GE2025 Madeleka: Wanaosema watazuia uchaguzi ni matapeli kama matapeli wengine

GE2025 Madeleka: Wanaosema watazuia uchaguzi ni matapeli kama matapeli wengine

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
20,725
Reaction score
31,305
Hii ni kauli ya nguli wa sheria na siasa, kwa MBA, uchaguzi hauzuiliki. Kauli hiyo ameitoa wakati akipasua anga za wilaya ya Busega akieneza sera za ACT Wazalendo.

===
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria kupitia ACT Wazalendo, Peter Madeleka, amesema kuwa serikali iliyoko madarakani sasa itafikia kikomo cha uhalali wake mwezi Oktoba mwaka huu, na hivyo Watanzania wana jukumu la kuunda serikali mpya kupitia uchaguzi.

Jana Julai 4, 2025 akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Busega, mkoani Simiyu, Madeleka alisisitiza umuhimu wa kushiriki uchaguzi kama njia ya kidemokrasia ya kuleta mabadiliko ya kweli.

"Serikali tuliyonayo leo hii itamaliza uhalali wake mwezi wa kumi. Tunao wajibu wa kutafuta Serikali nyingine. Serikali hiyo tutaipata kwa njia ya uchaguzi. Uchaguzi ni haki ya kidemokrasia. Anayekwambia usishiriki uchaguzi hakutakii mema," alisema Madeleka mbele ya umati wa wananchi waliojitokeza.

Ameonya kuwa wito wa kususia uchaguzi una manufaa kwa chama tawala pekee na unadhoofisha juhudi za kidemokrasia za wananchi.

Hotuba hiyo imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu ushiriki wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ukiendelea kushika kasi. ACT Wazalendo wamesisitiza dhamira yao ya kushiriki kikamilifu ili kuzuia kile wanachokiita "utawala wa mabavu bila ridhaa ya wananchi."

Viongozi wa ACT Wazalendo wanaendelea na Operesheni yao waliyoiita Majimaji katika mikoa mbalimbali kueleza msimamo wa chama chao na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi.


Source: Manara Tv
 
ACT imeshanunuliwa ili kipande kuwa chama cha kwanza cha upinzani tayari.NO REFORM NO ELECTION inabaki ni sera ya CDM peke yao
 
CCM ni shida, Tanzania ina changamoto ya uongozi.

Lakini akili za wafuasi wa CDM zina watosha wenyewe,

Watanzania wanasubiri ‘Messiah’ mwengine anaefanana Magufuli.

Huo ndio ukweli
 
Walisema wataasi halafu watakinukisha kwelikweli.

Wacha tuone
 
Huyu naye ni mwehu tu, apuuzwe. Eti watazuia wizi wa kura!! Akawadanganye waliokosa akili. Wasubiri nafasi za kupewa na CCM kwa kukubali kuwa vibaraka wao.
 
Walisema wataasi halafu watakinukisha kwelikweli.

Wacha tuone
Pengine nia yao siku ya uchaguzi wale mayai, maharage halafu waanze ku-pass wind kwa mashuzi yatayonuka nchi nzima
 
Huyu Mwanasheria ni Ndumila Kuwiri sijawahi kumuamini
Kwanza Mtu alikuwa askari wa Jeshi la Polisi bado kuna miiko inampeleka mpela mpela.
 
Hii ni kauli ya nguli wa sheria na siasa, kwa MBA, uchaguzi hauzuiliki. Kauli hiyo ameitoa wakati akipasua anga za wilaya ya Busega akieneza sera za ACT Wazalendo.
View attachment 3395907
Tuna tatizo la kutopenda fact bali hisia na kujazana upepo kitoto. Ni fact hakuna wa kuzuia uchaguzi na Madeleka ameongea fact. Unazuia uchaguzi kwa njia ipi? 🙏🙏🙏
 
Vipi si alikua chadema huyu au walimnyima mgao wake ruzuku?
 
Nguli wa sheria huyu?huyu huyu huyu.
lini?
Sokapo apa
 
Vipi si alikua chadema huyu au walimnyima mgao wake ruzuku?
Mwenye akili timamu hawezi kubaki kwenye chama kilichojitia kitanzi kwa kutoshiriki shughuli muhimu zaidi ya kisiasa kwa maana ya uchaguzi mkuu.
 
ACT imeshanunuliwa ili kipande kuwa chama cha kwanza cha upinzani tayari.NO REFORM NO ELECTION inabaki ni sera ya CDM peke yao
Katika Nchi ya demokrasia Kila chama kila sera zake na mtazamo wako kwa masuala mbalimbali ya kisiasa. Ni lazima mtazamo wao uheshimiwe. Chama cha kisiasa na viongozi wao ambao wanadhani kila chama na kila raia anawajibu wa kuwaunga Mkono basi hai viongozi ni wendawazimu na hicho chama ni cha kidikiteta. Ni chama hatari kikipata nafasi ya kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom