Madereva wa Serikali na mabosi zenu kwanini mnapenda mnaendesha vibaya?

Charliemic

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
585
919
Naomba kujibiwa hili swali, hv ni kwani hakuna hata siku moja mnatoka nyumban kwenu mapema kwenda ofisini?

Kwanini kila siku mtoke kwa kuchelewa halafu njiani ni kukimbia, wrong overtake na kutoafuata vibao vya speed?

Hivi ninyi ambao ni mabosi ni kwanini mnafurahia mwendokasi ile hali mnahatarisha maisha yenu? Mnaweka uhai wenu rehani!

Halafu cha ajabu eneo lolote utakalokutana na gari la serikali, basi huwa lipo mwendo kasi ukiwauliza wanasema wamechelewa hivyo wanawahi
 
Yaani hao wasamehe tu. Tatizo ni Maboss zao na Transport Officers wa ofisi husika. Pia matrafiki wanawachekea sana.
 
Yaani hao wasamehe tu. Tatizo ni Maboss zao na Transport Officers wa ofisi husika. Pia matrafiki wanawachekea sana.
Naunga mkono hoja.

Pia unaweza kukuta ofisi ina uhaba wa magari halafu ina viongozi wengi wanaohitaji huduma ya usafiri, hapo Transport Officer analazimika kuwapangia usafiri kila asubuhi hao viongozi wakaletwe na gari, yaani gari linapiga ruti za kuwabeba viongozi.

Huko road dereva ataendesha fast ili awahi kutua mzigo na kwenda kuchukua mzigo mwingine tena.

Swali: Serikali inanunua magari mengi kila mwaka, yanaenda wapi?

Wenye nchi tushakubaliana na hali, tuishi hivi hivi
 
Ujinga na kukosa ustaarabu barabarani.
Wamuulize Makonda na kilichomtokea huko mikoa ya kusini.
Magari kadhaa ya serikali kugongana yenyewe, na Makonda kuingia mitini.
 
Back
Top Bottom