yaBungeSheria ya1984 Na.15ib.14​
88​
.-(1) Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa nanafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa idadiatakayoagiza Rais.(2) Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi nangazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume yaUtumishi inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge.(3) Sekretariati ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu waBunge itaendeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa auzitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji borawa Bunge na wa Wabunge wa madaraka ya Bunge chini ya Katibahii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
66​
Utaratibu wa Shughuli Bungeni​
Kanuni zakudumu zaBungeSheria ya1984 Na.14ib.14​
89​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge lawezakutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wakutekeleza shughuli zake.(2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hiizaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuliza Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bungendani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge.
Kuitishwa kwamikutano yaBunge naKuvunjwa kwaBunge​
90​
.-(1) Baada ya Uchaguzi Mkuu Rais ataitisha Mkutano waBunge Jipya ufanyike kabla ya kupita siku saba tangu kutangazwamatokeo ya huo Uchaguzi Mkuu katika majimbo ya uchaguzi yoteisipokuwa katika majimbo yale ambako uchaguzi umefutwa nakufanywa upya.(2) Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakatiwowote, isipokuwa tu-(a) kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake kwamujibu wa ibara ya 65 ya Katiba hii; au wakati wowotekatika miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai waBunge, isipokuwa tu kama Spika amepokea taarifarasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalumya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumuondoa Raismadarakani kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba hii;(b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajetiiliyopendekezwa na Serikali;(c) kama Bunge limekataa kupitisha Muswada wa sheriakwa mujibu wa idara ya 97(4) ya Katiba hii;(d) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni yamsingi katika sera za Serikali, na Rais anaonakwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteuaWaziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu;(e) endapo, kutokana na uwiano wa uwakilishi wa Vyamavya Siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba hakunauhalali kwa Serikali iliyopo kuendelea kuwapo, na walahaiwezekani kuunda Serikali mpya.(3) Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwakuwa limevunjwa; isipokuwa kwamba muda huo ukisha wakatiwowote ambapo Jamhuri ya Muungano iko katika vita Bungelaweza mara kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibaraya 65 ya Katiba hii kwa muda usiozidi miezi kumi na miwili marakwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi kuongezwa kwamujibu wa masharti ya ibara ndogo kwa muda unaozidi miakamitano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
67​
(4) Kukitokea hali ya hatari au kama kuna hali ya hatariambayo Rais anaona inasababisha kuitisha Mkutano wa Bunge naiwapo wakati huo Bunge limevunjwa na matokeo ya kura zilizonyingi za Uchaguzi Mkuu hayajatangazwa basi Rais aweza kutoaTaarifa Maalum ya kuitisha Mkutano wa Bunge na kuangizakwamba Spika na watu wote waliokuwa Wabunge mara tu kablaBunge halijavunjwa wahudhurie Mkutano huo wa Bunge na watuhao pamoja na huyo Spika, watahesabiwa kuwa ndio Wajumbewa Bunge kwa madhumuni ya Mkutano huo na watahesabiwahivyo mpaka usiku wa manane wa siku yatakapotangazwamatokeo ya kura zilizo nyingi za Uchaguzi Mkuu.​
Rais awezakulihutubiaBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
91​
.-(1) Rais atalihurubia Bunge Jipya katika Mkutano wake waKwanza na kulifungua rasmi Bunge hilo.(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1); Rais awezawakati wowote kulihutubia Bunge au kupeleka kwenye Bungetaarifa ambayo itasomwa na Waziri.
Mikutano yaBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
92​
.-(1) Bunge litafanywa mikutano yake mahali ambapo nidesturi kufanya Mikutano hiyo au mahali pengine popote katikaJamhuri ya Muungano patakapotajwa na Rais kwa ajili hiyo.(2) Mkutano wa kwanza wa Bunge katika Maisha ya Bungeutaanza siku ile ambayo Bunge limeitwa kukutana, na kilaMkutano ufuatao utaanza siku yoytote itakayopangwa na Bungelenyewe au siku yoyote itakayopangwa kwa mujubu wa Kanuni zaBunge.(3) Rais aweza kuitisha Mkutano wa Bunge wakati wowote.
Uongozi naVikao vyaBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
93.​
Kila kikao cha Bunge kitaongozwa na mmojwawapo wawatu wafuatao, yaani-(a) Spika au;(b) ikiwa Spika hayupo, Naibu wa Spika, au
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
68​
(c) ikiwa Spika na Naibu wa Spika wote hawapo, Mbungeyeyote aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo, lakiniWaziri, au Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka yaaina yingine yoyote iliyotajwa na Sheria iliyotungwa naBunge kwa madhumuni ya ibara hii hatawezakuchaguliwa kwa mujibu wa mahsarti ya aya hii.​
Kiwango chavikao vyaBunge Sheriaya 1984 Na.15ib.14​
94​
.-(1) Kiwango cha kila kikao cha Bunge ni nusu ya Wabungewote.(2) Isipokuwa kama imeelezwa vingine katika Katiba hii, kilaswali litakalotolewa kwa ajili ya kupata uamuzi wa Bungelitaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura za Wabunge waliohudhuriana kupiga kura.(3) Spika, Naibu wa Spika, au mtu mwingine atakayeongozakikao cha Bunge, hatakuwa na kura ya kawaida bali atakuwa nakura ya uamuzi kukitokea usawa wa kura.(4) Kanuni za Bunge zaweza kuweka masharti kwambaMbunge yeyoyote atakayepiga kura juu ya jambo lolote ambaloyeye binafsi ana masilahi nalo atahesabiwa kuwa hakupiga kura.
Viti vilivyowazi katikaBungeSheria ya1984 Na.15ib.14​
95.​
Bunge laweza kutekeleza shughuli wakati wa vikao vyakebila ya kujali kwamba kuna kiti kilicho wazi miongoni mwa viti vyaWabunge (iwe kiti hicho kimekuwa wazi tangu Bunge lilipokutanakwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au kimekuwa wazibaada ya Mkutano huo wa kwanza) na iwapo katika shughuli hizoatashiriki mtu yeyote ambaye hana haki ya kushiriki au kamawakati wa shughuli hizo atakuwapo mtu yeyote ambaye hana hakiya kuwapo, basi kushiriki kwa mtu huyo au kuwapo kwakehakutabatilisha shughuli hizo.
Kamati zaBunge Sheriaya 1995 Na.12Ibara 16​
96​
.-(1) Bunge laweza kuunda Kamati za Bunge za namnambalimbali kadri litakavyoona infaa kwa ajili ya utekelezaji bora wamadaraka yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
69​
(2) Kanuni za Bunge zaweza kufafanua muundo na shughuliza Kamati za Bunge zitakazoundwa kwa mujibu wa masharti yaibara hii.​
Utaratibu wa Kutunga Sheria​
Namna yakutumiamadaraka yakutungasheria ya 1984Na.15 ib.4​
97​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katikaKatiba hii, Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwakufuata utaratibu wa kujadili na kupitisha Miswada ya Sheriaambayo hatimaye itabidi ipate kibali cha Rais, na Muswadahautakuwa Sheria mpaka uwe umepitishwa na Bunge nakukubaliwa na Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.(2) Baada ya Muswada kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili yakupata kibali chake, Rais aweza kuukubali au kukataa kuukubali,na iwapo Rais atakataa kuukubali Muswada basi ataurudisha kwaBunge pamoja na maelezo ya sababu zake za kukataa kuukubaliMuswada huo.(3) Baada ya Muswada kurudishwa kwa Bunge kwa mujibu wamasharti ya ibara hii, hauwezi kupelekwa te na kwa Rais kwa ajiliya kupata kibali chake kabla kumalizika muda wa miezi sita tanguuliporudishwa, isipokuwa kama katika hatua yake ya mwishokwenye Bunge kabla haujapelekwa tena kwa Rais Muswada huoumeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipunguitheluthi mbili ya Wabunge wote.(4) Iwapo Muswada umerudishwa kwa Bunge na Rais, halafuukaungwa mkono kwenye Bunge na Wabunge ambao idadi yaohaipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kama ilivyoelezwakatika ibara ndogo ya (3) na kupelekwa kwa Rais kwa ajili yakupata kibali chake kwa mara ya pili kabla haujamalizika muda wamiezi sita tangu uliporudishwa, basi Rais atatakiwa kuukubaliMuswada huo kabla ya kumalizika muda wa siku ishirini na mojatangu Muswada huo ulipowasilishwa kwake la sivyo basi itabidialivunje Bunge.(5) Masharti yaliyomo katika ibara hii au katika ibara ya 64ya Katiba hii hayatalizuia Bunge kutunga sheria na kuwekamasharti ambayo yaweza kukabidhi kwa mtu yeyote au kwa idarayoyote ya Serikali madaraka ya kuweka Kanuni za nguvu yakisheria au kuzipa nguvu ya kisheria Kanuni zozote zilizowekwana mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
70​
Utaratibu wakubadilishaKatiba hii nabaadhi yasheriaSheria ya1984 Na.15ib.14​
98​
.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilishamasharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha mashartiyoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika naaya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote yasheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanzakwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kuraza Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbiliya Wabunge wote;(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha mashartiyoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheriayoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mamboyaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza yaPili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tuiwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambaoidadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wotekutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabungewote kutoka Tanzania Zanzibar.(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogoya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheriamaana yake ifahamike kuwa ni pamoja na kurekebisha aukusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti menginebadala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya mashartihayo.
Utaratibu wakutunga sheriakuhusumamboya fedhaSheriaya 1984 Na.15ib.14​
99​
.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mamboyanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekezakwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo laRais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.(2) Mambo yanayohusika na ibara hii ni haya yafuatayo:-(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya lolote kati ya mamboyafuatayo:-(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namnanyingine yoyote isipokuwa kupunguza;(ii) kuangiza kwamba malipo au matumizi yafedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu waHazina ya Serikali au mfuko wa Serikalimwingine wowote au kubadilisha kiwangohicho na namna nyingine yoyte isipokuwakupunguza;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
71​
(iii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedhayafanywe kutokana na Mfuko Mkuu waHazina ya Serikali au mfuko wa Serikalimwingine wowote wakati ikifahamika kwambafedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwaitolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo,au kuagiza kwamba malipo au matumiziyanayofanywa kutokana na mifuko hiyoyaongezwe;(iv) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwalilipwe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;(b) hoja au mabadiliko yoyote ya Hoja kwa ajili ya lolotekati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya ibarahii ndogo.(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa muswada wowoteuliowasilishwa kwenye Bunge au Hoja yoyote iliyotolewa katikaBunge na Waziri au Naibu Waziri.​
Madaraka na Haki za Bunge​
Uhuru wamajadiliano nautaratibu washughuliSheria ya1984 Na.15ib.14​
100​
.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano nautaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwana chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.(2) Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingineyoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwashauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisemaau kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia yamaombi, muswada, hoja au vinginevyo.
Kuhifadhi nakutilia nguvuuhuru wamajadiliano nawa shughulisheria ya 1984Na.15 ib.14​
101​
. Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwekamasharti ya kuwezesha mahakama na sheria kuhifadhi na kutilianguvu uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu wa shughulikatika Bunge ambao kwa mujibu wa ibara ya 100 umedhaminiwana Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
72​
SURA YA NNESERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBARNA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBARSEHEMU YA KWANZASERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARNA RAIS WA ZANZIBAR​
Serikali yaMapinduzi yaZanzibar namamlaka yakeSheria ya1980 Na.45ib.55: naSheria ya1984Na.15 ib.14:Sheria ya1994 Na.34ib.16​
102​
.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikanakama "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" ambayo itakuwa namamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo yaMuungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(2) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii na katikaibara zifuatazo katika Sura hii ya Katiba hii, Serikali ya Mapinduziya Zanzibar itaundwa na itatekeleza madaraka yake kwa mujibuwa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984.
Kiongozi waSerikali yaMapinduzi yaZanzibar namamlaka yakeSheria ya1980 Na.15ib.14 1994Na.34 ib.17​
103​
.-(1) Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya MapinduziZanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu waSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi la Zanzibar.(2) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla yakushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanizibarkiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, nakiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibarkinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika nakutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina Katiba ya Zanzibar, 1984.(3) Pamoja na madaraka yake mengine kiongozi wa Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar ndiye atakayewateua na kuwakabidhimadaraka Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Mapinduziya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
73​
Uchaguzi wakiongozi waSerikali yaMapinduziZanzibar 1980Na.1 ib.11 na1984 Na.15ib.14 1990Na.16 ib.21992 Na.20ib.14​
104​
.-(1) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaratachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibuwa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibuuliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza laWawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla auuchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti chaKiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa ki wazi,na uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarutafanyika ili kujaza nafasi hiyo kila mara litokeapo lolote kati yamambo yafuatayo.(a) baada ya Baraza la Wawakilishi kuvunjwa;(b) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kujiuzulu bila ya kulivunjwa Baraza laWawakilishi kwanza;(c) baada ya kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kupoteza sifa za kushika nafasi ya madarakaya kuchaguliwa;(d) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kushtakiwa katika Baraza la Wawakilishi kwamujibu wa Katiba ya Zanzibar 1984 na kuondolewakatika madaraka.(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa Katiba yaZanzibar 1984 kwamba Kiongozi wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar hawezi kumudu kazi nashughuli zake;(f) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kufariki.
SEHEMU YA PILIBARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR​
Baraza laMapinduzi laZanzibar nakazi zake​
105​
.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibarlitakalokuwa na wajumbe wafuatao:(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katibaya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
74​
(2) Bila ya kuyaingilia madaraka ya Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi kama kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Baraza la Mapinduzi litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauriKiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yoteyanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake ya uongozi nausimamizi wa shughuli za Serikali ya Zanzibar na pia utekelezajiwa madaraka yake juu ya shughuli zote za Serikali kuhusu mamboyote yasiyo mambo ya Muungano, kwa mujibu wa masharti yaKatiba hii na yale ya Katiba ya Zanizbar.​
SEHEMU YA TATUBARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR​
Baraza laWawakilishiZanzibarMadaraka yakutungaSheriaza ZanzibarSheria ya1980Na.1 ib.93​
106​
.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Baraza la Wawakilishi litakuwa na sehemu mbili; sehemu mojaitakuwa ni ya wajumbe wa Baraza hilo waliochaguliwa nakuteuliwa kwa namna itakavyoelezwa na masharti ya Katiba yaZanzibar, ya mwaka 1984, na ambao watajulikana kama wajumbeWawakilishi; sehemu nyingine ya Baraza la Wawakilishi itakuwa niKiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezajiwa madaraka yake kwa mujibu wa mahsarti ya Katiba hii namasharti ya Katiba ya Zanzibar, ya mwaka 1984.(2) Iwapo kwa mujibu wa mahsarti ya Katiba hii, masharti yaKatiba ya Zanzibar, ya mwaka 1984, au masharti ya sheria yoyoteiliyowekwa na inayotumika Zanzibar, jambo lolote lahitajikuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Baraza laWawakilishi, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa nalimetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa aulimetekelezwa na Wajumbe wawakilishi na vile vile Kiongozi waSerikali ya Mapinduzi ya Zanizbar, kwa mujibu wa madaraka yaokuhusu jambo hilo.(3) Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu yamambo yote yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononimwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Madaraka yaBaraza laWawakilishiSheria ya1984 Na.15;ib.20​
107.-​
(1) Rais wa Zanzibar kama sehemu moja ya Barazala Wawakilishi la atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa naKatiba hii na pia Katiba ya Zanzaibar kwa ajili hiyo.(2) Wajumbe wawakilishi kama Baraza la Wawakilishiwatakuwa ndicho chombo kikuu cha Tanzania Zanzibar ambachokitakuwa na madaraka kwa lniaba ya wananchi wa TanzaniaZanzibar, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
75​
Zanzibar na vyombo lvyake vyote katika utekelezaji wa majukumuyake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar.(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yakeBaraza la Wawakilishi laweza -(a) kumuuliza Waziri yeyote wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar swali lolote kuhusu mambo ya umma katikaTanzania Zanzibar yaliyomo katika wajibu wake;(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar wakati wa Mkutano wa Barazala wawakilishi wa kila mwaka wa bajeti;(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefuau wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwaTanzania Zanzibar, na kutnga Sheria ya kusimamiautekelezaji wa mpango huo;(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitajikuwapo sheria;(e) kutayarisha au kuagiza itayarishwe na kuwasilishakwenye Chama taarifa kuhusu jambo lolote ambalo likochini ya mamlaka ya Bunge.​
SURA YA TANOUTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO,TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIABARA, MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR,MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YAMUUNGANO NA MAHAKAMA MAALUMYA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KKWANZAUTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO​
Mamlaka yautoaji hakiSheria ya2000Na.3 ib.17​
107A​
.-(1) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muunganoitakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara yaMahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikaliwala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibarkitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.(2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwakuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:(a) kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
76​
au kiuchumi;(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokanana makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheriamahususi iliyotungwa na Bunge;(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina yawanaohusika katika migogoro;​
Uhuru waMahakamaSheria ya2000Na.3 ib.17​
107B​
. Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakamazote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti yaKatiba na yale ya sheria za nchi.
MahakamaKuuya Jamhuri yaMuungano namamlaka yakeSheria ya1979 Na.14ib.6​
SEHEMU YA PILIMAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO108​
.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano(itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu") ambayomamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii aukatika sheria nyingine yoyote.(2) Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazikwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanzakatika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basiMahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri laaina hiyo. Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wakutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila zakisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwakawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu.Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bilaya kuathiri mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kamailivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.
Majaji waMahakamaKuuna uteuzi waoSheria ya1979 Na.14ib.6 1985Sheria ya1985 Na.15ib.22Sheria ya1990 Na.14ib.5​
109​
.-(1) Kutakuwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu(ambaye katika ibara zifuatzo kwenye Katiba Hii atatajwa tu kwakifupi kama "Jaji Kiongozi") na Majaji wengine wa Mahakama Kuuwasiopungua kumi na watano.(2) Jaji Kiongozi na Majaji wengineo wa Mahakama Kuuwatateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri yaMahakama.(3) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingineyoyote kuhusu madaraka ya Jaji Mkuu aliyetajwa katikaibara ya 118, Jaji Kiongozi atakuwa ndiye msaidizi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
77​
ibara ya 118, Jaji Kiongozi atakuwa ndiye msaidizimaalum wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katikaMahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngaziya chini yake, na katika madaraka hayo Jaji Kiongoziatatekeleza kazi na shughuli atakazoagizwa aukuelekezwa mara kwa mara na Jaji Mkuu, na kwamadhumuni ya ibara hii, Jaji Kiongozi atajulikana piakama Mkuu wa Mahakama Kuu.(4) Mbali ya madaraka yake ya kawaida ya Jaji wa MahakamaKuu kama Majaji wengine wote wa Mahakama Kuu, Jaji Kiongoziatakuwa pia na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli zotezinazoambatana na mamlaka ya Mahakama Kuu ambazo kwamujibu wa masharti ya Katiba hii au ya sheria nyingine yoyote aukufuatana na mila za kisheria zinazotumika hutakiwa zitekelezwena Mkuu wa Mahakama Kuu:Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo hayatatumikakwa ajili ya utekelezaji wa kazi au shughuli ambazo kwa mujibu wamasharti ya Katiba hii au ya Sheria nyingine yoyote au kufuatanana mila za kisheria zinazotumika Tanzania zimetajwa mahususi auzinafahamika kuwa ni kazi au shughuli zinazotakiwa kutekelezwatu na Jaji Mkuu.(5) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi auutekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (3) na ya (4) ya ibarahii, inatamkwa rasmi hapa kwamba isipokuwa kama masharti yaKatiba hii au ya sheria nyingine yoyote yameagiza vingine, JajiMkuu atakuwa na uwezo wa kutoa kwa Jaji Kiongozi mara kwamara maagizo au maelekezo kuhusu utendaji wa kazi na shughulizake kama Mkuu wa Mahakama Kuu: vile vile, Jaji Mkuu atakuwana uwezo wa kuwakilisha kwa Jaji Kiongozi baadhi ya madarakayake ya uongozi na usimamizi juu ya utekelezaji wa kazi katikaMahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi ya chiniyake, na kila inapohitajika, Jaji Mkuu anaweza kutekeleza yeyemwenyewe moja kwa moja madaraka yake yoyote aliyowakilishakwa Jaji Kiongozi.(6) Kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu haitafutwa wakati yupo mtualiyeshika madaraka ya kiti cha Jaji.(7) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii,mtu aweza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa anasifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (8) yaibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifamaalum kwa muda usiopungua miaka mitano.(8) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (7), ya (9)na ya (11) ya ibara hii, "sifa maalum" maana yake ni sifazilizotajwa katika Sheria ya Mawakili (au Sheria nyingine yoyoteinayobadilisha hiyo sheria ya Mawakili au inayotumika badalayake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
78​
yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo iliaweze kukubaliwa kuandikishwa kama Wakili Tanzania Bara.(9) Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenyesifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwamuda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzina kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji waMahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahilikukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile shartila kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, nabaada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Raisaweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.(10) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji Kiongozi kitakuwa wazi aukwamba Jaji Kiongozi atashindwa kutekeleza kazi zake kwasababu yoyote, basi kazi hizo zitatekelezwa na Jaji mmojwapoatakayeteuliwa na Rais kwa ajili hiyo, na na Jaji huyo atatekelezakazi hizo mpaka atakapoteuliwa Jaji Kiongozi mwingine nakushika madaraka ya kiti cha Jaji Kiongozi au mpaka Jaji Kiongozimwenyewe ambaye alikuwa hamudu kazi zake atakaporejeakazini.(11) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji yeyote kitakuwa wazi auikiwa Jaji yeyote atateuliwa kuwa Kaimu Jaji Kiongozi au kamaatashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au kamaJaji Mkuu atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama Kuu zilivyowakati huo zahitaji ateuliwe Kaimu Jaji, basi Rais aweza, baada yakushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kuteua Kaimu Jajikutoka miongoni mwa watu wenye sifa maalum.Isipokuwa kwamba(a) mtu hatahesabiwa kuwa hastahili kuteuliwa kwa mujibuwa masharti ya ibara hii ndogo kwa sababu tu kwambaametimiza umri uliotajwa katika ibara ndogo ya (1) yaibara ya 61 ya Katiba hii;(b) kwa madhumuni ya kumteua Kaimu Jaji kwa mujibu wamasharti ya ibara hii ndogo, Rais aweza kutangua lilesharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopunguamiaka mitano kwa sababu kama zile zilizotajwa katikaibara ndogo ya (9) ya ibara hii.(12) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji kwa mujibuwa masharti ya ibara ndogo ya (11) ya ibara hii, ataendeleakufanya kazi kama Kaimu Jaji kwa muda wowote utakaotajwawakati wa kuteuliwa kwake au, kama muda haukutajwa, mpakauteuzi wake utakapofutwa na Rais, lakini bila ya kujali kwambamuda wake wa kazi umemalizika au kwamba uteuzi wakeumefutwa, mtu huyo aweza kuendelea kufanya kazi kama KaimuJaji mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpakaakamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
79​
ambayo alikwisha anza kuyasiliza kabla ya muda wake wa kazihaujamalizika au kabla ya uteuzi wake haujafutwa.​
Muda waMajajiwa MahakamaKuu kushikamadarakaSheria ya1979 Na.14ib.6: naSheria ya1985Na.15 ib.22 na23Sheria ya1995 Na.12ib.17​
110.​
-(1) Kila Jaji wa Mahakama Kuu atalazimika kuacha kaziyake atakapotimiza umri wa miaka sitini lakini masharti ya ibara hiindogo yatatumika bila ya kuathiri masharti yafuatayo katika ibarahii.(2) Jaji yeyote wa Mahakama Kuu aweza kujiuzulu kazi katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakati wowotebaada ya kutimia umri wa miaka hamsini na tano, isipokuwa kamaRais ataagiza kwamba asijiuzulu, na iwapo Rais ataagiza hivyo,basi huyo Jaji atakayehusika na maagizo hayo ya Rais hatakuwana haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanza muda wowoteutakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo.(3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya manufaa ya Ummainafaa Jaji aliyetimiza umri wa miaka sitini aendelee kufanya kazi,na huyo Jaji mwenyewe anakubali kwa maandishi kuendeleakufanya kazi, basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo aendeleekufanya kazi kwa muda wowote utakaotajwa na Rais.(4) Bila ya kujali kwamba Jaji ametimiza umri ambaoanalazimika kuacha kazi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, mtuanayefanya kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu aweza kuendeleakufanya kazi baada ya kutimiza umri huo mpaka amalizekutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughulinyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwisha anzakuyasikiliza kabla hajatimiza umri huo wa kuacha kazi.(5) Jaji wa Mahakama Kuu aweza tu kuondolewa katikamadaraka ya kazi ya kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kaziyake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) aukwa sababu ya tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji ausheria ya maadili ya viongozi wa umma; na hataweza kuondolewakazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (7) ya ibarahii.(6) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazinilahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwaifuatavyo:-(a) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti naWajumbe wengine wasiopungua wawili. Na huyoMwenyekiti na angalau nusu ya Wajumbe wengine waTume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji waMahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchiyoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifakwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lolote naitamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusikaaondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
80​
kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana namaradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu yatabia mbaya.(7) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibarandogo ya (6) itamshauri Rais kwamba jaji ambaye habari zakezimechunguzwa na hiyo Tume aondolewe kazini kwa sababu yakushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingineyoyte au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoakazini Jaji huyo anayehusika.(8) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini limepelekwa kwenyeTume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibarandogo ya (6) ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi Jajihuyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzihuo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzihuo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba jaji huyoasiondolewe kazini.(9) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti yaibara ndogo ya (12) ya ibara ya 109 ya Katiba hii.​
Kiapo chaMajaji Sheriaya 1979 Na.14ib.6Sheria 1985Na.15 ib.22​
111​
. Jaji wa Mahakama Kuu hatashika madaraka yake ilampaka awe ameapishwa kwanza kiapo cha uaminifu na pia kiapokingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazikitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungw na Bunge.
SEHEMU YA TATUMADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMUNA WATUMISHI WENGINE WAMAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NATUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA​
Tume yaKuajiriya MahakamaSheria 1985Na.14 ib.7Sheria ya1985Na.15 ib.22Sheria ya1990Na.14 ib.6​
112​
.-(1) Kutakuwa na Tume ya Kuajiri kwa ajili ya Mahakimuna Watumishi wengineo wa Mahakam za Tanzania Bara.Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa hawa wafuatao:-(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti;(b) Mwanasheria Mkuu;(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ya Tanzaniaambaye atateuliwa kwa ajili hiyo na Rais baada yakushauriana na Jaji Mkuu(d) Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu;(e) Wajumbe wawili ambao watateuliwa na Rais.(2) Mtu hataweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kwamujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
81​
ikiwa mtu huyo ni Mbunge au ni mtu mwenye madaraka ya ainanyingine yoyote iliyotajwa kwa ajili hiyo na sheria iliyotungwa naBunge.​
Madaraka yakuajiriMahakimu nawatumishiwengine waMahakamaSheria ya1979 Na.14Ib.7Sheria ya1985 Na.15ib.22Sheria ya1985 Na.24ib….​
113​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria yoyote iliyotungwana Bunge inayohusika na suala la kuajiri Mahakimu na Watumishiwengineo wa Mahakama mgawanyo wa madaraka kwa ajili yasuala hilo utakuwa ifuatavyo:(a) madaraka ya kuwaajiri watu wa kushika madaraka yaaina zilizotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii(pamoja na madaraka ya kuwathibitisha watu haokazini na kuwapandisha vyeo) yatakuwa mikononi mwaRais;(b) madaraka ya kudhibiti nidhamu ya watu hao namadaraka ya kuwaondoa kazini yatakuwa mikononimwa Tume ya Kuajiri iliyotajwa katika ibara ya 112 yaKatiba hii.(2) Madaraka yanayohusika na masharti ya ibara hii nimadaraka ya Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania naNaibu wa Msajili huyo wa daraja lolote, madaraka ya Msajili waMahakama Kuu na Naibu wa Msajili huyo wa daraja lolote,madaraka ya Hakimu Mkazi na Hakimu wa aina nyingine yoyote,na madaraka ya aina nyingine yoyote yanayohusika naMahakama yoyote (isipokuwa Mahakama ya Kijeshi) itakayotajwana Sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katibahii.
Uanachamakatika Vyamavy a SiasaSheria ya1994 Na.34ib.19​
113A​
. Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani,Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa ngazi yoyote kujiunga nachama chochote cha Siasa, isipokuwa tu kwamba atakuwa nahaki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
SEHEMU YA NNEMAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR​
MahakamaKuuya ZanzibarSheria ya1985 Na.15ib.22​
114​
. Kwa madhaumuni ya ufafanuzi wa Sura hii ya Katiba hii,ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sura hii hayazuiikuendelea kuwapo au kuanzishwa, kwa mujibu wa Sheriazinazotumika Zanzibar kwa Mahakama Kuu ya Zanzibar auMahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
82​
Mamlaka yaMahakamaKuuya ZanzibarSheria ya1985 Na.15ib.22na 25​
115​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 83 na 116 yaKatiba hii, mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar yatakuwakama itakavyoelezwa katika Sheria zinazotumika Zanzibar.(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingineyoyote iliyotungwa na Bunge, iwapo sheria yoyote iliyotungwa naBunge inayotumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Visiwaniimekabidhi madaraka yoyote kwa Mahakama Kuu, basiMahakama Kuu ya Zanzibar yaweza kutekeleza madaraka hayokwa kiasi kile kile inavyoweza kutekeleza Mahakama Kuu yaJamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA TANOMAHAKAMA YA RUFANI YAJAMHURI YA MUUNGANO​
TafsiriSheria ya1984 Na.15ib.25 na 26​
116​
.-(1) Katika Sehemu hii ya Tano ya Sura hii ya Tano yaKatiba hii na katika sehemu nyingine za Katiba hii, ila iwapomaelezo yahitaji vinginevyo:"Idara ya Mahakama" maana yake ni Mahakama ya Rufani yaJamhuri ya Muungano iliyotajwa katika ibara ya 117 ya Katiba hii(au kwa kifupi "Mahakama ya Rufani"), Mahakama Kuu yaJamhuri ya Muungano iliyotajwa katika ibara ya 108 ya Katiba hii(ambayo itajulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu) pamoja naMahakama nyingine zozote za ngazi zilizo chini ya MahakamaKuu;"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani nani pamoja na Kaimu Jaji Mkuu au Jaji wa Rufani anayeshikilia aukutekeleza madaraka ya Jaji Mkuu;"Jaji wa Rufani" maana yake ni Jaji yoyote wa Mahakama yaRufani.(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Jaji Mkuuhatakuwa na madaraka juu ya jambo lolote linalohusu muundo nauendeshaji wa shughuli za siku hadi siku za Mahakamazilizoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar au sheria yoyoteya Tanzania Zanzibar.(3) Jaji Mkuu atashauriana mara kwa mara na Jaji Mkuu waZanzibar kuhusu uendeshaji wa shughuli za Mahakama ya Rufanikwa jumla, na pia kuhusu uteuzi wa Majaji wa Rufani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
83​
Mhakama yaRufani yaJamhuri yaMuungano namamlaka yakesheriaza 1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.27​
117​
.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri yaMuungano (itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama yaRufani") ambayo mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwakatika Katiba hii au katika Sheria nyingine yoyote.(2) Mahakama ya Rufani haitakuwa na mamlaka yoyotekuhusu usuluhishi wa suala lolote litakaloshughulikiwa kwa mujibuwa masharti ya ibara ya 126 ya Katiba hii ambayo inahusu ubishikati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya MapinduziZanzibar.(3) Kazi ya Mahakama ya Rufani itakuwa ni kusikiliza na kutoauamuzi juu ya kila rufaa inayoletwa mbele ya Mahakama yaRufani kutokana na hukumu au uamuzi wa namna nyingine yoyotewa Mahakama Kuu au Mahakama ya Hakimu.(4) Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii naBunge au na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar yaweza kuwekamasharti yatakayoeleza utaratibu wa kupeleka rufaa mbele yaMahakama ya Rufani, nyakati na sababu za kukata rufaa nanamna ya kushughulikia rufaa hizo.
Majaji waMahakama yaRufani nauteuzi waoSheria za1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.28​
118​
.-(1) Kutakuwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani(ambaye katika ibara zifuatazo kwenye Katiba hii atatajwa tu kwakifupi kama "Jaji Mkuu" na Majaji wengine wa Mahakama yaRufani wasiopungua wawili, isipokuwa kwamba kikao maalum chaMahakama nzima kitakuwa kamili kikiwa na Majaji wa Rufaniwasiopungua watano.(2) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais na atakuwa ndiye Kiongoziwa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Idara ya Mahakamakama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 116 ya Katiba hii.(3) Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa naRais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwawatu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuuya Jamhuri ya Muungano kama ilivyoelezwa katika ibara ya 109ya Katiba hii au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwakuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu waSheria zinazotumika Zanzibar.(4) Iwapo itatokea kwamba:-(a) Kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi; au(b) Jaji Mkuu hayupo Tanzania; au(c) Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kazi yake kwasababu yoyote na Rais akiona kuwa kwa muda watukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua KaimuJaji Mkuu, basi Rais aweza kumteua Kaimu Jaji Mkuukutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kustahilikuteuliwa kuwa Majaji wa Mhakama ya Rufani, na huyo
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
84​
Kaimu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpakaatakapoteuliwa Jaji Mkuu au mpaka Jaji Mkuumwingine ambaye alikuwa hayupo Tanzania au alikuwahamudu kazi zake atakaporejea kazini.(5) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji yeyote wa Mahakama yaRufani kitakuw wazi au ikiwa Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaniatateuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu au kama atashindwa kutekelezakazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwakazi za Mahakama kama ya Rufani ilivyo wakati huo zahitajiateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi Rais aweza,baada ya kushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kumteuaKaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa watuambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufanikwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii.(6) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakamaya Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibarahii, ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama yaRufani kwa muda wowote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake,au, kama muda haukutajwa, mpaka uteuzi wake utakapofutwa naRais, lakini bila ya kujali kwamba muda wake wa kazi umemalizikaau kwamba uteuzi wake umefutwa, mtu huyo aweza kuendeleakufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani mpakaamalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilisheshughuli nyingine yoyote inayohusika na rufaa au mashaurimengine yoyote ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla mudawake wa kazi haujamalizika au kabla ya uteuzi wake haujafutwa.(7) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi wamasharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 118 ya Katiba hii(inayotaja idadi ya Majaji wa kudumu wa Mahakama ya Rufani) namasharti ya ibara ya 119 ya Katiba hii (inayoeleza mamlaka yaMajaji wa Mahakama ya Rufani), inatamkwa rasmi hapa kwambaKaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeteuliwa kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, atakuwa na mamlakakamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na kwamb atatekeleza kazizake kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani bila ya kujali kuwakuteuliwa kwake kutakiuka idadi ya Majaji wa kudumu waMahakama ya Rufani iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara118 ya Katiba hii, lakini masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bilaya kuathiri masharti ya ibara ya 122 ya Katiba hii kuhusu kiwangocha vikao vya Mahakama ya Rufani.(8) Kazi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani haitafutwa wakatiyupo mtu aliyeshika madaraka ya kiti cha Jaji wa Mahakama yaRufani.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
85​
Mamlaka yaMajajiMahakama yaRufani Sheriaza 1979 Na.14ib.8 na 1984Na.14 ib.29​
119.​
Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani hatakuwa namamlaka ya kusikiliza shauri lolote katika Mahakama Kuu aukatika Mahakama ya Hakimu ya ngazi yoyote:Isipokuwa kwamba iwapo Jaji yeyote wa Mahakama Kuuatateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi hata baada yakuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji huyoaweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama Kuu mpakaamalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilisheshughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayoalikwisha anza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji waMahakama ya Rufani, na kwa ajili hiyo itakuwa halali kwake kutoahukumu au uamuzi mwingine wowote unaohusika kwa kwakutumia na kutaja madaraka aliyoshika kabla ya kuteuliwa kuwaJaji wa Mahakama ya Rufani, lakini endapo hatimaye hukumu hiyoau uamuzi huo mwingine utapangwa kwa njia ya rufaaitakayofikishwa mbele ya Mahakama ya Rufani, basi katika halihiyo Jaji huyo wa Mahakama ya Rufani, hatakuwa na mamlaka yakusikiliza rufaa hiyo.
Muda waMajajiwa Mahakamaya RufanikushikaMadarakasheriaza 1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.30​
120​
.-(1) Kila Jaji wa Mahakama ya Rufani atalazimika kuachakazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano, lakinimasharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila kuathiri mashartiyafuatayo katika ibara hii.(2) Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani aweza kujiuzulu kazikatika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakatiwowote baada ya kutimiza umri wa miaka sitini, isipokuwa kamaRais ataagiza kwamba asijiuzulu, na iwapo Rais ataagiza hivyo,basi huyo Jaji wa Mahakama ya Rufani atakayehusika na maagizohayo ya Rais hatakuwa na haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanzamuda wowote utakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
86​
(3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya manufaa ya Ummainafaa Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyetimiza umri wa miakasitini na tano aendelee kufanya kazi, na huyo Jaji mwenyewe waMahakama ya Rufani anakubali kwa maandishi kuendeleakufanya kazi; basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo waMahakama ya Rufani aendelee kufanya kazi kwa muda wowoteutakaotajwa na Rais.(4) Bila ya kujali kwamba Jaji wa Mahakama ya Rufaniametimiza umri ambao analazimika kuacha kazi kwa mujibu wamasharti ya ibara hii, mtu anayefanya kazi ya Jaji wa Mahakamaya Rufani aweza kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umrihuo mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpakaakamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauriambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri huo wakuacha kazi.(5) Jaji wa Mahakama ya Rufani aweza tu kuondolewa katikamadaraka ya kazi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sababu yakushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi ausababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, nahataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti yautaratibu unaofanana na ule uliowekwa kwa ajili ya kumwondoakazini Jaji wa Mahakama Kuu kama ilivyoelezwa katika ibarandogo ya (6) na ya (7) ya ibara ya 110 ya Katiba hii, na kwa ajilihiyo masharti ya ibara ndogo ya (8) ya ibara hiyo ya 110yatatumika kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa namna ile ileyanavyotumika kwa Jaji wa Mahakama Kuu.(6) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti yaibara ndogo ya (5) ya ibara ya 118 ya Katiba hii.​
Kiapo chaMajajiwa Mahakamaya RufaniSheria za1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.31​
121.​
Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashika madaraka yakeila mpaka awe ameapishwa kiapo cha uaminifu na kiapo kinginechochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwamujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
87​
Kiwango chavikao vyaMahakama yaRufaniSheria za1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.32​
122​
.-(1) Kiwango cha kila kikao cha Mahakama ya Rufani niMajaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua watatu.(2) Katika kila rufaa suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama yaRufani litaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majajiwa Mahakama ya Rufani waliosikiliza rufaa.
Mashauriyanayowezakuamuliwa naJaji mmoja waMahakama yaRufaaSheria za1979 Na.14ib.8 naSheria ya1984Na.15 ib.33​
123.​
Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani aweza kutekelezamadaraka yoyote ya Mahakama ya Rufani ambayo hayahusiki nakutoa uamuzi juu ya Rufaa:Isipokuwa kwamba:(a) Katika mashauri ya jinai, iwapo Jaji wa Mahakama yaRufani aliyeombwa kutekeleza madaraka hayo atatoauamuzi ambao mwombaji haridhiki nao, basi mwombajiatakuwa na haki kutaka maombi yake yaamuliwe naMahakama ya rufani;(b) Katika mashauri ya madai, Mahakama ya Rufaniyaweza kubatilisha au kubadilisha amri, agizo auuamuzi wa namna nyingine wowote uliotolewa na Jajimmoja wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wamasharti ya ibara hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
88​
SEHEMU YA SITAUTARATIBU WA KUPELEKA HATINA KUTEKELEZA MAAGIZOYALIYOMO KATIKA HATIZILIZOTOLEWA NA MAHAKAMA​
Utekelezaji wamaagizo yaMahakamautafanywanchini Tanzaniakote Sheria ya1984 Na.15ib.34​
124​
.-(1) Hati zenye maagizo yaliyotolewa na Mahakama zaTanzania Bara na Mahakama za Tanzania Zanzibar katikamashauri ya madai ya aina zote na mashauri ya jinai ya aina zote(pamoja na hati za kuamuru kukamata watu) zaweza kupelekwamahali popote nchini Tanzania na maagizo hayo yawezakutekelezwa mahali popote nchini Tanzania kwa kufuatamasharti yafuatayo:-(a) iwapo mahakama imetoa hati zenye maagizoyatakayotekelezwa mahali ambako mahakama hiyohaina mamlaka, basi hati hiyo itapelekwa huko namaagizo yaliyomo katika hati hiyo yatatekelezwa kwamujibu wa utaratibu unaotumika huko kwa ajili yakupeleka hati au kutekeleza maagizo yaliyomo katikahati iliyotolewa na mahakama yenye mamlaka hukoilikopelekwa hati; na(b) iwapo sheria inayotumika huko ilikopelekwa hatiimeweka masharti kwamba hati zilizotolewa namahakama ya mahali pengine ni lazima ithibitishwekwanza na Mahakama yenye mamlaka mahali hapoinapotumika sheria hiyo, basi kila hati iliyotolewa namahakama ya mahali pengine itabidi ithibitishwekwanza kwa mujibu wa sheria hiyo kabla maagizoyaliyomo katika hati hiyo hayajatekelezwa.(2) Iwapo mtu amekamatwa mahali popote nchini Tanzaniakwa mujibu wa hati ya kuamuru kukamatwa kwake iliyotolewa namahakama ambayo haina mamlaka mahali hapo alipokamatwamtu huyo, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa yuko chini ya ulinzihalali na aweza kufikishwa mbele ya mahakama iliyotoa hati hiyo,lakini masharti haya yaliyomo katika ibara hii ndogo itabidiyatumiwe bila kuathiri masharti ya sheria inayotumika hapomahali alipokamatwa mtu huyo.(3) Masharti yaliyomo katika ibara hii hayatazuia sheriakuweka utaratibu kwa ajili ya kupeleka nje ya Tanzania hatizilizotolewa na Mahakama za Tanzania Bara au mahakama zaTanzania Visiwani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
89​
SEHEMU YA SABAMAHAKAMA MAALUM YA KATIBAYA JAMHURI YA MUUNGANO​
MahakamaMaalum yaKatiba yaJamhuri yaMuunganoSheriaya 1984 Na.15ib.35​
125.​
Kutakuwa na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuriya Muungano ambayo Mamlaka yake, muundo wake na utaratibuwa shughuli zake ni kama ilivyoelezwa katika ibara ya 126, 127na 128 ya Katiba hii.
Mamlaka yaMahakamaMaalum yaKatiba Sheriaya 1979 Na.14ib.9na Sheria ya1984 Na.15ib.36​
126​
.-(1) Kazi pekee ya Mahakama Maalum ya Katiba yaJamhuri ya Muungano ni kusikiliza shauri lililotolewa mbele yake,kutoa uamuzi wa usuluhishi, juu ya suala lolote linalohusika natafsiri ya Katiba hii iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wakeunabishaniwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano naSerikali ya Mapinduzi Zanzibar.(2) Katika kutekeleza kazi yake kwa mujibu wa masharti yaibara hii, Mahakama Maalum ya Katiba haitakuwa na mamlakaya kuchunguza au kubadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu auuamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kwa mujibu wamasharti ya ibara ya 83 ya Katiba hii au uamuzi wa Mahakamaya Rufani uliotolewa kwa mujibu wa ibara ya 117 ya Katiba hii.(3) Kila uamuzi wa usuluhishi utakaotolewa na MahakamaMaalum ya Katiba kwa mujibu wa ibara hii utakuwa ndio wamwisho, hakutakuwa na haki ya kukata rufaa popote.
Muundo waMahakamaMaalum yaKatiba Sheriaya 1984 Na.15ib.37​
127​
.-(1) Mahakama Maalum ya Katiba itakuwa nawajumbe ambao nusu ya jumla ya wajumbe wote watateuliwa naSerikali ya Jamhuri ya Muungano na nusu nyingine ya jumla hiyowatateuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(2) Mtu anayeweza kuteuliwa kuwa Mjumbe waMahakama Maalum ya Katiba ni yule tu ambaye ni jaji aualiyepata kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa MahakamaKuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar,au mtu mwenye uwezo na ujuzi wa kazi ya Jaji na anayestahilikuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji kwa mujibu wa Sheriainayotumika Tanzania Bara na sheria inayotumika TanzaniaZanzibar, kadri hali itakavyokuwa.(3) Mtu aweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa MahakamaMaalum ya Katiba ama kwa ajili ya kusikiliza shauri moja tu aumashauri mawili au zaidi kama yatatokea. Mjumbe ataendeleakutekeleza madaraka ya kazi yake kama Mjumbe wa MahakamaMaalum ya Katiba mpaka shauri analohusika nalo litakapokwisha
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
90​
au mpaka uteuzi wake utakapofutwa au mpaka atakaposhindwakutekeleza kazi yake kama Mjumbe kwa sababu ya maradhi ausababu nyingine yoyote.​
Utaratibu katikavikao vyaMahakamaMaalum yaKatibaSheria ya 1984Na.15 ib.37​
128​
.-(1) Mahakama Maalum ya Katiba itafanya vikao vyakewakati ule tu kunapokuwa na shauri la kusikiliza, na itafanyavikao vyake mahali popote patakapoamuliwa kwa utaratibuutakaotumika kwa ajili ya mashauri yatakayosikilizwa naMahakama Maalum ya Katiba.(2) Kiwango cha kila kikao cha Mahakama Maalum yaKatiba ni wajumbe wote, na iwapo mjumbe yeyote atakuwahayupo au ikiwa kiti cha mjumbe yoyote kitakuwa wazi basiSerikali iliyomteua mjumbe huyo ambaye hayupo au ambaye kitichake ki wazi itamteua mjumbe mwingine wa kushika mahalipake. Mjumbe wa muda aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara hiindogo ataendelea kutekeleza kazi katika Mahakama Maalum yaKatiba mpaka mjumbe wa kawaida atakaporejea kazini au mpakamtu atakapoteuliwa kujaza nafasi iliyo wazi au mpaka shaurilitakapokwisha, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo litakalotokea mapema zaidi.(3) Kila suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama Maalum yaKatiba litaamuliwa kwa kufuata kauli ya theluthi mbili ya wajumebkutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutokaTanzania Zanzibar.(4) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwekamasharti kuhusu utaratibu wa uchaguzi wa Mwenyekiti waMahakama Maalum ya Katiba, utartibu wa kupeleka shauri mbeleya Mahakama hiyo, utaratibu wa kuendesha shauri katikaMahakama na utaratibu wa kuwasilisha Serikalini uamuzi waMahakama Maalum ya Katiba:Isipokuwa kwamba iwapo shauri lolote litafikishwa mbele yaMahakama Maalum ya Katiba wakati hakuna sheria yoyote yaaina iliyoelezwa katika ibara hii ndogo, basi shauri litasikilizwa nakuamuliwa kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na Mahakamayenyewe kabla ya kuanza kusikiliza shauri, au iwapo Wajumbewa Mahakama watashindwa kukubaliana juu ya utaratibu huo,basi shauri litasikilizwa na kuamuliwa kwa kufuata utaratibuutakaoamuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwakushirikiana na Serikali ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
91​
SURA YA SITASEHEMU YA KWANZATUME YA HAKI ZA BINADAMUNA UTAWALA BORA​
Tume ya Hakiza Binadamu naUtawala BoraSheria ya 2000Na.3 ib.17​
129​
.-(1) Kutakuwa na Tume itakayoitwa Tume ya Haki zaBinadamu na Utawala Bora, ambayo majukumu yake yatakuwakama ilivyoelezwa katika ibara ya 130 ya Katiba hii.(2) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora itakuwa naMakamishna wafuatao:(a) Mwenyekiti, ambaye atakuwa ni mtu mwenye sifa yakuweza kuteuliwa kuwa Jaji;(b) Makamu Mwenyekiti, ambaye atateuliwa kwakuzingatia kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtuanayetoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano,yeye atakuwa ni mtu wa kutoka upande mwingine waJamhuri ya Muungano;(c) Makamishna wengine wasiozidi watanowatakaoteuliwa kutoka miongoni mwa watu wenyeujuzi, uzoefu na upeo mkubwa katika mambo ya hakiza binadamu, sheria, utawala, siasa au mambo yajamii;(d) Makamishna Wasaidizi.(3) Makamishna na Makamishna Wasaidizi wote watateuliwana Rais baada ya kushauriana na Kamati ya Uteuzi.(4) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi kwa madhumuni ya ibarahii ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao:(a) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani;(b) Spika wa Bunge;(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar;(d) Spika wa Baraza la Wawakilishi; na(e) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambayeatakuwa ndiye Katibu wa Kamati hii.(5) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishnawengine wote kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindicha miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kinginekimoja tu cha miaka mitatu.(6) Kwa madhumuni ya kuwakinga Makamishna kutokana namigongano ya kimasilahi, mtu yeyote akiteuliwa kuwa Kamishnawa Tume atalazimika kuacha mara moja madaraka yoyote katikachama chochote cha siasa au madaraka ya aina nyingine yoyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
92​
itakayotajwa kwa ajili hiyo na sheria iliyotungwa na Bunge.(7) Kamishna au Kamishna Msaidizi wa Tume aweza tukuondolewa katika madaraka ya kazi yake katika Tume kwasababu ya kushindwa kutekeleza kazi yake, ama kutokana namaradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabiambaya inayoathiri maadili ya kazi ya Kamishna.(8) Tume yaweza kutekeleza shughuli zake bila ya kujalikwamba kuna nafasi iliyo wazi miongoni mwa viti vya wajumbeau kwamba mjumbe mmojawapo hayupo.​
Majukumu yaTume nataratibuza utekelezajiSheria ya 2000Na.3 ib.17​
130​
.-(1) Tume ya Haki na Utawala Bora itatekelezamajukumu yafuatayo:(a) kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu nawajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria zanchi;(b) kufanya shughuli za kupokea malalamiko ya uvunjajiwa haki za binadamu kwa jumla;(c) kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusuuvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingiya utawala bora.(d) kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwaumma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;(e) kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ilikuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu aukurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wahaki za binadamu, au ukiukwaji wa misingi ya utawalabora;(f) kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusikaau taasisi yoyote inayohusika na masharti ya ibara hiikatika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kaziau majukumu yake au utekelezaji unaokiukamadaraka hayo;(g) kutoa ushauri kwa Serikali na vyomno vingine vyaumma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki zabinadamu na utawala bora;(h) kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza nakuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watuna taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbeleya Tume.(2) Tume itakuwa ni idara inayojitegemea, na bila ya kuathirimasharti meingine ya ibara hii, katika kutekeleza madaraka yakekwa mujibu wa Katiba hii, Tume haitalazimika kufuata maagizoau amri ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali au maoni yachama chochote cha siasa au ya taasisi nyingine yoyote yaumma au ya sekta ya binafsi.(3) Masharti ya ibara ndogo ya (2) yasihesabiwe kuwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
93​
yanamzuia Rais kutoa maagizo au amri kwa Tume, wala hayatoiHaki kwa Tume kutofuata maagizo au amri, endapo Rais ataonakuwa, kuhusiana na jambo lolote au hali yoyote, masilahi ya taifayahitajia hivyo.(4) Tume itafanya uchunguzi kwa kufuata masharti ya ibarahii na masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, naitafanya uchunguzi juu ya mtu yeyote anayehusika au taasisiyoyote inayohusika kila itakapoagizwa na Rais kufanyauchunguzi; vilevile, isipokuwa kama Rais ameagiza Tumeisifanye uchunguzi, Tume yaweza kufanya uchunguzi wakatiwowote inapoona infaa kuchunguza mwenendo wa mtu yeyoteanayehusika, au taasisi yoyote inayohusika, na masharti ya ibarahii anayetuhumiwa au inayotuhumiwa kwa kukiuka madaraka yakazi yake, kutumia vibaya madaraka ya kazi yake au majukumuya taasisi hiyo au kwa uvunjaji wa haki za binadamu au misingiya utawala bora.(5) Tume haitakuwa na mamlaka yoyote, ama kwa mujibu wamasharti ya ibara hii au masharti ya sheria yoyote iliyotungwa naBunge kwa madhumuni ya sura hii ya Katiba hii ya kuchunguzauamuzi wa Jaji yeyote, Hakimu yeyote au wa Mahakama iwapouamuzi huo ameutoa katika kutekeleza madaraka ya kazi yake;vile vile Tume haitakuwa na mamlaka ya kuchunguza uamuziwowote uliotolewa na chombo chochote chenye asili yaMahakama kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria iwapo uamuzihuo umetolewa katika kutekeleza mamlaka yake.(6) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watumishi waSerikali ya Jamhuri ya Muungano na wale wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar, watumishi na viongozi wa vyama vyasiasa wanaoshughulikia mambo ya umma, wajumbe nawatumishi wa Tume zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano naza Serikali hizo, mashirika ya umma na vyombo vingine vyaumma au vya binafsi, kama ni kampuni, jumuiya, ushirika,wadhamini au muundo mwingine wowote, kadri itakavyoelezwakatika sheria iliyotungwa na Bunge; lakini masharti hayahayatatumika kwa Rais wala kwa Kiongozi wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar isipokuwa tu kwa kuzingatia masharti yaibara ya 46 ya Katiba hii au ibara ya 36 ya Katiba ya Zanzibar, ya1984.​
Mamlaka yaTume nautaratibu washughuli zakeSheria ya 2000Na.3 ib.17​
131​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii,Bunge laweza kutunga sheria kwa mujibu wa masharti ya Surahii ya Katiba hii kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mamlaka yaTume, utaratibu wa kuendesha shughuli zake na kuhusu kinga zakisheria watakazokuwa nazo Makamishna na watumishi waTume kwa makusudi ya kuwawezesha kutekeleza kazi zao bila
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
94​
ya matatizo ya kisheria.(2) Tume haitachunguza mambo yafuatayo, kwa madhumuniya kutekeleza majukumu yake, yaani:(a) jambo lolote ambalo liko mbele ya Mahakama auchombo kinginecho cha kimahakama;(b) jambo lolote linalohusu uhusiano au mashirikiano katiya Serikali na Serikali ya nchi yoyote ya nje au Shirikala Kimataifa;(c) jambo linalohusu madaraka ya Rais kutoa msamaha;(d) jambo jingine lolote lililotajwa na sheria yoyote.(3) Kila mwaka wa fedha Tume itatayarisha na kuwasilishakwa Waziri anayesimamia haki za binadamu taarifa kuhusu-(a) shughuli za Tume katika mwaka uliotangulia;(b) hali ya utekelezaji wa hifadhi ya haki za binadamukatika Jamhuri ya Muungano,Na Waziri atawasilisha mbele ya Bunge kila taarifailiyowasilishwa kwake na Tume mapema iwezekanavyo baada yakuipokea.(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3) hayatahesabiwa kuwayanaizuia Tume kuwasilisha taarifa nyingine yoyote kwa mtumwingine au mamlaka nyingine yoyote.​
SEHEMU YA PILISEKRETARIETI YA MAADILI YAVIONGOZI WA UMMA​
Sekretarieti yaMaadiliSheria ya 1995Na.12 ib.18​
132​
.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi waUmma ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia namwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni yakuhakikisha kwamba masharti ya sheria ya Maadili ya Viongoziwa Umma yanazingatiwa ipasavyo.(2) Kwa madhumuni ya ibara hii, maana ya kiongozi waumma na masharti ya maadili ya viongozi wa umma itabidiifahamike kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Maadili yaViongozi wa Umma au masharti ya sheria nyingine yoyoteiliyotungwa na Bunge kwa kadri masharti hayo yanavyohusikana suala la uongozi na ufafanuzi wake.(3) Sekretarieti ya Maadili itakuwa na Kamishna wa Maadilina wafanya kazi wengine ambao idadi yao itatajwa na sheriailiyotungwa na Bunge.(4) Bunge litatunga Sheria itakayoainisha misingi ya Maadili
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
95​
ya Viongozi wa Umma itakayozingatiwa na watu wotewanaoshika nafasi za madaraka zitakazotajwa na Bunge.(5) Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma:(a) itafafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenyekushika nafasi hizo watahusika nayo;(b) itawataka watu wanaoshika nafasi fulani zamadaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmikuhusu mapato, rasilimali na madeni yao;(c) itapiga marufuku mienendo na tabia inayopelekeakiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea ausi muadilifu au inaelekea kukuza au kuchochearushwa katika shughuli za umma au inahatarishamaslahi au ustawi wa jamii;(d) itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunjamisingi ya maadili;(e) itaelekeza taratibu, madaraka na desturizitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili;(f) itaweka masharti mengine yoyote yanayofaa auambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza nakudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na uadilifukatika shughuli za umma na kwa ajili ya kulindafedha na mali nyinginezo za umma.(6) Bunge laweza kwa sheria kuweka masharti ya mtukufukuzwa au kuondolewa kazini kutokana na kuvunja maadiliya viongozi, bila ya kujali kama kazi hiyo ni ya kuchaguliwa nakuteuliwa.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
96​
SURA YA SABAMASHARTI KUHUSU FEDHA ZAJAMHURI YA MUUNGANOSEHEMU YA KWANZAMCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATOYA JAMHURI YA MUUNGANO​
Akaunti ya Fedhaya pamojaSheria ya 1984Na.15 ib.42​
133​
. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akautimaalum itakayoitwa "Akaunti ya Fedha ya Pamoja" na ambayoitakuwa ni sehehmu ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali yaJamhuri ya Muungano, ambamo kutawekwa fedha yoteitakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi kitakachoamuliwa naTume ya pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria iliyotungwa naBunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muunganokwa Mambo ya Muungano.
Tume ya pamojaya FedhaSheria ya 1984Na.15 ib.42​
134​
.-(1) Kutakuwa na Tume ya pamoja ya Fedha yenyewajumbe wasiozidi saba ambao watateuliwa na Rais kwamujibu wa ibara hii na masharti ya sheria iliyotungw na Bunge.(2) Majukumu ya Tume yatakuwa ni:(a) kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na,au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano,na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusumchango na mgawo wa kila mojawapo ya Serikalihizo;(b) kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli zafedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusianokatika mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili;(c) kutekeleza majukumu mengine ambayo Raisataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwamujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
97​
SEHEMU YA PILIMFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHAZA JAMHURI YA MUUNGANO​
Mfuko Mkuu waHazina yaSerikali yaJamhuri yaMuunganoSheria ya 1984Na.15 ib.​
135​
.-(1) Fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbalikwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,isipokuwa fedha za aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) yaibara hii, zitawekwa katika mfuko mmoja maalum ambao utaitwaMfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.(2) Fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu waHazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na Sheriakwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katikamfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.
Masharti yakutoa fedha zamatumizi kutokamfukoMkuu wa Hazinaya SerikaliSheria ya 1984Na.15 ib.43​
136​
.-(1) Fedha hazitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazinaya Serikali kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa mashartiyafuatayo:-(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayoyameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katikaMfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iweimetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote;(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayoyameidhinishwa ama na sheria ya Matumizi yaSerikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheriailiyotungwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 140ya Katiba hii.(2) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa serikali,ukiachilia mbali Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, hazitatolewakutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizihayo yawe yameidhinishwa na sheria.(3) Fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikalihazitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpakamatumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali na pia kwa sharti kwamba fedhahizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajilihiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
98​
Utaratibu wakuidhinishamatumizi yafedha zilizomokatika MfukoMkuu wa Hazinaya Serikali Sheriaya 1984 Na.15ib.43​
137​
.-(1) Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusikakwamba watengeneze na kuwasilisha kwenye Bunge katika kilamwaka wa fedha wa Serikali, makadirio ya mapato na matumiziya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kipindi chamwaka wa fedha unaofuata.(2) Baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya matumizi(mbali na matumizi ambayo yameidhinishwa ama na Katiba hiiau sheria nyingine yoyote kuwa yatokane na fedha zilizomokatika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali) kutawasilishwakwenye Bunge Muswada ambao utaitwa Muswada wa Sheria yaMatumizi ya fedha za Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumiziya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, na fedhahizo zitatolewa kulipa gharama za shughuli mbalimbali zaSerikali zinazohusika na makadirio hayo.(3) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekanakwamba:Fedha za matumizi zilizoidhinishwa na sheria yamatumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya shughuli fulanihazitoshi au kwamba imekuwa lazima kulipa gharama zashughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibuwa sheria; auKuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughulifulani kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumiziyaliyoidhinishwa na sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikalikuhusu shughuli hiyo au kwamba fedha zimetumiwa kulipiagharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizikwa mujibu wa Sheria, kutawasilishwa kwenye Bunge makadirioya matumizi ya nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo yamatumizi ya ziada, na baada ya Bunge kuyakubali hayoMakadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya matumizi yaziada, kutawasilishwa kwenye Bunge Muswada wa Sheria yaMatumizi ya fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumiziya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na fedhahizo zitatumiwa kulipia gharama za shughuli zinazohusika nahayo makadirio au maelezo.
Masharti yakutoza kodiSheria ya 1984Na.15 ib.43​
138.​
-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwakwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wautaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria nasheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
99​
(2) Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hiihayatalizuia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kutumia mamlakayake ya kutoza kodi ya aina yoyote kwa mujibu wa madaraka yaBaraza hilo.​
Utaratibu wakuidhinishamatumizi yafedha kabla yaSheria zaMatumizi kuanzakutumikaSheria ya 1984Na.15 ib.43​
139​
.-(1) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwekamasharti ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuuwa Hazina ya Serikali kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katikaibara ndogo ya (2) ya ibara hii.(2) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na Sheria yaMatumizi ya Fedha za Serikali inayohusika na mwaka huohaijaanza kutumika basi Rais aweza kuidhinisha fedha itolewekutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya kulipiagharama za lazima za shughuli za Serikali, na fedha hizozitatumiwa mpaka ipite miezi minne tangu mwanzo wa mwakawa fedha mpaka Sheria ya matumizi ya Fedha za Serikaliitakapoanza kutumika, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayolitakalotokea mapema zaidi.
Mfuko wamatumizi yadharuraSheria ya 1984Na.15 ib.43​
140​
.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuwekamasharti kuhusu mambo yafuatayo:(a) kuanzisha mfuko wa matumizi ya dharura nakumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Raiskwa ajili hiyo kuazima fedha kutoka mfuko huokulipia gharama za jambo la haraka na la dharuraambalo halikutazamiwa kutokea na ambalohalikupangiwa fedha zozote za matumizi; na(b) kumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Raiskwa ajili hiyo kutumia fedha zilizotengwa mahsusikwa ajili ya shughuli fulani kulipia gharama za jambola haraka na la dharura kama ilivyoele zwa katika ayaya (a) ya ibara hii ndogo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
100​
(2) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi yadharura au fedha zilitengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulanizimetumiwa kulipia gharama za jambo la haraka na la dharura,basi kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi yanyongeza, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio hayoMuswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikaliutakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili ya kuidhinishaMatumizi hayo ya nyongeza utahakikisha kwamba fedha zozotezilizoazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya dharurazitarudishwa kwenye Mfuko huo kutokana na fedha za matumiziyatakayoidhinishwa na Muswada huo.​
Deni la TaifaSheria ya 1984Na.15 ib.43​
141​
.-(1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mufko Mkuu waHazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara hii deni la Taifamaana yake ni deni lenyewe na pia faida inayolipwa juu ya denihilo, fedha zinazowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni pole polena gharama zote zinazoambatana na usimamizi wa deni hilo.
Mishahara yawatumishi fulaniwa Serikalikudhaminiwa naMfuko Mkuu waHazina yaSerikali Sheria ya1984 Na.15 ib.43​
142​
.-(1) Watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti yaibara hii watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwana sheria iliyotungwa na Bunge.(2) Fedha za malipo ya mishahara na posho za watumishiwa Serikali wanaohusika na masharti ya ibara hii pamoja nafedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo kwa walewanaostahili malipo hayo miongoni mwa watumishi haozitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusikana masharti ya ibara hii pamoja na masharti yake ya kazihavitabadilishwa, baada ya mtumishi huyo kuteuliwa, kwa jinsiambayo itapunguza masilahi ya mtumishi huyo, lakini maelezohaya hayahusiki na posho anayolipwa mtumishi huyo.(4) Iwapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti yaibara hii ana hiari ya kuchagua kima cha mshahara au aina yamasharti ya kazi, basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa mashartiya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii, mshahara wa kima hichoatakachochagua na aina hiyo ya masharti ya kaziatakayochagua vitahesabiwa kuwa vina masilahi zaidi kwakekuliko kima cha mshahara kingine chochote angalichowezakuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyoteangaliyoweza kuchagua.(5) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa Jaji wa Mahakamaya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
101​
Mwenyekiti na kila Mjumbe wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzina Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuriya Muungano.​
Mdhibiti naMkaguzi Mkuuwa Hesabu zaSerikali waJamhuri yaMuunganoSheria za 1979Na.14 ib.11Sheria ya 1984Na.15 ib.43​
143​
.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali wa Jamhuri ya Muungano.(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa najukumu juu ya mambo yafuatayo:(a) kuhakikisha kwamba fedha zozotezinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu waHazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwana kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti yaibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatoshekakwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo,basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumiziyake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomokatika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedhaambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheriailiyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumika,zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo husika namatumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayoyamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusumatumizi hayo; na(c) angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzina kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu zaSerikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabuzinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali yaJamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakamazote za Jamhuri ya Muungano na hesabuzinazosimamiwa na Katibu wa Bunge.(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na kila mtumishiwa Serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu, kumbukumbu,hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina yoyoteiliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwaRais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibarandogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Raisatawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenyekikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Raiskupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hichokabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwaSpika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki waziwakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
102​
kutekeleza shughuli za kazi yake) ambaye atawasilisha taarifahiyo kwenye Bunge.(5) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia najukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa namadaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwana sheria kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muunganoau hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za Mashirika.(6) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri aumaagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali,lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakamanayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kamaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madarakayake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.​
Kumwondoakazini Mdhibiti naMkaguzi Mkuuwa HesabuSheria ya 1984Na.15 ib.43Sheria ya 1995Na.12 ib.19​
144​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katikaibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri yaMuungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wamiaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheriailiyotungwa na Bunge.(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tukuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu yakushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi ausababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, aukwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi waUmma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kaziniMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa mashartiya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mamboyatakuwa ifuatavyo:(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa naMwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopunguawawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu yawajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watuambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji waMahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchiyoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoataarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote naitamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wamasharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
103​
kufanya kazi kutokana na maradhi au sababunyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibarandogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwakufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyoteau kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili yauchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais awezakumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wakumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilikaikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aualiyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezikuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingineyoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.(7) Mashartiya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyotealiyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.​
SURA YA NANEMADARAKA YA UMMA​
Serikali za MitaaSheria ya 1984Na.15 ib.50​
145​
.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katikakila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano,ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheriailiyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa,litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombovya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapatona utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
Kazi za Serikaliza Mitaa Sheriaya 1984 Na.15ib.20​
146​
.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa nikupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali zaMitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikishawananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wamaendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibarandogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwakuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
104​
shughuli zifuatazo -(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneolake;(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wawananchi; na(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumiademokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.​
SURA YA TISAMAJESHI YA ULINZI​
Marufuku kuundamajeshi ya Ulinziyasiyo majeshiya ulinzi yaUmma Sheria ya1984 Na.15 ib.49Sheria ya 1992Na.4 ib.36​
147​
.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote aukikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda aukuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibuwa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya ainambalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchiwa Tanzania.(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga nachama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na hakiya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yakeni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumukatika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshila Kujenga Taifa.
Madaraka yaAmiri Jeshi MkuuSheria ya 1984Na.15 ib.49​
148​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheriayoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Raisakiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchiyatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri yaMuungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katikahali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuuataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu awezakuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani aunje ya Tanzania.(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheriailiyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayoyatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi yaulinzi ya Jamhuri ya Muungano;(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga namajeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshiniwanajeshi;(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
105​
vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi; na(d) madaraka ya kumwamuru mwanajeshi yeyoteasitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa naambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi.(3) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyumecha amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (1) na (2) ya ibara hii litakuwabatilifu.​
SURA YA KUMI NA MOJAMENGINEYO​
Maelezo yamamboyanayohusika namadaraka yaKazi mbalimbalizilizoanzishwa naKatiba hiiSheria za 1980Na.1 ib.16; naSheria ya 1984Na.15 ib.52Sheria ya 1992Na.4 ib.37​
149​
.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyoteiliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, NaibuWaziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwamujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoataarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwakufuata masharti yafuatayo:(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliwa na mtummoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilishakwa mtu huyo aliyemteua au aliyemchagua, auiwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu,basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenyekikao hicho;(b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzuluataiwasilisha kwa Spika;(c) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika waBunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilishakwenye Bunge; na(d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo yakujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa mashartiya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulutangu siku ile ambayo taarifa yake ya kujiuzulu itakapopokelewana mtu anayehusika au kikao kinachohusika naitakapopokelewa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuipokea taarifahiyo na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, lakini kamataarifa hiyo ya kujiuzulu imeeleza kwamba mtu huyo atajiuzulutangu siku nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtuanayehusika au kikao kinachohusika, basi mtu huyoatahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku hiyo nyingine yabaadaye.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
106​
(3) Iwapo mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyoteiliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, NaibuWaziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwamujibu wa madaraka ya kazi yake) amejiuzulu, basi ikiwa anazosifa zote zinazohitajika na kwa kila hali anastahili, awezakuteuliwa au kuchaguliwa tena kushika madaraka ya kazi hiyokwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(4) Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (3) ya ibara hiihayatamzuia mtu ambaye ni Rais kuchaguliwa tena kuwa Raiswakati bado ameshika madaraka ya kazi ya Rais.​
Maelezo kuhusuutaratibu wakukabidhimadaraka ya kazikatika utumishiwa SerikaliSheria ya 1979Na.14 ib.12Sheria ya 1980Na.1 ib.16 naSheria ya 1984Na.15 ib.52​
150​
.-(1) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti yaKatiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazikatika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ifahamikekuwa mtu yeyote mwenye mamlaka, kwa mujibu wa Katiba hii,ya kumteua au kumchagua mtu mwingine kushika madaraka yakazi fulani anao pia uwezo wa kumteua au kumchagua kaimuau mtu ambaye atashikilia kwa muda na kutekeleza madarakaya kazi hiyo:Isipokuwa kwamba maelezo hayo hayatatumika kwamadaraka ya kazi ya Waziri, Naibu Waziri, Jaji wa Mahakamaya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu, Mjumbe wa Tume yaKudumu ya Uchunguzi au Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.(2) Kanuni zifuatazo zitatumika pia kwa madhumuni yaufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wakukabidhiana madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali yaJamhuri ya Muungano, yaani:(a) iwapo kuna mtu mwenye madaraka ya kazi fulanialiyokabidhiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina mtu huyo yupo likizoni na wakati huo huoanangojea kuacha kazi hiyo, basi anaweza kuteuliwamtu mwingine na kukabidhiwa madaraka ya kazihiyo, bila ya kujali kuwapo kwa yule mtuanayengojea kuacha kazi hiyo;(b) iwapo kuna watu wawili au zaidi ambao kwa wakatimmoja wote wanashika madaraka ya kazi fulanikutokana na uteuzi wao uliofanywa kwa mujibu waKanuni iliyoelezwa katikaaya ya (a) ya ibara hii ndogo, basi katika hali hiyokukitokea haja ya kutekeleza shughuli yoyoteinayohusika na madaraka ya kazi hiyo yule mtu wamwisho kuteuliwa ndiye atakayehesabiwa kuwa mtupekee mwenye dhamana ya kazi hiyo;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
107​
(c) iwapo mtu ameteuliwa, kwa mujibu wa masharti yaKatiba hii, kuwa kaimu au kushikilia madaraka yakazi fulani wakati mtu maalum aliyeteuliwa kushikamadaraka ya kazi hiyo anashindwa kutekelezashughuli zinazohusika na kazi hiyo, basihaitaruhusiwa kufanya uchunguzi wowote au kutoahoja yoyote juu ya uteuzi wa huyo kaimu eti kwasababu kwamba huyo mtu maalum aliyeteuliwakushika madaraka ya kazi hiyo anashindwakutelekeza shughuli zinazohusika na kazi hiyo.​
Ufafanuzi Sheriaya 1984 Na.15ib.52 na 53Sheria ya 1992Na.4 ib.38Sheria ya 2000Na.3 ib.19​
151​
.-(1) Katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitajivinginevyo: "amri ya Jeshi" maana yake ni sheria au amriiliyotolewa kwa mujibu wa sheria, ya kusimamia nidhamu katikajeshi;"askari" likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake nipamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri yajeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu;"Baraza la Wawakilishi" maana yake ni Baraza la Wawakilishi,la Zanzibar lililotajwa katika ibara ya 106 ya Katiba hii nalinalotekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hiina Katiba ya Zanzibar 1984;"Bunge" maana yake ni bunge la Jamhuri ya Muunganolililotajwa katika ibara ya 62 ya Katiba hii;
Sheria Na.5 yaMwaka 1992​
"Chama cha Siasa" maana yake ni chama cha Siasakilichoandikishwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria yaVyama vya Siasa, ya Mwaka 1992;"Idara ya Mahakama" maana yake ni kama ilivyofafanuliwakatika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 116 ya Katiba hii;"Idara ya Mahakama ya Zanzibar" maana yake ni Idara yaMahakama inayojumlisha mahakama zote ambazo ziko katikaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufanialiyetajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 115 yaKatiba hii ambaye ameteuliwa kwa mujibu wa mashartiya ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo ya 118 au iwapo JajiMkuu hayupo au anashindwa kutekeleza kazi zake kwasababu yoyote, Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa mujibuwa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hiyo ya 118ya Katiba hii, na kama Kaimu Jaji Mkuu naye hayupo auanashindwa kutekeleza kazi za Jaji Mkuu, Jaji waMahakama ya Rufani iliyepo kazini kwa wakati huo naambaye yuko kwenye daraja la juu zaidi la madarakakupita majaji wote wa Rufani waliopo;​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
108​
"Jaji Mkuu wa Zanzibar" maana yake ni Jaji Mkuu waMahakama Kuu ya Zanzibar ambaye, kwa mujibu waKatiba ya Zanzibar 1984, ndiye Mkuu wa Idara yaMahakama ya Zanzibar;"Jeshi" maana yake ni lolote kati ya majeshi ya ulinzi na nipamoja na jeshi lolote jingine lililoundwa na Katiba hii aukwa mujibu wa sheria na linalotawaliwa kwa amri yajeshi;​
Sura 512;​
"Jumuiya ya Madola" maana yake ni jumuiya ambayowanachama wake ni Jamhuri ya Muungano na kila nchiambayo inahusika na masharti ya ibara ya 7 ya Sheria yaUraia, ya mwaka 1961;"kiapo" maana yake itabidi ifahamike kwa maana ya kawaida yaneno hilo na ni pamoja na tamko rasmi la namna yoyotelinaloruhusiwa kisheria kutumiwa badala ya kiapo;"kiapo cha uaminifu" maana yake ni kiapo cha kuwa mwaminifukwa nchi na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;"Maadili ya Kazi ya Jaji" maana yake ni masharti ya kimaadiliyanayoongoza mwenendo wa watu wafanyao kazi ya Jajiau ya Hakimu;"madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano" maana yake itabidi ifahamike kwa mujibu wamaana ya kawaida ya maneno hayo na ni pamoja nautumishi katika Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri yaMuungano na katika Jeshi la Polisi au jeshi linginelolililoundwa kwa mujibu wa Sheria;"mahakama" maana yake ni mahakama yoyote yenye mamlakakatika Jamhuri ya Muungano isipokuwa mahakamailiyoundwa kwa amri ya jeshi; lakini kwa ajili ya ibara ya13, ya 14 na ya 15 za Katiba hii, itakuwa ni pamoja namahakama iliyoundwa kwa amri ya jeshi."Mahakama Kuu" maana yake ni Mahakama Kuu ya Jamhuri yaMuungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar;"Mambo ya Muungano" maana yake ni mambo yote ya ummaambayo yametajwa na ibara ya 4 ya Katiba hii kuwa niMambo ya Muungano;"Mamlaka ya Nchi" ni pamoja na Serikali na Bunge la Jamhuriya Muungano, pamoja na Serikali na Baraza laWawakilishi la Zanzibar;"Mwanasheria Mkuu" maaana yake ni Mwanasheria mkuu waSerikali ya Jamhuri ya Muungano aliyetajwa katika ibaraya 59;"Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri yaMuungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar auHalmashauri ya Wilaya au ya Mji, na pia mtu yeyote​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
109​
anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niabaya Serikali au Halmashauri;"Serikali za Mitaa" maana yake ni vyombo vya kiserikalivilvyoundwa kwa mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba hiikwa madhumuni ya kutekeleza madaraka ya umma;"Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri yaMuungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri yaTanganyika;"Tanzania Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri yaMuungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri yawatu wa Zanzibar na ambalo kabla ya Sheria hiikutungwa liliitwa Tanzania Visiwani;"Uchaguzi Mkuu" au "uchaguzi unaofanywa na wananchi"maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi waWabunge wanaowakilisha wilaya za uchaguziunaaofanywa baada ya Bunge kuvunjwa;"Ujamaa" au "Ujamaa na Kujitegemea" maana yake ni misingiya maisha ya jamii ya kujenga Taifa linalozingatiademokrasia, kujitegemea, uhuru, haki, usawam udugu naumoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano;"Waziri" maana yake ni Mbunge aliyekabidhiwa madaraka yakazi ya Waziri, isipokuwa Naibu Waziri, na maana hiyoitatumika pia kwa Makamu wote wa Rais;"Zanzibar" maana yake ni sawa na maana ya TanzaniaZanzibar.(2) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa madhumuni yaufafanuzi wa masharti ya Katiba, yaani -(a) kila yanapotajwa madaraka ya Rais, ifahamike kuwamdaraka yanayohusika ni pamoja na mamlaka yakutekeleza shughuli za kazi mbalimbali na vile vilewajibu wa kutekeleza shughuli na kazi mbali malikama Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, napia mamlaka mengine kama hayo au wajibumwingine kama huo ikiwa imeelezwa katika Katibahii au katika sheria nyingine yoyote kwambamamlaka hayo mengine ni ya Rais au kwambawajibu huo mwingine ni wa Rais;(b) kila yanapotajwa madaraka ya kazi katika utumishiwa Serikali, ifahamike kuwa kazi inayohusika ni kazikatika Utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Munganoisipokuwa kama imeelezwa vingine, na kilainapotajwa Idara ya Serikali ifahamike kuwa idarainayohusika ni idara ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano, isipokuwa kama imeelezwa vingine;(c) iwapo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kunajambo lolote linalotakiwa litekelezwe aulishughulikiwe na chama chochote cha siasa, basi,​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
110​
lishughulikiwe na chama chochote cha siasa, basi,jambo hilo litatekelezwa au litashughulikiwa nachama hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa nachama hicho kwa ajili hiyo, na pia kwa kuzingatiamasharti ya Katiba hii au Sheria yoyote iliyotungwana Bunge kwa ajili hiyo;(d) kwa madhumuni ya Katiba hii, mtu hatahesabiwakuwa ana madaraka ya kazi katika utumishi waSerikali ya Jamhuri ya Muungano kwa sababu tukwamba anapokea malipo ya uzeeni au malipomengine ya aina hiyo kwa ajili ya utumishi wake wazamani katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano aukatika Serikali yoyote ya zamani ya Tanzania Baraau katika Jeshi la Ulinzi au la Polisi la Serikali yaJamhuri ya Muungano au Serikali ya zamani yaTanzania Bara au ya Zanzibar;(e) katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji vingine,kila anapotajwa mtu mwenye dhamana ya kazi fulanikwa kutaja madaraka ya kazi yake, ifahamike kuwamtu anayehusika ni pamoja na mtu yeyote ambaye niKaimu au aliyeteuliwa kwa njia ya halali kushikiliadhamana ya kazi hiyo;(f) katika Katiba hii, kila yalipotajwa mamlaka yakumwondoa mtu katika madaraka ya kazi katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,ifahamike kuwa mamlaka yanayohusika ni pamoja namamlaka yaliyotolewa kwa mujibu wa masharti yaSheria yoyote yanayomtaka mtu huyo auyanayomruhusu mtu huyo kustaafu:Isipokuwa kwamba maelezo ya Kanuni hiiyasifahamike kuwa yanampa mtu yeyote mamlaka yakumtaka Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji waMahakama Kuu au Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuastaafu;(g) katika Katiba hii, kila ilipotajwa sheria ambayoinabadilisha au kufuta sheria nyingine, ifahamikekuwa sheria inayohusika ni pamoja na sheriaambayo inarekebisha sheria hiyo nyingine auambayo inaendeleza kutumika kwa hiyo sherianyingine, ama bila mabadiliko au baada yakubadilishwa au kurekebishwa; au sheria ambayoinaweka masharti mapya katika sheria nyingine.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
111​
Jina kamili laKatiba tarehe yakuanza kutumikana matumizi yaKatiba hii.Sheria ya 1985Na.15 ib.52​
152​
.-(1) Jina kamili la Katiba ya Jamhuri ya Muugano waTanzania, ya mwaka 1977.(2) Katiba hii itaanza kutumika tarehe 26 Aprili, 1977.(3) Katiba hii itatumika Tanzania Bara na vile vileTanzania Visiwani.
_________NYONGEZA YA KWANZA_________(Imetajwa katika ibara ya 4)Mambo ya Muungano​
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.2. Mambo ya Nchi za Nje.3. Ulinzi na Usalama.4. Polisi.5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.6. Uraia.7. Uhamiaji.8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwanchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta nasimu.12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili yamalipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamojamabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za kigeni.13.Leseni ya viwanda na takwimu.14.Elimu ya juu.15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa yamotokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo zamafuta au bidhaa, na gesi asilia.16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yoteyanayohusika na kazi za Baraza hilo.17.Usafiri na usafirishaji wa anga.18.Utafiti.19.Utafiti wa hali ya hewa.20.Takwimu.21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengineyanayohusiana navyo.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
112​
__________NYONGEZA YA PILI___________ORODHA YA KWANZA(Imetajwa katika ibara ya 98 (1)(a))(​
Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono naheluthi mbili ya Wabunge wote).
Sura ya 500,Sheria yakluthibitishaTanganyikakuwa Jamhuriya mwaka 1962​
Ibara ya 3, 17,18, 23 na 26​
Sura ya 508,Sheria yaUtumishi katikaIdara yaMahakama yamwaka 1962​
Ibara ya 22, 23, na 24​
Sura ya 509,Sheria yaUtumishiSerikalini yamwaka 1962​
Ibara ya 22, 23, na 24.​
Sura ya 512,Sheria ya Uraia,ya mwaka 1961​
Sheria yote​
Sura ya 557,Sheria yaKuthibitishaMapatano yaMuungano waTanganyika naZanzibar yamwaka 1964​
Sheria yote.​
ORODHA YA PILI(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b))​
Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono natheluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthimbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.7. Orodha ya Mambo ya Muungano.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_________________________________________________________________​
113​
8. Idadi ya Wabunge kutoka Zanzibar.




TUIJADILI, TUIREKEBISHE?TUIBADILISHE?​
_____________
 
Back
Top Bottom