Madhara ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani

mbari

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
509
421
MADHARA YA KURUDIANA NA MPENZI WA ZAMANI:


Kwa kawaida watu walioishi kwenye mahusiano wanajua mazuri na mabaya waliyokutana nayo, wanajua kila aina ya changamoto walizopita..
Uzito wa mapenzi yao wanaujua wao.
Kuachana kwenye mahusiano ya kimapenzi ni jambo la kawaida lakini linaacha madhara makubwa ndani ya moyo wa mtu.

Kitendo cha kuachana na baadae kurudiana siyo kosa na ni hatua nzuri zaidi ya kujifunza mlipokuwa mmekosea.

Mpaka kufikia hatua ya kurudiana maana yake kuna mmojawapo ameleta hoja na nia ya kutaka kuurudisha uhusiano huo au kuna mtu amekuwa kiunganishi cha kutaka mrudiane,anaweza kuwa mtoto mliezaa au rafiki,ndugu au mchungaji...

Zipo sababu nyingi zinaweza kuwafanya mrudiane japo mlikuwa mmeachana muda mrefu..

Lakini kabla hujafanya maamzi hayo lazima ujiulize maswali yafuatayo:

1.Je, kwanini anataka mrudiane tena?
Ni vigumu sana kujua nia yake ya kutaka kurudiana,huenda kuna vitu alikuwa anapata kutoka kwako amevikosa huko alipokuwa amekimbilia,
Lakin pia huenda huko amepigwa chini ,au tabia za huyo alipokimbilia anaona bora ya zako,au kuna kitu anataka kulipa kisasi kwako au kukufanyia kibaya dhidi ya huyu ulienae ili umkose,au huenda kweli mwanzoni alipitiwa amekuja kwa nia ya dhati au kashauriwa na watu.
Yote haya ni ya kujiuliza na yanawezekana...

2. Je, ni kipi kilisababisha mwanzoni mkaachana?
Hili pia ni swali la msingi ili ufanye ulinganifu kama kweli ilikuwa sababu ya msingi kwake kukuacha. Mfano, kama alikuacha kwa kufumania SMS ya mapenzi kny simu yako, je, akija kuifumania tena kwa bahati mbaya na penyewe atakuacha?
Sababu iliyowaachanisha mwanzoni ifanyiwe ulinganifu .

3. Je, ni madhara gani yalikupata kipindi anakuacha?
Huenda kuna vitu mlikuwa mmefanya kwa maendeleo yenu hatimae vikasambaratika kwa sababu ya kuachana,uliumia,ulidhalilika,ulijutia muda wako uliopoteza nk..hayo yote yatazame...

4. Mlipoachana hapo kati kati amekutana na wangapi na kwann ameachana nao?
Kumbuka nae kama binadamu mlipoachana huenda aliingia kny mahusiano mapya..

Baada ya kujiuliza maswali yote hayo iruhusu akili yako ifanye maamzi yatakayofaa kwa usalama wa moyo wako...

MADHARA YAKE:

1. UAMINIFU KUPOTEA

Pamoja na kurudiana kwa ahadi nyingi na zenye mbwembwe za kila aina, ni vigumu kumwamini tena kama zamani kwa sababu ya kurudisha kumbu kumbu juu ya kile kilichowafanya muachane mwanzoni hasa pale mtakapokoseana tena.

2. KUPOTEZA HESHIMA YAKO.

Heshima yako inaweza kupotea au kushuka kwa yeye mwenyewe kukudharau na kukuona ulikosa soko ndo maana umekubali kurudiana nae..
Lakin pia jamii na wazaz wanaweza kukudharau na kukushushia heshima iwapo chanzo cha kuachana mwanzoni kilikuwa cha fedheha na walikijua.

3. KUUKARIBISHA UMASIKINI.

Huenda ulikuwa umefika hatua nzuri ya kimaendeleo ndo maana anataka mrudiane ili azitumie mali zako kupitia mlango wa kurudiana kimapenzi.
Kama alikuwa mwenye tamaa ya Mali ,amini utarudi kny umaskini wa kujitakia..

4. UWEZEKANO MKUBWA WA KUUMIZWA TENA.

Kutokana na sababu zake mwenyewe za kuamua kurudiana na wew,anaweza kukuumiza zaidi kwa sababu huenda hao aliokuwa nao kipindi mmeachana bado mapenzi yao yapo hai kwa hiyo kukuumiza kimapenzi tena inaweza kuwa rahisi kuliko hata mwanzo.

5. KUPOTEZA MUDA.

Siku zote wanasema muda ni Mali,kama alishindwa kuthamini muda wako uliotumia kwake mwanzoni, amini hata sasa ni nahisi kukupotezea tena muda wa kufanya mambo yako mhimu na kukuachanisha na waliokuwa na mapenzi ya dhati kwako

6. UWEZEKANO WA KULETEWA MAGONJWA.

Ni mara chache sana wapenzi wanaorudiana kukumbuka kupima afya tena,wanaporudi kwenye ulevi wa mapenzi husahau kuwa huenda ameshapata magonjwa humwamini moja kwa moja na kwenda kichwa kichwa kumbe kashaoza.

Mwisho:
Simaanishi haitakiwi kurudiana na wapenzi wa zamani lakin ni vema ukafahamu baadhi ya madhara yanayoweza kukupata baada ya kurudiana..
Ni vema ukatafakari kwa kina kabla ya kufanya maamzi ili ujiridhishe kwa hiari usiende kwa mihemko ya maneno.

Fikiria mara mbili mapenzi yasije amua maisha yako..
 
Mkuu madhara hayo ni kweli yapo ila kuumiza watu wengine sababu ya fulani nayo ni shida ndo maana namhitaji sana huyu mwanamke na niyeye tu ndo amebeba furaha yangu, hata nikiwa nae moyo huwa unatulia kwakujua upo sehem salama
 
Ukiona mtu amekubaliana na jambo alilokuwa akibishia ujue kuwa:
1) alikuwa sahihi lakini baadae amekubali kudanganywa au kupotoshwa 2) alikuwa ni mjinga au amepotoshwa lakini baadae ameona ukweli.
 
Back
Top Bottom