Madhara ya kukaa na kinyongo au hasira moyoni

Madhara ya kukaa na kinyongo au hasira moyoni

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
138
Katika magonjwa yanayoongoza kuua watu ni HASIRA au KINYONGO. HASIRA au KINYONGO ni chanzo cha magonjwa mengi na vifo. Vinapunguza sana siku za kuishi.

Uchungu usipoutoa moyoni utatokea sehemu nyingine, ๐Ÿ‘Œ ukitokea kwenye ziwa, ๐Ÿคฑ tunaita kansa ya titi, ๐ŸŒ ukitokea kwenye moyo tunaita presha, ๐Ÿ˜ฏ

Kila ukikasirika nyongo inamwagika. Watu wenye tabia ya kupandwa na hasira mara kwa mara wako kwenye hatari kubwa sana ya kupata vidonda vya tumbo.

Ukiwa na uchungu au hasira sana hata kinga za mwili zinashuka. Kinga zikishuka kila ugonjwa unaokuja utakupitia.

Chunga sana usikae na uchungu au hasira moyoni, ๐Ÿ˜” inazuia hata msamaha wa dhambi. ๐ŸŒ Maana kanuni ya Mungu inasema, โ€œutusamehe dhambi zetu, ๐Ÿ˜Ÿ kama sisi nasi tuwasamehevyo waliotukosea.โ€ Mathayo 6:12 ๐Ÿ“–

Usikubali kumuwekea mtu kinyongo. Mungu akisema uachilie ni kwa faida yako, kwanza unafungulia kusamehewa dhambi zako, pili unaponya afya yako.

Mungu anaposema samehe na usahau ni ili utoe nyongo moyoni, kusamehe ni kujipa uhuru, unajitoa kwenye gereza wewe mwenyewe.

Vitu vingine kwenye maisha potezea, ๐ŸŒ acha kubeba kila kitu. ๐Ÿ‘Œ Aliyekuacha unaweka moyoni, ๐Ÿ˜’ wakikusema vibaya unaweka moyoni. ๐Ÿฅฑ Utabeba wangapi mwisho moyo upasuke bure, mwisho sura izeeke mapema msemo wa mwimbaji fulani.

Tafadhali, usife na uchungu, toa hiyo nyongo. Hakuna maumivu yanayoshinda msamaha, ukitaka upone haraka we kubali kusamehe.

Msamaha haina maana ni udhaifu, ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ ukiendelea kumuweka mtu moyoni ๐Ÿ˜  unayeumia ni wewe. Hata dhambi zako hazitafutwa kama umeshindwa kuwasamehe waliokukosea. Mungu anasema โ€œHeri wenye rehema, ๐Ÿ˜Š Maana hao watapata rehema.โ€ ๐Ÿ˜Š Mathayo 5:7 ๐Ÿ“–

Rehema maana yake ni huruma. ๐Ÿ˜ฐ Kama unataka Mungu akuhurumie ๐Ÿ˜ฏ na wewe hurumia wengine. ๐Ÿ‘Œ

Kama kuna mtu hujamsamehe, ๐Ÿ˜ฏ kaa ukijua kabisa dhambi zako hazijafutwa. ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ โ€œBali msipowasamehe watu makosa yao, ๐ŸŒ wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.โ€ ๐Ÿ“– Mathayo 6:15

Kama kuna mtu bado una bifu naye, ๐Ÿ˜  hamsalimiani ๐Ÿ˜’ au hujamsamehe, โ˜บ๏ธ na wewe dhambi zako bado ziko hapo hewani ๐Ÿ‘Œ hazijapita hata sayari ya Mars kwenda kufutwa Mbinguni. ๐Ÿคญ Rejea sala ya Baba yetuinasema, โ€œutusamehe kama na sisi tunavyowasamehe waliotukoseaโ€ ๐ŸงŽ๐Ÿปโ€โ™‚๏ธ

Na msamaha hauna limit (kikomo). Siku moja petro alimuuliza Yesu, โœ๏ธ โ€œBwana, ๐Ÿ˜ฏ ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? ๐Ÿ˜’ Hata mara saba? ๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ Yesu akamwambia, ๐Ÿ˜ฏ Sikuambii hata mara saba, โœ‹ bali hata saba mara sabini. โ€๐Ÿ‘Œ Mathayo 18:22

7 x 70 = 490.๐Ÿ‘Œ Kwa hiyo mtu akukosee hata mara 490. ๐Ÿ‘Œ Hilo fungu linasema ili ifikie kikomo cha kumsamehe mtu โ˜บ๏ธ zifike mara 490 kwa kosa hilo hilo, ๐Ÿคญ na hayo makosa yafanyike kwa siku moja. ๐Ÿ‘‡

โ€œKama ndugu yako akikosa, ๐Ÿ˜ฐ mwonye; akitubu msamehe. ๐Ÿ™ Na kama akikukosa mara saba katika SIKU MOJA,๐Ÿ˜’ na kurudi kwako mara saba, ๐ŸงŽ๐Ÿปโ€โ™‚๏ธ akisema, Nimetubu, ๐Ÿ™‡โ€โ™‚๏ธ msamehe.โ€ ๐Ÿ™‚ Luka 17:3-4

Ikimbie migogoro isiyo na sababu. ๐ŸŒ Hakuna haja ya kupigana ili kudhihirishia ulimwengu ๐ŸŒ kwamba wewe ni mwanaume au ni mwema. ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ

Hapo kale mliambiwa, โ€œJicho ๐Ÿ‘๏ธ kwa jicho, ๐Ÿ‘๏ธ na jino ๐Ÿฆท kwa jino. ๐Ÿฆท Lakini mimi (Yesu) nawaambia, Msishindane na mtu; ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ lakini mtu akupigaye shavu la kuume, ๐Ÿฅฑ mgeuzie na la pili.โ€ ๐Ÿ‘‹ Mathayo 5:38-39

โ€œA wise man was asked what is anger? He gave a beautiful answer: It is a punishment we give to ourselves for somebody elseโ€™s mistake.โ€ (Mwenye hekima aliulizwa, hasira ni nini? Akajibu vizuri sana, kwamba ni adhabu tunayojipa wenyewe kwa makosa ya mtu mwingine. โ€“ Unknown

Sulemani yeye anatuambia, โ€œUsifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavuโ€ Mhubiri 7:9

Kuna nukuu moja inasema, โ€œKama tungelipiza visasi โ˜น๏ธ kama tungewachafua waliotuchafua, ๐Ÿคง kama tungewaharibia walio tuharibia, ๐Ÿ˜’ leo tusingefika hapa tulipo. โ˜บ๏ธ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ Kuna nguvu katika kukubali aibu, ๐Ÿ™ˆ kusamehe, ๐Ÿ™ kukaa kimya, ๐Ÿ˜ท kuachilia, ๐Ÿ™Œ lakini zaidi kusimama na Mungu.โ€๐Ÿ™‡โ€โ™‚๏ธ

By Zakaria Maseke
(0754575246 WhatsApp)
Piga bure.
 

Attachments

  • IMG-20230110-WA0001.jpg
    IMG-20230110-WA0001.jpg
    66 KB · Views: 32
Kwanza sijamaliza kusoma.

Kwani ukisamehe ndio hufi? Yaani unitendee ufilauni afu niwe najichekesha kwako?
Ni aidha kisasi au chuki ya directly na siwezi kuehirikiana na wewe Kwa chochote.
 
Back
Top Bottom