Madanguro ya makahaba Mwananyamala mpaka lini?

WamLola

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
343
122
Habari wanajamvi

Kwa hali isiyokuwa ya kawaida biashara ya dada zetu kujiuza inazidi kushamiri maeneo ya Mwananyamala. Maeneo haya yamejengwa vibanda vingi sana na wanawake hujiuza hata mchana ikisemekana biashara hii huwakumba vijana wa kiume hata wenye miaka 16-21.

Biashara hii iliyopo karibu na hospitali ya Mwananyamala upande wa juu ukivuka barabara, je viongozi wa mkoa na wa serikali za mitaa hawajui uchafu huu unaoendelea kuwakwaza wakazi wa maeneo haya?

Naiomba serikali na mamlaka zake kukomesha biashara hii na kuwachukulia hatua wamiliki wa vibanda hivi ambao huvikodisha kwa wanawake hao wanaofanya biashara haramu.
 
Ni kweli na mimi ni mkazi wa hapo.

Kihistoria hao wahaya ambao wapo hapo wapo toka 80s huko,ni wazamani sana kwenye hiyo biashara na watu wengi sana washapona hapo.

Alafu wale wanakaa katika vyumba vyao,kwao sasa utawezaje kumkamata mtu kwake?

Mi naona kama serikali imewaruhusu kiana wale watu maaana sijawahi kuskia anakamatwa mtu pale.
 
Hiyo biashara maeneo hayo ipo muda mrefu sana maeneo hayo.

Mimi bahati nzuli niliwahi kupanga maeneo karibu na hiyo biashara na nimekuwa na ukaribu flani na wanaoifanya hiyo biashara kwa sababu nilikuwa nina duka maeneo ya hapo.........

KWA KIFUPI wenye kulaumiwa na hiyo biashara ni wenye nyumba kwa sababu wao kama wao ndio wanaokodishiwa nyumba kufanya biashara yao...

Pili serikali na haswa TRA kwa sababu hizo nyumba huwa zinalipiwa kodi za majengo serikalini

Tatu mahakama ya city hawa watu hata wakikamatwa wakipelekwa mahakama city wanalipa faini kisha wanarudi,

KIPINDI CHA NYUMA KUNA KUNA KAMANDA WA POLISI WILAYA KINONDONI KWA JINA CHARLES KENYELAA ALIWAHI KUFIKA HAYO MAENEO ALIWAKAMATA WENGI LAKINI MWISHO ALICHEMKAA.

SIO HUYO TUU KULIKUWA NA YUSSUFU MAKAMBA AKIWA MKUU WA MKOA pia ABBASS KANDORO licha ya kupiga kazi kuwaondoa lakini ikaishia njianii hao watu wamerudiii
 
Habari wanajamvi

Kwa hali isiyokuwa ya kawaida biashara ya dada zetu kujiuza inazidi kushamiri maeneo ya Mwananyamala. Maeneo haya yamejengwa vibanda vingi sana na wanawake hujiuza hata mchana ikisemekana biashara hii huwakumba vijana wa kiume hata wenye miaka 16-21.

Biashara hii iliyopo karibu na hospitali ya Mwananyamala upande wa juu ukivuka barabara, je viongozi wa mkoa na wa serikali za mitaa hawajui uchafu huu unaoendelea kuwakwaza wakazi wa maeneo haya?

Naiomba serikali na mamlaka zake kukomesha biashara hii na kuwachukulia hatua wamiliki wa vibanda hivi ambao huvikodisha kwa wanawake hao wanaofanya biashara haramu.

WamLola nine NakuLola.
 
Tafuta namba za IGP Sirro umwambie, labda vijana wake wana hizo taarifa lakini wanakuwa wanapoozwa na hao wamiliki wa madanguro kwa kupewa hela ya kiwi
 
Back
Top Bottom