sambeke
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 713
- 652
Ulishawahi kujiuliza kaanini Nchi za Kiafrika kwa maana ya viongozi pamoja na watu wake wengi wamegubikwa na ubinafsi, uchoyo na ubaya uliokithiri dhidi ya waafrika we wenzao?
Lipo jambo moja ambalo nataka sote tulitafakari kama sehemu ya tafakuri zetu za mchana labda tutaweza kuona sababu na hivyo kutufanya kuwa chachu ya mabadiliko!
1. Kwanza kabisa Historia ya Bara la Afrika imepotezwa! Kwa kupachikwa historia ya uwongo au sehemu nyingine kuachwa kama hakuna chochote cha kuongelea kuhusu eneo hilo na hivyo kufanya kama vile hakuna lolote lililowahi kutokea mahali hapo!
Sasa hii madhara yake ni nini? Madhara yake ni kwamba pale mtu anapokupndolea historia yako anakupoteza (He makes you NO BODY) kwa sababu historia inakuthibitisha (History makes you SOMEBODY)
utaniuliza kivipi?
Nitatoa mfano:- Moja ya sifa kubwa ambayo watu hujivunia ni pamoja na UKOO anaotoka! (Clan) zipo koo zinazotokana na #UCHIFU, #MSHILI = :kwa wenzetu kule Meru" #MANGI = kwa wachaga n.k! Na sababu kuu ya jina la ukoo kuwa la Muhimu ni kwasababu lenyewe ndilo linalobeba Historia yako! Jina la ukoo ndilo linalobeba #thamani yako! Na thamani hii huimarishwa na #historia ya ukoo wenyewe! Bila historia leo hii tusingekua na heshima tunayojivunia katika familia zetu!
Sasa nini kilifanyika? Walipokuja wazungu kututawala, walihakikisha kwanza wanatuondolea heshima yetu ambayo ni historia yetu na kutupandia historia yao! Wakatuondolea majina yetu ambayo yalikua na maana kuungana na historia zetu kila mmoja na kutubatiza kwa majina yao ambayo wengine hata maana zake hatujui! Haya yote yalifanikiwa kwa kupitia dini walizozileta hulu wakituogofya kwa jehanamu ijayo kama hatakubali kugeuzwa (converted) namnawaliyotaka wao na iliyowatukuza wao!
Kwa kuogopa jehanam tukakubali kupoteza utu wetu, historia yetu, imani yetu ya asili (natural) na kuanza kuishi maisha ya hofu na mashaka wakati wote na mwisho wake ni kufupisha uhai wa maisha! Sote tutakubaliana kwamba wazee wetu waliishi miaka mingi na moja ya siri ni kwamba waliishi maisha yasiyo na hofu za kupandikizwa wala pasipo na mashaka ya mambo ambayo kiuhalisia ni nadharia tu na wala sio chochote hivyo tukapoteza jinsi ya kuwaza, (reasoning) tukapoteza fahari yetu (our pride) na historia kwa jumla.
Haya yote yametuacha kuwa utupu; (NO BODY) leo hii angalia historia zinazofundishwa mashuleni! Zote zimejaa utukufu wa wakoloni kama vile nchi hizi hazikuwahi kukaliwa na watu kabla ya wakoloni hawa!
Dunia hii inasemekana imeishi miaka zaidi ya Mamilioni iliyopita! Lakini angalia historia ya nchi zetu yote inaanzia miaka sio zaidi ya mia mbili iliyopita na historia inayoenda mbali zaidi ya hapo inajaribu kufutwa kwa kutoizungumzia sana maana haijabeba fahari ya wakoloni bali ya mashujaa babu zetu waliokua watu wakuu sana na wenye kutukuka!
Tumefanywa sio kitu (NO BODY) Tumeondolewa uhalisia wetu na hivyo kujikuta tunaishi maisha yasiyo halisi (an artificial life) ambayo ni ya kuchanganya sana (very stressful) na hii kazi yake ni kutufupishia siku zetu za kuishi (life span) kwa ujumla!.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Imani kwa Mungu na #DINI, babu zetu walikua na imani kwa Mungu bila dini! Hawakufundishwa na mtu yeyote maana Mungu huishi ndani yetu na sisi ndani yake hivyo unapozaliwa unazaliwa na uungu ndani yako na huo ndio uliowaongoza babu zetu kuabudu! Walifanya ibada kwa Mungu asiyeonekana! (Invisible God) na huyo ndiye Mungu halisi! Mungu ambaye hakua na dini! Mungu ambaye hakua na sura! Hivyo kutufanya sote tujione wamoja bila kubaguana maana wote walijiona wanatoka kwa Mungu mmoja, asiyeonekana na asiye na sura!
Sasa walipokuja watawala hawa, wakatuletea mpaka sura ya Mungu!
Matokeo yake ni nini?Matokeo yake kukatokea kugaqanyika! wakatokea waliosema Mungu hana sura na wale waliokubali mafundisho ya Mungu mwenye sura na umbo fulani kwa hofu ya jehanam (ambayo uhalisia wake nao haupo) wakajitenga! Ndani ya waliojitenga nako kukawa na tofauti zilizopelekea kuwepo kwa msururu wa dini ambazo kila mmoja akijaribu kujiaminisha kwa Mungu mmoja ambaye mwanzo walimwabudu wote kwa pamoja!
Unaweza kuona athari za kuifuta historia ya jambo au ya mahali au ya nchi au ya Dunia kwa ujumla! Athari ni kubwa sana! Leo hii mwanadamu amekua kiumbe hatari sana kwa mwanadamu mwenzake na sababu ni moja tu! Amepotezewa kumbukumbu ya historia yake! Hakumbuki tena kama sote sisi tunatoka kwa mtu mmoja #MUNGU. Na kama ni hivyo sisi sote bila kujali rangi, Kabila, Utaifa, dini, na lugha, sisi sote tunatoka kwa mmoja. Na ndiyo maana pamoja na yote haya sisi sote tunao mwisho mmoja!! Kama tulikua hatuna mwanzo mmoja basi tusingekua na mwisho mmoja!
Turudi tulikoanguka tukaanze upya, naamini hatujachelewa, tupendane tukianza na familia zetu mpaka nchi na ulinwengu kwa ujumla. Hiyo ndiyo familia aloijenga Mungu! Kama vile ambavyo hakuna baba anaetaka familia yake ifarakane kadhalika Mungu anatutaka tuwe wamoja.
Waliotuletea dini hizi wao wameachana nazo! Lakini angalia walivyo na umoja! Wote wanapendana bila kujali nchi wanazotoka akimuona yeyote mwenye rangi kama yakwake humpa msaada na kumuhudumia kidugu bila kujali utaifa wake!
Sisi waafrika ni wakati wetu sasa kuamka! Tuondoe dhana ya ukoloni ndani yetu na tutambue sisi sote ni wamoja! Tunatoka kwa baba mmoja.
Jumapili njema kwenu nyote.
Sent using Jamii Forums mobile app