Madawa ya kulevya; Serikali kama ina nia ya dhati kutokomeza ianzie hapa kwa sasa!!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,113
24,642
Kwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!

Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwanini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwanini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?

Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?

Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!

Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana.

Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!

Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya?

Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!

Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!

Nawasilisha
 
Serikali ya Rais Magufuri kwenye hili sijawahi hata kuhisi nimeota wakilizingumzia.

Kama Rais ana nia ya dhati ya kupambana na umaskini ni vema apambane na kuimarisha Nguvu kazi ambayo moja wapo ni hii inayoangamia na madawa ya kulevya!
 
Umesahau mheshimiwa yule aliepita alipelekewa orodha ya drug dealers wa nchi hii lakini hakuna lolote lililofanyika.. Au umesahau??

Njia pekee ya kupambana na madawa ya kulevya kwa nchi za kiafrica ni wewe binafsi kuacha kutumia drugs
 
freyzem! hoja yako haina mashiko ndugu yangu, hv kwa mtazamo wako vijana walioathirika na madawa nchi hii wako wangapi? napinga kauli yako kwa 100%, we unaacha kuishaur serikal itatue kero na changamoto mbali mbali muhim zinazowakabili wananchi wake, eti unashaur iwaangalie wa akina chid, kwan chid yeye nan? umejishusha sana ndugu yangu, hv ww mvuta unga unamjua vzr? mvuta unga si bwege tu, kwan kuna mtu alimtuma akavute? ww mbona huvut si kwa sababu unayajua madhara yake? kwa iyo mi naishaur serikali isihangaike kabisa na hao wajinga sababu ni maisha waliojichagulia ayo, kama ni nguvu kazi wapo vijana kibao tu mtaan ambao hawajaathirika na ayo madawa
 
Mkuu moja kati ya biashara mbaya na yenye mizizi mikubwa na ushawishi mkubwa hapa duniani.....ni hii ya madawa yanayoitwa ya kulevya........

Ni biashara ambayo inafanyika hata katika nchi ambazo wewe unaweza kuona ulinzi uko juu.....

Ni biashara inayohusisha watu walioshika mihimiri yote ya kiuchumi ya ulimwengu huu......fedha chafu zinazotokana na biashara hii....ndizo zinazotakatishwa na kuendesha shughuli mbali mbali za kiuchumi.......

Ni kama sigara ambayo ni hatari kwa maisha ya mwanadamu....lakini pato lake haramu....ni muhimu kiuchumi......

Jukumu lako ni wewe kuwa balozi kwa wale wapendwa wako....wasijihusishe na ushetani huu.....
 
kama hujui vzr, mvuta unga hata umsaidie vp , hawez akaacha kuvuta ndugu yangu, na kama unakumbuka vzr rais wa awamu iliyopita alifanya juhud za makusud kumsaidia yule dada mwanamuziz ray . lakin umeona kilichotokea?
 
Sidhani kama ni juu ya serikali kuzuia kula ngada wakati wanajua ngada ni msala.wale wabwie wajidunge na ikiwezekana wale kabisa wakifa tutawazika tu kama akina Banza,ngwea,aisha n.k
 
still vijana wa namna iyo wako wengi na wako nchi nzima , sasa ebu piga hesabu ni kias gan cha fedha kitatumika kuwaokoa hao watu ambao wenyewe wanaona ni starehe na ww unaona ni kero, na iyo pesa unayosema ww ya kuwasaidia hao itatoka wapi? maana uyo unayesema ww hana iyo pesa, kinachotakiwa muswada upelekwe bungen ikiwezekan itengwe bajet kwa ajili ya kuwahudumia ha wajinga, sasa ni mtanzania gan mwenye akili finyu atakaa kujadili huo ujinga wakati nchi inavitu vingi vya kujadili? watu waache kujadili jins ya kupunguza vifo vya mama na mtoto wakat wa kujifungua! wajadili wavuta unga huo si utakuwa ujunga? bado tuna kero za maji, umeme, elim nk tukajadili chid na wenzake hao ni akina nan nch hii, waendelee kuvuta tu sisi hatuna faida nao
 
kama hujui vzr, mvuta unga hata umsaidie vp , hawez akaacha kuvuta ndugu yangu, na kama unakumbuka vzr rais wa awamu iliyopita alifanya juhud za makusud kumsaidia yule dada mwanamuziz ray . lakin umeona kilichotokea?
P Funk alikua anatumia na ameacha, kuna wengine wengi tu. Yule jamaa aliyeenda Big Brother Africa, nadhani anaitwa Nando, alikua anatumia naye yupo sawa.
Kila Jumamosi au Jumapili nenda hospitali kubwa kama Muhimbili au Mwananyamala uone vijana waliofanikiwa kuacha madawa.
 
Kwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!
Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwa nini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwa nini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?
Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?
Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!
Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana..
Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!
Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya??
Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!!
Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!
Nawasilisha...
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hao watu wanajiingiza kwenye hiyo mitandao kwa kutaka utajiri Wa haraka huku wakiwa watumiaji wakuu Wa madawa hayo, wanapoathirika kwa ulevi Wa kupindukia serikali inalaumiwa, Wa kulaumiwa ni yy mtumiaji maana hakulazimishwa na MTU ila alianza kutumia kwa utashi wake ,hivyo apambane yy mwenyewe kujiokoa kuliko kuingizia garama serikali tena
 
Kwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!
Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwa nini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwa nini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?
Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?
Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!
Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana..
Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!
Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya??
Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!!
Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!
Nawasilisha...
Yani madawa unywe chumbani kwako na mmeo alafu uje kusumbua serikali ikusaidia ??

Yani serikali iache kutoa elimu bure, kununua ndege, kuboresha bei ya mazao, ikalie kukusaidia wewe jitu zima lisilojielewa??
 
freyzem! hoja yako haina mashiko ndugu yangu, hv kwa mtazamo wako vijana walioathirika na madawa nchi hii wako wangapi? napinga kauli yako kwa 100%, we unaacha kuishaur serikal itatue kero na changamoto mbali mbali muhim zinazowakabili wananchi wake, eti unashaur iwaangalie wa akina chid, kwan chid yeye nan? umejishusha sana ndugu yangu, hv ww mvuta unga unamjua vzr? mvuta unga si bwege tu, kwan kuna mtu alimtuma akavute? ww mbona huvut si kwa sababu unayajua madhara yake? kwa iyo mi naishaur serikali isihangaike kabisa na hao wajinga sababu ni maisha waliojichagulia ayo, kama ni nguvu kazi wapo vijana kibao tu mtaan ambao hawajaathirika na ayo madawa
Kwa hiyo mkuu suala LA waathirika wa madawa ya kulevya(mateja) kwako siyo kero??
Ila kero ya hawa jamaa inajulikana kabisa
 
Kama niambie wanayo, maguire angefanya kama yule jamaa anaowauwa kule kwake....
 
Drug ni kitu cha kusimuliwa na kusoma hadithi zake tu. Si kitu cha kuomba hata ndugu yako wa mbali anase! Hivi mtu mwenye maralia kali anahisi maumivu na joto
Kali mwilini ukimwambia acha kutumia dawa ambayo akitumia anarudi normal atakuelewa? Drug hubali chemistry ya mwili na kuipindua ili normal state ya mwili itegemee uwepo wa drug kwenye blood. Without drug ni hivi mtu anakuwa SICK. so the best alternative of all is NEVER EVER GIVE IT A TRY. Sio kazi ya serikali hiyo. Kodi ninayolipa nipate huduma ndo ikamhudumie mpumbavu aliyechagua slow and expensive death kuwa starehe yake? Hebu tuwe serious.
 
Back
Top Bottom