chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,367
- 27,773
Habari wana JamiiForums
Kama inavyojulikana hapa Jamvini kwamba mimi ni mteja mzuri wa SuperFeo kwa route ya Dar Songea basi sitokaa kimya kuona wazembe wachache wasiowajibika katika majukumu yao hasa madereva wanaopakia roho za watu
Ni mwezi tu mmoja uliopita nikitokea Dar kuelekea Songea na basi la SuperFeo ambalo namba zake ninazo katika tiketi niliyosafiria kwa wahusika nitawapatia kwa hatua zaidi za kinidhamu
Kama inavyofahamika safari ya Dar kwenda Songea siyo safari fupi nikimaanisha inahitaji dereva zaidi ya mmoja ukizingatia ni basi la abiria ili waweze kusaidiana pale mmoja wao anapochoka
Katika hali inayoshangaza ni kwamba tangu Dar mpaka Songea alikuwa akiendesha dereva mmoja tu na mwenzake alikuwa akimpigisha stori tu na kulala
Hakika huku ni kuziweka roho za watu rehani kwani dereva hutokea kuchoka na hivyo kushindwa kulimiliki gari na hatimaye kupelekea ajali
Namshukuru Mungu tulifika salama lakini pia nisingependa hali hii itokee tena kwani ni hatari
Naamini wawakilishi wa Superfeo mpo humu Jamiiforum fanyieni kazi hili tafadhali