Madereva wa malori mnatutesa sisi tulio na gari ndogo

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Nimeona nilifikishe hili naona kama issue inazidi kuwa serious.

Siku hizi bwana hizi gari kubwa zinazobeba mafuta au zilizo na tela nyuma zimekuwa zikiwekwa ngao kubwa sana kwa mbele ngao ambazo pindi gari ndogo litapogongana na lori hata kwa speed ya 30kmph basi ujue gari yako ni ya kutupa na alafu hawa madereva huwa viburi sana na wanajiamini na hizo ngao.

Kuna siku nilikuwa na navara sasa nilikuwa nafosi king kuingia katika foleni jamaa alipiga horn huyo kwa sifa na kunipumulia alikuwa na bonge ngao kama treni jamaa aliniingiza mtaroni na kusepa sikutaka kumfukuzia kwa sababu tungesumbuana.

Kwa hili wenye magari ya kutembelea lazima tuliangalie kwa jicho la tatu.
 
Hawa jamaa ni wababe sana. Hata hawa wa mabasi makubwa, pia na hizi gari ndogo za abiria wanaitwa daradara/vi.ford nk. Utafikiri barabara ni za kwao, kama vile magari madogo hayalipii ushuru wa barabara! I hate them
 
Tafuta bastola mkuu mtu akizengua una mdito fasta.Ndiyo dawa yao shenz....hao

Umenikumbusha kuna jamaa alivamia Prado akataka kuwaua wakishua, hii! Jamaa aliacha chombo akatoka nduki mbaya sana, washua kwa hasira walipiga risasi tairi mbili kisha wakapotea.
 
Pia suala la honi liangaliwe, kuna magari hasa malori na mabasi kama yale ya uda... Eicher kama sikosei, yana honi kali ambazo zinaweza kusababisha hatari kwa watumiajiw wa barabara.
Mbaya zaidi ni kuwa madereva wa hayo magari wamekuwa wakitumia honi hizo kipuuzi kabisa, unakuta daladala iko kituoni dereva anapiga hayo mahoni eti anaita abiria.
 
Madereva mfuate sheria za barabarani.
Hata wamiliki wa hao magari wanajua mnapenda kufodi king kuingia ndio maana wameweka ngao ili mnaopenda kufosi kama wewe yawakute mtulie..

Ingawa hii mijamaa wakati mw8ngine inaudhi kwa kukupelekea mgari wao makusudi wanajua utawapisha tu
 
Madereva wa maroli wa Tanzania wanaitwa Boko haramu upande wa Zambia inakadiliwa kwa siku roli tatu zinadondoka njia ya Nakonde mpaka Kapiri Mposhi njia ni nyembamba wanakwenda speed ya hatari na kona za kali pia..madereva wengi huishia mtaroni..siku zingine zinadondoka mpaka zaidi ya 5 inategemeana na idadi ya viroba walivyokunywa Nakonde.
 
Endesha vizuri kwa adabu hio ngao haitakuhusu.....Kuna wakati huwa natamani niwe na ngao au lori bovu niwanyooshe kwa kuwapiga pasi watu kama nyinyi.
 
Ha! Ha! Ha! Wanaitwa boko haramu nimeipenda hii.
 
Ni kweli wana ubabe sana barabarani utafikiri sisi hatuna haki kwenye barabara. We ngoja tufufue treni yetu tuone kama watapata mizigo. Wananiudhi sana.

Yaani ukiwa mbele yao watakupigia honi hadi kero. Hizo mbio je!!! utawapisha mwenyewe bila kupenda maana hawana breki wanaweza kukugonga na kama ulivyosema magari yao hayataharibika ila lako.

Dawa yao iko jikoni.
 
ha ha ha!! Inategemea viroba walivyokunywa!!!!!! Umenichekesha sana.
Madereva wa maroli wa Tanzania wanaitwa Boko haramu upande wa Zambia inakadiliwa kwa siku roli tatu zinadondoka njia ya Nakonde mpaka Kapiri Mposhi njia ni nyembamba wanakwenda speed ya hatari na kona za kali pia..madereva wengi huishia mtaroni..siku zingine zinadondoka mpaka zaidi ya 5 inategemeana na idadi ya viroba walivyokunywa Nakonde.
 
Angalia unaweza mkwangua mtu akakuchukua akaenda kufunga nae ndoa.

Endesha vizuri kwa adabu hio ngao haitakuhusu.....Kuna wakati huwa natamani niwe na ngao au lori bovu niwanyooshe kwa kuwapiga pasi watu kama nyinyi.
 
Sasa bora uwe machana usiku ndo balaaa zaidi wengine wana mjitaa juu ya migari yao tofauti na hizi taa za kawaida sasa wengine akiiwasha full ni mwanzo mpaka mwisho wa safari sasa ukikutana naye dereva ka huyu lazima gari yako uiweke pembeni maana huwezi kuona
 
Kweli Kuna Baadhi Ya Madereva Wa Malori Ni Wakorofi, Kama Ilivyo Kwa Madereva Wengine Tu!! Mf. Ww Mleta UZI Huu Pia Sio MSTAARABU, Why Usiombe Kwanzaa Kwa DEREVA MWENZIO? Ili Akuruhusu Kuingia Ktk FOLENI!! Lkn Hapo Umejifanya Ww Ndiye Mwenye HARAKA Na Yeye Hana HARAKA Yoyote!!! Kumbukeni Hayo Magari Yanatoka Masafa Marefu Mno, Na Yaenda Kwa Timetable MAALUMU!!

Na Wkt Mwingine Utakuta Mzigo Unawasubiria, Coz BIASHARA Hiyo Imekuwa Ya Ushindani Na MATAJIRI Uwa Wanaandaa Oda Mapema Hasa Kwa Magari Ambayo Hayana MATENGENEZO Makubwa!!! Pia Kutokana Na Kutembea UMBALI Mrefu Madereva Wanakuwa Wamechoka, Hivyo WANAHITAJI Kuyafikisha Magari Hayo Sehemu Husika, Ili Wakapumzike Na Kuwaona Wake Na Wtt Zao!!!

Au Utakuta DEREVA Amepigwa Shot Ya Mzigo Alioupeleka Huko Alikotoka, Na TAJIRI Amekuwa Mbogo!! Sasa Yupo Ktk. Stress Zake Hizo Au Amechoka, Ww Na Kagali Kako Unaleta DHARAU!! Lazima Akubomoe Tu Mkuu!!! Hiyo Kazi Ya Kuendesha Magari MAKUBWA Yana Changamoto Mno!!!! Na Ukizingatia Huko, Walikotoka Wamepambana Mno Na Madereva Wa Mabasi!!!!

ALAFU Anafika Mjini Salama, Wanatokea Wa Daladala Na Private Ndogo Ndogo Wanasumbua, Tena Kwa DHARAU KIBAO!!
 
Ile ngao inawekwa kulinda bodi ya gari.. ni kama unavoiona mikonge ya safari na gari za jeshi. Gari yenye boneti ndefu au lori kubwa dereva kuona kitu cha chini si rahisi sana hasa kikiwa karibu nae zaidi ndio maana wanafunga ngao kubwa na nzito ili akigonga visiki taa na mwonekano wa gari usiharibike. Ila wenye ulimbukeni wa gari kama mleta uzi ndio wanahaha maana wanahisi ngao zmewekwa ili msitumie barabara.

Mind you ktk madereva wafata sheria barabarani madereva wa magari makubwa wana nidhamu na wanafuata sheria kwa asilimia kubwa, ila sie wenye vitz,funcargo na gari za uridhi au za kuazima ndio tukiwa barabarani tunataka show off ili kila mtu ajue na ww leo umedrive, na ndio tunaishia kupushiwa mtaroni kama sio kubamizwa kabisa na magari makubwa.
 
Sasa bora uwe machana usiku ndo balaaa zaidi wengine wana mjitaa juu ya migari yao tofauti na hizi taa za kawaida sasa wengine akiiwasha full ni mwanzo mpaka mwisho wa safari sasa ukikutana naye dereva ka huyu lazima gari yako uiweke pembeni maana huwezi kuona

Kweli Wapo Madereva Wanaozitumia Vibaya Hizo Taa, Na Wengine Wanaozitumia Kwa Kuwapa Onyo Madereva Wa Magari Madogo Walio Na Viburi Kwa Kuwasha Full Hata Wanapoona Mbele Kuna Gari Linakuja, Tena Hizi Taa Zao Za Kisasa Ni Balaa!! Sasa Hapo Ndio Na Wao Uzitumia Kuwaonya!! Ila Wengi Uzitumia Maeneo Yenye Misitu Mikubwa Kama Ya SAO HILL, MAENEO Yenye Wanyama Pori Wanakatiza Barabara!!!
 
Back
Top Bottom