Madaraka ya kulevya kwa madiwani wa ACT-Wazalendo

Kali _D

Senior Member
Feb 10, 2019
145
132
Hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu juu ya mienendo ya madiwani wa ACT kigoma mjini, ambao ndio wanaounda na kulimiliki baraza la madiwani katika manispaa ya kigoma ujiji.

Kwanza, kumekua na uelewa mfinyu wa mambo. Unaweza kusema ni kutokana na uhaba wa elimu lakini hapana kwakua elimu ya shule ni sehemu tu katika kujitambua. Lakini kinachoendelea ni unaona kabisa ni ufahamu finyu wa harakati za kisiasa na kimaendeleo kiasi kwamba madiwani wamekua wakishindwa kuchambua kipi kinawahusu na kipi wakielezee namna ipi mbele ya wananchi wao.

Hilo limewafanya madiwani hao kuhisi kwamba wanaowaongoza nao ni vipofu wa mambo kama wao. Mathalani kumekuwa na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya JMT chini ya udhamini wa Benki ya Dunia katika manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo usanifu wake umeanza tangu miaka ya 2010, tena kwa nchi nzima katika maeneo ambayo yamependekezwa, lakini madiwani hao kwa pressure na kiu ya kutaka waonekane mbele za wapiga kura wao ambao si wajinga tena, wanatamka waziwazi kwamba chama cha ACT wazalendo kimeleta miradi na kinaitekeleza kwa kiasi flani cha pesa.

Sawa kwa wananchi wa sasa ambao tayari washaielewa huwa wanawauliza tu swali dogo..." je mmeanza lini mipango/ upembuzi na pesa mmezipata kwa chanzo kipi mlichonacho hadi leo hii ndio mnaitekeleza miradi hiyo?" hapo huishia kuporomosha matusi yanguoni na kukutishia kukuroga.

Pili, kumekuwa na hofu kali kuelekea uchaguzi wa madiwani 2020.hapo ndipo kina diwani Kalyango, Baba revo, Meya Hussein na na wengingieo wa kariba hiyo wanapozidi kuvurugwa, kwani ni dhahiri viongozi hao hakuna hata mmoja anaekubalika tena mbele ya wananchi wake.

Kwa mfano tu ukianzia kule Mwanga Kaskazini ambapo diwani wao ni baba revo ambae kwasasa ni mfungwa wa miezi 5, wananchi wake wamejikuta katika furaha isiyo na kifani mara baada ya hukumu iliyotelewa kwa Baba Revo.

Wananchi hao wamesikika kwa nyakati tofauti wakisema diwani huyo amezidi, amekuwa ni mtu asiye na hekima wala busara, amekuwa akiwatukana wazee hadharani bila kujali, amekua na mambo yasiyo na haiba mbele ya wapiga kura wake kama vile kutembea na wanawake tofautitofauti mitaani humo na KUWADHALILISHA, kujiunga na kulea vikundi vya vibaka kama wale TELEZA nk. kiufupi diwani huyo kapoteza sifa na wala haaminiki tena.

Achilia mbali zile bangi za kuwapiga madaktari na matrafiki. hiyo ni hofu tu ya uchaguzi mkuu mwakani. Pia kuna diwani bubu wakule Bagwe, hahaha huyu wanaBangwe wameamua kumpa jina la ROBOT kutokana na udhaifu wake mkubwa katika kuisimamia manispaa huku akiwa anaendeshwa hovyohovyo na mbunge zitto kabwe.

Madhaifu yake ni mengi sana kuanzia binafsi mpaka utawala wake ambapo amekua akihusika na upigaji wa madeal ya mbunge bila kujielewa, ameshindwa kabisa kuwasemea wapiga kura wake wa bangwe.

Ameshindwa hata kuwafungua vijana katika fursa zilizopo kama meya huku vijana wakiwa na imani kubwa kwake kwamba watakua na kipaumbele na kutokana na nguvu yake katika maamuzi ya baraza na nguvu ya ushawishi katika sekta binafsi hasa za kisanaa, kibiashara na michezo lakini jamaa huyu hana habari na wala hajua namna ya kuziendea fursa hizo. wanacnhi wamebaki na butwaa.

Kuna yule diwani wa Kigoma Mjini wao wanamwita VUVUZELA kutokana na jinsi anavyotumia nguvu kubwa kuongea mitandaoni na kwenye vijiwe vya kahawa huku akishindwa kujibu hoja maswali ya wanaomsikiliza na kumfuatilia.

Amekua akiongelea masuala mbalimbali bila kua na muendelezo wake, bila kua na hoja ma mtririko unaoeleweka, huku vitendo vikiwa ni sifuri kabisa. huyu ndie diwani ambaye amechukua taswira ya mkoa, yaani diwani wa "kigoma mjini" lakini ukifika iyo inayoitwa kigoma mjini utachoka.

Diwani yupo busy kwenye vijiwe vya kahawa akihangaika kutafuta huruma ya wapiga kura mwakani, huku akiwa amejisahau kabisa katika uwajibikaji wake. kazi kubwa anayoifanya diwani huyu ni kujitafutia sifa mbele ya madiwani wenzake, hadi wamekuwa wakimsema vibaya kwamba jamaa anajiona yeye ndio diwani pekee ake, kujipendekeza kwa mbunge na viongozi wengine wa Kiserikali kiasi kwamba hataki viongozi hao wawafahamu madiwani wengine, hiyo imekua kero kubwa sana ndani ya baraza lao la madiwani, achilia mbali huku mitaani ambako amekuwa akiwaacha hoi wapiga kura wake pindi anapokuwa anajiachia tu hovyo hovyo bila kujali haiba yake binafsi na ya familia yake.


Kifupi huyu kasahau kabisa majukumu yake kama diwani.
Tatu, kupigwa tikitaka na zitto, yaani kutelekezwa na Zitto Kabwe, no doubt zitto ni mwanasiasa anaejua namna ya kujijenga yeye kupitia migongo ya wenzie.

Zitto amekuwa mara zote machaguo yake ni mambumbumbu na siku akijua kama umejielewa na kuanza ladba kutumia akili zako kuchambua mambo na maamuzi binafsi basi anakukacha kiana na hutomuona tena zaidi ya kukutana na uchawi wake na misukosuko katika maisha yako, ndicho kitu kikubwa kinachowafanya hawa madiwani kupagawa na maisha na kufikiria uchaguzi ujao, huku wengi wao wameshajua kwamba haweawezi kurudi kama hawa kina baba Revo na Meya Hussein na wengine wakitumia nguvu kubwa wakidhani wanajijenga kumbe wanaharibu tu kama hawa kina kalyango.

Leo, baba Revo katupiwa jela kwa miezi 5 kwakosa la kipuuzi sana kufanywa na kiongozi levo ya udiwani, kosa lenyewe ni kumshambulia trafic.

Hawa matrafic wanaohangaika wakati wa mvua na jua kusimamia usalama barabarani leo anashambuliwa kirahisi kabisa na mwanasiasa wa mpito, hii si sawa. Na ndomana hata mbunge na chama chake wala hawajawahi kumzungumzia popote wala kushughulika nae kwasababu za kipuuzi za KUVIMBIWA NA SHIBE YA MADARAKA.

Picha ni diwani Kalyango akiwa katika shibe ya madaraka.
 
Huna inshu ccm mlikuwa na kigoma miaka mingi lakin mmeahindwa.kaeni benchi tu
 
Back
Top Bottom