Diesel generator
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 706
- 660
Wenye gari mnamatatizo sana ya uelewa. Ivi mtu unakopa, inanunua gari, kisha unamkabidhi mtu kisa analeseni!! Nilinunua bajaji na nilipokamilisha vibali niliipaki mbele ya nyumba nikaweka kibao inaitaji dreva. Wakaja wengi sharti langu unapaswa kulipa malipo ya mwezi mmoja. Wakasema hutapata mtu! Ilikaa siku nane akatokea mtu anaeitaji ,akanilipa pesa ya wiki tatu. Huwezi weka milioni saba alafu umpe mtu bila kushea chochote!! Hatakuwa makini!! Akishea atatunza chombo, akizingatia atoe pesa yake, apate faida. Ndugu huu mwaka wa nne nina bajaji tatu. Zote nalipwa pesa ya mwezi kabla ya kazi. Sina tatizo.