Madereva wazembe wafutiwe leseni –Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madereva wazembe wafutiwe leseni –Kikwete

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Tuesday, August 11, 2009 11:30 AM
  RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewataka madereva watakaopatiakana na makosa ya kusababisha ajali kizembe wafutiwe leseni na kutoruhisiwa kupewa leseni hizo tena Rai hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa barabara mpya Mkoani Singida na kutoa agizo hilo kali juu ya madereva hao.

  Kikwete aliitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kubadilisha adhabu zinazowakabili madereva hao na kutaka adhabu hiyo kali itumike mara moja ili kuweza kumaliza wimbi la ajali zisizo za msingi nchini.

  Amesema hayo baada ya kuongezeka kwa ajali sizizo za lazima kila kukicha na kupoteza nguvu kazi na watu wasio na hatia kutokana na uzembe wa madereva.

  Amesema madereva wamekuwa wakivunja sheria za udereva na matokeo yake kusababisha ajali na kumaliza wananchi pasipo na sababu.

  Hivyo ameitaka wizara hiyo kuwafutia madereva wataopatikana na makosa ya kuua abiria pasipo na sababu za msingi wafutiwe lesini na kutoruhisiwa tena kuendesha magari ya abiria tena.


  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2793674&&Cat=1
   
Loading...