Madhambi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Status
Not open for further replies.
Sera gani iliwahi fanikiwa nchi hiii tangu butiama era hadi kizimkazi era?
Honestly mkuu ni zeros, hakuna, ndio maana ukiwauliza wa Lumumba street nini walichoifanyia nchi yetu kwa kodi zetu ,wanakuaga hawana majibu na majibu yao ni matusi tu,Dar ya mkoloni ilijengwa vema,kariakoo ya mkoloni ilikua safi, mitaa ipo safi, huduma safi, sasa ukiingia kariakoo ya sasa ni uchafu mtupu, ujenzi holela, parking hakuna,public toilets hakuna,garden za watu kupumzika hakuna yaani ni vurugu tupu
 
Never ever President Nyerere kuwa mwenye heri, haitatokea....Vatican sio mazezeta
Kinacho zuia asiwe mtakatifu ni sababu kama hizo hapo juu.
Ni ngumu kwa mtu maarufu sana sana mwanasiasa kuwa mtakatifu unless kumbukumbu zake zote ziwe zimefutwa.
 
Na Hayati Mchungaji Christopher Mtikila.

[Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Democratic party]

JULIUS KAMBARAGE NYERERE MWENYEWE HERI ?

Tulikuwa hatuamini kabisa kwamba kweli mlikuwa mnataka kumpa dikteta Julius Nyerere kwamba "mwenye heri",ile eti baadaye mmpe "utakatifu".Lakini baada ya kuona haukuwa mzaha,tunalazimika kuwashauri kwamba muachane kabisa na upuzi na kufuru hiyo,kwa sababu sisi tunaandaa kitabu muhimu sana kitakachosomwa na dunia nzima kwa kiingereza,kifaransa na Kiswahili,kinacho elezea kwa kina ushetanj wa mtu ambaye ninyi mmependa aitwe"mwenye heri". Democratic party (DP) tunajenga maadili mapya ya Taifa ya kuwa na hofu kwa mwenyezi Mungu,ndiyo maana tunawajibika hata katika suala hili.

Tumewajibika kuufahamisha Ulimwengu ukweli ufuatao kwa kifupi sana,ambao ambao ulipaswa kuzingatiwa kuhusu mtu huyu kabla ya kufikia kumvika sifa hiyo,isipokuwa kama mmeamua kujitengenezea "cult" ambayo kwa misingi ya haki ya uhuru wa kuabudu hampaswi kuingiliwa na mtu ,mradi hamvunji Sheria wala hamlazimishi wananchi wengine kushiriki katika cult yenu hiyo.Tunaamini kwamba cult hiyo imekuwa ikiimarishwa na wapambe wa huyo dikteta wanaojiita "Mwalimu Nyerere Foundation".

Kwani watu hao ambao wamekuwa wakichotewa hata mamilioni ya fedha ya walalahoi na kuchangisha mapema mengi ndani na nje ya nchi,hawafanyi Kazi yoyote ya kusaidia kuleta maendeleo au misaada ya kijamii.kwa vile wananeemeka kwa kujificha nyuma ya cult hii inawalazimu kuipambisha moto cult hiyo.

UKATILI WA NYERERE,NA JINSI ALIVYOJIJENGEA UMAARUFU.

Julius Kambarage Nyerere alijitengenezea yeye mwenyewe umaarufu wake,kutokana na roho ya kupenda kuabudiwa yaani ile iliyozuka hata ndani ya moyo wa Lucifer ambaye ni shetani ikapelekea kutupwa kwake chini.Nyerere ametumia kwa umakini sana udikteta uliokuwa katika damu yake .Ili kauli yake yeye tu ndiyo isikike katika taifa na iwe kama ya Mungu, dikteta huyo alifuta kabisa haki ya msingi ya uhuru wa maoni na kujieleza bila kuingiliwa,akapiga marufuki vyombo vya habari nchini na kubakiza vya serikali tu,kwa ajili ya kujisikiliza yeye peke yake kwa binadamu wote wa nchi hii.Binadamu yeyote aliyethubutu kusema au kushukiwa kwamba anawaza kinyume na mapenzi yake,aliangukiwa kinyama na nguvu ya dola kama haini.

ALIVYOUA ELIMU ILI ATAWALE WATANGANYIKA KAMA MIFUGO YAKE:

Ili kuwa Mungu wa taifa hili ,dikteta Nyerere alilazimika kuwatiisha watu wa nchi hii kwa kuwapofushwa kabisa kifikra mpaka tukawa kama mataahira,kwa kufuta elimu bora iliyotolewa awali na kubakiza kwa mfano kwa shule ya msingi ambazo alizikomeshea darasa la Saba ,masomo makuu yakawa Kiswahili,Siasa ya kuwapofusha kifikra na kuwafanya wamwabudu,na utamaduni au halaiiki ,walimu wakiwa mbumbumbu wa UPE.

Kwahiyo kila mwaka watoto takribani laki Saba wakawa wanaishia darasa la Saba na upofu huo,na hawa ndio sehemu kubwa ya Taifa letu Leo.Elimu aliifisha mpaka chuo kikuu na kuondoa hata umuhimu wa Lugha ya kiingereza,ili kuwatenga kabisa Watanganyika na Ulimwengu wa uhuru na maendeleo ya kifikra na teknolijia baada ya kuwapofusha.Vinginevyo kwa utajiri wa nchi yetu,leo kila mkoa ungekuwa na chuo kikuu na Tanganyika ingekuwa Ulimwengu wa kwanza kiuchumi.

ALIVYOBOBEA KATIKA NGUVU ZA KISHETANI:

Katika katawala watu wa nchi hii na kuwafanya wamtii na kumwogopa wakiwa kama mifugo yake, Nyerere alitumia sana nguvu za giza,zikiwa ni pamoja na shetani lake liitwalo "Murhunda" na dini ya huyo Mungu wake ya "Nyamurhunda".Mwenye ambao aliutumia kupovusha fikra za wananchi wote wa nchi hii ni kafara ya Nyamurhunda,na hata ninyi bilashaka mnajua kabisa! Nguvu za kuzimu na mashetani yake hakuacha nazo hata sekunde moja katika uhai wake,na alizibeba katika kifimbo chake.

Mbali na Nyamurhunda lake , dikteta huyo alijilimbikizia pia uchawi na mazindiko ya kila kabila nchini,kama alivyoshuhudiwa akifanyiwa hata Jakaya Kikwete katika maeneo ya mbali mbali safari hii.Tena dikteta huyo anakiri yeye mwenyewe katika Kanda zilizopigwa sana alipokufa na kurudi kuzimu milele,kwamba walifanya sana makafara ya uchawi huko Tanga na Bagamoyo,walikochinja mbuzi makaburini na kufanya waliyofanya.Isitoshe hata kiitwacho "Nembo ya taifa ni zindiko la Nyerere"!

Zindiko hili halina mjadala kwa vile limethibitishwa na Bibi yetu Khadija Kamba mwenyewe aonekanaye katika nembo hiyo,kwa njia ya magazeti ,Televisheni ya Taifa na Redio.Kuzindika kitu ni kukikabidhisha kwa mamlaka kuu ya kuzimu yaani Ibilisi,kwa maana kwamba Nyerere alikabidhusha nchi yetu kwa Ibilisi,yaani CCM na utawala kutoka kuzima au ni Ibilisi akiwa katika umbo la chama.

Sisi sote tunakumbuka vioja vya shetani vilivyo tawala kifo cha dikteta huyo,ikiwa ni pamoja na watu kufa wakati wa kutembezwa maiti yake,kwa sababu rahisi kabisa kwamba mashetani yake yalihitaji damu kwahiyo walalahoi wakafanyika kafara.kule alikozikwa kulitokea mauzauza mengi ya kishetani,ambayo vyombo vya habari viliripoti bayana kabisa na kumbukumbu zimehifadhiwa kwa ajili ya vizazi vyote vijavyo,vipate kuufahamu ushetani wa dikteta huyo aliyekuwa mwamba wa ushirikina duniani,kama alivyomsifu hata dada yake aliyeitwa Bi Magige kwamba "mizimu ya Nyerere ina nguvu kuliko serikali",na watu wa chama chake wanaotafuta utawala kishirikina,mpaka Leo hupiga ripoti kwenye Kaburi lake!

ALIVYOTUMIA DOLA KUFANIKISHA MALENGO YAKE YA KISHETANI:

Dikteta huyo alitumia pia vitisho na ukatilii wa kimya kimya ,vilivyowajengea hofu na woga na kuwafunga kabisa vinywa binadamu wote nchini,kwa kutumia mtandao wake mkali sana wa usalama wa Taifa au dola kwa jumla,ambao aliwafunza katika nchi zenye tawala za kikandamizaji,hasa za kikomonisti.Hawa aliwafunza kutesa watu vibaya sana kwa njia mbalimbali,na kuwaua kwa utaalamu ambao ilikuwa vigumu kuhusisha vifo vyao na yeye au serikali yake.

Nyerere alitesa watu wengi sana kizuizini miaka mingi sana bila kuwafikisha mbele ya sheria,wengi walikufa wakiwa kizuizini,ama muda mfupi baada ya kuachiwa huru.kutoka na mateso wengi walitoka ndani wakiwa hawaoni,wengine wakiwa kama punguani,wanaume wengi wakiwa wameuawa kiume.

Dikteta Nyerere alikosa kabisa Kipawa cha kuwavumilia watu waliotofautiana naye kifikra,au waliojaribu kumshauri tofauti na alivyoona yeye,hata akaitwa "Mzee Haambiliki".Wale aliowaogopa kuwa wanamzidi kiakili,au aliodhania ni tishio kwake kisiasa alitesa mpaka na familia zao,ndugu zao na hata rafiki zao! Miongoni mwa waliotofautiana na Nyerere ni hayati Edward Moringe Ole Sokoine,ambaye dikteta huyo hakukanusha alipotuhumiwa hadharani kuhusika na kifo chake katika mkutano mkubwa sana wa kisiasa Jangwani tarehe 23 January 1993.Wengine waliotofautiana naye hatimaye wakakutana na mauti ni Dk Mwanjisi,mchumi profesa Rweyemamu ,Jaji Mwakasendo na wengine wengi.

HAYATI OSCAR KAMBONA KATIKA KIELELEZO CHA UNYAMA WA NYERERE:

..............................

nitarudi.
Mnaamua kuchafua watu tu. Tanzania ndiyo nchi iliyo stable kuliko nchi zote za Afrika Mashariki na Kati. Amani yetu na utulivu ndivyo vinatufanya tuwe Kimbolton la majirani wakigombana kama DRC, Burundi, Uganda na hata Kenya.

Mchango wa Tanzania kwenye ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kama Mozambique, Angola, Namibia, South Africa na Zimbabwe siyo wa ku underestimate.

Nchi hii ya Tanzania ni kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika.

Sasa nashangaa vijana vichwa maji kama mtoa mada anaropoka tu anayoyataka ili kufurahisha genge. Ninaamini kama Nyerere asingekuwa mtu mwema hata yeye asingekuwa anaandika muda huu huo Utopolo wake
 
Akatuletea wachawi shule za msingi watu fundishe mazingaombwe tuliosoma 1976-80s watakumbuka hili, akatufundisha kuichukia israel na kuikumbatia Waarabu, leo laana inatutafuna kila kona
Tumelaaniwa na taifa teule. Ndiyo maana tunaongoza hadi dakika ya 89 bado dakika moja game iishe ila tunafungwa na kupoteza matumaini
 
Umeshapima malaria, naona imepanda kichwani.
 
Akatuletea wachawi shule za msingi watu fundishe mazingaombwe tuliosoma 1976-80s watakumbuka hili, akatufundisha kuichukia israel na kuikumbatia Waarabu, leo laana inatutafuna kila kona
Mbona mazingaombwe nayaona hata leo kwenye runinga dunia ya kwanza wakionyesha, yana ubaya gani. Huna point kunywa maji ukalale ukue.
 
Acheni porojo enzi za utawala wake lazima mkono wa chuma ulihitajika ili nchi ikae stable... What about Mao, Hitler na wengine wengi walio tumia mkono wa chuma kuleta maendeleo kwenye nchi zao??
 
Mwenye Heri gani mtu aliwanyang'anya watu nyumba zao walizojenga kwa fedha zao bila Soni, haya wala tahayuri
 
Mnaamua kuchafua watu tu. Tanzania ndiyo nchi iliyo stable kuliko nchi zote za Afrika Mashariki na Kati. Amani yetu na utulivu ndivyo vinatufanya tuwe Kimbolton la majirani wakigombana kama DRC, Burundi, Uganda na hata Kenya.

Mchango wa Tanzania kwenye ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kama Mozambique, Angola, Namibia, South Africa na Zimbabwe siyo wa ku underestimate.

Nchi hii ya Tanzania ni kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika.

Sasa nashangaa vijana vichwa maji kama mtoa mada anaropoka tu anayoyataka ili kufurahisha genge. Ninaamini kama Nyerere asingekuwa mtu mwema hata yeye asingekuwa anaandika muda huu huo Utopolo wake
Hilo liko wazi Tanzania ni nchi tulivu,lakini ukweli ni kwamba utulivu wa Watanzania ni kutokana na upumbavu wao wenyewe.

Maana Leo hii taifa hili limejaa wezi kila Kona na ambao wanaweka mifumo ya kulindana,ndio maana imefika hatua viongozi wanawaandaa watoto wao kuja kulinda wizi wao.

Kila taasisi na sekta zimejaa uozo kwa sifa ulizo taja hapo juu zingekuwa zunakwenda sambamba na huduma basi vijana wengi wasingekiwa wanazamia Afrika kusini kusaka fursa.
 
Nyerere atakuwa Mwenyeheri na kisha kutangazwa Mtakatifu na wala wewe pimbi huwezi kuzuia.

Andikeni vitabu vyenu lakini Wakatoliki wana sheria zao na mchakato wao. Akiwa ni mtakatifu ni wa madhehebu yao wala hakuhusu wewe na hivyo vitabu vyako.
Ni bora ujadili nilicho andika kuliko kuniita majina ya ajabu kisa tu, nimeandika kile usicho taka kukisikia hii ndo Kazi ya kalamu siku zote.

Mwl.Nyerere kama kiongozi lazima ajadiliwe katika pande zote za shilingi, maamuzi ya kuchagua upande uko juu yako.

Karibu kwa mjadala.
 
Muendelezo:

HAYATI OSCAR KAMBONA KATIKA KIELELEZO CHA UNYAMA WA NYERERE:

Ushetani wa dikteta huyo unatisha zaidi katika unyama aliomfanyia swahiba wake,hayati Oscar Kambona ambaye siyo tu ndiye aliyemwinua sana kisiasa,bali bali ndiye aliyeokoa hata uhai wake na utawala wake majeshi yalipotaka kimpindua mwaka 1964,ambapo nchi ilikwishakuwa mikononi mwa Kambona,kama angekuwa na uchu na roho ya ubinafsi kama ya Nyerere.

Oscar Kambona ndiye aliyemwokoa Nyerere hata alipokumbwa na ile kashfa ya rushwa ya nyumba ya Magomeni kutoka kwa Wahindi,alipokuwa Waziri Mkuu kwa miezi minne,kwa kumfundusha kama rafiki wa kweli kwamba ajiuzulu kabla ya hatua ya kamati ya TANU,kwa kisingizio kwamba anakwenda kuimarisha chama,ndipo dikteta huyo akapona na wadhifa akapewa Rashid Kawawa.

Tena ni Oscar Kambona aliyemfuata huyo rafika yake kwao Butiama mwaka 1958,alikokuwa anafanya Kazi mpya ya kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kizanaki baada ya kujiuzulu TANU ilipoishiwa pesa, Kambona akachangisha fedha ukanda wa ziwa alipotoka Uingereza kusoma,ndipo kwa sababu ya pesa rafiki yake akakubali kurudi TANU,na hatimaye akaupata na huo udikteta.

Isitoshe,Kambona ndiye aliyeasisi ukombozi wa kijeshi wa nchi za kusini mwa Afrika,baada ya kuwashawishi vizito watatu yaani Ahmed Sekou Toure,Kwame Nkuruma na Haile Selassie.Lakini sifa zote hatimaye akazibeba yeye Nyerere,ambaye kwa sababu wivu alimwondoa Kambona katika wizara ya mambo ya nje.

Kambona ndiye aliyekwenda China akaomba na kupata msaada wa ujenzi wa reli hii ya Uhuru,ambayo ilikuwa iwe katika Mtwara Corridor kwa sababu ya chuma Cha Liganga na mkaa wa Mchuchuma,mafuta na gesi vilivyopo kusini,na ukweli kwamba huko ndiko ambako kustawisha Taifa na Afrika kwa ujumla baadaye,lakini Nyerere akamtukana Kambona kwamba ni mkabila na kuihamishia reli hapo ilipo.Baada ya kutofautiana naye kifikra hasa juu ya ujamaa,Kambona alilazimika kutoroshea roho yake uhamishoni.

Kwa unyama wake dikteta huyo alisahau mema yote aliyotendewa na Oscar Kambona,akataifisha nyumba zake zote na kuamuru ukoo wote wa Kambona wasakwe na kuteswa.Mwanamke mmoja ambaye kwa kosa la kuwa na undugu na Kambona,akifanyiwa unyama wa kutisha mpaka kushindiliwa machupa na mawe sehemu zake za Siri na kubaki hana kizazi mpaka leo,pia ilibidi akimbilie Ulaya.

Kambona alifuatiliwa mpaka huko alikojificha akakoswa koswa mara nyingi kuuawa,hatimaye akauliwa mtoto wake wa kwanza aliyeitwa David Kambona kwa risasi.Nyerere aliuonyesha ukatilii wake kwa kuikimbia miili ya hayati Oscar Kambona na ndunguye Otini Kambon,siku ilipokuwa inawasili kutoka Uingereza.Hakutaka kabisa kuuona mwili wa mfadhili na mdhamini wake aliyemfanyia mema yote haya,akaukwepa pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam wakati anatorokea Butiama! Wala hatusemi kuhusu kiini Cha kifo chenyewe Cha hayati Oscar Kambona.Huu hauwezi kuitwa uwenyeheri.

Kusini mwa Tanganyika kumeathirika sana kimaendeleo tangu zamani hizo,kwa sababu ya kisasi Cha mwenyeheri huyo kwa Kambona.Wasomi na wanataaluma wengi wa huko wameishi nchini mwao kama ukimbizini,hata kama Mungu aliwapa vya kuibariki nchi yetu kama akina David Mattaka,Chiombola n.k waliofanya miujiza ya PPF nchini,lakini badala ya kupewa sifa na heshima waliyostahili,wakaangamia kama panya aliyethubutu kuinuka kutenda mema mbele ya paka,akidhani watamfurahuia na kumhesabu kuwa mwenzao.

Hayati Oscar Kambona alipotukanwa na dikteta huyo kwamba ni mkabila,kwa sababu ya kuipeleka reli ya uhuru kusini kwa ajili ya mapinduzi ya maendeleo ya Taifa letu na Afrika kwa ujumla,alimjibu kwa upole kwamba"Mimi unanionea,kwa sababu kama ni makosa aliyeyafanya ni Mungu mwenyewe"Alipoulizwa na Nyerere kwa ukali kwamba ana maana gani, Kambona alimjibu "kwa sababu Chuma Cha Liganga,mkaa wa mawe wa Mchuchuma,hazina za mawe ya thamani duniani,gesi na mafuta zilizoko kule kusini,kama Mungu angeviweka kule Musoma au Kilimanjaro bilashaka reli ingepita Kule,ila sasa alikosea na akaviweka Kusini."

Kisa hiki kilichangia kustawisha mbegu ya kisirani ndani ya dikteta huyo juu ya Kambona,ingawa urafiki wao usingedumu kwa muda mrefu kwa jinsi usivyoweza kuwepo umoja baina ya nuru na giza.Oscar Kambona alikuwa uzao wa ukuhani wa kikristo,wakati dikteta huyo mwenye Nyamurhunda ni wa mamlaka kuu ya kuzimu.

Kwa vile msingi wa utawala wa CCM ni ule ule wa kuzimu,mpaka leo nchi imo gizani kwa sehemu kubwa,kwa sababu mamlaka kuu ya giza kuzimu imezuia tusizalishe umeme wa mkaa wa mawe alioshauri Oscar Kambona,ambao ndio umeme wa uhakika unaoaminika (stable) kuliko wa maji ambao hupungua na hata kukauka kabisa ,au wa mafuta ambao ni ghali mno au wa nuclier ambao hata mataifa makubwa sasa wanauacha na kurudi ule wa uhakika na salama zaidi yaani wa mkaa wa mawe,kwa sababu ya hatari na athari zingine nyingi za nuclier.

Ni kweli kwamba umeme hauwezi kupelekwa vijijini kwa walalahoi ambao katika sehemu nyingine bado wanaenda uchi wa nyama na kuishi katika vibanda vya nyasi au tembe,miaka 60 baada ya uhuru,hali ambayo ni sura halisi ya utawala toka kuzimu!Lakini shangingi la mbunge baada ya kuiba Kura na mamilioni ya marupurupu yake yangetosha kugawa vile vimashine vya kutengeneza matofali ya udongo katika vijiji vya jimbo lake ,pamoja na vigae vya udongo,ili kila kijiji kikishajikamilisha kwa nyumba bora kwa wananchi wote kipelekewe umeme na kukomesha kabisa kugusa misitu,kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo.

Nyerere alimvika Oscar Kambona sura ya kuwa haini na msaliti mkuu wa Taifa kwa kupinga Azimio la Arusha au Ujamaa ambao alisema ni utu, na kupendelea ubepari ambao ni alitufundisha kwamba ni Unyama.Lakini unabii wa Oscar Kambona kwamba nchi ingeathirika vibaya sana kiuchumi,kijamii na kisiasa,na kurudi nyuma sana kimaendeleo na wananchi kuteseka sana ulitimia,na Nyerere akakiri kwamba "Tulifanya makosa".Kwahiyo kama dikteta huyo angekuwa na toba ya kweli kama mtu mwenye heri basi angeukiri unabii wa Oscar Kambona na kufanya naye suluhu,na kuyafanyia Kazi. Maono yake ya neema kwa nchi yetu,jambo ambalo Nyerere hakuweza kwa sababu ya roho yake chafu.Ndio maana haishangazi kutokuwepo nchini hata mtaa mmoja wenye jina la Shujaa Oscar Kambona licha ya mchango wake kwa uhuru na heshima ya nchi yetu na Afrika.

DIKTETA HUYO ALIVYOANGAMIZA DAMU YA WAHUTU:

................................

nitarudi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom