Madereva wagoma kupinga "Unyanyasaji"

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
zaidi ya magari 200 yako katika eneo la mzani wilayani Biharamulo mkoani kagera kutokana na mgomo wa madereva wanaopinga unyanyasaji wa wadfanyakazi wa TANROADS katika kituo hicho

habari zinasema msururu wa zaidi ya kilomita mbili za magari uko katika pande zote za mzani huokufuatia mgomo wa madereva wa magari ya mizigo

Mgomo huo umeanza jana jioni ambapo magari ya abiri pamoja na yaleya kubeba wagonjwa ndio yanaruhusiwa na madereva hao kupita katika mzani huo

mgomo huo ulianza jana baada ya dereva mmoja kukatiwa kulipa faini ya shilingi milioni mbili baada ya lori alilokuwa akiendesha kukanyaga waya na kudaiwa kuuharibu

hali hiyo imewapelekea madereva wengine kupiga kuendelea na safari zao wakidai kwmaba watatakiwa pia kulipa faini kwani kila gari halina budi kukanyaga chini na hivyo kuwa katika hatari ya kukanyaga waya huo

aidha wamedai kuwepo kwa usumbufu katika mzani wa biharamulo kwani magari hayapimwi ifikapo saa 12 jioni licha ya barabara hiyo kuhudumia mataifa jirani ya rwanda, Burundi na Uganda, pamoja na kulazimisha magari kupimwa hata kama hayana mzigo

maneja wa TANROADS mkoani kagera Bw kalupale amewalaumu madereva hao kw akuendesha mgomo huku wakiwashawishi wengine kuacha kupita wakati hakuna gari iliyozuliwa isipokuwa lililokanyanga waya
 
Back
Top Bottom