ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,556
Jamani ni haki kweli mtu umelipa Tsh 650/=then mnasubiri gari kituoni kwa muda lakini baadae mnaona gari inakuja mnajiandaa kujiweka tayari ghafla linapokaribia dereva anaongeza spidi anaamua kupitiliza kituo na kuwaacheni midomo wazi!..cha ajabu hilo basi lipo na watu kumi tu ,tupu kabisa!sijui nini kimewakuta hawa ndugu?
Jioni pale kituo cha Gerezani wasafiri mmerundikana mkisubiri usafiri hasa wa Kimara/Mbezi gari zingine zimepark pembeni kabisa madereva wanapiga story nyie wasafiri mnazidi kurundikana...basi hata hapo mnaweza shangaa dereva mmoja anaingia ktk gari anaondoja peke yake bila abiria tena kwa mbwembwe na kwa speed kali!
Tunaomba wahusika kama ni Tamisemi tuondoleeni usumbufu tuupatao kila siku,,nauli tunayotoa ni kubwa basi ilingane na huduma tunayostahili ikibidi na magari yaongezwe njia zote,maana mpaka sasa njia iliyofanikiwa ni moja tu ya gerezani=muhimbili.
Tunaomba tutendewe haki,madereva waache kutunyanyasa vituoni ikibidi wawe na msimamizi wao atakayekua anawa monitor muda wote.