Madawati ya ‘Chenji ya Rada’ yameota mbawa?

idoyo

JF-Expert Member
Jan 13, 2013
3,050
1,401
madawati+px.jpg

Sote ni mashahidi kwamba Serikali hatimaye iliamuru fedha hizo zielekezwe katika ununuzi wa vitabu na madawati kwa shule za msingi, kwa kutambua kwamba wananchi wangeunga mkono hatua hiyo kutokana na shule zetu kuwa katika hali mbaya ya ukosefu mkubwa wa madawati na vitabu.

Ni jambo la kushangaza kwamba madawati hayo yameota mbawa. Taarifa zilizomo kwenye wavuti wa mradi wa usambazaji vitabu na madawati kwa shule za msingi (PESP), zinaonyesha kuwa, hadi juzi jioni mgawanyo wa madawati ulionyesha kwamba mikoa 18 haijapata hata dawati moja, wakati Sh18.4 zilizotengwa zilipaswa kununua madawati 87,148 na kuyasambaza katika mikoa 25. Hadi Mei, mwaka huu ni madawati 28,728 tu yaliyonunuliwa na kusambazwa katika mikoa sita tu.

Linahoji gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom