Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,614
Rais anaenda ziara Mwanza.
Hoja:-
1. Anaenda kuondoa wakfu wa serikali toka kwenye bandari hiyo ili kuruhusu DP World kuweka wakfu wao?
2. Anaenda kuwapooza Wasukuma kwa maneno matamu?
3. Ili utawale vizuri JMT, Kanda ya Ziwa ni lazima ushinde uchaguzi kwa sababu ndiyo inayotengeneza quorum ya kuongoza taifa, pia ndiko 75% ya rasilimali za nchi (watu na mali) zinakopatikana kwa wingi. Wasukuma pekee wako 19% ya idadi yote ya watu wa nchi.
4. Ni Kanda inayotegemewa sana kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiulinzi. Kwahiyo ni Kanda ya kimkakati. Inayo ndani yake shoroba kadhaa za maendeleo e.g. madini, utalii, ufugaji, kilimo, uvuvi nk.
5. Maprofesa na Maaskari wengi wanatoka Kanda hiyo.
Tusiyoyaona leo kuhusiana na madhara ya DP World:-
1. Nyufa mpya za muungano hazikwepeki.
2. Makanisa yajiandae kupoteza ardhi wakfu zao. Nchi haina dini ila ina udini. Kama Waarabu wataamua kueneza dini yao, na kwa kuwa sharti mojawapo la mkataba linasema wakiomba ardhi wanayotaka (watayopoint kwa kidole) bila kujali ndani ya ardhi kuna mali gani wala mpangaji wa ardhi ni nani wapewe bila masharti ya sheria ya kumiliki ardhi na serikali ndiyo iwajibike kuwafidia wanaohamishwa toka ardhi hiyo.
3. Kwa jinsi hiyo ni rahisi kwao kutaka eneo wakfu la Kanisa na kuweka miradi yao ikiwemo kujenga Msikiti ndani ya mradi. Wanaondoa Kanisa kwenye eneo na wanajenga Msikiti. Vitega uchumi vikubwa vyote vinavyomilikiwa na watu wa imani ya Kiislamu vina Misikiti imejengwa humo kwa ajili ya ibada.
4. Kiulinzi na usalama je, vikosi vyetu vitalazimika kutumia bandari ya Mombasa kutunza siri za kiulinzi na usalama vinapoagiza vifaa vya kijeshi?
Dhara baya zaidi:
JMT kupitia mkataba wake na DP World, (Kenya waliikataa DP World) haikuzingatia ukomo wa muda wa kuwekeza. Hii itatatiza baadhi ya itifaki za EAC zikiwemo za Uhamiaji, Forodha, Soko la Pamoja, Sarafu moja, Kiswahili (EAKC) na Shirikisho la Kisiasa; kusababisha sintojuwa kwa nchi wanachama kuhusiana na itifaki hizo zilizokwisharidhiwa na zinazotarajiwa kuridhiwa nje ya mkataba wa DP World na JMT.
Je, Serikali na Bunge zilizingatia haya?
Je, zilishauriana na serikali wanachama wa EAC kuhusu JMT kujiingiza DP World kwa mkataba usiojulikana muda wake?
Serikali moja ya EA itakapoanza kazi na kuzitaka hizo bandari, viwanda, shoroba za biashara, zoni za kiuchumi nk je, kutaibuka mgogoro na DP World?
Mkataba unasema utatuzi wake utakuwaje?
DP World walijulishwa wakati wa majadiliano kwamba nchi yetu iko na inaelekea kwy itifaki ya serikali moja ya EA?
Itifaki ya Shirikisho la Kisiasa la EAC litafikiwa chini ya miaka 100 kuanzia sasa, kama JMT itazipa DP World bandari zote maji na kavu, viwanda, ardhi, zoni za kiuchumi na shoroba za kibiashara itakuwaje pale ambapo EAC itakuwa nchi moja mapema ya muda wa mkataba wa DP World (kabla ya uhai wa DP World kuhitimika?)
Bandari ya Znz inaangukia wapi kwenye abracadabra hii kimahusiano ya EAC?
Je, wahusika waliwaza haya wakati wa kufikiria kujiingiza DP World na pia wakati wa kujadili na kupitisha Azimio la Bunge?
Tukiishawapa wageni kila kitu kutokana na kwamba sisi tumeshindwa kuviendesha licha ya utaalam tulio nao, bajeti tunazotengewa kila mwaka na pia soko la uhakika kuwepo, tutajikuta tumebaki bila kitu tunachoendesha wenyewe.
Hii maana yake ni kwamba serikali itakosa uhalali wa kuwepo kutokana na kwamba itakuwa haina tena kazi ya kufanya maana nchi yote itakuwa kwy ugenishwaji. Ni dhahir shahir kwamba ukoloni mpya huu ndiyo utajipa uhalali wa kuwepo!?
Tukiwapa wageni kila kitu maana yake tumeuza uhuru wa kiuchumi tumebakisha uhuru wa kisiasa kwa muda tu. Kitakachofuata mbeleni huko hawa wageni ndiyo watakaoamua nani awe kiongozi.
Tukifika hapo (na ni jirani sana kufika hapo) tutakuwa pia tumeuza uhuru wa kisiasa na sasa itakuwa ni ukoloni mpya 1000% ambao hautatanguka milele yote.
Nina uhakika serikali hii ikishindwa kuendesha bandari za Tanganyika haitoweza kamwe kuendesha SGR, MGR, CGR, JNHPP na ATCL. Hii ni miradi migumu sana kuendesha, hivyo Waarabu wajipange kuja kupewa.
Marais Jomo Kenyatta na Idd Amin matendo yao mafu yalizonga na kuhitimisha uhai wa EAC ya kwanza 1967 - 1977 miaka 10 tu. Safari hii naona ni JMT ndiyo itakayoua EAC hii ya sasa.
NB.
Baada ya ziara ya rais Kanda ya Ziwa, CHADEMA wanatakiwa kwenda Kanda ya Ziwa kuelezea upande wa pili (mbadala) wa mkataba wa DP World ili wananchi waelewe ukweli ni upi. Kazi ya msingi ya upinzani ni check and balance.
Taifa la Tanganyika halikwepeki.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app