Madhara ya michoro mwilini (Tattoo)

Madhara ya michoro mwilini (Tattoo)

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
1578916527793.png

Japo michoro ya mwilini(Tattoo) ni kitu kinachopendwa na watu wengi. Asilimia 40 ya vijana wana michoro hiyo mwilini walau picha moja

Hatua zenyewe za uchoraji kwanza huhitaji sindano ambayo kimsingi huiumiza ngozi ili kuweka michoro, sindano huweka matone ya rangi. Kama ngozi itapona vizuri ndio huacha mchoro mzuri kwenye ngozi ambayo huwa urembo

Madhara ya tattoo ni haya yafuatayo

1. Unaweza kukosa fursa mbalimbali
Mfano katika mashindano ya ulimbwende hayaruhusu mtu mwenye tattoo inayoonekana kushiriki katika kinyang’anyiro hicho.
Suala hilo liliwahi kudhihirika kwa Rachel George ambaye alikuwa akishiriki mashindano hayo ngazi ya wilaya jijini Dar es Salam. “Ilibaki kidogo nitolewe lakini nikawahi kuifuta na kwa sababu haikuwa kubwa sana kovu halikuleta shida na rangi ya ngozi yangu nyeusi ilisaidia katika kuficha uangavu wa kovu lile,”

Vijana wanaoiga kuchora tattoo za maisha wamekuwa wakikosa fursa walizozitamani na wengine wamekuwa wakiponea chupuchupu

Mh. Temba, alifanya kila awezalo na kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya jeshi zaidi ya mara tatu, na mara zote alifanikiwa kuhitimu mafunzo, lakini mara nyingine kabla hajakabidhiwa ajira anajikuta anaachishwa au anaacha na kisha anarudia tena mafunzo

2. Maambukizi ya ngozi
Namna nzima ya kuchora michoro hiyo huipa michubuko ngozi yako, ambayo huimuzi tabaka la juu na la kati la ngozi.
Mtu huwa katika hatari ya kupata maambukizi kwa wiki mbili za mwanzo baada ya kujichora. Dalili zake huwa ni pamoja na wekundu kwenye ngozi, kuwashwa, au kutoa usaha.

Maambukizi hayo yakiendelea yanaweza kusababisha homa. Mara nyingi maambukizi hayo huwa sugu

3. Kuwa na aleji/mzio
Watu wengine huanza kuwa na aleji mara baada ya kujichora. Hii huhusianishwa sana na wino uliotumika kuchora, haswa kama wino ukiwa na plastiki. Mayo clinic wanasema rangi nyeundu, njano, buluu na kijanii huwa na uwezekano mkubwa wa kutengeneza aleji kwa aliyejichora

Madhara ya aleji huweza kutokea miaka kadhaa baada ya kujichora.

4. Matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI
Ikitokea daktari akisema inabidi kufanyiwa MRI Scan, mara nyingi tatuu huwa kikwazo. Na pia huvimbana kuwasha kisha kupotea yenyewe

Hatari huongezeka kama umetumia wino wa ubora wa chini au kama michoro ni ya muda mrefu

5. Saratani ya ngozi
Kwa kiasi kikubwa saratani ya ngozi inaweza kusababishwa na michoro hii na magnjwa mengine yanayohusika na ngozi. Kwa sababu unapotoboa layer ya juu ya ngozi ya binadamui na kuweka wino wenye kemikali huweza kuleta madhara tofauri kati ya mtu mmoja na mwingine.

6. Kushindwa kuchangia damu
Mtu mwenye michoro mwili hawezi kuchangia damu hata kama kundi la damu yake linafanana na mgonjwa, hali hii itafanya kupeteza watu ikiwa kuna mgonjwa anayehitaji damu kwa haraka

Watu waliochora tattoo hukosa pia fursa ya kuchangia damu hata ikiwa ni kwa dharula hiyo ni kutokana na uwepo wa hatari ya kusambaza ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine,

======
Maoni ya wachangiaji

Kwa mtu wa Tanzania kutofahamu Tattoo ni kitu gani, ni kitu cha Kawaida sana .Kwa maana Tattoo wengi tunaziona kwa Watu maarufu ambao wengi wana maisha ya ajabu ajabu kama ya ha Wakina Irene

Lakini mtoa mada na wadau wengine nataka kukwambia kuwa Tattoo ni kitu muhimu sana kwa jamii tena za kiafrika kwani Tattoo ilikuwepo hata kabla ya Ukoloni.

Na Tattoo wakati huo hazikupakwa kama sehemu ya Urembo hapana, na haikuwa kwa ajili ya Watu maarufu pia.

Wakat huo tattoo ilikuwa ni kwa jamii nzima na ilikuwa ni sehemu ya Utamaduni. Kupitia Tattoo watu waliweza kuwasiliana na kupeana Utambulisho kwa mfano Kabila la Wamakonde

Lakini pia ukija huko Amerika hasa kwa Hao Watu weusi Tattoo zilikuwa sehemu ya Harakati za Ukombozi. Kwani ilikuwa kazi ngumu kusimama hadharani na kudai uhuru mbele ya Watu weupe uko Amerika.

Hivyo kupitia Tattoo watu walijichora na kuwalilisha Ujumbe kadri wawezavyo bila watu wengine kujua.

Hivyo ni asilimia kubwa sana ukiwa USA ukikutana na Watu wamechor tattoo watakwambia sababu za kuchora, na sababu zao zinafungamana na historia halisi ya maisha aidha ya mtu mmoja au ya jamii nzima. Na ndio maana huko unakuta mtu kachora Tattoo ya Rosa Park.

Lakini huku kwetu kwa kuwa tunaiga kupitia Video na kuona tu Wanawake wanaovaa vichupi na wanaume ambao ni Wasanii. Hudhani kuwa Tattoo ni kitu cha Starehe na hivyo ni kinyume na Dini zetu wa hapa Afrika.

Hapo hapo kuna mtu ambaye pengine yeye ni Mwislamu bado haelewi Tattoo ni kitu gani wakati huo huo kuna Wanamke kavaa ijabu na bado kapaka Ina. Ambayo kimsingi ni michiro ile ile na rangi ni zile zile. Na ina dhamira sawa na waliochora Tattoo.

️Hoja zangu hizi zinasimama kwa watu wanaoamini kuwa Tattoo ni Dhambi na wale wanadhani Tattoo ni Uhuni pia. Kwani kuna Watu wana Tattoo za Yesu, nao tunawaweka kwenye kundi gani??

Dhambi ya tattoo ni ipi? Kile ulichochora au tabia zako baada ya kuchora?

Leo hii Lil Wayne wa Cash Money akija Tanzania na kutaka kutoa ufadhiri wa ujenzi wa kanisa, kuna watu watamkataza kisa ana Tattoo mwilini?

Ni kweli kuna madhara yake lakini jamii pia lazima ifahami Tattoo ni kitu gani na sio tu kuwa majibu ya Kidini dini bila kujua historia kamili.
View attachment 1322625
 
Mi tattoo hua naona kama uchafu fulani mwilini. Yaani fikiria eti unakuta binti mweupee ana ngozi yake nyororo kabisa paja limenona halafu anaenda kuchora litattoo la maua maua hapo kwenye paja na kufanya ule uzuri wote usionekane tena! Sasa hapo ndio unakua umefanya nini..?
 
21356e4d-462c-4da3-bb85-4e8535e30c16.jpg
 
ANCIENT FROM EGYPT, Hommie umetapika sana kidogo umeweza kuweka sawa kwenye hili kimtazamo wangu nachojua kidogo kwenye tattoo ni kumbukumbu yakitu fulani mtu anaiweka kwenye mwili mfano Wayne zile tattoos ni kumbukumbu za vitu vyake sasa sijui hao wanaochora nao ni kwajili ya kumbukumbu pia.
 
Huu ni ukweli halisi kuna watu wanajua ibada zake hata kwenye biashara michezo muziki nk wanafanikiwa lkn wanaochora kwa kufuata mkumbo kwa kuwa hawajui kuwa zile alama ni uwakilishi wa miungu huwa wanakwama sana
7. Kuingiliwa na mapepo
Michoro mingi inawakilisha kazi za ulimwengu wa giza na wengi au wote wenye tatoo wana pepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hommie umetapika sana kidogo umeweza kuweka sawa kwenye hili kimtazamo wangu nachojua kidogo kwenye tattoo ni kumbukumbu yakitu fulani mtu anaiweka kwenye mwili mfano Wayne zile tattoos ni kumbukumbu za vitu vyake sasa sijui hao wanaochora nao ni kwajili ya kumbukumbu pia.

Ndio maana nakwambia kuwa tulio wengi hapa Tanzania hatufahamu mengi juu ya Tattoo na wengi huchora tu bila kuwa na sababu.

Ukikutana na Mdada wa Buza huko ukamuuliza sababu ya Tattoo yake utakupq jibu la jumla kuwa urembo tu.

Japo wapo wachache watakwambia sababu za wao kuchora.

Mimi ni mwalimu nafundisha shule fulani katika nchi fulani hapa barani Afrika. Ni mwalimu wa Historia na hapa shuleni nafundisha Mada za Black American History pamoja na Pure African History. Mwilini mwangu nina Tattoo Nane.

1. Ramani ya Afrika
2. Mwalimu nyerere
3. Olauda Equano
4. King Haile S.
5. Nelson Mandera
6. Neno la Ubuntu
7. Rosa Park
8. Neno history

So ndugu natamani nikueleze mengi kuhusu Tattoo lets me end here.
 
EP PRO,

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]

" jambo lolote lenye kumuhusu binadamu na ukakuta wanadamu wanajadili gafla akatokea mtu akaingia Nguvu za Mungu, basi hapo ndio ukomo wa binadamu kufikiri"

Sasa ndugu hapa tunajadili masuala ya Tattoo kwa mitazamo ya kawaida na sio ya Kishirikina. Unaposema chale maana yake unaingiza mambo mengine hasa ya Uchawi.

Kuna tofauti za kimatumizi na dhamira kati ya Tattoo na Chale.
Usichanganye mambo
 
Mi tattoo hua naona kama uchafu fulani mwilini. Yaani fikiria eti unakuta binti mweupee ana ngozi yake nyororo kabisa paja limenona halafu anaenda kuchora litattoo la maua maua hapo kwenye paja na kufanya ule uzuri wote usionekane tena! Sasa hapo ndio unakua umefanya nini..?
Kiukweli awe mwanamke au mwanaume nikiashakuona una tattoo tu nakushusha thamani ni mhuni fulani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kupotosha chale ndio tattoo na Mungu hapendi huo ujinga na amekwisha weka tahadhari

Hata uandike vipi kwa akili/hekima za kibinadamu ila ni kinyume na Mungu pamoja na kuwa zilitumiwa enzi na enzi haikupi uhalali wa kujichora leo wewe uliyepewa maarifa zaidi ya wale
" jambo lolote lenye kumuhusu binadamu na ukakuta wanadamu wanajadili gafla akatokea mtu akaingia Nguvu za Mungu, basi hapo ndio ukomo wa binadamu kufikiri"

Sasa ndugu hapa tunajadili masuala ya Tattoo kwa mitazamo ya kawaida na sio ya Kishirikina. Unaposema chale maana yake unaingiza mambo mengine hasa ya Uchawi.

Kuna tofauti za kimatumizi na dhamira kati ya Tattoo na Chale.
Usichanganye mambo
 
Mkuu naona umetaja hina na chale ndo tatoo acha ujinga bana zile chale sio tatoo wala hina sio tatoo wala hawatumii wino kufanya hayo mambo Hinna ni asili na nimti majani yake ndo yanatumika wala haina madhara nayanatoka kirahisi mwilini hata mwezi haupiti na yanatumika kwenye mafuta pia.

Lakini wino wa tatoo umejaa titanium dioxide, iron oxide, carbon na mazonge mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom