Kipi kinakufanya kurudiana na mtu uliyemuacha kwa kuamini kuwa sio mwenza sahihi?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,059
10,519
Based on true events.

Ni jamaa ambaye tulikutana katika harakati za maisha ni mtu ambaye tumesaidiana katika nyakati ngumu ni kama brother from another mother.. anaitwa Juma sio jina lake halisi kwa sasa anaishi mikoa ya kaskazini Juzi kanipigia simu.

Juma: Mambo vipi kaka!

Mimi: Poa harakati niaje?

Juma: Fresh mjini hapo vipi!

Mimi: Tunapambana mzee.

Juma: Kaka mimi nina swali

Mimi: Ndio kaka.

Juma: Kwa nini gari unaponunua japan bei inakuwa chini lakini ikifika bongo bei inakuwa kubwa mara mbili.

Mimi: Ishu ni kodi ya TRA pamoja na gharama za kulisafirisha kwenye meli pamoja na charges za Bandarini.

Juma: Duh! Sasa kipi bora kwenda showroom au kuagiza

Mimi: Kuagiza ndio unyama maana kuna gharama unakuwa unazipunguza.

Juma: Poa kaka nimekupata.. sema nini brother mimi kuna jambo nilikuwa nataka unipe ushauri

Mimi: Mzee jambo gani tena?

Juma: Unajua hii wiki nzima nimewaza sana kurudiana na shemeji yako najua utaona nazingua ila kimsingi Mambo yangu hayaendi afu si unajua tena mtoto anahitaji malezi ya pande mbili yaan kimsingi bado nipo njia panda maana kuna time naona nikomae ila nikifikiria sana naona bora turudiane..

Mimi: Aisee kaka case yako kama ya kwangu mimi jana nimewaza sana kuhusu Mama Morgan natamani sana turudiane ili tulee mtoto wetu napenda kuona mwanangu anavyokuwa nimtengeneze vile navyotaka

Juma: Umeona kaka zile ni damu zetu alafu familia ni baraka.

Mimi: Sure mzee ila nikifikiria sana naona bora nikomae mwenyewe tu

Juma: Sasa Bro mi unanishauri vipi.?

Mimi: Dah sema nini kaka we utakachoamua mimi nakibless mzee si unajua tena mambo ya mahusiano

Juma: Poapoa kaka nashukuru usiku mwema

Mimi: Haina noma na kwako pia

Hizi case za watu kurudiana imekuwa jambo la kawaida sana lakini swali la msingi ni je kipi kilisababisha umuache? Na kipi kinafanya mrudiane?

Sometimes Wanawake muache kucheza na mitishamba mnafanya Wanaume tuonekane vituko mtu nimekufumania live bila chenga nikatoa talaka na kuwatangazia ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimekuacha sababu ya uzinzi haijapita hata mwezi nakutafuta turudiane.. mtuhurumie watoto wa wanawake wenzenu
 
Yaani takataka nishaitupa ishafika jalalani huko inaliwa na kila aina ya wadudu na ndege kama mzoga. Leo eti nafikiria niirejeshe tena ile takataka ndani hivi mimi kichaaa🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom