Tatizo ni ufisadi wa viongozi wa serikali!! Ukiangalia vizuri vitu vinavyoongeza uchafu jijini Da es salaam ni vyenye asili ya plastic na ni kwasababu kwa asili yake plastic haiozi. Sasa kama mkikumbuka serikali iliwahi kujaribu kupiga marufuku utengenezwaji wa mifuko ya plastic ambayo ndio inachafua sana mazingira ya jiji, lakini punde si punde serikali ikabadili azma yake hiyo ya kupiga marufuku utengenezwaji wa hiyo mifuko baada ya wenye viwanda kuwatembelea wakubwa!!! Zanzibar hawana tatizo hilo la mifuko ya plastic kwani walikwisha ipiga marufuku utumiaji wake! Tatizo liko kwa viongozi wa serikali kuendekeza njaa zao hivyo kuhadaika na hizo 10% wanazohongwa huku wakutuharibia nchi.