Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Posts
10,590
Reaction score
7,951
Wana JF wenzangu, ebu angalieni mauza uza haya ya nchi yetu. Hivi kweli tuna utawala mathubuti hapa nchini? Yaani nchi inaibiwa kweupee na wajanja, kiongozi yuko bize na misafara isiyo na faida. Hapa habari imetolewa na CAG juu ya ufilisi wa hii nchi, sote tunajuwa hakutachukuliwa hatua yeyote ile. Je huu ni uungwana jamani?


headline_bullet.jpg
Ni mfuko wa wafanyakazi wa serikali
headline_bullet.jpg
Shilingi trilioni 6.48 hazijulikani ziliko
headline_bullet.jpg
Yakopesha Takukuru, Bodi ya Mikopo 67bn/- bure


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amewasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, mwaka 2012, ikionyesha hali mbaya kwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali Kuu (PSPF) ukikadiriwa kuwa na hasara ya Sh. trilioni 6.487.Mbali na hali hiyo ya kutisha katika usimamizi na uendeshaji wa mfuko wa kutegemewa kwa watumishi wa umma watakaostaafu, ukaguzi wa CAG kwa ujumla umegundua matatizo makubwa katika kusimamia fedha za umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Utouh alisema pamoja na serikali kuchukua hatua mbalimbali ambazo zimesaidia kupunguza baadhi ya kasoro katikausimamizi wa fedha za umma, lakini bado zinapotea.

Utouh alisema katika ukaguzi wa PSPF alibaini kwamba ukadiriaji thamani uliofanywa na Kampuni ya Uthaminishaji Genesis Actuarial Solution Limited na kutoa ripoti 2010, uliashiria kwamba uwezo wa kifedha wa PSPF uliendelea kushuka.

"Ukadiriaji thamani ulibaini hasara halisi ya Shilingi trilioni 6.487, hivyo Mfuko uko kwenye hatari ya kutoweza kujiendesha kama juhudi hazitachukuliwa na serikali," alisema Utouh na kuongeza:

"Pamoja na mfuko kuwa katika hali mbaya kifedha, nilibaini kuwa mfuko ulitoa mikopo kwa mashirika ya umma na taasisi nyingine ambayo yamedhaminiwa na serikali yenye jumla ya Shilingi bilioni 67.2 bila riba."

Taasisi za serikali ambazo zilinufaika na mkopo kutoka PSPF ni Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambayo bado inadaiwa Sh. 54,644,657,534; Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambayo inadaiwa Sh. 6,678,150,000; Tan Power Resources inayodaiwa Sh. 5,421,551,370 pamoja na taasisi isiyo ya kiserikali ambacho ni Kiwanda cha Madawa Tanzania kinachodaiwa Sh. 435,057,632.

MABILIONI KWENYE H/SHAURI YALIPWA KINYEMELA
Aidha, alisema halmashauri 22 kati ya 134 zilifanya malipo yenye jumla ya Sh. 1,509,529,810 ambayo hayakuwa na hati za malipo wakati malipo yenye hati pungufu yalibainika katika halmashauri 74 yenye jumla ya Sh. 3,367,208,321.

Aidha, alisema vitabu 2,990 vya stakabadhi za mapato kutoka halmashauri 36 havikutolewa kwa ajili ya ukaguzi na kwamba ulegevu katika udhibiti wa ndani wa halmashauri 30 ulisababisha jumla ya Sh. 8,008,669,844 kutoka kwa wadaiwa wa kodi mbalimbali za vyanzo vya ndani vya mapato kutokusanywa kama kodi ya huduma, ushuru wa mazao na ushuru wa hoteli.

Pia halmashauri 56 zilikuwa na jumla ya Sh. 4,466,028,478 zikiwa ni mapato yaliyokusanywa na mawakala, lakini yalikuwa hayajawasilishwa kwenye halmashauri. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa halmashauri 17 hazikukusanya kodi ya majengo kiasi cha Sh. 4,345,570,497 sawa na asilimia 38 ya makisio.

Jumla ya Sh. 650,356,980 katika halmashauri 20 zililipwa kwa taasisi mbalimbali na katika ngazi za vijiji, lakini fedha hizo hazikuthibitika kupokelewa kutokana na kukosekana kwa stakabadhi za mapokezi.

MISHAHARA HEWA
Ukaguzi wa CAG ulibaini kuwa Sh. 693,132,772 zililipwa katika halmashauri 24 kama mishahara kwa wastaafu, watoro, watumishi waliofariki, watumishi walioacha kazi au walioachishwa kazi kupitia akaunti zao za benki.

Vile vile kutokana na kuwapo na kiwango cha chini cha uzingatiaji wa taratibu na Sheria ya Manunuzi, manunuzi yenye thamani ya Sh. 443,107,149 yalifanyika katika halmashauri 25 kutoka kwa wauzaji wa bidhaa na huduma bila ushindani wa bei huku ununuzi wa bidhaa na huduma wa thamani ya Sh. 541,013,405 ukifanyika katika halmashauri 24 bila kibali cha Bodi ya Zabuni.

Alisema mapato ya Sh bilioni 3.9 yalipotea hatika Halmashauri ya Arusha kutokana na halmashauri kutoza bei ya chini ambayo ilikuwa na tofauti kubwa kulinganisha na bei ya soko na kukusanya kodi za vyumba na vibanda walivyopangisha ambavyo vinamilikiwa na halmashauri. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hati za malipo ya Sh. 4,996,685 na viambatanisho vyenye jumla ya Sh. 1,075,263,998 havikuwasilishwa wakati wa ukaguzi.

Pamoja na mapungufu katika usimamizi wa fedha, Utouh alisema pia kuwa changamoto katika utekelezaji wa bajeti na kutoa mfano kwamba Bunge lilipitisha Sh. 595,064,422,505 za maendeleo katika halmashauri 113, lakini ni Sh. 345,568,067,477 tu ndizo zilizopokelewa na halmashauri husika na kufanya kuwapo upungufu wa Sh. 249,498,355,027 ambayo ni asilimia 42.

Kwa mujibu wa Utouh, jumla ya Sh. 2,561,882,820, zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za Mfuko wa Maendeleo wa Jimbo, hazikutumika katika halmashauri 29 kutokana na fedha hizo kutokupelekwa kwa wakati.

Hata hivyo, alisema licha ya kuwapo kwa mapungufu, hatua ambazo zimeanza kutelekezwa na serikali zimewafanya watumishi wengi katika halmashauri kuogopa kujihusisha katika vitendo vya ubadhirifu.

UJANGILI TISHIO
Ukaguzi wa CAG ulibaini kuongezeka kwa matukio ya uwindaji haramu katika Hifadhi za Taifa (Tanapa). Utouh alisema katika kupitia ripoti za robo mwaka za idara za ulinzi za Tanapa ilibainika kuwa vitendo vya uwindaji haramu hususani tembo vimeongezeka.

Alisema taarifa kutoka mbuga saba zinaonyesha kuwa tembo 110 waliuawa mwaka 2011/12 na kuongeza kuwa hali hiyo ina athari kubwa katika juhudi za serikali za kuendesha utalii na hatimaye kuathiri pato la taifa.

MKATABA WA TBC, SMT
Utouh alisema kuwa ukaguzi wake ulibaini kwamba mwaka 2010 Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) lililipa Sh. milioni 618.3 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa niaba ya Kampuni ya Star Media (SMT) kwa ajili ya leseni ya biashara.

Alisema ukaguzi pia ulibaini kwamba kampuni hiyo ina mkataba wa utendaji uliosainiwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) huku SMT ikiwa imepewa msamaha wa kulipa leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka kumi. "Kiasi hicho cha fedha kilicholipwa na TBC kingeweza kuwa ni sehemu ya hisa za shirika kwa SMT kama kusingekuwapo na msamaha wa leseni ya biashara. Malipo haya yaliyolipwa kimakosa na TBC hayajarejeshwa na TCRA," alisema.

CAG KUKAGUA MISAMAHA YA KODI
Katika hatua nyingine, kuanzia mwaka ujao wa fedha, CAG ataanza kukagua misamaha ya kodi kwa lengo la kuangalia manufaa yake.

Utouh alisema anao uwezo huo kisheria na kwamba ofisi yake imejipanga kuitekeleza.
"Kwa kuwa fedha ambazo zingelipwa kutokana na misamaha ya kodi ni fedha za serikali, ambazo zinatolewa kama ruzuku kwa wanaopewa misamaha hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameamua kukagua kwa kina misamaha yote ya kodi kuanzia mwaka wa 2013/2014 kwa madhumuni ya kuangalia manufaa ya misamaha hii kwa uchumi wa Taifa letu," alisema Utouh.

MAPENDEKEZO YA CAG
Kutokana na kasoro zilizobainika, CAG ametoa mapendekezo mbalimbali kwa serikali kama njia ya mapato likiwamo la mikataba ya kuchimba madini kujadiliwa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na ushauri kutolewa kwa waziri husika kabla ya kusainiwa.

Utouh anapendekeza hati za misamaha ya kodi ziwekwe bayana kwamba msamaha wa kodi ni wa muda gani, unaanza lini na kumalizika lini. Pia misamaha ya kodi iainishwe ikionyesha malengo yanayokusudiwa na kuwa na utaratibu wa serikali wa kusimamia utekelezaji wake.

Kwamba mikataba yote yenye vipengele vya misamaha ya kodi ipitiwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya ushauri kabla ya kusainiwa na pande husika. Baada ya CAG kuwasilisha taarifa hiyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilisema misamaha ya kodi bado ni sugu na kwamba kuanzia Juni mwaka huu iwekwe wazi na ukaguzi utasaidia kuweka wazi ili aliyepewa ajulikane.

Ilisema kuwa deni la Taifa linazidi kuongezeka na kamati ilishatoa maelezo bungeni kutaka lifanyiwe ukaguzi, lakini serikali imeendelea kuwa kimya.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, ripoti ya CAG imebainisha kuwa bado kuna matatizo makubwa katika kusimamia rasilimali za nchi na kusema kuwa kwa kuanzia itamuita Waziri wa Nishati na Madini pamoja na wasaidizi wake kuwahoji kuhusiana na kitendo cha kutotoa taarifa za ukusanyaji wa maduhuli.

Nayo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilieleza kuwa upungufu mkubwa wa watumishi katika halmashauri unafanywa makusudi na mtandao ulioko Tamisemi na halmashauri husika kwa lengo la kuhujumu fedha za halmashauri.

Kamati hiyo ilieleza kukerwa na uamuzi wa kuzuia ripoti ya CAG isijadiliwe bungeni kwamba lengo lake ni kutaka kuwalinda watumishi na viongozi wake kutokana na mwaka jana kuwang'oa mawaziri sita.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo, alisema wabunge hususani kamati za PAC na LAAC hawapaswi kulegeza kamba katika suala zima la uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.


CHANZO: NIPASHE (IPP Media Group)

 
Kwanini makato yetu yakopeshwe TAKUKURU? Imedeliver kitu gani so far tangia ianzishwe? Inafanya biashara gani kiasi cha kukopeshwa pesa? Nchi hii nimenawa mikono/
 
Kama mtu anaeza kuchagua vitu personal kama dini, spouce, kazi, makazi etc kwanini alazimishwe kuingia kwene mifuko ya hifadhi ya jamii bila ridhaa yake? kuna nini kimejificha ktk ubabe wa serikali kulazimu wafanyakazi wake kuingia kinguvu ktk mifuko hii? Je ni kweli kuna faida yoyote kwa mchangiaji? au ni serikali kujifanya inajali wafanyakazi wake ilhali sote tunajui hii ni miradi(uizi wa wazi) wa wachache. Ni wakati watz tuamke tudai chetu, hamna atakaye-serve haki yetu kwene silver platter.
 
Serikali hii badala ya kuwaondolea wananchi wake umaskini yenyewe ndio inawafanya wawe maskini zaidi kwa ku guarantee mikopo ambayo ni dhahili haiwezi kulipwa na hivyo sisi walipa kodi ndio itatubidi kuongezewa kodi ili kulipa mikopo mibovu iliyodhaminiwa na hii serikali mbovu!! Mnawadhamini TAKUKURU wachukue mabillioni ya shillingi ,watakuja kulipa kwa vyanzo gani kama sio kodi zetu?

Serikali kwa kutufumba macho ilianzisha National Social security fund Regulatory Authority chombo ambacho kimepewa jukumu la kuthibiti mwenendo na matumuzi ya fedha za mifuko ya jamii. Unfortunately, chombo hiki hakifanyi kazi yake kama ilivyokusudiwa kwani hakina uongozi mzuri toka kwenye bodi yake ambayo haina Mwenyekiti mpaka watendaji wake; na ndio maana fedha za watumishi ambazo zingewafaa baada ya kustaafu zinatumiwa visivyo!!!
 
Hii ishu itakuja leta vit, akina mukoba na mgaya mpo haya wafanyakazi wenu wanaibiwa, maana nyie ndio majembe makuu.
 
Haiya, our fear has been confirmed. Nchi ya ajabu sana hii, kwa mujibu wa duru kutoka hukohuko PSPF zinasema mfuko utakolapsi baada ya miaka 3.
Lakini mi nawalaumu watz wenyewe, sijui wanasubiri mpaka wadhulumiwe nini ili wachukue hatua za kuiondoa serikali hii dhalimu isiojali chochote bali matumbo yao/
 
Ngoja kwanza niache mlumbane, ccm ina wenyewe..!
Hapa nani analumbana? mlipakodi yeyote ambae yuko serious ataupitia uzi huu na kuufanyia kazi ujumbe badala ya kujitia ukingwendu na kutoa matapishi yasiomeki sense/
 
Hapa nani analumbana? mlipakodi yeyote ambae yuko serious ataupitia uzi huu na kuufanyia kazi ujumbe badala ya kujitia ukingwendu na kutoa matapishi yasiomeki sense/
Akili yako ni ndogo ndo maana hujanielewa. Malumbano (serious discussion) yapo and they are genuine, lakini ccm ina wenyewe and we must kick them out.! Siku nyingine usikurupuke.
 
Akili yako ni ndogo ndo maana hujanielewa. Malumbano (serious discussion) yapo and they are genuine, lakini ccm ina wenyewe and we must kick them out.! Siku nyingine usikurupuke.

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, imetoa wiki moja kwa Serikali iwe imelipa Sh50 bilioni kati ya Sh716 bilioni inazodaiwa na Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali (PSPF) na ieleze jinsi itakavyolipa sehemu ya deni iliyosalia.

Pia, ndani ya muda huo, Serikali, Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Jamii (SSRA), zinatakiwa kukaa pamoja kujadiliana jinsi mkopo wa Sh14 bilioni zilizotolewa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zitakavyolipwa.


Kikao cha Kamati ya Hesabu za Serikali kilichoketi hapa jana kilifikia uamuzi kuwa Serikali inatakiwa kubeba madeni yote inayodaiwa PSPF kwa sababu hilo ni jukumu lake kwa mujibu wa sheria.


Uamuzi huo ulitolewa kamati hiyo jana baada ya kukutana na pande zote zinazohusika na kwamba, ndani ya wiki moja Serikali inatakiwa kupeleka taarifa kwenye kamati hiyo kueleza hatua iliyofikiwa. Katika maelezo yake, Serikali inatakiwa pia kuainisha jinsi watakavyoandaa mfumo wa ulipaji madeni yote ya mfuko huo yanayofikia Sh6.4 trilioni.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu alisema awali watumishi wa Serikali walikuwa wanalipwa mafao bila kuchangia, lakini mwaka 1999 iliamriwa kuanzishwa mfuko huo na Serikali kuamuru kuwaingiza watumishi ambao walikuwa hawachangii.

Mayingu alisema wakati mfuko unaanzishwa, wataalamu walishauri Serikali kuweka Sh250 bilioni kwa ajili ya malipo ya watumishi waliohamishwa kutoka kwenye mfumo wa zamani, lakini haikufanya hivyo na kusababisha deni hilo kukua na ilipofika mwaka 2003 deni hilo lilikuwa limefikia Sh933.4 bilioni.


Alisema tathmini ya pili ilifanywa mwaka 2006, ambayo ilibainisha Serikali ilikuwa inadaiwa Sh716 bilioni lakini tathmini hiyo ilitiliwa shaka na mwaka 2007 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), alitakiwa kufanya ukaguzi maalumu na alibainisha kuwa deni halisi lilikuwa limefikia Sh3.3 trilioni.


Hata hivyo, Serikali ilikuwa imekubali kulipa Sh71 bilioni kila mwaka kwa muda wa miaka 10, lakini ililipa Sh30 bilioni tu na kuacha kulipa na kusababisha deni kuendelea kukua.


Mayingu alisema tathmini ya tatu ilifanyika mwaka 2010, na kuonyesha deni hilo linafikia Sh6.4 trilioni, huku uwezo wa mfuko kulipa mafao ukishuka hadi asilimia 10 chini ya kiwango cha asilimia 40 kinachoruhusiwa kwa mfuko wa pensheni. Hatua hiyo inaashiria kufilisiwa kwa mfuko.

Kauli ya Serikali
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene aliomba radhi kwa Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake na kuahidi kusimamia ulipaji wa deni hilo ingawa alisema si rahisi Serikali kulipa deni hilo kwa mkupuo kwani ikifanya hivyo itaathiri baadhi ya shughuli, huku akiomba mwaka huu ilipe Sh50 bilioni.


"Jambo hili ni nyeti na limefika sehemu ambayo lazima lishughulikiwe, hivyo naomba mniamini nitasimamia fedha hizi zilipwe," alisema Mbene.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka aliwatoa hofu wanachama wa mfuko huo kuwa hakuna atakayekosa mafao yake kwa sababu kisheria Serikali ndiyo mdhamini wa mifuko ya jamii.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisema bado Serikali inapiga blahblah na haijawa na dhamira ya kulipa deni hilo. Alisema watumishi wote wa Serikali ni wanachama wa mfuko huo, lakini hakuna uzito wa kulipa madai hayo.

Source
 
Sasa mmepata jibu lile fao la kujitoa kwa nini hawa wapumbavu walikuwa wana ng'ang'ania
 
Baada ya kupata jibu?
Kukiwa na provision ya consensual subscription, ndio itakua mwisho ya hii mifuko ambayo obviously ni miradi ya wajanja wachache kupiga bingo without consequences/
 
dah inauma, ndio maana serikali inakuwa kimya..........., tutakutana bungeni
 
tatizo haya mambo yanapita tu, inakuwa kama tunaanglia Cinema tusiyo na uamuzi nayo, sana sana ni kushangilia ua kisikitika!
 
Nakanusha, haijakaribia kifo (limesimama kwenye nguzo imara bado).

Tamko/Shinikizo la kukataa wanachama wasiruhusiwe kujitoa hadi hapo watakapo staafu ndo naanza kulielewa kwa sasa

Tupeni taarifa za mifuko mingineyo (NSSF, etc)
 
Wajanja wamekula Trilioni kazi kwenu waajiriwa


Si kila mtu anaweza kureport mambo ya fedha... hawa waandishi wetu hawa!!! Ukisoma magazeti ya kingereza ndo utaona utofauti/upotoshaji wa habari.... Hawa jamaa wameanza mwaka 1999 wanalipa watu walioanza kazi kuanzia miaka ya sabini... kuidai serikali hayo mabilioni ndo kuwa yameliwa?? Ndio kusema hazijilikani hazipo?? Acturial deficit ndio loss??... Wawa waandishi wa DSJ!! Janga!
 
[h=2]Serikali yakiri 'kuiua' PSPF[/h]


Bunge limeingilia kati kuunusuru Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali (PSPF), ambao umeelezwa kwamba umefilisika huku serikali ikikiri kuwa chanzo cha hali hiyo, na kuomba radhi.


Katika kufilisika huko, PSPF imepoteza uwezo wake wa kuwalipa wastaafu mafao yao kwa kiwango cha kutisha.

“Naomba niombe radhi. Tumekuwa si waungwana, kwani tulijicomit kwanini tusitimize? Nikubalieni na consolidated fund. Naomba mniamini, mnipe muda nikaendelee kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Serikali inashindwa kulipa hizi fedha kwa pamoja kwani ina majukumu mengi,” alisema Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, katika mkutano ulioshirikisha Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Hazina.

Uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hao mafao yao umeelezwa kuwa umeshuka kufikia asilimia 10 kutoka asilimia 40, kutokana na upungufu wa thamani ya mfuko huo unaofikia Sh. trilioni 6.4 hadi sasa.

Fedha hizo zinatokana na malimbikizo ya madeni sugu na ya muda mrefu ya fedha za PSPF, zilizokopwa kwenye mfuko huo na baadhi ya taasisi, zikiwamo za umma kwa kudhaminiwa na serikali.

Taasisi za serikali zinazodaiwa na PSPF ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Kiwanda cha Dawa (TPI), Kagera Sugar Limited, Kiwira Coal Mine, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Chuo Kikuu Dodoma (Udom), ujenzi wa nyumba za polisi, Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), 21st Century Textile, ujenzi wa ukumbi wa Bunge, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi (TISS).

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa.

Hatua hiyo ilifikiwa jana na Bunge kupitia Kamati yake ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) baada ya kuiagiza serikali kuhakikisha inaanza kulipa madeni hayo na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kupelekwa mara moja kwenye kamati hiyo ndani ya wiki hii.

Katika maagizo hayo ya PAC, la kwanza linaitaka serikali kulipa fedha hizo kwa kuanza kutoa Sh. bilioni 50 kwa mfuko huo.

Maagizo hayo yalitolewa na PAC baada ya kukutana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PSPF, Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Wizara ya Fedha, kutaka kupata picha halisi ya tatizo la mfuko huo na namna ya kulipatia ufumbuzi, katika Ofisi za Bunge, mjini hapa jana.

Mayingu alisema katika kikao hicho malimbikizo ya madeni hayo yalianza baada ya serikali kushindwa kulipa Sh. bilioni 250.

Alisema fedha hizo zilitakiwa zilipwe na serikali baada ya kuwaingiza watumishi wake kwenye mfuko huo ulipoanzishwa mwaka 1999.

Mayingu alisema kabla ya PSPF kuanzishwa, watumishi wa umma wastaafu walikuwa wakilipwa fedha za mafao yao kupitia Hazina.

Alisema kikosi kazi kilichoundwa na serikali mwaka 1997, kilifanya tathmini na kutabiri kwamba, kama serikali isingekuwa imelipa fedha hizo (Sh. bilioni 250), kufikia mwaka 2006, upungufu wa thamani ya fedha za PSPF ungefikia Sh. bilioni 658.

Alisema pia mwaka 2003 ilifanyika tathmini nyingine na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu ni Sh. bilioni 933.4

Vilevile, alisema tathmini nyingine ilifanyika mwaka 2007 na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu ni Sh. trilioni 3.3.
Alisema kutokana na upungufu huo, uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu kipindi hicho ulishuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 43.

Mayingu alisema kutokana na malimbikizo ya madeni hayo, hivi sasa upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu umefikia Sh. trilioni 6.4.

“Thamani ya sasa ya kuwalipa wastaafu ni Sh. trilioni 6.4. Wanachama wanaongezeka, muda unaongezeka na nakisi (upungufu) inakwenda, inakua. Tunaweza kufikia mahali tukashindwa kulipa,” alisema Mayingu.

Alisema hali hiyo inatokana na uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hivi sasa kushuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 10. Kutokana na hali hiyo, alionya kuwa kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa.

Alisema kuanzia mwaka 2010, serikali ilichukua dhima ya kulipa Sh. bilioni 71, lakini hadi sasa haijalipa Sh. bilioni 716.

“Ukishaonyesha kushindwa kuwalipa watumishi imani itawavunjika,” alionya Mayingu.

Alishauri kwamba, pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni hayo, serikali pia inapaswa kuongeza michango kutoka asilimia 15 za sasa hadi asilimia 25 ili kufidia upungufu uliopo.

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, alisema kulingana na tathmini waliyoifanya, wamebaini kuwa PSPF ina hali mbaya. Alisema kutokana na hali hiyo, Machi, mwaka huu, walitoa mwongozo, ikiwamo kutaka wanachama wa mfuko huo kutolipwa kiasi chote, bali kile tu walichochangia.

Alisema mbali na mwongo huo, pia wanashauri pamoja na mambo mengine, serikali kulipa Sh. trilioni 1.2, ambazo ni sawa na asilimia 70 ili malimbikizo ya madeni kufidia upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu mafao yao.

“Lazima bajeti ya mwaka huu ionyeshe hilo,” alisema Irene.
Hata hivyo, alisema hakuna mwanachama atakayepoteza haki yake na kusisitiza kuwa zile Sh. bilioni 70 lazima zilipwe.

Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, alisema wanakubali kwa asilimia 100 kwamba, PSPF inaidai serikali. Hata hivyo, alisema kwa sasa hivi serikali haiwezi kutoa kiasi hicho cha fedha kwani kinaweza kuathiri mipango mingine ya maendeleo.

“Itabidi tupangepange hivyo. Mwaka huu tutatoa Sh. bilioni 50. Kuanzia sasa hivi deni hili tutalipa kipaumbele. Tutajitahidi,” alisema Mbene na kuongeza:

“Sehemu ambayo haijalipwa ya mwaka 1999, tutahakikisha tunaipeleka kwenye bajeti, lakini siwezi kutaja namba. Siwezi kusema ukweli zaidi ya huo.”

Alisema suala hilo kwa sasa limekuwa nyeti, hivyo jukumu la serikali hivi sasa ni kufuatilia madeni, yakiwamo yanayolipwa na wanafunzi wa elimu ya juu na Takukuru ili wailipe PSPF.

Pia alisema mapendekezo yote yaliyotolewa na PSPF na SSRA katika kikao hicho, likiwamo lile la kutaka rasilimali zilizopo wizarani kuhamishiwa kwenye mfuko huo yatafanyiwa kazi.

“Naomba niombe radhi. Tumekuwa si waungwana, kwani tulijicomit kwanini tusitimize? Nikubalieni na consolidated fund. Naomba mniamini, mnipe muda nikaendelee kulitafutia ufumbuzi wa kudumu. Serikali inashindwa kulipa hizi fedha kwa pamoja ina majukumu,” alisema Mbene.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Elizabeth Nyambibo, naye aliungana na Mbene akisema wanakubali madeni, ambayo PSPF inaidai serikali.

Alisema kama serikali ingetoa hizo Sh. bilioni 250 suala hilo lisingefika lilipofika leo na kusema kikwazo kikubwa kilichokwamisha ni uwezo wa kulipa.

Alisema tayari wameshaanza kulipa deni hilo kwa kutoa awamu ya kwanza Sh. bilioni 10 na awamu ya pili Sh. bilioni 20 na kwamba, katika mwaka huu mpya wa fedha watatoa Sh. bilioni 50.

Hata hivyo, alisema anavyofahamu yeye ni kwamba, tangu mwaka 1999 deni, ambalo serikali inadaiwa ni Sh. bilioni 250, hivyo, akaomba ufafanuzi wa hiyo nakisi ya Sh. trilioni 6.4.

Mmoja wa viongozi wa PAC, akijibu hoja hiyo, alisema baada ya kuiagiza Wizara ya Fedha kufuatia kikao kati ya iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na PSPF Machi 25, mwaka juzi, ililipa Sh. bilioni 10 na baadaye ikalipa Sh. bilioni 20 kati ya Sh. bilioni 70.

Alisema hatua hiyo iliifanya POAC kuishangilia serikali bungeni, lakini baada ya hapo, haijalipa tena.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, alisema hajui sababu ya serikali kutokuwa muungwana, kwani haionyeshi dhamira ya dhati ya kulipa malimbikizo ya madeni hayo.

Alisema PSPF hawana matatizo, bali yenye matatizo ni serikali, kwani Sh. bilioni 250 hazikuwa fedha nyingi kwake, lakini wameshindwa kuzitoa.

“Ninachokiona hapa ni kwamba, watu wameshapiga sana. Tuisihi serikali ilipe fedha hizi kila mwaka,” alisema Filikunjombe, ambaye ni Mbunge wa Ludewa (CCM).

Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, alisema deni hilo ni la taifa, hivyo dawa yake ni kulipa.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Zainab Kawawa, alisema pamoja na kwamba, yeye ni mfanyakazi wa PSPF, hafurahishwi, kwani anaamini kuwa mfuko huo umefilisika, hivyo suala lililopo ni kwa serikali kulipa.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy, alihoji sababu za PSPF kukopesha taasisi za umma, kama Takukuru, ambayo haifanyi biashara kuweza kulipa madeni.

SOURCE: NIPASHE 25/04/2013.
 
Back
Top Bottom