Madaraka ya DDP yaangaliwe upya

Madaraka ya DDP yaangaliwe upya

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=1][/h]


Julius+Samweli.jpg


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Kessy yeye alikwenda mbali zaidi ya kueleza kuwa mahakimu na waendesha mashtaka wamegeuka miungu watu, huku wakishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo



Kumekuwapo mjadala mzito unaoendelea nchini kuhusu madaraka ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuwa ni makubwa na kwamba yanapaswa kupunguzwa.

Wapo ambao wanadai kuwa kutokana na kuwa na madaraka makubwa mtu ambaye anateuliwa kushika wadhifa huo anaweza kuyatumia kwa manufaa yake kufuta kesi au kushindwa kuzifikisha mahakamani kwa visingizio mbalimbali.

Baadhi ya watu wanaoinyoshea kidole ofisi ya DPP ni pamoja na Wabunge na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Dk Edward Hoseah.

Hoseah anasema Taasisi yake imekuwa ikipeleka majalada ya kesi zinazohusu rushwa kwa DPP, lakini majalada hayo yamekuwa yakiishi katika ofisi ya mkurugenzi huyo wa mashtaka.

Sio mara moja Hoseah amelalamika kuhusiana na DPP ni mara nyingi , na ionaonyesha kuna tatizo zito lipo katika ofisi hii.

Hata hivyo, wiki hii wabunge nao waliamua kulizungumzia tatizo la madaraka ya DPP wakisema amekuwa akichelewesha mashtaka kwa makusudi yanayowahusu vigogo.

Walisema kuna ubaguzi mkubwa katika utekelezaji wa sheria mbalimbali za nchi hali ambayo inakuza uhalifu nchini hasa ule mkubwa wa udokozi wa fedha za serikali.

Wanasema umefika wakati sheria zikirekebishwe ili kumpunguzia madaraka DPP, ili kumbana asiendelee kutumia madaraka vibaya.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Kessy yeye alikwenda mbali zaidi ya kueleza kuwa mahakimu na waendesha mashtaka wamegeuka miungu watu, huku wakishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema Kuna kesi zipo zimekaa katika ofisi ya DPP kwa miaka zaidi ya mitano hasa zile za mali za Serikali, amekuwa akifuta kesi nzito na kwamba ana ushahidi wa mtu mmoja aliyeiba Sh11milioni kwa kuandika risiti ya uongo, lakini mpaka leo hii kesi ipo kwa DPP.

Alisema kuwa matokeo yake watu wanaochukuliwa hatua ni wale walioiba kuku na vitu vidogo vidogo, huku akifafanua kwamba wanaoiba mali za Serikali wamekuwa wakihamishiwa maeneo mengine ya kazi.

Ni vyema sasa kilio hiki cha wananchi nchini kisikike kwa mamlaka zinazopaswa kuchukua hatua.
 
Kuna umuhimu mkubwa sana kwa DPP kuangaliwa utendaji wake. Demokrasia na utawala bora vinashamili pale kunapokuwa na checks and balances katika taasisi za jamii.

Inashangaza na kusikitisha pale nchi inapokuwa ma mtumishi wa umma ambaye hana taasisi inayomwajibisha/kumulika utendaji wake pale anapoteuliwa na Rais.

Hata Rais hawezi kuhoji utendaji wake wa kazi.

Katiba mpya ya nchi lazima ilitizame hili tatizo, otherwise, DDP anakuwa Mungu mtu
 
Mbona ushachelewa kutoa hjoa? Hukuiandika wakati wa ziara ya Warioba ya kutoa maoni ya Katiba? Maana humu kwenye mtandao hakkuna atakayekusikia wala kufuatilia hili. Si DPP tu, hata Rais mwenyewe apunguziwe. Na kama Rais hawezi kuhoji utendaji kazi wa DPP basi DPP ni Rais ila hajitangazi tu kama JK.
 
Bado hatujachelewa,kwani tunategemea wawakilishi wetu kufanya tulichowatuma huko mjengoni.Kama wameliona hili basi wanauwezo wa kulisemea na likatatuliwa,kwani hata Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ana madaraka makubwa ya kuamua nani anakuwa rais au mbunge,hata kama aliona kuwa kilichofanyika kisheria ni kosa la jinai.
 
Back
Top Bottom