Madam Wema Sepetu, tusamehe Watanzania

Mbilimbi Mbovu

Senior Member
May 25, 2015
185
119
Naandika uzi huu kwa niaba ya Watanzania, kumhusu Madam Wema Sepetu, mlimbwende wa zamani wa Tanzania, akishinda Taji hilo mwaka 2006 mbele ya Jokate Mwegelo, mjasiriamali, msanii wa filamu, muziki na mwanaharakati na Lisa Jensen, aliyekuja kuwa Redds Miss World Tanzania mwaka 2012.
Wema_na_Jokate.jpg

Wema Abraham Sepetu, alipotawazwa kuwa Malkia wa Urembo Tanzania mwaka 2006

Kwa muda mrefu Madam amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa wema na kwa ubaya, kama lilivyo jina lake, Wema Sepetu a.k.a Mama Ubaya, lakini ubaya ukionekana kuzidi wema wake machoni pa kundi la 'Watanzania Wastaarabu'.

Wema, kama washindi wengine wa taji hilo la Umiss, amelitendea haki kwa kufanya kazi zinazotakiwa, na walau kuka nalo vema hadi alipolikabidhi kwa mrithi wake, Richa Adhia mwaka 2007.

wema6.jpg

Wema Abraham Sepetu akiwa na Diamond Platinumz, msanii wa kimataifa wa Tanzania, enzi za mapenzi yao, kwenye Tuzo za MTV Afrika.

Licha ya ushindi huo, madam amekuwa na 'kismati', kama wenyewe wanavyodai. Wachumba aliokuwa anatembea nao walipata mafanikio makubwa kwenye kazi zao, iwe muziki, uzalishaji au uigizaji wa filamu na pengine hata biashara zisizohusisha sanaa.

Ukikaa na Waridi utanukia, bila shaka mada amekuwa waridi kwa watu wengi, akiwaangazia nyota na kuwatangaza kimataifa. Madam akiwa upande wako, nani aliye juu yako? Kwa hili tuna deni kwake...

Madam amemsaidia sana msanii Diamond Platinumz, licha ya kuwa pumziko lake kwa miaka kadhaa, alimfundisha mambo mengi ya msingi ikiwemo lugha ya Kiingereza, nyenzo muhimu kwenye utandawazi.

Madam alimtoa Diamond kutoka uselebriti kunuka na kumfanya kuwa wa kisasa, msanii wa kimataifa. Popote tunapomsifia Chibu, tujue tuna deni kwa Madam Wema Sepetu.

wema2.jpg

Rangi za midomo za Kiss, kazi ya ubunifu wa Wema Abraham Sepetu

Licha ya umaarufu wa magazeti na Blogu, madam ana juhudi binafsi za kimaisha, uzinduzi wa Kampuni ya Endeless Fame (inayomsimamia msanii Mirror), brand yake ya ' Kiss Lipstick' na maajabu mengine kibao.

Madam ni msanii, NDIO, mmoja wa wasanii wakubwa kabisa wa Bongo Movie... Tunapoona mafanikio yoyote kwenye tasnia, madam ana mchango wake mkubwa sana, kwa kweli anatudai.

Madam amewahi kushiriki kwenye Siasa ngazi ya kitaifa, kwa kugombea Ubunge Viti Maalum ndani ya Chama cha Mapinduzi. Licha ya kuwepo kwa dalili za ushindi wake kuchakachuliwa, alionesha uungwana wa hali ya juu kwa kukubali matokeo na kushiriki kikamilifu kwenye kampeni za Uchaguzi 2015.

wema4.jpg

Wema Abraham Sepetu akihutubia hadhara kwenye moja ya mikutano yake ya kisiasa.

Madam ni Celeb pekee kuwahi kuwa na Timu yake, timu inayojitambulisha kama #TeamMadam na ikijumuisha watu wakubwa na maarufu; Kajala, Petit Man, Aunt Ezekiel, DJ Rommie Jones (DJ wa Diamond Platinumz) na wengine wengi... Huu ni umaarufu wa Kiwango cha Kimataifa.

wema7.jpg

Kava la filamu ya Madame, moja ya kazi maarufu na bora za Wema Abraham Sepetu

Licha ya kupumzika kidogo shughuli za filamu, bado hayuko nyuma kuwaunga mkono wasanii wenzake. Juzi alienda na gari lake kumpokea Elizabeth Michael Lulu, huu ni upendo uliopitiliza.

Madam ni mshiriki mzuri wa matukio ya kijamii na kindugu. Anahudhuria misiba, sherehe na matukio mengine kwa ukamilifu.Hata uhusiano wake na washabiki wake sio wa kunata wala kujidai, kama wadada wengine maarufu.

Sijasahau alivyojitolea kumtoa jela Kajala Masanja, wakati ambao wasanii wengine maarufu walipomsusa. Huu ni wema usio na kipimo...

Licha ya utu wake huu, madam amesakamwa na magazeti, blogu, mitandao na watanzania kwa ujumla. Wakimtusi, wakimkejeli, wakitengeneza picha za uongo, wakimuita malaya na wakati huo wakinufaika na kuuza habari zake.

Licha ya ubaya huu tuliomlipa, bado Wema ameendelea kuwa mzalendo, na mtu anayejitolea kwa taifa, kwa wasanii wenzake na jamii kwa ujumla. Kwa ambao wamewahi kuroll na Mama Lao, watakubaliana na mimi kuwa hayuko namna ambavyo watu wanamchukulia.

Kwa kweli wema wa Madam ungekuwa unaandikwa, vitabu vya dunia hii visingetosha kuuelezea wote.

Natoa wito kwa sisi kama taifa, kutafakari ubaya huu tuliomvika madame, na tumuombe radhi kwa ujumla wetu... Ikiwezekana tumjengee na mnara wa kumbukumbu.
 
Thread nzuri sana hii.

Natumia nafasi hii kumuomba msamaha madam pia. Nimekua nikichekelea pindi watanzania Wenzangu wanapomchafua bila kujali Umuhimu wake. Watu wametajirika kwa kuuza magazeti ya kumchafua wala hajawa na kinyongo na Mtu.

Wema Sepetu sio malaya tena hana tabia chafu. Hajui kubadilisha mabwana hadi labda mabwana wamuumize na kumuacha bila sababu. Kwenye mapenzi Wema hajui kuchanganya mabwana, akipenda amependa na yupo wazi si sawa na Wasanii wengine ambao hujui mumewe ni nani kwani wanao wengi.

Madam Wema Sepetu anafaa kuwa Mke na Mama wa Familia kwani kapitia mikimikiki mingi ya maisha na ana uvumilivu wa hali ya juu. Kama kuumizwa kaumizwa sana.

Wema Sepetu tusamehe Sisi Watanzania, tumekukosea sana. Sijawahi sikia Wema kagonganisha mabwana, kafumaniwa wala kachukua mume wa Mtu.

Tusamehe Madam Wema, tupo chini ya Miguu yako

Naona kakutuma uje umsifie, vp umepewa bei gani mkuu huyu madame wako si ndio kishoka aliyechakachua LUKU?

Leo hii unakuja kutusumbua hapa?

Binafsi na familia yangu sitaweza kumuomba msamaha mtu aliyekwepa kulipa umeme.
 
hakika umenena ukweli huyu ni mtanzania mwenzetu pia hajawahi kutuletea shemeji nje ya nchi hii ni kuonyesha kwamba vijana wetu wana nufaika nae
 
Thread nzuri sana hii.

Natumia nafasi hii kumuomba msamaha madam pia. Nimekua nikichekelea pindi watanzania Wenzangu wanapomchafua bila kujali Umuhimu wake. Watu wametajirika kwa kuuza magazeti ya kumchafua wala hajawa na kinyongo na Mtu.

Wema Sepetu sio malaya tena hana tabia chafu. Hajui kubadilisha mabwana hadi labda mabwana wamuumize na kumuacha bila sababu. Kwenye mapenzi Wema hajui kuchanganya mabwana, akipenda amependa na yupo wazi si sawa na Wasanii wengine ambao hujui mumewe ni nani kwani wanao wengi.

Madam Wema Sepetu anafaa kuwa Mke na Mama wa Familia kwani kapitia mikimikiki mingi ya maisha na ana uvumilivu wa hali ya juu. Kama kuumizwa kaumizwa sana.

Wema Sepetu tusamehe Sisi Watanzania, tumekukosea sana. Sijawahi sikia Wema kagonganisha mabwana, kafumaniwa wala kachukua mume wa Mtu.

Tusamehe Madam Wema, tupo chini ya Miguu yako

Bora umesema wewe. Ingekuwa kina siye tungejuta. Ahsante kwa niaba ya madam Sepenga
 
Naona hapa kuna watu wanaanza kujipendekeza, jina la madame wema linaweza kuwepo kwenye list ya wakuu wapya wa wilaya, hongera zake kwa kumnadi vyema mama samia suluhu na Magufuli.
 
Naona kakutuma uje umsifie, vp umepewa bei gani mkuu huyu madame wako si ndio kishoka aliyechakachua LUKU?

Leo hii unakuja kutusumbua hapa?

Binafsi na familia yangu sitaweza kumuomba msamaha mtu aliyekwepa kulipa umeme.
Mtafuta Free P huyo
 
Thread nzuri sana hii.

Natumia nafasi hii kumuomba msamaha madam pia. Nimekua nikichekelea pindi watanzania Wenzangu wanapomchafua bila kujali Umuhimu wake. Watu wametajirika kwa kuuza magazeti ya kumchafua wala hajawa na kinyongo na Mtu.

Wema Sepetu sio malaya tena hana tabia chafu. Hajui kubadilisha mabwana hadi labda mabwana wamuumize na kumuacha bila sababu. Kwenye mapenzi Wema hajui kuchanganya mabwana, akipenda amependa na yupo wazi si sawa na Wasanii wengine ambao hujui mumewe ni nani kwani wanao wengi.

Madam Wema Sepetu anafaa kuwa Mke na Mama wa Familia kwani kapitia mikimikiki mingi ya maisha na ana uvumilivu wa hali ya juu. Kama kuumizwa kaumizwa sana.

Wema Sepetu tusamehe Sisi Watanzania, tumekukosea sana. Sijawahi sikia Wema kagonganisha mabwana, kafumaniwa wala kachukua mume wa Mtu.

Tusamehe Madam Wema, tupo chini ya Miguu yako

Inaniuma sana mkuu. Wakati mwingine hizi ni laana za Kitaifa. Imagine mtu anamchukia Wema wakati hajawahi kumfanya lolote, wanaacha kuwamaindi waandishi uchwara ambao kila leo wanawaharibia watu wanyonge maisha, kwa kuandika habari zao bila faraga wala kificho.

Naamini tukiwachukuza GPL na programu zao kama OFM tutakuta wameharibu sana ndoa, mahusiano, saikolojia na hata kuwafanya wengine wajiue. Ila mmiliki ni mfano wa kuigwa na Wema ndio Mama Ubaya!
 
Kuwa miss ndio mafanikio?..
Huyo sio Miss, ni Miss Tanzania 2006, nafasi ya kitaifa na ambayo mshindi huwakilisha Taifa. Kuna kipindi interest za Madam zilikuwa ndio interest za Taifa na siku ikitokea Madam akatangulia basi ni msiba wa kitaifa.

Ndio maana 'Wema Sepetu' wa 2014 alipokutwa na sakata la kufoji umri alijadiliwa na Bunge la Jamhuri, na kurekodiwa kwenye Kumbukumbu Rasmi za Bunge. Dig it!

Kama una tatizo na hilo pole!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom