Swali kwa madereva wenzangu.
Hivi ni hatua gani mnachukua ikiwa umekutana na gari kubwa( ROLI ) limepaki kwenye njia upande wako
(LEFT WAY) ikiwa wewe na waliopo nyuma yako mpo speed?
Binafsi leo ninekutana na iyo shida, niliamua kuovertake (uvivu wa kupunguza gia ) lakini kabla sijaingia mazima nilipishana na Land Cruiser ilikua kibati na sikua nimeona maana mbele ya ile njia kuna kona ndogo, nilipaki pembeni baada ya tukio na nikawaza ni vipi nifanye sikunyingine nikikutwa na hali kama hii ila sijapata majibu.