Madaktari wote wa umma waongezwe mishahara na wasiruhusiwe kuwa na hospitali zao binafsi

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
WanaJF bila shaka wengi tumesikia athari za madakatari wa umma kukosa maadili kwa kuwa wanalipwa mishahara midogo kwa kazi ngumu na nyeti inayohusu maisha ya watu.

Tatizo lilianza baada ya serikali kuwaruhusu madaktari kuwa na hospitali zao badala ya kuwaongeza mishahara.

Kwa kuwa sasa serikali imeanza vizuri kwa kukusanya kodi kikamilifu, ni wakati muafaka madakari wakaongezwa mishahara inayofikia hata tzs 10m kwa mwezi ili wale wanaotaka kutumikia umma wabaki serikalini na wale wenye kupenda biashara waondoke.

Kwa sasa kuna watu wanalipwa hadi tzs 20m kwa kazi za kiutawala na siasa ambazo siyo nyeti kama za madaktari. Changieni kwa hoja ila msiseme kuwa serikali haina fedha za kutosha.
 
Sawa kabisa, madaktari ndo wokozi wa uhai wetu ukiacha mwenyezi mungu, walipwe vizuri, at least Tsh 10 million per month. Jiulize iweje afisa wa TRA alipwe 25 million per month huku daktari anaeokoa maisha yetu alipwe milion 1 tu kwa mwezi? Hapo haki iko wapi?? Magufuli wathamini madaktari.
 
Kweli kabisa wanastahili walipwe mshahara mzur ili wafanye kaz waloisomea.. Waache kufungua viduka vya ajabu
 
Leo tunajifunza umuhimu wa Azimio la Arusha kwa vitendo baada ya kuitupa nadharia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere
 
Tupo katika Mixed Economy, Serikali Pekee yake haiwezi kutoa huduma zote kiukamilifu, wanahitajika watu binafsi watakaoweza kusaidiana na Serikali katika kutoa huduma. Kwa msingi huo ni sahihi kwa Serikali kuongeza mishahara kwa Wafanyakazi wa kada ya afya kama njia moja ya kuwapa motisha lakini pia iwaruhusu kumiliki Hospitali zao kwa wale ambao wanaoweza kuziendesha hospitali zao kwa Tija bila ya kuingiliana na majukumu yao ya msingi ya utumishi wa umma.
 
Na sisi walimu ambao ndio tunawafundisha watu wote had kuwa wataalam!je hamtupigii debe

Tatizo ninyi walimu hampendani ninyi kwa ninyi,
  • Magreth Sitta ni Mwl, alikuwa Waziri wa Elimu hakuwaona
  • Mwananzila ni Mwl. alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, naye hakuwaona
  • Mulugo nae pia tulidokezwa kuwa ni Rabi, alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, hakuwaona
  • Jenister Mhagama ni Mwl naye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu naye alipita kwenye Wizara hiyo lakini hakuwaona
  • Who else?
 
Kwa maoni yangu watumishi wote wa afya waongezewe sio madaktari pekeyao lakn sio kwa kiwango pendekezwa hapo juu,
Pia naona hao maofisa wa tra na taasisi zingine za serikali wapunguziwe mshahara na marupurupu yao ili fedha nying ipelekwe kwenye mambo ya kimaendeleo na sio matumiz ya serikali
 
WanaJF bila shaka wengi tumesikia athari za madakatari wa umma kukosa maadili kwa kuwa wanalipwa mishahara midogo kwa kazi ngumu na nyeti inayohusu maisha ya watu.

Tatizo lilianza baada ya serikali kuwaruhusu madaktari kuwa na hospitali zao badala ya kuwaongeza mishahara.

Kwa kuwa sasa serikali imeanza vizuri kwa kukusanya kodi kikamilifu, ni wakati muafaka madakari wakaongezwa mishahara inayofikia hata tzs 10m kwa mwezi ili wale wanaotaka kutumikia umma wabaki serikalini na wale wenye kupenda biashara waondoke.

Kwa sasa kuna watu wanalipwa hadi tzs 20m kwa kazi za kiutawala na siasa ambazo siyo nyeti kama za madaktari. Changieni kwa hoja ila msiseme kuwa serikali haina fedha za kutosha.

Mkuu naunga hoja mkono! Inafaa walipwe mishahara na marupurupu ya kufaa na kutosheleza na wapewe katazo la kufungua biashara binafsi zinazoenanda na taaluma yao, na pia wasiruhusiwe kwenda kufanya kazi part-time kwenye Hospitali nyingine watakakolipwa chochote cha ziada! Hii itasaidia wa devote muda wao wote kwenye Hospital/vituo vyao vya kazi!!
 
Na sisi walimu ambao ndio tunawafundisha watu wote had kuwa wataalam!je hamtupigii debe

kama kuna taaluma inayopaswa watumishi wake walipwe vizuri ni waalimu. wote lazima tupitie kwa mwalimu. pia waalimu nao lazima wapitie kwa mwalimu. mwalimu ndo kila kitu.
mwalimu tulia, ngoja upatikane uwanja mzuri nitawatetea kwa nguvu zote.
 
Naam!!! bilashaka watu wanaanza kusikia kilio chetu na kuona umuhimu wetu
 
Nadhani mnazungumzia watoa huduma za afya kwa sababu madaktari ni kundi dogo tu kati ya jumuiya nzima ya watoa huduma za afya kama manesi,wafamasia,wateknolojia maabara,watu wa viungo bandia,wafiziotherapia,wakemia tiba,wapasuaji wa kinywa na meno etc.
 
Tatizo lililopo kwa kada ya afya ukiongezea na walimu na maaskari ni wengi sana nadhan wanaweza kuzidi nusu ya wafanyakaz wote serkalin, kuongeza mshahara ni hela nying mkumbuke pia kutaongezeka mchango wa mwajir kwenye pension, na health insurance, cdhan kama wataweza, jambo linalotakiwa ni kuondoa nyongeza za mishahara kwenye mashirika ambayo mishahara iko juu, halafu kuendelea kuongeza kidogo kidogo kwenye kada ambazo ziko underpaid, huku juhudi kubwa zikiwa kuimarisha thamani ya pesa yetu
 
Mkuu kwa tanzania bado tupo mbali kusema kuwa tuna health care providers wengi.The recommended physician to patients ratio is far from where we are now
 
kama kuna taaluma inayopaswa watumishi wake walipwe vizuri ni waalimu. wote lazima tupitie kwa mwalimu. pia waalimu nao lazima wapitie kwa mwalimu. mwalimu ndo kila kitu.
mwalimu tulia, ngoja upatikane uwanja mzuri nitawatetea kwa nguvu zote.

Hapa tunazungumzia maisha ya watu pamoja na ya waalimu. Acheni wivu ni lazima tuwe ni vipaumbele kwa mambo yanayovuruga maadili kama madaktari kutumia muda wao kwenye biashara. Tunataka wasiwaze fedha wakiwa THEATRE. Wenzetu walioendelea hawaruhusu hali hiyo ndiyo maana tunazifuata huduma nzuri nchi za nje.
 
kama kuna taaluma inayopaswa watumishi wake walipwe vizuri ni waalimu. wote lazima tupitie kwa mwalimu. pia waalimu nao lazima wapitie kwa mwalimu. mwalimu ndo kila kitu.
mwalimu tulia, ngoja upatikane uwanja mzuri nitawatetea kwa nguvu zote.

Sio walimu hawa wa generation hii.

Kama tukitaka kufanya reforms kwenye elimu kupitia walimu basi itabidi tuanze upya kwa kurecruit wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi kwenda vyuo vya ualimu(tofauti na sasa).Yaani minimum required qualifications za kwenda kusomea ualimu zilingane na udaktari au engineering na kuanzia hapo tuanze kuwalipa pesa ndefu walimu wetu
 
Tatizo kubwa la watanzania ni ubinafsi. Kila mtu anataka yeye tu ndio awe juu. Hata wewe mleta mada umo kwenye kundi la wabinafsi. Nilitarajia useme wafanyakazi wote waongezewe mishahara kulingana na majukumu yao wewe unalenga madaktari tu. Hivi hujui kama sekta zote hapa nchini zinategemeana? Mfano wakikosekana wakulima, daktari hawezi kula dawa wala wagonjwa wake, na wala mtu wa TRA au mhasibu hawatakula pesa zao, hali kadhalika akikosekana mtu wa TRA daktari hatolipwa mshahara. Kama ni suala la umuhimu, basi Mwalimu aliyemfundisha daktari au mtu wa TRA au wa BOT alistahili alipwe zaidi kuliko wanafunzi wake. Hali kadhalika tukikaa maofisini, wote tunatumia masaa yale yale na kama kuna ya ziada ni suala jingine ambalo hata wa tra anaweza kuwa nayo. Jambo la msingi ni serikali kuongeza mishahara kwa kila sekta ili watumishi wasiachane saaana. Wakiona hilo haliwezekani basi wapunguze mishahara ya hao TRA, Bandari, BOT na watawala wengine.
 
Na sisi walimu ambao ndio tunawafundisha watu wote had kuwa wataalam!je hamtupigii debe
Ni kweli watumishi wa kuangaliwa kabla ya wote ni sisi walimu kwakuwa ndo kila kitu doctors lazima atoke kwa mwalimu hivyo sisi ni zaidi ya wote hao.
 
Ni kweli watumishi wa kuangaliwa kabla ya wote ni sisi walimu kwakuwa ndo kila kitu doctors lazima atoke kwa mwalimu hivyo sisi ni zaidi ya wote hao.
tuko pamoja mwalimu. mwalimu ndo kila kitu. unapoanza shule ya msingi, mwalimu kwako ni:
daktari kwa kukufundisha elimu ya msingi katika afya(magonjwa, lishe usafi nk)
engineer kwa kukufundisha stadi za kazi.
mwanasiasa kwa kukufundisha uraia.
endelea hivyo kwa masomo mengine.
kumbuka siku ya kwanza ulipokaa mbele ya mwalimu ulikuwa kama shamba ambalo halijalimwa, limejaa magugu, manyasi nk(ujinga nk). leo hii umekuwa shamba lenye zao la thamani(daktari, m/siasa nk). je, umefika hapo bila mwalimu? je, si mwalimu aliyeibua hicho kipaji ndani yako?
maendeleo tunayoyaona na tunayoyataka chanzo ni mwalimu, kubali kataa.
ni wakati muafaka sasa mwalimu apewe kipaumbele kimaslahi hata kufikia fani nyingine au kuzidi.
mwalimu ndo kila kitu jamani, mbona hamwelewi? au mpaka aje Mungu ambae ni mwalimu pia awafundishe hili nalo? hapana, mtaelewa tu.
 
Back
Top Bottom