Madhara ya ukeketaji ni kweli au exaggeration?

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Nafuatilia kipindi Star TV - mwanasheria anahojiana na mtangazaji kuhush madhara ya ukeketaji, nashangaa kusikia kumbe sheria haikatazi mwanamke mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kukeketwa!

Mie nilizaliwa katika kijiji ambacho ukeketaji ulikuwepo kwa kiwango cha kutosha, na sidhani kama kuna mama mtu mzima hata mmoja alikwepo ambaye hakukeketwa wakati huo, lakini madhara wanayoyataja kwa mfano mwanamke kushindwa/kujifungua kwa operesheni kwa sababu viungo vya uzazi kushindwa kutanuka, sijawahi kushuhudia wala kusikia pale kijijini kwamba kuna mama kajifungua kwa operesheni mida hiyo nikiwa naishi huko! Na cha ajabu watu vijijini unakuta mama amezaa watoto 11, 12, 13 nyakati hizo!

Swala la ukeketaji lipo pia nchi za ulaya, asia hata Marekani, kuna siri gani kuhusu hili swala?

Swali langu ni je, haya madhara yanayosemwa ni ya kweli kwa kiasi hicho? Kama ni ya kweli inakuwaje wamama wa zamani hawakukumbana nayo? Halafu inakuwaje kuna wanawake wanapata matatizo wakati wa kujifungua hadi kufanyiwa operesheni hali hawajakeketwa hasa Dar?

Bado madai kwamba hawana hisia za kimapenzi! Mbona kuna wanawake naowajua wamekeketwa lakini chupi zao wameshika mkononi?
 
Mkuu LifeHacker hakuna exaggeration katika madhara ya kukeketwa kwa wanawake na hii ni kwa sababu sehemu inayotolewa wakati wa kukeketwa kwa mwanamke haikudizainiwa itolewe kama sehemu ya wanaume inavyotolewa bali ikae hapo hapo kwa makusudi yake maalum.


kuhusu hisia za mapenzi,kwa mwanamke sehemu inayotolewa wakati wa kukukeketwa ndiyo hasa sehemu inayompa msisimko wa kufanya mapenzi na hivyo ikondolewa hakuna tena hisia kama hizo,swala hilo lipo wazi sana kwani hasa ndiyo chanzo cha wanawake kufanyiwa tohara katika maeneno mbali mbali kwa kigezo cha kuepusha uhuni kwa wanawake au kudumisha uaminifu wa wanawake kwenye ndoa zao.
 
Last edited by a moderator:

Kuhusu hisia inakuwaje ukimkuta mwanamke amekeketwa lakini ny.ege zake ni juujuu? Kama nilivyoeleza kwa nini madhara hayo kwa mama zetu hayakuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…