Madaraka CCM, Uongozi CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaraka CCM, Uongozi CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jazzie, Apr 26, 2012.

 1. Jazzie

  Jazzie Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hata siku moja sikudhani nitashuhudia haya yanayotokea Tanzania – kwamba kuna watu wako madarakani lakini si viongozi.

  Kilichotokea bungeni hivi karibuni, ni hitimisho ya kile ambacho kilikuwa kimeanza kujitokeza, kwamba CCM wana mamlaka ya kuongoza nchi, lakini wameishiwa haki ya uongozi. Uongozi, ninavyoelewa mimi ni kuwa mstari wa mbele katika kujielekeza mwenyewe, kundi fulani, au jamii nzima kuelekea mahali ambapo pameainishwa wazi (leadership is directional, with a clear definition of a desired destion). Kwa Tanzania, safari yetu ni kuelekea katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Sehemu ya uongozi, kwa maana hiyo, ni kuwa mstari wa mbele katika uhodari, mawazo mapya, maono, mikakati, kutia moyo (inspiration) na kadhalika. Kinachotokea sasa hivi ni CCM kusubiri CDM waongoze nchi. Kama hiyo si kweli, ni lini (hasa siku za karibuni), umesikia wazo jipya limetoka ndani ya CCM? Ni lini, siku za karibuni, umetiwa moyo na CCM kama Mtanzania?
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Punguza ndumu na ganja!!
   
Loading...