Madaraka Nyerere aliukacha Mwenge Kilimanjaro

mpinga shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,237
954
Mtoto wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere aliukimbia 'Mwenge wa Uhuru' wakati yeye na kundi la watanzania wengine walipokuwa wanapanda mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

Kipindi hicho pia wakimbiza mwenge walikuwa wakiupandisha mwenge kileleni na wangekutana na kundi la Madaraka kwenye summit.

Mmoja wa watu waliokuwa na Madaraka amebainisha kuwa Mtoto huyo wa Kambarage alilazimika kusimamisha msafara wake ili kwanza mwenge uondoke kileleni ndipo nao waende.

"Makongoro siyo msemaji sana yeye alitamka maneno machache tu ya kwamba "Huo Mwenge sio ule wa Baba yangu!"
 
Acha uongo nilikwepo kwenye msafara, na wala hakuzungumzia kabisa suala la mwenge kwa kuwa kila watu walikuwa na programme yao ya safari na hatukupanga kwenda au kuukuta mwenge kileleni.
 
Daaah! Afadhali umemjibu hivyo. Tusubiri reaction yake sasa. Kuna sehemu amemnukuu Makongoro, Je, naye alikuwemo kwenye msafara?
 
Acha uongo nilikwepo kwenye msafara, na wala hakuzungumzia kabisa suala la mwenge kwa kuwa kila watu walikuwa na programme yao ya safari na hatukupanga kwenda au kuukuta mwenge kileleni.
Ah nyinyi ndio wale wale waliodhaminiwa na serikali kupitia TTB kupanda mlima na posho juu ndio maana unapinga.
si ajabu utapinga pia kuwa wapagazi waliowabebea mizigo nusura wafe kwa kulemewa huku ujira wao kwa siku zote 7 ukiwa mdogo kuliko posho yako ya siku moja kwenye ile safari.
 
makuubwa!
 
Mtoto wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere aliukimbia 'Mwenge wa Uhuru' wakati yeye na kundi la watanzania wengine walipokuwa wanapanda mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

Kipindi hicho pia wakimbiza mwenge walikuwa wakiupandisha mwenge kileleni na wangekutana na kundi la Madaraka kwenye summit.

Mmoja wa watu waliokuwa na Madaraka amebainisha kuwa Mtoto huyo wa Kambarage alilazimika kusimamisha msafara wake ili kwanza mwenge uondoke kileleni ndipo nao waende.

"Makongoro siyo msemaji sana yeye alitamka maneno machache tu ya kwamba "Huo Mwenge sio ule wa Baba yangu!"
mkuu mbona umenichanganya hapo mwisho,unamaanisha ni madaraka nyerere au makongoro nyerere?
 
mbona nasikia mwenge wenyewe haukufika kileleni? tupe habari kamili. Mia
 
mwenge haukufika mlimani..kama ulifika picha ziko wapi??????? Mwenye picha aweke hapa ..
 
Nasikia haukufika kileleni ndio maana hata haikwenda live TBC kama ilivopangwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom