Ramesses II
JF-Expert Member
- Sep 29, 2013
- 4,218
- 5,888
Bwana mmoja alikwenda kutembea ukweni kwake. Alipokelewa kwa upendo baada ya chakula cha usiku alipewa chumba cha kulala. Ilipofika usiku wa manane alitoka kwenda kujisaidia. Taa zimezimwa na hakujua ni wapi pa kuwashia na kwa bahati mbaya akapamia vyombo vya chakula sebleni. Kipindi anajaribu kupapasa aviweke sawa mara taa ikawashwa na mama mkwe akaona ameshika vyombo na kumwambia,“Baba kama hukushiba ungesema.” Hapa mama mkwe hakujipa nafasi ya kufikiri kabla ya kuzungumza, badala yake alitumia hisia kusema. Shida ya hisia inakupa majibu ya haraka ambayo yanaweza kukuletea shida. Unadhani yule bwana aliendelea kukaa ukweni? Ndio yale yale unaenda kutembea sehemu unaskia wanasema sisi humu hatujawahi kuibiwa kitu. Wengi tuko hivyo.
Hisia ni matokea ya kutojipa muda katika kuutafuta ukweli na kujikuta katika mtego wa haraka haraka haina baraka. Wengi wameumia kwa sababu ya hisia. Siku moja ndoa inafungwa kanisani, Mchungaji akauliza, “Yeyote mwenye pingamizi la ndoa hii kufungwa aje mbele.” Kibabu kimoja kikasimama na kwenda mbele. Bi harusi kuona hivyo akaanguka na akazimia ghafla! Mchungaji, akakiuliza kibabu, “Tuambie babu pingamizi lako!” Kibabu kikajibu, “Nimeamua kuja mbele, kule nyuma sisikii vizuri!” Hisia ilimuua Bi harusi.
Tuwe na subira katika kuungoja ukweli wakati tukiutautafuta. Ukweli unatabia ya kuchelewa lakini lazima ufike. Ukiwa na subira kitambo kidogo ya kupanic utaepuka siku mia za majonzi. Subira ni ufunguzi wa matatizo mengi ni methali ya Sudani. Mtu mmoja alikuwa anaendesha gari kuelekea mjini, akapishana na mtu mwingine akiendesha gari kutoka mjini. Anayeenda mjini akashusha kioo na kupaza sauti akisema Punda! Yule anayetoka mjini akajibu Punda mwenyewe! Mita chache mbele akavamia kundi la punda na gari lake likapinduka. Ndipo akaelewa kwamba dereva mwenzake alikuwa akimtahadharisha na siyo kumtukana kama yeye alivyodhani. Kuna wakati unamtukana mtu aliyekuwa na nia ya kukusaidia wewe! Subira yaweza kuivisha mawe inasema methali ya Kiafrika. Subira huvuta kilichombali.
Hisia ni uwezo wa kujiuliza maswali mengi sana kichwani na kuyatolea majibu kwa haraka ambayo unayaamini kuwa ni ya kweli ili yakusaidie kufanya maamuzi ya haraka. Babu mmoja alipoibiwa pesa kwenye daladala aliwauliza abiria kwa ukali, jamani aliyechukua pesa yangu arudishe la sivyo nitafanya kama nilivyofanya juzi? Mwizi alivyosikia hivyo akamrudishia pesa yake halafu.Lakini walipomuuliza babu kwani ulifanyaje? Babu akajibu Nilitembea mpaka nyumbani kwa mguu. Kwa jinsi abiria walivyouliza swali hilo hawakutegemea hayo majibu. Pengine walikuwa na majibu yao. Tuko hivyo!
Afisa masoko kutoka kampuni ya kutengeneza viatu alivyofika kisiwani Ukerewe alikuta watu wako pekupeku. Akapiga simu haraka kuomba kampuni yao ipeleke mzigo wa viatu Ukerewe maana kuna soko kubwa. Kabla ya kutuma mzigo, meneja wa kiwanda akamtuma kijana mwingine aende kuhakikisha kama ni kweli kuna uhitaji wa viatu. Kijana alivyofika pale kisiwani, aliwauliza watu sababu ya kutembea pekupeku. Wale watu wakamwambia ni utamaduni wao kutembea pekupeku! Unaweza kuona huyo bwana alivyotaka kuitia hasara kampuni yao. Ndio yale yale kila mtu anataka kulima matikiti kwa sababu tu msimu uliopita waliolima walipata faida. Huwezi kupata maendeleo kwa kufanya kilimo nyemelezi!
Hisia ni kitu kibaya sana. Kinaweza kuvuruga mahusiano yako mazuri na Mungu wako. Jamaa alipoingia msikitini na panga na kuuliza nani mwislam hapa? Watu wakabaki kimya, akauliza tena, nani mwislamu hapa?? Halafu akamchukua mtu mmoja na kwenda nae nje na kumwomba amchinjie mbuzi. Halafu akarudi msikitini na panga yenye damu na kuuliza tena, "Nani mwislamu hapa?” Waumini wakamnyooshea imam kidole kwamba ndio mwislamu, Imam akasema, “Jamani mimi kuswalisha siku mbili tu ndio mniite mwislamu? Mi hapa najifunza tu.” Halafu jamaa akasema, “Nataka unisaidie kumchuna mbuzi wangu.”
Kuna wakati matani ya MC kwenye harusi yalikaribia kuharibu sherehe kwa sababu ya hisia. Wakati wa sherehe MC akasema, “Sasa nawapa sifa kubwa ya bibi harusi wetu huyu. Tangu namfahamu dada huyu huwa havai nguo za ndani kabisa. Watu wote ukumbini wakaduwaa! Bwana harusi naye macho yakamtoka. Bi harusi akaanza kutetemeka. Narudia tena kwa msisitizo na sijakosea. Bi harusi huyu havai kabisa nguo za ndani. Yeye anavaa za nje ya nchi tu, kutoka Italy, England na USA si za Tanzania. Hebu mshangilieni." Kila mtu "Ahaaaa kuuumbe!!!" Je, asingefafanua ingekuwaje?
Tunaishi kwa hisia lakini hebu tuwe tunajipa muda kabla ya kufanya maamuzi yoyote! “People don’t like to think, if one thinks, one must reach conclusions. Conclusions are not always pleasant,” by Helen Keller.
Mwendeshaji semina akauliza kama wamekuwa na desturi ya kuwatumia wanaume wao ujumbe wa “Nakupenda” au “I love you.” Wengine wakasema hawana. Wengine wakasema ni muda mrefu wamefanya hivyo. Basi akawaambia watume sasa ujumbe huo. Baada ya muda wakasikio milio ya ujumbe kwenye simu zao. Mwendesha semina akasema wabadilishane simu na kila mmoja asome ujumbe wa mwenzake. Mwanaume mmoja aliandika: “Utaniambia ujumbe huu ulikuwa unamtumia nani?” Mwanaume mwingine aliandika: “Usijikombe kombe utaniambia una nani huko?” Mwingine alindika: “Nani mwenzangu.” Hawa wanaume waliongozwa na hisia ya ngono na wakajaji wake zao vibaya..
Peter Newness ambaye alikuwa hajawahi kutoa mchango wowote katika tukio lolote pale kazini kwao. Siku moja mkusanya michango alimfuata atoe mchango wake kwa sababu rekodi zake zinaonyesha hajawahi kutoa mchango wowote licha ya kuwa na kipato kikubwa. Bwana Newness alimjibu: “Je unajua kuwa mama yangu ni mgonjwa na bili zake ni nusu ya mapato yangu? Je unajua kuwa kaka yangu ni kipofu na hana kazi? Je, unajua kuwa mme wa dada alikufa katika ajali akimwacha bila pesa na wakati ana watoto watatu?” Mkusanya michango akajibu, “Sikujua, samahani sana brother, ningejua hayo yote nisingekuja kukuomba mchango.” Peter Newness akaendelea, “Sasa, niambie, kama hawa wote siwapi hata shilingi nitakupaje wewe pesa.” Mtoa michango aliomba msamaha pasipohitaji msamha kwa sababu majibu ya hisia yalimletea huruma.
Tuachane na kufanya maamuzi kwa hisia, tujipe muda kuupata ukweli!
This is the work of Mwl Mchomvu Kienja, Copied from Facebook.