Madhara makubwa watakayopata Chama Tawala baada ya msanii Wema kuhamia CHADEMA

Small Axe

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
652
500
Kwa weledi wangu wa siasa za Tanzania na hali ya saisa inavyokwenda kuna mambo kadhaa wa kadha ambayo yataleta madhara ya chama tawala kwa hapo baadae.

Katika sakata lililobamba zaidi ya wiki mbili (namaanisha toka majibu ya form four yatoke na mkoa wa Dar kuongoza kufeli) mambo ya madawa ya kulevya.

Suala la msanii Wema linaonekana ni dogo lkn lina madhara makubwa mbeleni, hasa kwa CCM.

Kwanini nasema hivyo...

Moja- Wema ni celebrity ana wafuasi wengi zaidi ya milioni hasa vijana wa kisasa kama unataka kujua angalia vijana wengi wanapenda magazeti ya upashukuna na yeye karibu kila siku anapamba kwenye front page. Aliwashawishi vijana wengi wawe na imani na CCM kwenye kampeni za uchaguzi.

Pamoja na hivyo ana kipaji kikubwa sana cha kushawishi, wasanii wanamjua hata Diamond kuwa superstar katoka mikononi mwa Wema. Hivyo vijana wengi wataenda CHADEMA wale ambao waliona CHADEMA si chochote kwa CCM.

Rejea kuhama kwa Mzee Kingunge, Waziri mkuu mstaafu Sumaye, Waziri mkuu mstaafu Lowasa,waziri mstaafu Masha na wengine wengi na maelezo yake inaonyesha CCM ni chama kisicho na demokrasia ya kweli bali kinatawaliwa na ubabe,umimi.

Pili- Wema ni binti anayetoka mkoa wa Singida ambapo ni ngome kuu ya CCM. Kwenye kura kutokana na majority ni wajinga wanaona Wema ni icon yao. Sasa wakiungana na Tundu Lissu,Esta K. Kafulila na wengine wengi kuna hatari ya kupoteza kura nyingi endapo uchaguzi ujao utakuwa halali(Tume huru).

Tatu- Huyu binti anaamini anachokifanya, kifupi ana confidence hii kutokana na malezi aliyokulia.Akikutana na mama Lowassa,Halima Mdee,E.Bulaya na wengine wengi naamini atakuwa ana uwezo mzuri sana wa kujenga hoja.

Nne- Kutokana na yeye Wema amethubutu basi kwa hali ilivyo sasa utasikia wasanii wengine wengi wakakihama chama. Hii kutokana na kutumiwa na kuachwa tena bila hata kulipwa hii ndio aibu sana kwa wasanii wa kitanzania wanaoishi kwa kujaza tumbo badala ya kutetea freedom kama wasanii wa enzi zile.

Namalizia kusema haki uinua Taifa. Tuheshimu utu wa watu. Kutengeneza heshima inachukua miaka mingi na jasho kubwa lkn kuporomoa heshima ya mtu ni mara moja na kuirudisha ni kazi ngumu.

Pinga madawa ya kulevya lkn fuata misingi ya haki za watu.

RIP Amina Chifupa
 

mahutu

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
766
1,000
Utakua umekoswa unga...sio bure...akashindwa lowasa aliekua hadi na mkono usalam wa taifa..makanisani akishika waumini na wanywa viroba wote walikuwepo wakadeki hadi lami ili apite itakuaje huyu demu asiye jua hata kuongea...wema sio mwanasiasa huyo ni kama kara jeremaya...tu wapo akina roma mkatololiki bt bado hawana ushawishi kwa siasa...huyo anatafta msaada maana kaisha ona chadema siku hizi kazi yao ni mutetea waharifu...sasa kwa nin asihamie ili asaidke
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,441
2,000
kwenda zako wewe. pelekeni unga na bangi zenu chadema. ccm ni chama makini kuleta maendeleo ya wananchi sio jopo kwa ajili ya walimbwende wavuta bangi. ccm hakuna mtu mashuhuri ila chama ndio mashuhuri. watu waliofanya makosa ya kudhani ni mashuhuri kuliko ccm wapo wema angewauliza angejua yeye si chochote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom