Madampo ya Maji taka jijini Dar es Salaam

M

Marrina

Member
29
0
Maajabu mengine jijini Dar es Salaam, katika pitapita yangu nimekutana na wananchi wanalalamika wanaitaji magari ya maji taka yafike kuwanyonyea vyoo vyao vimejaa na wenye magari wamegoma maana hawana sehemu yakumwaga majitaka maana madampo yamefungwa ghafla, madreva wamedai dampo la tabata lilifungwa na baada ya kufungwa wakawa wanaenda kumwaga Kurasini jana ghafla na dampo la kurasini lilifungwa nakusababisha usumbufu mkubwa kwa wale waliokuwa wameishakuwa na taka kwenye mgari yao. Hapa nimeshindwa kuelewa hawa wahusika wa madambo wanachozingatia katika swala zima la afya. Inamaana wanachi vyoo vinapojaa wafanyeje? au hawa wenye magari wakayamwage wapi!!!! anayefahamu swala zima la haya madambo naomba nieleweshwe. la afya, kurasini lilifungwa
 
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
2,346
2,000
Kama vp waje kumwaga nyumbani kwangu.
 
Mchumba

Mchumba

JF-Expert Member
272
250
Huku uswazi kwetu hakunaga haja ya dampo..

Mvua ikinyesha tunafunguliaga tu vitu, vinamwagika kiulainiii mbaka baharini
 
K

kabindi

JF-Expert Member
334
195
Kwa ushauri wangu, serikali inatakiwa kuanzisha Agency itakayokuwa inashughulikia taka za aina zote (solid, gaseous and liquid wastes). Ukitembelea sehemu nyingi nchini hari inatisha na mamlaka zilizopo ni kama zimeshindwa kuja na ubunifu wa kuwa na njia za kisasa za kudhibiti taka. Tukipata watu wenye akili timamu taka ni malighafi, kwa sasa nchi zilizoendelea lugha ya takataka inabadilika na kutakuwa hakuna takataka, kwani taka nyingi kwa sasa ni malighafi za aina mbambali kulingana na aina ya taka. Kwani nchi nyingine kwa sasa wanazalisha mbolea, umeme, au recycling kama zile za karatasi, glasses, chuma chakavu na plastics. Hivyo taka imekuwa sehemu kubwa ya ajira. Lakini pia taka zile hatarishi zenye kemikali kutoka viwandani zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara makubwa katika jamii, kama vile vifo na ulemavu. Hivyo, kwa unyeti wa suala hili naishauri serikali ianzishe taasisi yenye mamlaka kamili kushughulikia tatizo hili .
 
M

Marrina

Member
29
0
Serikali hadi leo hii haijato tamko kuhusu haya madampo kufunguliwa hali ni mbaya sana hata kwawenye sehemu za biashara kama mabaa na mahotel hali sio. good advise @ kabindi. Ila sasa wakuchukua huo ushauri na kuufanyia kazi ndo pagumu hapo.
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
3,229
1,195
Nchi ina mapori mengi sana, hawawezi kwenda hata nje kidogo ya Dar wakamwaga hata porini tu?
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom