Madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
KUTOPATA CHOO.jpg


MADHARA YA KUKOSA CHOO KWA MUDA MREFU

Habari za leo rafiki ni matumaini yangu unaendelea vyema na kufurahia uwepo wa blog hii, Nimepokea email nyingi kuhusu tatizo la kutopata choo hvyo nimeona ni heri kuzungumzia hapa ili wote mfahamu tatizo hili

tatizo Hili ni sugu sana miongoni mwa watu wengi na kwa watoto wadogo pia Bila kujua ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka hata hivyo wengi huwa wanapuuzia na kuona ni tatizo la kawaida,
LAHASHA!!! Napenda kukuambia rafiki tatizo la kutopata choo kwa Muda mrefu ndio chanzo cha magonjwa mengine tena ya hatari zaidi kwasababu mtu unapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa

uchafu unaotakiwa kutoka hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea unahamia kwenye damu na kuwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kukuathiri zaidi

~kwa kawaida mtu anapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku na mara Tatu kwa wiki hivyo iwapo unakosa choo kwa siku Tatu ilhali unakula elewa moja kwa moja una tatizo katika mfumo wa mmeng'enyo

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUTOPATA CHOO
~tatizo hili husababishwa zaidi na ulaji mbovu wa vyakula na kutokujizoesha kwenda haja mara kwa mara pia kula vyakula vilivyokobolewa na matumizi mabaya ya dawa na magonjwa mengine pia mabadiliko ya hormone

DALILI ZA KUTOPATA CHOO

Dalili za tatizo hili ni ÷

KUPATA HOMA KALI
KUTETEMEKA KWA BARIDI
KUTUMIA NGUVU NYINGI NA MUDA MWINGI KUJISAIDIA
ULIMI KUWA NA UTANDU MWEUPE NA KUTOA HARUFU MBAYA
KUKOSA HAMU YA KULA
TUMBO KUJAA GESI
KUPATA VIDONDA SEHEMU YA NNJE YA HAJA KUBWA

NAMNA YA KUTIBU NA KUEPUKA TATIZO LA KUTOPATA CHOO
~matibabu ya tatizo la kutopata choo kwa ufup ni magumu na marahisi pia kutokana na ukubwa wa tatizo pia hata hivyo kila mtu
anaweza kujikinga na tatizo hili kwa kufuata kanuni za ulaji wa lishe bora kwasababu tatizo la kutopata choo husababishwa na namna
unavyokula au kuishi hivyo ukifuata kanuni za lishe bora tatizo hili

halitakupata hivyo njia sahihi ya kujikinga na tatizo la kutopata choo ni kula nafaka zsizokobolewa, matunda, mbogamboga na maji kwa wingi

~matibabu hufanyika kwa kuangalia ukubwa wa tatizo na Hali ya mhusika kwan matibabu ya mtoto sio sawa na ya mtu mzima mwenye miaka 70 Hali kadhalika tatizo hili likijulikana mapema huwa rahisi kulikabili tofauti na tatizo la mda mrefu ambapo tiba

Yake huweza kuwa kubwa haswa ambapo tiba Yake huhusisha vidonge na chakula na hata kufanyiwa upasuaji kuondoa kinyesi kilichoganda katika damu na kuendelea na matibabu ya chakula

MADHARA YA KUKOSA CHOO KWA MUDA MREFU

madhara ya kukosa choo kwa Muda mrefu ni÷
KUPATA SARATANI YA UTUMBO
FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI
KUPATA PRESHA NA KUPATA UGONJWA WA INI
KUPATA MAGONJWA YA MOYO NK

KUMBUKA :zingatia kula milo mitatu kila siku, kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi (high fibre diet), kunywa maji mengi na fanya mazoezi mara kwa mara pia usizoee kutumia dawa za kemikali ovyo ovyo ovyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom