Madaktari wanahaki Muajiri je ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wanahaki Muajiri je ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 28, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwanza ieleweke wao madaktari ni binadamu kama binadamu wengine ,ujuzi wao usikufanye wewe kuwaona wao wabaya wanapodai hela na kusema wapo kimaslahi ,maslahi hayo ndio hayo hayo yanayoifanya Mareakani na vikaragosi vyake kusema wanapigana kwa ajili ya kulinda maslahi.

  Hivyo madaktari nao wana haki yao kugoma ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa ,kumbuka hawapo hapo Muhimbili na kwengineko kwa ajili ya kujitolea ,wapo hapo wakifanya kazi ya kuajiriwa ,wanazo sababu za kila aina kudai nyongeza na mambo mingine ikiwemo vitendea kazi.

  Kukubali au kukataa inategemea kujitosheleza kwao ,kwa zile hoja walizodai ,mbunge anapokea milioni 12 cash money ,kazi za wabunge wetu zinajulikana ,mtu yeyote yule anawezakuifanya ,haihitaji ujuzi wala shahada wala elimu si kigezo cha kuwa mbunge ,ngekewa au kismati kikikuangukia unaweza kuwa mbunge ,ei jamani si vijijini huko unapiga longolongo unakuwa mbunge tu shida ipo wapi ? Kaa pale bungeni ukicheka ukinuna ,ukipiga makofi hakuna anae kuuliza ,wangapi wamo mle , yaani hata kazi ya yule nasi anaetandika vitanda pale hospitali ni kubwa sana mbali ya daktari muelewa bingwa wa kazi aliyetupa miaka kuisomea ,maada udaktari si chini ya miaka saba.

  Milioni 12 kwa mwezi analipwa mbunge ,ni hela nyingi sana na hii italiletea Taifa hili matatizo ,madaktari wameanza walimu na wengine watafuatia tu ,kwani waajiriwa wa serikali si madaktari peke yao.

  Sasa hawa wanaowachoka madaktari waelewe tu kuwa Madaktari hawa hawapo kazini kwa kujitolea ni lazima iwepo tofauti kati ya kazi ya kujitolea na ya kuajiriwa.

  Leo hii wanaweza kutangaza kuwa watarudi kazini kwa kujitolea na hapo watakuwa na hiari yao inawezekana akafika kazini sa mbili kufika saa nne akaondoka zake. Hivyo mimi siwalaumu kabisa ,kwani kazi kama kazi inahitaji kulipwa na muajiri kama malipo hayatoshi mfanyakazi anahiari yake kuendelea kugomaau kuacha kazi.

  Sasa tuseme muajiri hana uwezo wa kutimiza matakwa ya madaktari ,je awapunguze ,awafukuze kazi aafanye nini?
   
 2. M

  Mchili JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tatizo wabongo wengi wanrukia mambo bila kujua. Wanachodai madaktari sio maslahi yao tu, ni pamoja na mazingira mazuri ya kazi ambayo ni mazingira mazuri ya wagonjwa.

  Nawashangaa watu wanaowalaumu madaktari badala ya kuilaumu serikali yao.
   
 3. m

  mwelimishaji Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashauri masihara yasifanyike kwa madai ya madaktari. Umuhimu wao hauwezi kulinganishwa na fani nyingine yoyote. Wanaokoa maisha wanapotibu na Mungu anapoponya. Daktari yuko katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kila iitwapo leo. Nafasi ya daktari kustarehe baada ya kazi ni ndogo mno kwani saa yoyote huhitajika kazini.
  Ni vizuri kama madaktari watawekwa kwenye kundi maalum wanaostahili malipo maalum ili wasifanye kazi wakiwa na msongo wa mawazo, kazi haitafanyika vizuri.
   
Loading...