BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Madeni yatoboa bakuli la bajeti Mwandishi Wetu Toleo la 357 11 Jun 2014 Uhalisia wavurugwa, ni bajeti ya tarakimu WAKATI Bajeti Kuu ya Serikali ya takriban Sh. trilioni 19.6 ikisomwa rasmi Alhamisi wiki hii, bakuli linaloshikilia bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 limeanza kutoboka kwa madeni makubwa. Tayari Serikali imekwishakomba trilioni 7.1 kutoka katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii bila kuzirejesha kwa muda mrefu sasa, na zaidi ya hapo, nyongeza ya takriban shilingi bilioni 787 zimechotwa tena kutoka katika michango ya wafanyakazi. Katika deni hilo la trilioni 7.1, Mfuko wa PSPF ndiyo unaoidai Serikali fedha nyingi zaidi, kiasi cha mfuko huo kuwa katika hatari ya kufa ifikapo mwakani kama fedha hizo hazitarejeshwa. Tayari Bunge kupitia kamati yake ya mashirika ya umma limewahi kupigia kelele suala hilo ambalo hata hivyo, Serikali imelipuuza.
Katika mchanganuo huo wa shilingi trilioni 7.1, mfuko wa PSPF hadi kufikia Machi 31, mwaka huu, unaidai Serikali 4,827,800,000,000.00, LAPF unadai shilingi 207,700,000,000.00, NSSF 1,333,600,000.00, PPF shilingi 288,600,000,000.00, GEPF 18,000,000,000.00 na NHIF shilingi 458,600,000,000.00. Kutokana na hali hiyo, taarifa kutoka serikalini zinaeleza kwamba mbinu kadhaa zimekuwa zikiandaliwa ili kufukia pengo hilo na hatimaye mifuko inayodai mabilioni ya fedha iweze kuokolewa kutoka katika hatari ya kifo hasa PSPF.
Hata hivyo, mbinu hiyo mpya imeanza kuzua mvutano wa chini kwa chini miongoni mwa watendaji wakuu serikalini, wakiwamo baadhi ya makatibu wakuu. Mpango mpya Mpango huo mpya unahusisha kanuni za ukokotoaji mafao ambazo itatakiwa mifuko yote itumie kanuni moja ya utoaji mafao. Kinachozua mvutano miongoni mwa watendaji waandamizi serikalini ni ukweli kwamba, wale waliokuwa wakinufaika na kanuni za awali za ukokotoaji viwango vyao vya mafao vitashushwa ili kulingana na wengine lakini wakati huo huo, wale wanaopata mafao kidogo, yataongezwa.
Yaani wenye kingi watapunguziwa na wenye kidogo kuongezwa na hapo ndipo kilipo kiini cha mgongano wa maslahi miongoni mwa watumishi waandamizi serikalini ambao wengi wamekuwa wakipata mafao ya kutosha tofauti na wengine. Kwa mfano, kwa kuzingatia ulinganisho wa malipo ya mkupuo wa pensheni, mfanyakazi mwenye mshahara wa shilingi milioni moja, atakayefanya kazi kwa miaka 30 badala ya kupata malipo ya mkupuo (mafao) ya shilingi 12,600,000 pamoja na pensheni ya mwezi ya shilingi 525,000.00. Mifuko iunganishwe Hatua nyingine inayotarajiwa kupendekezwa na ambayo imezua mvutano ni kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuondoa ushindani kati yao. Taarifa zilizopo zinabainisha kwamba mifuko hiyo inapendekezwa kuunganishwa ili kupata mifuko mitatu.
Inapendekezwa kwamba mifuko hiyo iunganishwe kutoka mitano ya sasa hadi mitatu ili wanachama wachangiaji wawe wengi, kwamba kuwe na Mfuko wa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma, Mfuko wa Wafanyakazi wa Sekta Binafsi na Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote. Ni katika mapendekezo hayo, inaelezwa kwamba wizara ambazo mifuko ya sasa ipo chini yake zimekuwa zikipinga mapendekezo hayo kutokana na wizara hizo kwa namna moja ama nyingine, kunufaika na usimamizi wake katika mifuko husika.
Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo Vijana inayosimamia mfuko wa NSSF, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayosimamia mfuko wa LAPF pamoja na Wizara ya Fedha (PPF, GEPF na PSPF). Mfumo wa utendaji Kwa mujibu wa mapendekezo ambayo gazeti hili limeyaona, inashauriwa kwamba mifuko miwili inapendekezwa iwe chini ya uangalizi wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana na kwamba mfuko wa Bima ya Afya ndiyo uwe chini ya uangalizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Vile vile NSSF katika uunganishaji huo iwe maalumu kwa ajili ya sekta binafsi kwa sababu sehemu kubwa ya wanachama wake ni kutoka sekta binafsi, na mifuko mingine iunganishwe kuunda Mfuko wa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma. - See more at: Raia Mwema - Madeni yatoboa bakuli la bajeti