Mamboz wana jf!, bila mko poa.
Ni swala ambalo huwa najiuliza mara kwa mara je kuna ka ukweli ndani yake. (kuvuka stage namaanisha kutofanya mambo yale ambayo foolish age wengi wakiyafanya).
Dhana iko kwa me zaidi
Iko hivi, mara kwa mara tangu nasoma utasikia mtu akifanya jambo lisilo la kawaida kwa jamii husika utasikia ndo madhara ya kuvuka stage mwingine utasikia anasema ngoja niwe totoz(wapenzi) sahivi baadaye nikioa nitatulia, ukiona babu anahangaika na vitoto ati alivuka stage, professor/lecturer/mwalimu amempa denti mimba ati ndo wakati wa ujana ati alikuwa bize na kusoma tu. je wadau hapo kuna ka ukweli?, na kama kuna ka ukweli nini kifanyike, ndo kusema tuacha waendelee ili wasivuke stage?
Mtakubaliana nami kuwa kizazi cha sasa (doti.com) ndo naweza kusema kinaongoza kwa watoto/Vijana kuanza mambo mapema kuliko vijana wa miaka ya 80's ikiwemo mapenzi na kadhalika ndo tusema baadaye hatutashuhudia kupungua kama si kuisha kabisa matukio ya wababu/wabibi kutembea na wajukuu wao kwa kigezo cha kutovuka stage?
maoni yako mdau we wasemaje,
Karibuni!!!!