Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,250
- 44,578
Neno la Kuzingatia: Madaraka ni matamu sana. Na hakuna madaraka matamu kama ya kuwatawala wengine hasa ukiwa unaamini wamekuchagua uwatawale (haijalishi sana kama ni kweli au la walikuchagua).
Katika nchi zilizoweka utaratibu wa ukomo wa muda wa kutawaliwa unafika wakati muda ule ukifika watawala wanakuwa na kigugumizi kidogo. Bahati mbaya watu wanafikiria wenye kigugumizi cha kuachilia madaraka ni Marais wenyewe; la hasha! Nyuma yao kuna watu wanaonufaika na maraia hao kubakia madarakani.
Ukishangaa watu kama Mugabe, Kabila na sasa Nkurunzinza walivyonogewa na madaraka utakosa picha kamili. Picha kamili ni mamia (kama siyo maelfu) ya watu ambao wananufaika na viongozi hao kuendelea kuwepo madarakani. Ni sawasawa na kumtaka kumtoa kiboko ziwani ati aje pembeni kupumzika. Unasahau kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwasumbua ndege, kupe na wadudu wengine walioko mgongoni ambao wananufaika sana na yeye kutulia mahali kama pale ili na wao wale bila kusumbuliwa.
Ndio maana ni muhimu sana kutoyaombea mabadiliko yatokee; mabadiliko yanasubiri yaletwe na wengine mara nyingi hayaji! Mabadiliko ni yale tu ambayo watu wanajiletea wenyewe. Unapoambiwa jiandikishe kupiga kura usije ukakaa pembeni na kusema "ah wengine watajiandikisha" au "hata nikijiandikisha kura yangu watachakachua".
Sasa usipojiandikisha na upo katika nafasi ya kufanya hivyo basi unajinyima nafasi ya kujiletea mabadiliko.
Uzuri mmoja wa mfumo wetu wa uchaguzi ni kuwa sisi tunahesabu kura tu za wananchi (kura moja moja). SIyo kama mfumo wa Kenya, Afrika ya Kusini na hata NIgeria ulivyo ambapo licha kuhesabu kura moja moja wanahesabu asilimia/namba ya majimbo ambayo mgombea wa Urais anatakiwa kushinda ili ushindi wake uwe halali. Hili bila ya shaka lina uzuri na ubaya.
Uzuri wake ni kuwa kila kura ina thamani sawa bila kujali inatokea wapi. Ubaya wake ni kuwa chama au mtu anaweza kuweka mkazo kwenye maeneo fulani tu (katika kuandikisha na katika kuhamasisha) na akapata kura nyingi huko zinazoweza kumbeba kwenda Ikulu (sijui kama kwa aliyeshinda hili linaweza kuwa baya).
Tatizo bado linabaki pale pale tu; wakishaingia madarakani kuwatoa kwa kweli ni kazi sana. Wengine hawatoki hadi wamwage damu na wengine hawatoki hadi alama za kuwa hawatakiwi kweli kweli ziwe hadharani.
Vyovyote vile ile ilivyo mwananchi ni lazima awe tayari kuonesha kuwa muda wa kuondoka kwa mtu au chama umefika. Na hili lisiwe la kujutia au kusikia aibu. Vinginevyo kama walivyosema wahenga - ukicheka na nyani utavuna mabua. Huku unachekelea.