Madaktari warejea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari warejea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 6, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kipaumbele ni huduma za dharura kwanza
  [​IMG] Suluhu kujulikana kikao chao na wabunge kesho


  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka


  Kufuatia mgomo wa madaktari ambao umetikisa nchini kwa takriban wiki ya tatu sasa, hatimaye wameguswa na utu, hivyo kuamua kurejea kazini wakati Bunge likiingilia kati kutaka mgomo wao upate suluhu ya kudumu.
  Kiashiria cha kurejea kwa madaktari hao kinafuatia hatua ya Bunge kuiagiza Kamati ya Bunge ya huduma za Jamii kushughulikia mzozo huo.
  Akizungumza na NIPASHE Jumapili jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao chao cha jana.
  Hata hivyo, alisema kipaumbele kitakachowaongoza madaktari hao ni utoaji wa huduma za dharura kwa wagonjwa wanaofika hospitalini.
  Alisema huduma zitakazotolewa ni zile za dharura peke yake na sehemu nyingine wanaendelea na mgomo wao kama kawaida mpaka hapo watakapokutana na kamati hiyo.
  "Tumeona si vizuri kuacha kutoa huduma za dharura, unakuta mgonjwa anatolewa hospitali ya Mwananyamala amezidiwa labda kuja Muhimbili… wakati Bunge limeonyesha nia nzuri na sisi hivyo tumekubaliana kutoa huduma za dharura," alisema
  Alisema bado hawajaafiki suala la kurejea kazini moja kwa moja mpaka watakapozungumza na wabunge kujua hatima ya maslahi yao.
  Hata hivyo, Dk. Ulimboka alisema tayari kamati hiyo imewapigia simu jana na kuwajulisha kuwa watakutana nao kesho Jumatatu ili kujadiliana suala lao.
  Alisema eneo ambalo watakutana kwa ajili ya mkutano huo bado halijafahamika, kwa kuwa kamati hiyo imewajulisha watatafuta ukumbi na baada ya hapo watajulishwa.

  Dk. Ulimboka alisema amemshangaa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda kulipotosha Bunge badala ya kujibu hoja za msingi ambazo alitakiwa kuzielezea.
  "Dk. Mponda jana(juzi) ametoka nje ya hoja na kuanza kuzungumzia mambo ambayo hayapo, anaanza kunizungumzia mimi sio Daktari, hilo jambo si la kweli kwa maana nina cheti cha kufuzu udaktari,” alisema.
  Pia Dk Ulimboka alisema kutokana na kukidhi vigezo vikiwemo vya kitaaluma, alikubaliwa kuwa mwanachama wa Chama cha Madaktari nchini (MAT).
  Dk Ulimboka alisema madaktari wapo tayari kukutana na kamati ya Bunge, kujadiliana matatizo yao na kufikiana muafaka ili warejee kazini kwani mgomo huo umeleta madhara kwa wananchi kutokana na huduma za afya.
  Wakati huo huo, wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, wamewasili jijini Dar es Salaam kutafuta suluhu ya mgomo wa madaktari.
  Hatua hiyo imekuja takribani siku mbili baada ya Naibu Spika wa Bunge, kutoa agizo kwa kamati hiyo, huku tisho la serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwafukuza kazi, likionekana ‘kugonga mwamba.’
  Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta, ilitarajiwa kuwasili jijini humo jana ikitokea Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, aliimbia NIPASHE Jumapili kwa njia ya simu jana kuwa kamati hiyo, pamoja na kuangalia njia bora ya kumaliza mgogoro uliopo, itatoa mapendekezo ya hatua stahili za kuchukuliwa kwa waliosababisha tatizo hilo kuwa kubwa.
  Alisema wajumbe wa kamati hiyo walianza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya kuanza rasmi kazi.
  "Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii tumeanza safari ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza kazi, kesho (leo) tutafanya mkutano wetu wa kwanza kuangalia tuanze na hatua gani katika suala hili," alisema.
  Dk. Ndugulile alisema mjadala wa kwanza katika kikao chao utakuwa kuchambua kikamilifu tamko la serikali, lililotolewa kwenye kikao cha Februari 4 mwaka huu, kabla ya kwenda hatua ya pili ya kukutana na makundi mbalimbali yanayohusishwa katika mgogoro huo.
  "Kule bungeni tumesikia kauli ya serikali, lakini kuna upande mwingine ambao una haki ya kusikilizwa ili tupate ukweli wa mgogoro huu, nadhani madaktari katika makundi yote yatafikiwa na kamati kwa ajili ya kujieleza," alisema.
  Hata hivyo alisema kamati hiyo haitatoa hukumu kwa watu watakaohusika na kusababisha mgomo huo, bali mapendekezo ili serikali iyatekeleze.
  Dk. Ndgulile alisema kamati hiyo haijapewa muda kamili wa kufanya kazi hiyo, hata hivyo wanafanya mawasiliano na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kuwaeleza mchakato huo uwe wa muda gani.
  Katika taarifa ya serikali iliyosomwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, ilielezwa kuwa mgomo huo si halali kwa mujibu wa sheria ya ajira inayowakataza wafanyakazi wa sekta muhimu kugoma.
  Alisema tangu mgomo huo uanze, serikali imechukua hatua mbalimbali kuutatua ikiwa pamoja na kuwa na nia ya kuongea na madaktari, lakini hawakuonyesha dhamira ya kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo.
  Dk. Mponda alisema hatua walizochukua baada ya Waziri Mkuu kutoa tamko la kumaliza mgomo ni kuunda kamati maalum ya kufuatilia maazimio yaliyowasilishwa kwa Waziri MKuu ili yachambuliwe na kutolewa mapendekezo yatakayisaidia kutatua mgogoro huo.
  Habari hii imeandikwa na Beatrice Shayo na Moshi Lusonzo


  SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,091
  Likes Received: 10,449
  Trophy Points: 280
  the movie is still continue!!!
   
 3. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  safi ..na sisi walimu tutafuata!
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Walim nyie hamna tofautina na serikali yetu bora mwendelee kutulia hivyo hivyo
   
 5. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hicho ndicho walitakiwa wafanye tangu awali: watoa huduma muhimu sharti wajigawe-wengine wakiendelea na mgomo baadhi yao wanashauriwa kuendelea kutoa hudumu hasa ktk sehemu iliyomuhimu. (ref.ELRA No 6/2004 and Code of Conduct & Good Practice 2007)
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  toka mwanzo huduma za dharula zilikuwepo lakini baada ya kuchefuliwa na pinda ndipo nazo zikasitishwa ili kumuonesha ametumia ****** kutoa matamshi. Baada ya bunge kutaka kuongea na madaktari ndipo walikaa na kuamua kurudisha emergency service. KAULI ZA SERIKALI INALISHUGHULIKIA HILI SUALA HAZITAKIWI TENA,!
   
 7. bona

  bona JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  nadhan walimu ndo watajifunza haki inadaiwia KWA NGUVU IKIBIDI, wataangamia na mgaya wao anayewazungusha kila kukicha, yule jamaa ni hmanzo sana, we mgogo unatngaza eti utafanyika next month, kuna mgomo wa ivyo kweli?
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,508
  Trophy Points: 280
  Madoctor mkomae mkijilegeza tu mmeumiaj
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Tunaomba heri itawale shari, na suluhu ipatikane.
   
Loading...